Lumumba kwafukuta; Ya Dodoma yaanza kutoa cheche

Lumumba kwafukuta; Ya Dodoma yaanza kutoa cheche

Hivi kuna mtu kweli anasikiliza radio tumaini kweli?

kaka siyo Redio tumaini, ni Redio uhuru . Redio Tumaini ni Radio ya kanisa katoliki, ambayo pia wana TV yao TV -tumaini.

Wapo wengi wanaisikiliza including mimi.


Redio Uhuru ni ya CCM. nina miaka mingi sijaisikiliza. Hope Umeelewa
 
VUTA-NKUVUTE


Bintiyo nilikuwa nakusubiri kwa HAMU kubwa utupe ukoko uliobaki kule Dodomya.Niliona UNAFIKI toka Dodomya watu wakipiga makofi mengiiiiiiiiiiiiii lakini nikajiemea kamwe usiusemee moyo wa mtu.

Hakika Mwenyekigoda hakutumia BUSARA wala HEKIMA.Ningekuwa mimi kwenye viatu vyake ningefanya haya:

1.Kwenye Kamati ya maadili ningewaomba wagombea wote waliojipigia debe mapema wenyewe wajiondoe ili CHAMA kisipate mushkeli kwenye UCHAGUZI mkuu kwa kuambiwa kwamba CCM ilianza kampeni mapema.

2.Ningejiondoa kwenye uenyekiti nikamwachia Mangula kiti kwa kisingizio kwamba ....SITAKUWA huru kwenye kuamua wathungu wangesema 'INTEREST OF CONFLICTS'

3.Ningeacha waliobaki wajieleze kwenye kamati ya maadili na kila mmoja ajibu kulingana na INTERVIEW atakayokuwa amepewa na jopo la KAMATI ya maadili

4.Ningesubiri kwenye mkutano mkuu yale majina yakiwa yameshachambuliwa.

Kutoka hapo ningekuwa nimenawa mikono kama alivyofanya PONSIO PILATO,makundi yangekuwepo,lakini yangeweza kuelewa kwa uwazi kabisa bila kuleta CHUKI wala mvurugano kwenye chama, nina uhakiak ningetoka kifua mbele kwa uamuzi huu.

Simfagilii LOHASSA ila kilichofanyika ndiyo siyo sahihi.............

Naomaba ya tafakari haya kisha unijibu kama ningekuwa MSHINDI au?Na ndiyo maana nasema 'Tupewe nafasi Tu, Tusiwezeshwe kwani Tunaweza bila Kuwezeshwa'.

Binti yangu Tetty, mambo sasa ni mchafukoge

Mzee Tupatupa
 
Kwani wewe umekuwa ccm tangu lini nadhani imefika wakati tukutaje kwa majina yako mpaka ulipo ili ujue kuwa tunakujua wewe ni bavicha tena kwenu tunapajua mpaka unapofanyia kazi hata jina lako halisi unalotuia humu jf tunarijua.

Hizi ni ramli chonganishi. Huna jipya. Umeumbuka

Mzee Tupatupa
 
Binti yangu Tetty, mambo sasa ni mchafukoge

Mzee Tupatupa

Mzee wangu Tupatupa,sentensi fupi lakini yenye MSHINDO mkuu.Inabidi nielewe japo umekuwa kama Mashairi ya kile kitabu cha KULI ulichoninunulia nikiwa namaliza kidato cha tatu kuingia cha nne.

Haya tumeyasikia hata matusi kwa vijana wakimtukana Mzee Kingunge wa Ngombale,kwa maana heshima yake imekwisha?

Au mlichelewa kuwakunja SAMAKI akingali mbichi?Maana kwenye zile methali kuu za enzi hizo mtoto akitukana mkubwa basi huambiwa wazaziwe hawakumkunja angali mbichi.

Sasa mmekosea wapi wazee wangu kuwafunda vijana wenu?:disapointed::disapointed::disapointed:

Mbona enzi zetu mlitufunda vyema?Imekuwaje VIJANA wa LEO mmewaacha kama MBUZI aliyekosa MCHUNGAJI?

Au ni kati ya zile misemo ya Nabii Issa,ambaye wengine twamwita YESU,kuwa MCHUNGAJI mwema hujua kondoo wa kundile,sasa wapi mmekosea?

Mzee wangu sentensi yako fupi lakini ina maswali mengi mpaka kueleweka...........
 
Tangu makada warudi toka Dodoma (mimi nilitangulia kurudi Dar es Salaam), hali si shwari ndani ya Ofisi Ndogo za CCM hapa Lumumba. Makada wanapingana kimakundi yaliyopata na kukosa ushindi kule Dodoma. Wapo makada wenye tabasamu la hamu na wale wenye sura zilzosheheni hasira. Hali si ile. Imebadilika.

Kazi zinakwenda polepole na hata hakuna wa kumuuliza mwingine kwa staha na raha. Maneno na matendo ya makada yamebadilika. Utaniutani uliokuwa ukituunganisha,umepungua na kuonekana unasumbua. Sasa ni urafiki wa kinafiki tu. Kwa werevu,tunayaona makovu ya Dodoma. Yanafanya kazi sasa. Kununiananuniana ofisini kumekwamisha hata Redio Uhuru kutenda kazi zake ipasavyo. TCRA wanaivizia kuifunga kwa kutolipa kodi. Kodi imekwamishwa.

