Luhanjo kuchapa lapa baada ya kuvurunda na kupata chake mapemaaaaa...

Chiwaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
5,604
3,560
Sijui hali itakuwaje, na sijui hali ikoje kule jumba jeupe, pale mheshimiwa na mtuhumiwa wa bunge anapoamuliwa achomoke. Hope kwa jinsi ilivyo siamini kama ni maamuzi yake binafsi. Wakuu mnasemaje?
 
KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,380
8,135
Pale jumba jeupe ni wewe unaona mtazamo tofauti yule hawezi kwenda kokote!!
 
MAGEUZI KWELI

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,947
253
.BAADA YA KUCHAFUA HALI YA HEWA NDANI YA MAGOGONI NA KUJIWEKA MSEMAJI NA MSAFISHA MAKOSA SASA

Luhanjo kung’oka na miaka 50 uhuru

.JE HII INATOSHA KUTOCHUNGUZWA KWA KULIDHARAU BUNGE???
.. Send to a friend
Wednesday, 12 October 2011 21:00
0digg
Boniface Meena
BAADA ya kuongezewa mkataba kwa vipindi takriban viwili, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo sasa anatarajiwa kustaafu wadhifa wake huo, ifikapo mwishoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.Taarifa za kukaribia kustaafu kwa Luhanjo zimekuja wakati Mkuu huyo wa Utumishi wa Umma, akichunguzwa na Kamati Teule ya Bunge kufuati tuhuma kwamba aliingilia Haki na Mamlala ya Bunge.

Uchunguzi huo unafuatia hatua yake ya kumrejesha kazini Katibu Mkuu wa Nishati na Madini (alisyesimamishwa), David Jairo anayetuhumiwa kuandika waraka wa kuomba fedha kutoka katika mashirika yaliyo chini ya wizara yake kwa lengo la kusaidia mchakato wa kupitisha bungeni bajeti ya wizara yake, kinyume cha sheria.

Kamati hiyo inachunguza iwapo hatua ya Luhanjo kutoa “uamuzi wa mwisho” kwa jambo ambalo lilianzia bungeni bila kuwasiliana na Waziri Mkuu ambaye ni kiongozi wa shughuli za Serika bungeni, inaingilia uhuru, haki na madaraka ya bunge.

Kadhalika, Luhanjo katika Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi, alituhumiwa na wabunge kwamba ni chanzo cha uozo na ufisadi katika Wizara ya Maliasili na Utalii, tuhuma ambazo hata hivyo, alizikanusha kwamba zilikuwa na lengo la kuchafua rekodi yake ya utumishi mwema serikalini.

Katibu Mkuu Kiongozi aliyeingia Ikulu siku chache baada ya kuapishwa kwa mara ya kwanza Rais Jakaya Kikwete Desemba 2005, alipaswa kustaafu tangu mwishoni mwa mwaka jana, lakini aliongezewa mkataba mwingine.

Sasa imetangazwa rasmi kwamba anastaafu rasmi Desemba 9, mwaka huu, siku ambayo pia ni kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, kauli iliyotolewa na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia.
 
ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,721
6,465
Wanataka kumsevisha na kashifa? Kama atakutwa na hatia, apelekwe mahakamani akamalizie mda wake wa kuishi na babu seya aliyeonewa
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
24,668
18,870
.BAADA YA KUCHAFUA HALI YA HEWA NDANI YA MAGOGONI NA KUJIWEKA MSEMAJI NA MSAFISHA MAKOSA SASA

Luhanjo kung'oka na miaka 50 uhuru

.JE HII INATOSHA KUTOCHUNGUZWA KWA KULIDHARAU BUNGE???
.. Send to a friend

Wednesday, 12 October 2011 21:00

0digg

Boniface Meena
BAADA ya kuongezewa mkataba kwa vipindi takriban viwili, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo sasa anatarajiwa kustaafu wadhifa wake huo, ifikapo mwishoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.Taarifa za kukaribia kustaafu kwa Luhanjo zimekuja wakati Mkuu huyo wa Utumishi wa Umma, akichunguzwa na Kamati Teule ya Bunge kufuati tuhuma kwamba aliingilia Haki na Mamlala ya Bunge.

Uchunguzi huo unafuatia hatua yake ya kumrejesha kazini Katibu Mkuu wa Nishati na Madini (alisyesimamishwa), David Jairo anayetuhumiwa kuandika waraka wa kuomba fedha kutoka katika mashirika yaliyo chini ya wizara yake kwa lengo la kusaidia mchakato wa kupitisha bungeni bajeti ya wizara yake, kinyume cha sheria.

Kamati hiyo inachunguza iwapo hatua ya Luhanjo kutoa "uamuzi wa mwisho" kwa jambo ambalo lilianzia bungeni bila kuwasiliana na Waziri Mkuu ambaye ni kiongozi wa shughuli za Serika bungeni, inaingilia uhuru, haki na madaraka ya bunge.

Kadhalika, Luhanjo katika Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi, alituhumiwa na wabunge kwamba ni chanzo cha uozo na ufisadi katika Wizara ya Maliasili na Utalii, tuhuma ambazo hata hivyo, alizikanusha kwamba zilikuwa na lengo la kuchafua rekodi yake ya utumishi mwema serikalini.

Katibu Mkuu Kiongozi aliyeingia Ikulu siku chache baada ya kuapishwa kwa mara ya kwanza Rais Jakaya Kikwete Desemba 2005, alipaswa kustaafu tangu mwishoni mwa mwaka jana, lakini aliongezewa mkataba mwingine.

Sasa imetangazwa rasmi kwamba anastaafu rasmi Desemba 9, mwaka huu, siku ambayo pia ni kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, kauli iliyotolewa na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia.
Ni kawaida yao.......
 
AlamaZA NYAKATI

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
274
28
Kwa nini anaondoka wakati kamati ya bunde bado haijatoa ripot ya uchunguzi kuhusu yeye na jairo. S wamuongezee tena muda kama walivyofanya huko nyuma. Au sheria inasemaje atakapokutwa na hati hata kama atakuwa amestaafu. tunaamini atapatikana na makosa sheria imfuate hukohuko atakapokuwa ili ajibu tuhuma
 
BornTown

JF-Expert Member
May 7, 2008
1,716
478
ukiona hivyo ujue katimuliwa tayari ila kulindana wanasema anastaafu kwani mwanzoni walikuwa hawajui kuwa anatakiwa kustaafu?? sheria ifuate mkondo wake ikate kotekote sio tu kwa sie walalahoi hata hao mafisadi iwakate ******* zao!
 
Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,536
5,642
Bora aondoke, kipindi alichoichafua ofisi yetu kinatosha.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom