VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Tangu makada warudi toka Dodoma (mimi nilitangulia kurudi Dar es Salaam), hali si shwari ndani ya Ofisi Ndogo za CCM hapa Lumumba. Makada wanapingana kimakundi yaliyopata na kukosa ushindi kule Dodoma. Wapo makada wenye tabasamu la hamu na wale wenye sura zilzosheheni hasira. Hali si ile. Imebadilika.
Kazi zinakwenda polepole na hata hakuna wa kumuuliza mwingine kwa staha na raha. Maneno na matendo ya makada yamebadilika. Utaniutani uliokuwa ukituunganisha,umepungua na kuonekana unasumbua. Sasa ni urafiki wa kinafiki tu. Kwa werevu,tunayaona makovu ya Dodoma. Yanafanya kazi sasa. Kununiananuniana ofisini kumekwamisha hata Redio Uhuru kutenda kazi zake ipasavyo. TCRA wanaivizia kuifunga kwa kutolipa kodi. Kodi imekwamishwa.
Viongozi mpo? Hali si shwari chamani!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam