tangu makada warudi toka dodoma (mimi nilitangulia kurudi dar es salaam), hali si shwari ndani ya ofisi ndogo za ccm hapa lumumba. Makada wanapingana kimakundi yaliyopata na kukosa ushindi kule dodoma. Wapo makada wenye tabasamu la hamu na wale wenye sura zilzosheheni hasira. Hali si ile. Imebadilika.
Kazi zinakwenda polepole na hata hakuna wa kumuuliza mwingine kwa staha na raha. Maneno na matendo ya makada yamebadilika. Utaniutani uliokuwa ukituunganisha,umepungua na kuonekana unasumbua. Sasa ni urafiki wa kinafiki tu. Kwa werevu,tunayaona makovu ya dodoma. Yanafanya kazi sasa. Kununiananuniana ofisini kumekwamisha hata redio uhuru kutenda kazi zake ipasavyo. Tcra wanaivizia kuifunga kwa kutolipa kodi. Kodi imekwamishwa.
Viongozi mpo? Hali si shwari chamani!
Mzee tupatupa wa lumumba, dar es salaam
Na bado, mwaka huu lazimacmgawane mbao,
Hizi wishful thinking zenu mpaka lini?? Kama Mh.Magufuli aliweza kupata zaidi ya asilimia 80% ya kura zote,which means CCM sasa ni kitu kimoja i.e wana mshikamano thabiti,kama kuna watu waliokua wanasubiria igawanyike ili weweze kuishinda kirahisi hiyo wasahau.Japangeni upya who knows labda mwaka 2055 mnaweza kufanikiwa,UKAWA mnashindwa kuelewana nani abebe bendera ya upinzani nani anaweza kuwakabidhi Nchi Viongozi ambao masaa yote wapo kwenya chaotic Motion kama atoms za gesi ya Mnazi Bay/Songosongo!!
Kingunge chochea moto.Magufuli atatawara kwa remote kutoka msoga.Mzee kinukishe Lowasa arudishwe
Hivi kuna mtu kweli anasikiliza radio tumaini kweli?
Story za chini ya mwembe kazi ya Dodoma imeisha na Tingatinga liko mzigoni mtoa uzi inaonekana na wewe ni miongoni mwao kama vipi tupia picha zao kama hilo haliwezekani waambie watoke CCM maana hawalazimishwi kubakia huko!
VUTA-NKUVUTE
Bintiyo nilikuwa nakusubiri kwa HAMU kubwa utupe ukoko uliobaki kule Dodomya.Niliona UNAFIKI toka Dodomya watu wakipiga makofi mengiiiiiiiiiiiiii lakini nikajiemea kamwe usiusemee moyo wa mtu.
Hakika Mwenyekigoda hakutumia BUSARA wala HEKIMA.Ningekuwa mimi kwenye viatu vyake ningefanya haya:
1.Kwenye Kamati ya maadili ningewaomba wagombea wote waliojipigia debe mapema wenyewe wajiondoe ili CHAMA kisipate mushkeli kwenye UCHAGUZI mkuu kwa kuambiwa kwamba CCM ilianza kampeni mapema.
2.Ningejiondoa kwenye uenyekiti nikamwachia Mangula kiti kwa kisingizio kwamba ....SITAKUWA huru kwenye kuamua wathungu wangesema 'INTEREST OF CONFLICTS'
3.Ningeacha waliobaki wajieleze kwenye kamati ya maadili na kila mmoja ajibu kulingana na INTERVIEW atakayokuwa amepewa na jopo la KAMATI ya maadili
4.Ningesubiri kwenye mkutano mkuu yale majina yakiwa yameshachambuliwa.
Kutoka hapo ningekuwa nimenawa mikono kama alivyofanya PONSIO PILATO,makundi yangekuwepo,lakini yangeweza kuelewa kwa uwazi kabisa bila kuleta CHUKI wala mvurugano kwenye chama, nina uhakiak ningetoka kifua mbele kwa uamuzi huu.
Simfagilii LOHASSA ila kilichofanyika ndiyo siyo sahihi.............
Naomaba ya tafakari haya kisha unijibu kama ningekuwa MSHINDI au?Na ndiyo maana nasema 'Tupewe nafasi Tu, Tusiwezeshwe kwani Tunaweza bila Kuwezeshwa'.