WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Je umewahi kujiuliza ni kwa jinsi gani kiswahili chetu kitamu cha Tanzania kinavyochangia kudumaza au kurudisha nyuma maendeleo au harakati za kuondoa uovu katika jamii?
Hebu angalia mifano michache:
1. Watu hawa watafikishwa mbele ya vyombo husika na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ( Je ni vyombo gani? nani atakusika kwa minajili ya uwajibikaji? lini hatua hizo zitachukuliwa?)- kauli kama hii inajenga matumaini makubwa lakini ndani hamna kitu!
2. Jambo hili linafanyiwa kazi ( kazi gani?,nani anafanyia kazi? atafanya kazi hiyo katika timeframe gani? lini watu watarajie matokeo?)- kauli hii inanyamzisha maswali zaidi
3. Kwa sababu zisizozuilika nimechelewa kidogo (tutajuaje kweli hazikuwa zinazuilika? mtu anaweza kulala baada ya kukesha kwenye starehe akachelewa kufika sehemu husika na kutoa statement kama hii na ikawa mwisho wa mazungumzo) - kauli hii inamaanisha usiniulize wala usitake kujua zaidi...
Unaweza kuongeza mifano mingine mingi tu....
Swali:
1.Tukiendekeza misemo kama hii, hatuoni tunazidi kuwa wadanganyika maana semi kama hizi zinafunga mazungumzo, haziruhusu mijadala wala uwajibikaji/uwajibishaji?
2. Wale wataalamu wa lugha, hamuwezi kuja na lugha mbadala yenye ku leta mabadiliko na kuchagiza uwajibikaji zaidi?