.BAADA YA KUCHAFUA HALI YA HEWA NDANI YA MAGOGONI NA KUJIWEKA MSEMAJI NA MSAFISHA MAKOSA SASA Luhanjo kungoka na miaka 50 uhuru .JE HII INATOSHA KUTOCHUNGUZWA KWA KULIDHARAU BUNGE??? | .. Send to a friend |
Wednesday, 12 October 2011 21:00 |
0digg BAADA ya kuongezewa mkataba kwa vipindi takriban viwili, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo sasa anatarajiwa kustaafu wadhifa wake huo, ifikapo mwishoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.Taarifa za kukaribia kustaafu kwa Luhanjo zimekuja wakati Mkuu huyo wa Utumishi wa Umma, akichunguzwa na Kamati Teule ya Bunge kufuati tuhuma kwamba aliingilia Haki na Mamlala ya Bunge. Uchunguzi huo unafuatia hatua yake ya kumrejesha kazini Katibu Mkuu wa Nishati na Madini (alisyesimamishwa), David Jairo anayetuhumiwa kuandika waraka wa kuomba fedha kutoka katika mashirika yaliyo chini ya wizara yake kwa lengo la kusaidia mchakato wa kupitisha bungeni bajeti ya wizara yake, kinyume cha sheria. Kamati hiyo inachunguza iwapo hatua ya Luhanjo kutoa uamuzi wa mwisho kwa jambo ambalo lilianzia bungeni bila kuwasiliana na Waziri Mkuu ambaye ni kiongozi wa shughuli za Serika bungeni, inaingilia uhuru, haki na madaraka ya bunge. Kadhalika, Luhanjo katika Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi, alituhumiwa na wabunge kwamba ni chanzo cha uozo na ufisadi katika Wizara ya Maliasili na Utalii, tuhuma ambazo hata hivyo, alizikanusha kwamba zilikuwa na lengo la kuchafua rekodi yake ya utumishi mwema serikalini. Katibu Mkuu Kiongozi aliyeingia Ikulu siku chache baada ya kuapishwa kwa mara ya kwanza Rais Jakaya Kikwete Desemba 2005, alipaswa kustaafu tangu mwishoni mwa mwaka jana, lakini aliongezewa mkataba mwingine. Sasa imetangazwa rasmi kwamba anastaafu rasmi Desemba 9, mwaka huu, siku ambayo pia ni kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, kauli iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia. |
chiwaso hebu sema vizuri....una maana gani...?
Ni kawaida yao.......
.BAADA YA KUCHAFUA HALI YA HEWA NDANI YA MAGOGONI NA KUJIWEKA MSEMAJI NA MSAFISHA MAKOSA SASA
Luhanjo kung'oka na miaka 50 uhuru
.JE HII INATOSHA KUTOCHUNGUZWA KWA KULIDHARAU BUNGE???
.. Send to a friend
Wednesday, 12 October 2011 21:00
0digg
Boniface Meena
BAADA ya kuongezewa mkataba kwa vipindi takriban viwili, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo sasa anatarajiwa kustaafu wadhifa wake huo, ifikapo mwishoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.Taarifa za kukaribia kustaafu kwa Luhanjo zimekuja wakati Mkuu huyo wa Utumishi wa Umma, akichunguzwa na Kamati Teule ya Bunge kufuati tuhuma kwamba aliingilia Haki na Mamlala ya Bunge.
Uchunguzi huo unafuatia hatua yake ya kumrejesha kazini Katibu Mkuu wa Nishati na Madini (alisyesimamishwa), David Jairo anayetuhumiwa kuandika waraka wa kuomba fedha kutoka katika mashirika yaliyo chini ya wizara yake kwa lengo la kusaidia mchakato wa kupitisha bungeni bajeti ya wizara yake, kinyume cha sheria.
Kamati hiyo inachunguza iwapo hatua ya Luhanjo kutoa "uamuzi wa mwisho" kwa jambo ambalo lilianzia bungeni bila kuwasiliana na Waziri Mkuu ambaye ni kiongozi wa shughuli za Serika bungeni, inaingilia uhuru, haki na madaraka ya bunge.
Kadhalika, Luhanjo katika Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi, alituhumiwa na wabunge kwamba ni chanzo cha uozo na ufisadi katika Wizara ya Maliasili na Utalii, tuhuma ambazo hata hivyo, alizikanusha kwamba zilikuwa na lengo la kuchafua rekodi yake ya utumishi mwema serikalini.
Katibu Mkuu Kiongozi aliyeingia Ikulu siku chache baada ya kuapishwa kwa mara ya kwanza Rais Jakaya Kikwete Desemba 2005, alipaswa kustaafu tangu mwishoni mwa mwaka jana, lakini aliongezewa mkataba mwingine.
Sasa imetangazwa rasmi kwamba anastaafu rasmi Desemba 9, mwaka huu, siku ambayo pia ni kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, kauli iliyotolewa na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia.