Lowassa watajie CHADEMA mali unazomiliki

Lowassa watajie CHADEMA mali unazomiliki

Mimi ninawasikitikia wabunge wa CHADEMA ambao ni wazalendo kwa sababu kila wakigusa wanajikuta wanampiga ''madongo'' Lowassa kwa sababu hawamjui.

Ni wabunge gani wa CCM wanaomuunga mkono magufuli kwa sababu "wanamjua?" Unaweza
Usinipe cheo ambacho sina.

Kama mimi ni kiongozi wao, kwa hiyo wewe ni kiongozi wa nani katika social media?

Nimekuambia acha kujenga hoja kwa kutumia hisia.
Kwanini Magufuli hajatangazia CCM na wananchi kwa ujumla mali anazomiliki?
 
Mimi huwa sielewi watu kila Mara kumsema Lowassa wakasahau kuwa ufisadi ni kila kona ya CCM.

Lowassa sidhani kama aliuza nyumba za serikali, aliyeuza yupo lakini haguswi

Baada ya Lowassa kujiengua toka serikalini tumeona EPA, Escrow, mikataba mibovu ya Gas na madini, Lugumi na mengine mengi. Ni kwa nini yote haya yanafumbiwa macho na badala yake anatajwa lLowassa? CCM mnataka kutuaminisha nini Watanzania? Mwenye macho haambiwi tazama!

Wabunge pamoja na mawaziri ndo wanaomiliki shule za binafsi, biashara kubwa na makàmpuni ambayo ndo uzao wa ufisadi katika nchi hii, lakini hao hao ndo viongozi wa nchi, tutegemee nini? Kama tunategemea mabadiliko nadhani ni ndoto ya alinacha.

Kwa namna nchi inavyokwenda, kama tunataka kuona madiliko ya kweli sio Leo wala kesho, labda miaka hamsini ijayo, lakini kwa sasa tusjidanganye
 
Mangula alifanya nini? Alishiriki kutungua matokeo ya kura hewani na watalaam wenu kutoka nje pale nyuma ya mayfair plaza, mlimani city estate, na pia alikuwa na wale vijana wa Bulembo pale double tree? Nielimishe tafadhali.


Kipi muhimu kwa taifa hivi sasa kati ya umma kujua mali za lowassa na mali za rais aliyepo madarakani? Kwanini yaliyowasilishwa na JPM tume ya maadili hayawekwi hadharani na badala yake mmeyaficha kwenye mkoba?

Kama mnazijua mali haramu za lowassa kwanini msemaji wenu Mkuu Ole Sendeka asizitangaze hadharani au vyombo vyenu vya dola visisimamie sheria? Hivi na akili zenu mnaona kwamba Jamiiforums ni mbadala wa Ole Sendeka na vyombo vyenu vya dola kumshughulikia lowassa juu ya mali zake haramu?

Sheria ni sheria tu, iwe ni Lowassa au nani.

Vinginevyo Kiongozi wenu wa social media MsemajiUkweli kwa kweli needs a new strategy. Kuelekea 2020, mnachofanya humu hakiwezi kupunguza kibaba cha kura mlichokitoboa 2015 na kubakiza milioni sita kwa ajili ya lowassa.
Watu wanaishi kwa kuhisi kuliko kutumia akiri lowassa aliwakosea nini acheni mzee apumuzike
 
HIVI KAMA LUKUVI AKISAINI HATI ZA VIWANJA NA MASHAMBA YATAKUWA YA LUKUVI? NAONA MWANADIWANI ANATOKWA POVU KISA LOWASSA ALISAINI HATI YA SHAMBA NA HILO SHAMBA UMILIKI UMEBADILISHWA? MSITULETEE UKENGE HAPA MWACHENI LOWASSA AFANYE YAKE
 
MsemajiUkweli katika suala la kutaja mali ninapata wakati mgumu kukuelewa

Kuna kamisheni ya maadili ya viongozi inayowalazimu wataje mali zao wanapoingia na kutoka.

Tuambie nani anajua mali za viongozi waliotangulia wakati wanaingia au wanatoka?
Mkuu Nguruvi3
Wanaojua mali za viongozi ni viongozi wenyewe na pia taasisi iliyokabidhiwa jukumu la kujua mali za viongozi.
Na kuna umuhimu gani wa watu katika vyama kutaja mali zao, ikiwa wale wanaosimamiwa na kamisheni hatujui wanamiliki nini chini ya sheria?
Umuhimu upo ndiyo maana kwa sasa wabunge wa CHADEMA wanajikuta wanamshambulia Lowassa bila kufahamu kwa sababu hawafahamu mali zake.
Pili, kama nyumba inabomolewa kwa kukiuka sheria sina tatizo na hilo.
Kama inafanyika kwa nia njema sina tatizo na hilo.

