WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Naendeleleza mada:
Fikiria nini kilitokea miaka ya mwisho ya sabini ( 1978-79) pale baba wa Taifa alipoamua kutumia lugha hii hii ya kiswahili na kusema..
SABABU YA KUMPIGA TUNAYO.....
NIA TUNAYO
UWEZO TUNAO......
NADHANI WANANCHI WALIOSIKILIZA HOTUBA YA MWALIMU PALE OFISI ZA CCM KIRUMBA MWANZA WATAKUJA WATUAMBIE NINI KILITOKEA BAADA YA HAPO!
IDDI AMIN DADA ALIPATA KIPONDO KUTOKA KWA WATANZANIA... WOTE BILA KUJALI MTU NI MWANAJESHI AU LA!
Simulizi zinasema kuwa hadi wanafunzi waliokuwa wamemaliza kidato cha sita na kwenda JKT waliingia vitani na kupigana kwa nia na ujasiri kabisa hadi kumtoa nduli ndani ya mipaka...
Iweje siku hizi imeshindikana kutumia maneno mazito yenye kugusa hisia za watu kupambana na maovu?
Hata mada hii hakuna anayechangia kwa maana tumeridhika kabisa na yale yanayotamkwa kutupumbuza!
UWEZO WA KUMPIGA TUNAO!!!
Tuko pamoja Mkuu!kwanza dada nataka ujue kuwa lugha ni "sauti za nasibu" hivyo hakuna mtu anaweza kukaa chini na akaja na "maneno mbadala" bali maneno ya lugha huzuka yenyewe na watumiaji hujikuta tu wameshamirisha kutumia maneno yenyewe kuwasilisha maana anuai zilizokusudiwa (na hapa sizungumzii suala zima la usanifu wa lugha)
kuna maneno yalizuka siku za karibuni na kutoa mchango mkubwa japao watu wa siku hizi tu tofauti kidoko katika kudodosa. mfan maneno "ARI MPYA, NGUVU MPYA KASI MPYA" hya yalitoka katika hotuba ya kikwete akitangaza nia yake ya kuchukua fomu kukiomba chama chake kimteue kugombea urais. toka hapo yamesikika mra nyingi na wote tunajua alifanikiwa kuteuliwa na kushinda uchaguzi, hivyo ni maneno yaliyofanikiwa lengo lake. hata wanaohoki leo utelelezaji wa ahadi zake huyarejea tene na tene manaeno yale ili kueleweka zaidi kama si kutanabaisha.
kwa maoni yangu, tusichukie maneno bali tuhoji mantiki na matumizi yake huku tukitambua kuwa watumiaji wake hawana uchaguzi bali kutumia kama hayo ndiyo yako kwenye maumizi kwa wakati huo (misimu)
lol!hehehe!just for my records:
the following user says thank you to geoff for this useful post: womanofsubstance (today)
lol!
What is the meaning of this ?
SipoNafikiri mada yako iko sahihi lakini ndio muundo wa lugha na ukitaka kuondoa haya hakika utapoteza ladha na chachu ya lugha yeyote ile. Kumbuka sio Kiswahili tu kina stahili hizi ila ni lugha zote. Wazo langu ni kuwa kinachohitajika ni nidhamu ya kila mtu kutokana a kile anachiotakiwa kukisema na kukitenda lakini sio kuiondolea lugha utamu na uhalisia wake