Ridhiwani Kikwete amezitaka Taasisi za TPSC na Uongozi kuandaa programu za mafunzo zitakazoboresha utendaji kazi kwa Watumishi na Viongozi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,890
939
TPSC NA TAASISI YA UONGOZI ZATAKIWA KUANDAA PROGRAMU ZA MAFUNZO ZITAKAZOBORESHA UTENDAJI KAZI WA WATUMISHI WA UMMA NA VIONGOZI.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amekitaka Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) na Taasisi ya UONGOZI kuandaa programu za mafunzo zitakazowajengea uwezo kiutendaji watumishi wa umma na viongozi ili watoe huduma bora kwa wananchi na mchango katika maendeleo ya taifa.

Mhe. Kikwete ametoa maelekezo hayo jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Chuo cha Utumishi wa Umma na Taasisi ya UONGOZI iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hizo.

Mhe. Kikwete amesema, watumishi wa umma na viongozi walio katika taasisi zote za umma wanahitaji kupata mafunzo yenye tija kwa ajili ya kukuza taaluma zao na kuongeza ufanisi kiutendaji, hivyo ni jukumu la Chuo cha Utumishi wa Umma na Taasisi ya UONGOZI kuhakikisha watumishi na viongozi wanapata mafunzo yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Mhe. Kikwete amesisitiza kuwa, Chuo cha Utumishi wa Umma kinatoa mafunzo kwa watumishi ambao wameshaajiriwa na Serikali, hivyo wanahitaji kuandaliwa programu nzuri za mafunzo zitakazoimarisha utendaji kazi wao.

Sanjari na hilo, Mhe. Kikwete amekipongeza Chuo cha Utumishi wa Umma kwa kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma wanaokaribia kustaafu ili kuwaandaa wawe na maisha mazuri baada ya kustaafu kuutumikia umma.

“Binafsi naamini Chuo cha Utumishi wa Umma mnafanya jambo zuri kuwapatia mafunzo watumishi wanaokaribia kustaafu kwa mujibu wa sheria, hivyo mkijipanga vizuri nina uhakika hawataharibikiwa pindi wakistaafu,” Mhe. Kikwete amesisitiza.

Akizungumza na Menejimenti ya Taasisi ya UONGOZI, Mhe. Kikwete ameusisitiza uongozi wa taasisi hiyo kubuni programu za mafunzo ambazo zitawaandaa viongozi wa baadae, kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekusudia.

Mhe. Kikwete ameongeza kuwa, Rais wa Awamu ya Sita, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatamani kuona Taasisi ya UONGOZI inatoa mchango wa kuwaandaa viongozi watakaoendeleza kazi nzuri iliyofanywa na uongozi wake


WhatsApp Image 2023-03-28 at 11.36.38(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-28 at 11.36.38(2).jpeg
 
Back
Top Bottom