Nina tatizo iwapo hilo linafanyika katika kulipa visasi vya kisiasa
Huo utakuwa mwanzo mzuri mbele ya safari na hata sasa
Hata mimi sifahamu kama linafanywa kwa kulipa kisasi lakini ninachokiona ni kuwa nyumba zinabomolewa kwa sababu sheria imevunjwa.

Kufahamu ni kisasi au siyo kisasi ni vigumu sana kama kinachofanyika kiko kisheria.
Tungependa kujua zile meli zenye meno ya tembo kesi ziliiashaje?
Tungependa kujua mkataba wa Lugumi ulikuwaje, ulitekelezwaje na akina nani?
Tungependa kujua hivi nyumba za umma ziliuzwajwe kwa kina nani na kwanini?
Orodha ni ndefu inaendelea
Haya maswali siwezi kuyajibu kwa sababu sihusiki na masuala unayoyauliza.
Tukianza kubomoa nyumba ya milioni 80 au 100 au 150 kwa mfano tu, tutakuwa tunachukua hatua nzuri. Twende mbele ili tujue Bilioni 37 zilitokaje?
Hizi ni nyingi sana zinaweza kujenga bomba kubwa zaidi kuliko nyumba moja

Tusibomoe nyumba, tukifumbia macho Lugumi!

Sheria ni msumemo inakata mbele na nyuma. Ikianza kwenye nyumba hizo isiishie hapo iendelee kutupa majibu ya maswali yanayosumbua akili zetu
Suala la Lugumi kuna Kamati Ndogo ya Bunge inafanya kazi nani matumaini yangu mwisho wa mwezi huu itakuja na majibu ya maswali yako.
 
Napata mashaka kuwa huu waweza kuwa mchezo wa kisiasa unaochezwa kisayansi na Waziri ameingia king.
Shamba kubwa kama hilo sio rahisi Mbunge na wananchi jirani wasifahamu kuwa linamilikiwa na Lowassa. Pengine Lowasa kesha ridhia lirudi serikalini ili wapewe watu, lakini waziri kutamka kuwa wanalirudisha kutokana na kauli ya Mbunge tuu basi sasa mashamba mengi ya viongozi itabidi yarudishwe kama la Lowasa pale Mbunge yeyote atakapo mention wapi kuna shamba halijaendelezwa.
Baada ya hapo ni wangapi walio madarakani wataumia?
 
Swali la kujiuliza ni je, kama kuna dhamira ya kweli, kwanini Wabunge wa CCM wamepinga wazo la muswada wa kutenganisha biashara na siasa? Hapa ndio utajua jinsi gani ccm ni wanafiki. Kwani kwa biashara ya real estate kati ya Lukuvi na wafanyabiashara WAKUBWA WAKUBWA, na pia biashara za viongozi wengine wengi tu ngazi 'zooooote', wataathirika.

Mimi sipingi suala la viongozi kutangaza mali zao, nachopinga ni mchezo mchafu wa kisiasa wa CCM unaotumika kutenga walio wenzetu na wasio wenzetu. Basi. Njooni na objective approach, tutawaunga mkono.

cc MsemajiUkweli
Unaposema wabunge wa CCM pekee wanapinga unakuwa unapotosha ukweli kwa sababu hata wabunge wa vyama vya upinzani pia wanapinga. Jaribu kuwa mkweli.

Suala la mswaada wa kutenganisha biashara na siasa ni sawa na suala la posho za wabunge.

Suala la posho za wabunge, unakuta wabunge wengi wa CCM na CHADEMA wanakubaliana.

Suala la kutenganisha biashara na siasa inasemekana kuna wabunge wa upinzani na CCM hawaliafiki.
 
Hapa ishu sio ukongwe JF, kituko ni Mbunge wa Chadema alieteuliwa na Chadema na kupitishwa na Chadema kwa ushawishi wa Lowasa kwenda bungeni kulalamikia shamba lilliporwa na Lowasa.

Sidhani kama angejua lile shamba ni miliki ya Lowasa angethubutu hata kufungua mdomo bungeni kuhoji umiliki wa hilo shamba.!
Nani kataja UKONGWE hapo?

Halafu hata kama shamba ni la Lowasa kwanini Mbunge anayepaswa kuwasemea wananchi akae kimya?

Hayo maswala ya patronage yapo CCM...

Nilichofanya ni kusema background ya ID husika...

I refuse to a cheap sycophant...
 
Kwa wananchi hapa makao mapya watu wamepanga foleni dukani "Makofia" imeisha na wengine hawajapata.Kuna nini waelezeni wananchi ukweli.
Kwani wao hawana mdomo mpaka unakuwa msemaji wao?

Waambie sukari ya kutengeneza siyo salama kiafya. Waende wakatumie asali.
 
Mkuu MsemajiUkweli umewaita wenyewe awa sasa wamekuja na maji, sabuni na madodoki kwa ajili ya kazi ya kumsafisha bwana mkubwa hahahahah ama kweli Mungu hamfichi mnafiki.
Kinachonishangaza ukitamka jina la Lowassa kwenye thread, wanajeshi wake wanaibuka kutoka mafichoni na kuanza kurusha risasi bila kuangalia hata sababu za jina lake kutamkwa.

