Lukuvi: Heko Kamuhanda kwa Kazi Nzuri!

Ndugu wana JF,

Tumeshuhudia viongozi wetu tunaowategemea kukomesha huu uonevu tunaofanyiwa na baadhi ya waliopewa mamlaka katika jeshi la polisi na vyombo vingine.

Badala ya kukemea wao wanasifia.kwa mfano lukuvi anamsifia kamhanda. Sasa ninachokiona mbele yetu ni mateso bin taabu
 
Halafu kuna wstu humu wanajiita wana CCM wanatetea upuuzi huu. RIP Mwangosi
 
Lukuvi atakuwa alikuwa na Bifu na Mwangosi,huyu na Kamuhanda ni dugu moja mahakamani january 2016,jimbo la Lukuvi ni umasikini mtupu.
 
Tanzania inaongozwa na maharamia, watu wema wamekaa majumbani, viongozi wetu wanatuteulia mafia kuongoza majeshi yetu. Tanzania hatutakuwa kuwa salama sio kielimu,kiafya,kiulinzi na hata kwa umoja wa taifa letu mpaka hiki chama kilichopanga ikulu kiondoke madarakani, maana kimelewa chakari!
 
Hii nchi inaongozwa kihuni huni tu hakuna uwajibikaji,viongozi hawajui waongee nini na mda gani!,kila mtu ni Rais hii nchi

Sasa RPC yupo kwenye kashfa ya mauaji waziri wa Serikali anasifia kazi yake aliyoifanya wakati shauri bado linaendelea hii inajenga picha gani?

Kwanini hawa watu hawawajibiki?

Alafu naona kama watu siku hizi wamekata tamaa hakuna anayeshinikiza sasa watu wajiudhuru wanaishia kusema aaah!yule kanunua cheti...yule gamba....!

Hii kauli kwa nchi nyingine zenye "serikali" na "wanaharakati makini" isingeisha juu juu bila maelezo sahihi ila kwa Wanaharakati na Waandishi njaa hawa wa kibongo hakuna atayetilia maanani....ni upepo tu utapita

Afadhali hata CHADEMA huwa wanawapigia kelele na maandamano juu lakini hawa wanaharakati wengine wamekaa kimya tu wameiachia CHADEMA peke yake kupambana na hili Genge la Majangili...


Sent from BlackBerry
 
943645_397825230330664_1760656867_a.jpg


Ee Mungu uipoke roho ya mtumishi wako Daudi Mwangosi umpumzishe kwa amani. Mungu wetu, Mungu mwenye uweza na mamlaka, uonaye yote haya tunakusihi usikawie uweza wako ukapate kuonekana.
 
Mojawapo ya madhara ya Global Warming ni kuathiri brain cells, zinakuwa denatured na hivyo kushindwa kufanya kazi vizuri, akili za mhusika kurudi katika zama za Ujima kama kwamba yeye hakuelimika(anakuwa hajielewi) na anawaona wanaomsikilza ni vilaza wa ufahamu zaidi ya vichaa. Chakushangaza huu ugonjwa umewaathiri watawala wale wa Magamba pekee, popote pale walipo Duniani.
 
kamuhanda ana kosa gani. mnampiga tu mawe huku anayetakiwa kujibu mnamuacha. kwenye mauwaji wa mwangosi wakuadhibiwa ocd hata kama rpc alikuwa pale hii ni kutokana na protoko za kijeshi so tukijaribu kuzipitia hutaona kosa lake na ndo mana mpaka leo wamemuacha iringa.
 
Yani napatwa na mashaka na wajumbe wa humu JF!

Wajumbe wa JF ni wavivu wa kufikiri tena kwenye mambo ya kawaida sana.

Hali hii inatokana na kukubali na kukumbatia fikra za kikundi cha watu wachache na waganga njaa yaani CHADEMA.

Mtanzania jitambue na huwe huru kifikra, acha kuwa balozi wa hao WASALITI wa taifa lao kwakuwa vibaraka wa watu wa magharibi yaani CHADEMA.

Turudi kwenye mada;

Alichosema mwanasiasa makini sana na mzalendo Mhe. Lukuvi ni katika kuijenga hoja yake ya kuwahamasisha polisi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa na kuzingatia maadili ya kazi kama kanuni na sheria zao zinavyo elekeza.

Katika kufanya hivyo basi, alimtaja kamanda Kamuhanda kama mfano wa makamanda ambao wanabidii kubwa kazini jambo ambalo hakuna mtanzania mwenye hekima na busara anaeweza kupinga kuhusu kamanda Kamuhanda.

Lakini haya yote yametokana na sababu kubwa ya kamanda kamuhanda kusemwa sana kwenye hotuba kivuli, na kama wote tujuavyo, mti wenye matunda siku zote ndio unapigwa mawe.

Kwa kumalizia tu, nichukue fursa hii kuwahasa watanzania wote bila kujali itikadi, epuka vitendo vinavyo fanywa na CHADEMA katika kushinikiza maandamano, ni mambo yanayo peleka machafuko na kuhatarisha amani ya nchi, kwa kufanya hivyo basi, tutawapa askari wetu muda na nguvu zaidi yakupambana na vitendo halisi vya uhalifu nchini. Haya yana mwisho lkn! Inaonekana we una maisha mazuri sasa nenda huko vijijin
 
Hakika lukuvi alitakiwa asizungumze maneno kama hayo katika mazingira ambayo kulitokea kifo cha mwangosi kama kawaida amewakosea wananchi na kuwapa polisi kiburi ingelikua ni mm nimgeomba msamaha
 
Lukuvi hajitambui kabisa na sijui hata familia yake anaiongoza vipi, tukumbuke alifanya kituko kwa kutoa agizo Lile gorofa pacha na lile lililoanguka libomolewe haraka sijui kama kauli yake imeishatekelezwa
 
Kuna wakati si busara sana kusema kila kitu. Ulimi unaumba. Pengine Lukuvi angegua ya kusema na yepi ataweka rohoni kwake au ayaongelee chumbani na mama watoto wake.

Kamuhunda alikuwa alikuwa mita chache sana kutoka mahali alipouliwa Mwangosi. Na kama Kamuhunda angesema 'acha' upo uwezekano watoto wa Mwangosi wangekuwa na baba yao mzazi. Hii kauli ya Lukuvi, inawezekana ni joto la siasa za bungeni, lakini kwa bahati mbaya inaingia kwenye kumbukumbu na huko mbeleni watoto wa Marehemu watasoma. Sijui watajisikiaje kusoma pengezi kwa mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kuzuia maujai lakini akaangalia upande wa pili?

Tanzania tusilee kizazi chenye hasira!
 
Back
Top Bottom