Viongozi mpo? Hali si shwari chamani!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Kutofautiana ndani ya chama/kampuni au entity yoyote ile siyo jambo la ajabu. CCM ilikuwa na tofauti tangu enzi za mwalimu na ndio sababu kina Kambona hawakuridhika na azimio la Arusha wakakimbilia nje. Tumeona pia kina Mzee Masha walitofautiana na Mwalimu wakaondoka ndani ya chama. Same for Aboud Jumbe, Maalim Seif, Mrema, etc.

Isitoshe siyo CCM tu wanaotofautiana, tumeona CHADEMA mpaka kina Zitto na Kitila Mkumbo wakaondoka. Sasa hoja yako katika bandiko hilo hapo juu ni nini?

Maana hakuna cha ajabu sana kwa watu kutofautiana kimitazamo.
 
Kikwete amewaulia Chama hivi hivi,mnatia huruma sana!
 
Kikwete amewaulia Chama hivi hivi,mnatia huruma sana!

Lowassa akamwambia jk ...." Sawa umenikata Mimi kwa sababu unasema fisadi ...SASA Hadi Makongoro Naye unamkata ..NA Hana kashfa ....."

WAZIRI MKUU NA MAKAMU wa Rais ..kiprotocal huwa wanaingia 5 bora ..NA Kama hawatakiwi kugombea huwa wanaambiwa mapema ..ILI kutikuwadhalilisha ....
Vivyo Hivyo waliopata KUWA mawaziri wakuu Kama hawatakiwi hutumiwa kabisa watu NA mapema wasichukue fomu ILI presidency usidhalilishwe
 
Hata mm ni gekuwa makam au waziri mkuu ningemaind.kiukweli kawadharau na kuwaona bawana uwezo
 
Hizi wishful thinking zenu mpaka lini?? Kama Mh.Magufuli aliweza kupata zaidi ya asilimia 80% ya kura zote,which means CCM sasa ni kitu kimoja i.e wana mshikamano thabiti,kama kuna watu waliokua wanasubiria igawanyike ili weweze kuishinda kirahisi hiyo wasahau.

Wacheni kuleta jamvini stori za kubuni ,mimi nawashaurini japangeni upya who knows labda mwaka 2055 mnaweza kufanikiwa mkiacha ubinafsi wa kugawa vyeo na Ubunge kwa marafiki zenu,ndugu zenu,wake zenu na washikaji zenu-je mkienda Ikulu si Taifa letu litafanana la URUSI enzi za Yelstin.
.

Hata ingekuwa %100 kwa ninavyowafahamu wana CCM haimaanishi kuwa wanamkubali JPM na pia haimaanishi kuwa hakuna makundi. Inamaanisha kwamba wanachama hawakubali kupoteza nafasi wanazotazamia kupata ama kuendelea nazo, chezea CCM weye
 
Hizi wishful thinking zenu mpaka lini?? Kama Mh.Magufuli aliweza kupata zaidi ya asilimia 80% ya kura zote,which means CCM sasa ni kitu kimoja i.e wana mshikamano thabiti,kama kuna watu waliokua wanasubiria igawanyike ili weweze kuishinda kirahisi hiyo wasahau.

Wacheni kuleta jamvini stori za kubuni ,mimi nawashaurini japangeni upya who knows labda mwaka 2055 mnaweza kufanikiwa mkiacha ubinafsi wa kugawa vyeo na Ubunge kwa marafiki zenu,ndugu zenu,wake zenu na washikaji zenu-je mkienda Ikulu si Taifa letu litafanana la URUSI enzi za Yelstin.

Hatusemi mambo ya kubuni hapa mifano/vihashilia vipo vya kuthibitisha hamjajipanga sawa sawa - kama UKAWA mnashindwa kuelewana nani abebe bendera ya upinzani nani anaweza kuwakabidhi Nchi Viongozi ambao masaa yote wapo kwenye chaotic Motions kama atoms za gesi ya Mnazi Bay/Songosongo!! Siwasem vibaya ila tukubaliane kwamba linapo kuja suala la kukabidhiwa Nchi - nyinyi bado saana ndio maana CUF wanawakacha.

Mkuu utakuwa umechanganya mambo,nadhani Mzee vuta nikuvute amesign Lumumba na kwa uelewa wangu Lumumba ni makao makuu ya CCM si UKAWA, napendekeza urudi kwenye mada Lumumba huko watu wananuniana
 
"Watauana, watazozana kwa tonge la ugali, watatukanana, watasengenyana kwa tonge la ugali.. na watatengana kwa tonge la ugali..MAALIM SEIF KHATIBU" WASAKATONGE KAZINI
 
Lowassa akamwambia jk ...." Sawa umenikata Mimi kwa sababu unasema fisadi ...SASA Hadi Makongoro Naye unamkata ..NA Hana kashfa ....."

WAZIRI MKUU NA MAKAMU wa Rais ..kiprotocal huwa wanaingia 5 bora ..NA Kama hawatakiwi kugombea huwa wanaambiwa mapema ..ILI kutikuwadhalilisha ....
Vivyo Hivyo waliopata KUWA mawaziri wakuu Kama hawatakiwi hutumiwa kabisa watu NA mapema wasichukue fomu ILI presidency usidhalilishwe

Kwi kwi kwi kwi kwi!
 
Back
Top Bottom