Ludovic Uttoh: Kama Kodi ni kwa maendeleo ya Nchi kwanini Wabunge hawakatwi wakati nao wanalipwa Mshahara kama wengine?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
CAG Mstaafu, Ludovic Uttoh amesema hakuna sababu za kwanini Wabunge wa #Tanzania hawalipi Kodi licha ya kwamba wana Mishahara kama walivyo Watumishi wengine wanaokatwa Kodi.

Uttoh amesema "Siku zote msingi wa Kodi ni Usawa na wala kodi haitakiwi kuwa na Matabaka. Ikiwa tunasema tunalipa Kodi kwa maendeleo ya Nchi ni kwanini Wabunge hawakatwi?"

Akieleza zaidi, amesema hafahamu kama kuna Nchi nyingine Duniani ambayo Wabunge wake hawalipi kodi. Kwanza logic ya kufanya hivyo haipo".
 
Wabunge wanalipa kodi kutoka kwenye mshahara wao ambao ni mil 4 na ushee,ila hawalipi kodi kwenye maposho yao wanayopata ambapo ndiyo wanapata pesa nyingi huko,karibu mil 7 na ushee,sababu wanayotoa ni kuwa eti kazi yao ni ya mkataba wa miaka 5.
 
CAG Mstaafu, Ludovic Uttoh amesema hakuna sababu za kwanini Wabunge wa #Tanzania hawalipi Kodi licha ya kwamba wana Mishahara kama walivyo Watumishi wengine wanaokatwa Kodi

... hii kitu inawatia doa sana sema mshipa wa aibu hawana! Ngoja niwape trick rahisi sana namna ya kuondokana na aibu hii; wa-double mshahara yao halafu wakatwe kodi; kwanza watakuwa kipato kizuri kuliko ilivyo sasa na pili kashfa ya kukwepa kodi itakuwa imeondoka automatically.
 
Wabunge wanalipa kodi kutoka kwenye mshahara wao ambao ni mil 4 na ushee,ila hawalipi kodi kwenye maposho yao wanayopata ambapo ndiyo wanapata pesa nyingi huko,karibu mil 7 na ushee,sababu wanayotoa ni kuwa eti kazi yao ni ya mkataba wa miaka 5.
... wabunge sio wa kwanza kuwa na kazi za mikataba nchini na duniani! Nchi nyingine uwakilishi ni miaka minne minne na kodi wanalipa. Nchini hapa kuna wenye kazi za mikataba ya mwaka kodi wanalipa sembuse miaka mitano na mishahara, posho, mamikopo, viinua mgongo vya kufuru!
 
Wabunge wanalipa kodi kutoka kwenye mshahara wao ambao ni mil 4 na ushee,ila hawalipi kodi kwenye maposho yao wanayopata ambapo ndiyo wanapata pesa nyingi huko,karibu mil 7 na ushee,sababu wanayotoa ni kuwa eti kazi yao ni ya mkataba wa miaka 5.
Kwa maana hiyo na wafanyakazi wenye mikataba ya muda maalum kama miaka mitano na kushuka nao wasilipe kodi? Na marupurupu wanayopewa kwa nini hayajumlishwi kwenye mapato yao kama ilivyo kwa watumishi wengine na kisha kukatwa kodi?
 
Wabunge wa Tanzania ni waporaji wa pesa za nchi. Hili la wao kulipa kodi lipigiwe mbiu ya mkoa ama La mgambo. Wakilipa kodi kila wakilipwa wataacha kulala Bungeni.
 
Nasikia Wawekezaji huwa hawalipi kodi kwa 5 years,
Labda wametumia tafsiri hiyo,
Vinginevyo wanafanya kazi kubwa sana(kutunga sheria si mchezo)
Hakuna ubaya tukiwasamehe kidogo
 
CAG Mstaafu, Ludovic Uttoh amesema hakuna sababu za kwanini Wabunge wa #Tanzania hawalipi Kodi licha ya kwamba wana Mishahara kama walivyo Watumishi wengine wanaokatwa Kodi
Huyu si ndo alikuwa CAG.

Anyways. Tufanye alisahau kuhoji mda ule.
 
Back
Top Bottom