Nafasi ya Wananchi wenye taarifa kama Kichocheo cha Demokrasia Huru

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,908
12,187
Kwa kutambua umuhimu wa ushiriki wa vijana, hasa katika vyuo vikuu, kushiriki katika mazungumzo na mijadala yenye habari kuhusu masuala na matarajio yao ya sasa, JamiiForums imeandaa mazungumzo yanayohusisha wanafunzi wa kozi mbalimbali wa chuo cha St. Augustine University of Tanzania (SAUT).

Mazungumzo hayo yanajadili Nafasi ya “Wananchi wenye Taarifa kama Kichocheo cha Demokrasia Iliyo Hai”

Mazungumzo haya yanalenga kuunda majukwaa ambayo wataalamu hawa chipukizi wanaweza kushiriki katika mazungumzo yenye tija, kukuza imani na maelewano kati yao. Tunaamini kwamba utawala wenye tija hauwezi kutimizwa bila ushiriki wenye ufanisi wa vijana.

Shukuru Buyemba, Mhadhiri - SAUT
Kukosa taarifa ni sawa na kupofusha fikra ndio maana ni muhimu sana kuwa na taarifa sahihi. Kama Raia, unakuwa na uwezo wa kuhoji unapokuwa na taarifa sahihi...

Msomi mmoja akasema "what is not known cannot be ruined", kwamba chochote usichokijua, Waswahili tunasema ni sawa na usiku wa giza. Unakuwa na uwezo wa kuhoji pale unapofahamu kitu... kwahiyo ni muhimu sana kwa watu kuwa na taarifa.

Inabidi waanze watu ije taasisi. Democracy, governmet of the people. The more informed the citizenry are the more democracy is likely to be in place kwa sababu watahoji, wata-demand, watauliza na watashiriki.

Mtu ambaye yupo informed anajiandaa, inamsaidia kuweka vipaumbele…anahoji ni wapi kuna shida n na ni wapi tumepiga hatua. Ikiwa huna taarifa kuhusu jambo fulani inakuwa ni changamoto kufanya maamuzi sahihi kuhusu jambo hilo.

…Kwahiyo taarifa zinasaidia watu kuchukua hatua. Mtu mmoja akasema “you cannot hope for progress in areas where you have taken no action”. Hivyo, kuwa na taarifa ni jambo moja lakini kuzifanyia kazi ni jambo lingine.

Lakini pia taarifa zitasaidia watu kujiepusha na siasa chafu... ukiwa na taarifa utafanya siasa za kistaarabu kwakuwa kuna Maisha baada ya kampeni.

Tukiwa na sheria sheria nzuri zitakazowezesha tukawa na viongozi wa kisiasa ambao watachukulia ukosoaji kama sehemu ya Maisha, kwamba kama binadamu tunapaswa kukubaliana kutokukubaliana, kukubaliana kukubaliana, kutokukubali kukubaliana – hapo tutapata hiyo demokrasia tunayoitaka.

Dkt. Kaanaeli Kaale, Mhadhiri - SAUT
Raia wanategemea vyombo vya habari kama daraja kati ya wananchi na serikali. Serikali au wanasiasa wakitaka kufikisha ujumbe wao kwa serikali lazima watumie vyombo vya habari.

Waandishi wa habari wana majukumu mane. Kwanza wana editorial role – kwamba wakipata hizo habari lazima wazichuje na waweze kuzisambaza kwa wananchi ili wabnanchi waweze kupata taarifa sahihi. Hiyo ndiyo kazi yao ya kila siku.

Nyingine ni facilitative role. Waandishi wa habari ni lazima wa-facilitate, ni lazima waendeshe mijadala, ni lazima wachambue kwa kina zile taarifa ambazo wamezipata halafu wazisambaze kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Wajibu mwingine ni collaborative role. Mwandishi wa habari lazima ashiriki kuwezesha wananchi kupata zile taarifa. Ni lazima atoe elimu – elimu ya uraia, elimu ya mpiga kura n.k

Wajibu mwingine katika kuchochea haya masuala ya kidemokrasia, mwandishi wa habari ana critical role.
Serikali isipokuwa na utashi wa kiksiasa, waandishi wa habari watashindwa kufikisha taarifa kwa watu ama serikali wenyewe watazificha. Na hii ina maana kwamba raia hawatakuwa na taarifa sahihi ama hawatakuwa na taarifa kabisa.

Ukishakuwa na taarifa kamili sasa mwandishi wa habari ndiyo anaweza kutumia zile roles ambazo nimezitaja hapo juu.

Madhara makubwa ya wananchi kutokuwa na taarifa ni kufifisha demokrasia. Watu watakaa kimya na kuacha wachache waendelee kutumia rasilimali za taifa kwa maslahi yao wenyewe.

Adv. Moses Matiko, Mhadhiri – SAUT
Mimi nishachaguliwa; nilishapita kwenye hiyo michakato ya kidemokrasia. Haki ya kupata taarifa niliigeuza kuwa mtaji kwa wananchi na baada ya hapo wakanichagua kuwa kiongozi wao kwa maana ya Diwani na baadaye nikawa Mstahiki Meya 2015 – 2020.

Ninachokifahamu katika uhalisia, wote tunafahamu kuwa information is power. Kama huna information sijui kama una uwezo wa kufanya chochote kinachohusu maamuzi.

