KWELI Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hukatwa PAYE kama wafanyakazi wengine

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Nimekuwa nikisikia kuwa wabunge wetu hawalipi kodi kwenye mshahara mnono wanaopata. Kuwa walimu wanalipwa Tsh 400,000 lakini kamshahara hako kanaliwa na PAYE.

bungeni.JPG

Wabunge wetu wakiwa kwenye vikao, sitting allowance na Perdiem wanakunja 470,000 kwa siku, Mshahara wa mwisho wa mwezi nao mnono hatari. Je, hakuna sababu ya wabunge kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi?

Tena napendekeza hata yale marupurupu wanayopata nayo yakatwe kodi.
 
Tunachokijua
Julai 23, 2021, Mbunge Mbunge wa Ukonga (CCM) Jerry Silaa, katika mkutano wa hadhara uliowashirikisha wananchi wa Mzinga, Ukonga jijini Dar es Salaam alisema imefikia hatua Wabunge waanze kulipa kodi kupitia mishahara yao ili wapate uwezo wa kuwaambia Wananchi na wao walipe kodi.

“Ni wakati muafaka sisi Waheshimiwa Wabunge ili tupate uwezo wa kuwaambia Watu waanze kulipa kodi na sisi tuanze kulipa kodi katika mishahara yetu, hakuna sababu ya kuwa wengine wanalipa wengine hawalipi ukishakuwa haulipi unakosa ile nguvu ya kumwambia mwenzako alipe” alisema Silaa.

Kauli hii iliibua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii huku maoni ya watu wengi yakihoji sababu inayowapa upekee wabunge kutokukatwa PAYE kwenye mishahara yao kama walivyo wafanyakazi wengine.

PAYE ni nini hasa?
PAYE ni kifupi cha ‘Pay As You Earn’ (Lipa kadiri unavyopata) inahusu kodi ambayo hutozwa moja kwa moja kwenye mishahara ya wafanyakazi na TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) kulingana na mapato yao. Yaani, kiasi cha kodi kinachotolewa moja kwa moja kutoka kwenye mshahara kabla ya mfanyakazi kupokea fedha zao.

Kikokotoo kinachotumika kupiga hesabu ya kiasi cha pesa kinachopaswa kukatwa kutoka kwenye malipo ya mashahara hupatikana kwenye tovuti rasmi ya TRA.

Wabunge wanakatwa PAYE?
Sintofahamu kuhusu suala hili zimekuwepo kwa muda mrefu, lakini mjadala uliongezeka ukubwa baada ya mbunge Silaa kutoa kauli iliyotaka wabunge waanze kukatwa kodi hiyo.

Agosti 3, 2021, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitoa taarifa inayokanusha madai haya na kuutaka umma kuyapuuza.

img_20210803_162352-jpg.1878724

Barua ya Bunge ikikanusha madai hayo ( Chanzo: Bunge)

Pia, Agosti 7, 2021, Mamlaka ya Mapato Tanzania ilitolea ufafanuzi suala hili kwa kusema kuwa wabunge, kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine, walikuwa wanakatwa kodi ya PAYE.

"Wabunge wanalipa kodi, wanapolipwa mishahara wanakatwa kodi inayotokana na ajira inayotambulika kama Pay As You Earn (PAYE) kama ambavyo kwa watumishi wote wengine wanavyokatwa" alisema Richard Kayombo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi TRA

Ushahidi mwingine wa suala hili ulitolewa Septemba 1, 2021 na Kiongozi wa Chama cha ACT na Mbunge wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zitto Kabwe akisema Wabunge wanalipa Kodi ya Mapato (PAYE) kutoka kwenye mishahara yao ya kila Mwezi. Kama ilivyo kwa Watumishi wote wa Umma, Wabunge hawalipi Kodi kwenye posho zao zote wanazopata kitu ambacho sio sahihi kwani posho ni Pato linalopaswa kukatwa Kodi ya zuio kwa mujibu wa Sheria.

JamiiCheck imejiridhisha kuwa tofauti na jinsi ilivyodaiwa, wabunge hukatwa PAYE kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine.
Kumbe walikua hawakatwi? Sema wajanja wanaweza tafuta njia ya kuingiza ka posho juu kwa juu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom