bornagain
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 3,383
- 1,354
Akiwa anachangia hotuba ya wizara ya mambo ya ndani leo,mheshimiwa huyu waziri wan chi na uratibu wa Bunge ndugu Lukuvi amemsifia sana Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa RPC Kamhanda eti kwa kazi nzuri anayoifanya kwa wanaIringa,anasema kuwa eti ukiona kitabu kizima cha kambi ya wapinzani kila page imejaa neno Kamhanda basi ujue kuwa eti ni mwanaume wa shoka na anasema kuwa angetamani sana hata yeye angekuwa anaona live jinsi anavotajwa.Sasa cha kujiuliza ina maana waziri huyu Lukuvi anashabikia mauaji ya Mwangosi na yale ya Songea ambayo yote yalifanyika wakati Kamhanda akiwa RPC? Na pia amesema kuwa jimbo la Ismani lina wenyewe na wenyewe ni yeye Lukuvi yaani kana kwamba watu wa Ismani hawahemi na wala hawawezi kuwa na pumzi kama Lukuvi asipokuwa mbunge wa Isamani.Kazi kwenu wana Iringa sasa na waTanzania kwa ujumla