Ludovick Joseph akamatwa na Polisi...

Ludovick Joseph akamatwa na Polisi...

551313_345095595527704_1063897382_n.jpg

mr JL
 
Huyu mtu nimemfahamu kupitia jukwaa la wanabidii na nimeongea naye kwa simu mara kadhaa!Msimamo wake kisiasa kule wanabidii alijonesha kama chadema, sasa haya ya video na hili la kukamatwa linanitatiza!Ila kama ni kafara Mungua amrehemu kama ni mnafiki apelekwe kunakostahili!
 
Yote haya yataongelewa ,
lakini iko siku taifa zima litajua na ndio utakuwa mwisho wa haya mambo ya afande mshuti!
 
Siasa zetu na nchi yetu inazidi kuchukua sura mpya kila uchao.
 
Mungu mkubwa! Habari za uhakika nilizozipata dakika kadhaa zilizopita zinasema mtuhumiwa mkuu wa utekaji na utesaji wa Kibanda, Joseph Ludovick, amekamatwa punde tu mjini Iringa.

Na wewe Manyerere Jackton mbona unaruka ruka haueleweki? Mtuhumiwa namba moja kwa mujibu wa nani? wako au? si ueleze unachojua au kama ni kwa mujibu wa polisi si ueleze hapa...Natilia mashaka mnaendeleza sinema yenu ya kihindi na kijamaa kitasema Nilitumwa na Lwakatare..nalazimika kukuona unaweza kuwa wakala na muumini wa hii sinema ya kihindi!!
 
Mimi nina wasi wasi na source yenyewe ya hizi habari yaani huyu Manyerere kwani jamaa kwa bahasha hajambo hivyo inawezekana amechukua mshiko kuja kutuchanganya kama alivyofanya 2005 akiwa na mtandao!! Akaishia kupewa trip ya Cuba ndio ikawa kwishney!!
 
kwa mtazamo wangu hata Manyerer Jackton anapaswa kukamatwa ili kuisaidia polisi, maana inaonekana kuna mambo mengi nyuma ya pazia anayajua.
 
Ili niweze kuamini kuwa yeye ndio mhusika na siyo kapandikizwa lazima awe na affiliation na jamii inayojiita "afande" maana hilo ndo lililotamkwa na muathirika. Tofauti na hapo inaweza ikawa ni movie nyingine kama ya Joshua Mulundi.
 
kwenye clip ya video ya lwakatare:

15:59 ...sauti inasika ikisema ‘’ unamuweka kwenye dilemma hajui adui ni nani yaani anakuja hapa anakukuta wewe ‘’LUDOVICK’’ ndiye unamfatilia’’...huyu Ludovick ni nani?( some dots needs to be collected and connected here ) yawezekana ni mmoja wa vijana waliokuwa wanajirekodi na hili ni jina lake halisi na wametajana pasi kujua au ni code name?..

17:10 kijana anayepewa maelekezo (‘’Ludovick) anauliza ‘’ kwa hiyo kama kila kitu kitaenda well inakwenda mpaka lini?’’ lakini katika kujibu clip inayomuonyesha lwakatarea akijibu swali hilo akisema ‘’ Bahati mbaya umekuja na majibu yasiyojitosheleza’’ ....katika majibu haya kuna mkanganyiko mkubwa maana hakuna uhusiano wa swali lililoulizwa na jibu lililotolewa....tangu dakika ya 15 ya clip hii maelezo ya sauti zinazosikika hayana mpangilio wa manaa... mengi yalilenga kufuatisha ishara na vitendo vya lwakatare alivyokuwa akiongea na ukitizama kwa makini hakuna uhusiano kati ya maneno yenyewe na mdomo wa lwakatare.............

katika kuishepu iwe mbaya, naona ukataji na uungaji ukasababisha mkanganyiko
 
Back
Top Bottom