Hiki tunachokizungumza asilimia kubwa ya Watanzania hawakifahamu. Hiyo haki ya kwenda kwa Mkuu wa Mkoa au wa Wilaya kufuatilia, kwa mfano, barabara hii mbona mkandarasi amefanya mobilization ya material na amefanya kazi kidogo lakini vifaa vyake vimeondoka na hakuna taarifa yoyote kwa M/Kiti wa Mtaa au Diwani au, mathalani, na mbunge au wale watendaji.

Katiba inatupatia haki ya kupata taarifa na kuzisambaza; maana yake unaweza ukapata halafu na wewe uitoe regardless of boundaries. Ukipata taarifa maana yake usiwe mchoyo, inatakiwa uwaite watu uwaeleze.

Mfano mimi kwenye sakata la DP World niliona hapa mjini wajuaji ni wengi nikaenda kijijini nikaita kabisa mkutano wa Kijiji nika mwambia M/kiti wa Kijiji kuwa nina moja, mbili, tatu – niitie mkutano wa Kijiji niwaoneshe hii kitu imekaaje halafu muwe na uamuzi hata kama hakutakuwa na polling station ya kufanya maamuzi basi mtakuwa mnajua vizuri kwa uhakika ili vyombo vya habari visichanganye watu.

Nimetolea mfano sakata la DP World kwakuwa kila mtu alikuwa na mtazamo wake na huo mtazamo haukatazwi kurushwa na vyombo vya habari. Kwahiyo unaweza kumuona Mwijaku ameenda kuhojiwa akatoa mtazamo wake, halafu ukamwona Madeleka naye ametoa mtazamo wake. Utamwona Wakili Mwabukusi naye ametoa mtazamo wake kwahiyo wananchi wanakuwa confused na hawajui waende na lipi.

Unaweza kumwona Jerry Silaa ndani ya Bunge amesema huu si mkataba, lakini anahojiwa na chombo cha habari akiwa nje ya Bunge anasema huu ni mkataba. Kwahiyo wananchi wanashindwa kuelewa kuwa huu ni mkataba au si mkataba.

Wale mnaosoma sheria, kuna mkataba wowote ambao hauna timeframe? Hauwezi ukawa na mkataba ambao hauna timeframe. Lakini sasa umemsikiliza huyu na yule na umekuwa confused. Sasa ni lipi jukumu lako wewe unayejua kwa jamii yako?

Wewe unayejua kuwa a contract must have a duration unachukua hatua gani?
JamiiForums, kwa mfano, tunaona unafungua akaunti si lazima kwa jina lako, basi unaweza ukatumia nafasi hiyo kuelimisha basi wasomaji. U-deal na kipengele kimoja tu cha kuwa a contract must have a timeframe; uelimishe pale ili wale watakaosoma waka-disseminate hizo information kwa wengine na kwa wengine.

Tuache kabisa mambo ya uchawa. Uchawa sasa hivi ni kama tunu ya taifa na ndiyo vitu ambavyo vinatuangusha sana. Taaluma zinaharibika kwakuwa unajua kabisa kuwa suala fulani si sawa lakini kwa kuwa unategemea labda Kesho unaweza ukateuliwa…

Kuna mambo inabidi uwe mkweli, ili hata mteuzi ajue huyu kijana ni mkweli na anafundisha watu ukweli.

Wewe mwenye ufahamu unaponyamaza kule kijijini wasio na ufahamu wanasinzia kabisa.

Katika vyama vya siasa vilivyopo, kwa mfano, hivi unawezaje kumchagua mtu wa ACT kama hujui hata anavyoongea, hujawahi kusikia kazi wanazozifanya, hujawahi kusikia ilani yao?

Capture 2.PNG

Shukuru Buyemba (kushoto) akichangia mada. Pembeni yake ni wahadhiri wa SAUT ambao wameshiriki katika mazungumzo hayo. Katikati ni Dkt. Kaanaeli Kaale na wa mwisho kulia ni Adv. Moses Matiko.

Capture 1.PNG

Mmoja wa wanafunzi walioshiriki akichangia mada.

Capture 3.PNG

Washiriki wakisikiliza mawasilisho kwa umakini


Capture 4.PNG

Wanafunzi wakifuatilia michango ya wanajopo

Capture 5.PNG

Mmoja wa wanafunzi akitoa mchango wake
 
Naomba kushauri juu ya hili,, jamii za kiafrica nyingi zinamaitaji ambayo yote yanabaki kua ndoto,, ushiliki wa serikali na mashirika mengine hupo kwenye kulinda sheria na kuadhibu,, sasa kwa kwakatii huu tuliopo tungejenga mifumo ya kuibua hisia za umoja na maendeleo,, serikali ikishilikiana na vyombo vya habari vinalinda na kutangaza usalam ila akuna utohaji haki wa moja kwa moja
 
Akutawai kuepo na democracia huru bia Uhuru wa kiakili kujitambua na kujisimamia,, kwati tuliopo ni wakujijenga kifikra na kujiuliza maswali ya kimaendeleo
 
Vijana wenyewe hawana muda wa kutafuta taarifa. Ukimuuliza mtu kwanini unasapoti chama X hana sababu zaidi ya kusema "hiki chama ndiyo baba lao" 😂😂😂

Na unakuta huyo mtu anamiliki kadi ya hicho chama kwa miaka kadhaa lakini hata ilani yake haifahamu wala hajawahi kuisoma. Mtu wa namna hii anapelekwa pelekwa tu. Anakuwa mbishi asiye na taarifa.
 
Back
Top Bottom