Wengi hawatumii nguvu za hoja bali wanatumia jaziba na hoja za nguvu.
 
Hii ID zamani ilikuwa inatumiwa na kiongozi mkuu wa chama chenye mbunge mmoja bungeni kudhoofisha chadema...

Sasa naona inatumiwa kimkakati either na mtu huyohuyo au imeuzwa CCM...

Inasemekana huyo kiongozi ni mole... aka snitch..

So mada kama hizi zitakuja sana na kushereheshwa na vilaza wa Lumumba waloingia JF mapema mwaka jana kwa mission maalumu...
Watu wasioweza kujenga hoja zenye nguvu za hoja hukimbilia kuangalia mleta hoja ili watumie character assassination kwenye hoja za nguvu.

Kutaka kuifahamu ID ya mleta mada ni moja ya haiba ya watu walioshiwa nguvu za hoja.

Kunifahahamu mimi hakuwezi kubadilisha ukweli wa hoja ninazozileta.

Jikite kwenye hoja na kama unadhani hakuna hoja, basi hata kusoma na kuondoka pia ni moja ya mchango kwenye mada!
 
Magu muongo sana:

Nitatoa salary slip yangu,wakuu nani ameiona?

Tutagawa sukari bure:jamani kuna mtu kapata walau nusu kilo?

Mmeshahoji?Au mzimu wenu lowassa unawakojoza usiku kucha!
Kumbe!
Nilikuwa sifahamu kama ni muongo!
 
Kutoka kwa vijana wa UVCCM hii ni thread ya 9 hii inayomuhusu Lowasa punde baada ya Lowasa kutangaza atazunguka kufanya mikutano.

CCM will always dance the song played by Lowasa.
 
Uongozi bora ni msingi wa kujenga jamii yenye maadili mema, kuthamini utamaduni, uadilifu, kuheshimu utawala wa sheria na kutokuwepo na rushwa na maovu mengine.

Uwazi wa viongozi kuhusu mali zao na mienendo yao ya kiuongozi ni takwa la chini kabisa katika uongozi wenye kuzingatia misingi ya maadili, nidhamu na uwajibikaji kwa umma.

Kwa msingi huu ndiyo maana vyama vya siasa kama ACT-Wazalendo kinamtaka kikatiba kila kiongozi wake kutaja mali zake.

Umuhimu wa dhana ya uwazi umedhihirika ndani ya CHADEMA baada ya kujikuta baadhi ya wabunge wa CHADEMA wakimshambulia Lowassa bila kufahamu kutokana na kutofahamu vizuri mali zake.

Mbunge Mnyika alianza kulalamika na kulaani wale ambao wamezuia Mradi wa Maji kuwafikia wana Dar es Salaam kwa sababu wamejenga nyumba juu ya njia ya mabomba ya maji na kusababisha mradi wa maji kusimama. Bahati mbaya Mnyika hakufahamu kuwa aliyejenga hiyo nyumba ni Kaka yake na Edward Lowassa ambaye alipewa kiwanja na Edward Lowassa kinyume cha sheria wakati akiwa Waziri wa Ardhi na Makazi mwaka 1993–1995.

Mbunge mwingine aliyelalamika ni Mbunge wa CHADEMA wa Jimbo la Monduli, Julius Karanga wakati akichangia majadiliano ya makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, bungeni.

Karanga aliitaka serikali iwagawie wananchi shamba la Makuyuni lenye ekali zaidi ya 380,000 ililopo wilayani Monduli kwa sababu serikali imelitelekeza. Karanga alidhani mwenye shamba kwa sasa ni serikali bila kufahamu kuwa baada ya serikali kulitaifisha kutoka kwa Mfanyabiashara Stein ili ligawiwe kwa wananchi, Edward Lowassa alijimilikisha hilo shamba.

Mbunge huyu pamoja na wabunge wangine wa CHADEMA walipigwa butwaa baada ya kuambiwa hilo shamba alijimilikisha Edward Lowassa lakini Waziri Lukuvi, akasema kuwa serikali imesikia kilio cha mbunge Karanga kwa sasa iko mbioni kuligawa kwa wananchi.

‘’Kama Mheshimiwa Mbunge, Karanga alikuwa hajui kwamba shamba hilo la makuyuni alijimilikisha Lowassa, basi imekula kwake, shamba linachukuliwa na serikali na kuligawa kwa wananchi. Najua kazi ni ngumu kwako, lakini naomba tushirikiane shamba hili liende kwa wananchi. "Ninayo hati hapa ya shamba hilo imesainiwa na Lowassa, nasema tutairekebisha ili shamba hilo ligawiwe kwa wananchi." alisema Lukuvi huku wabunge wengine wakicheka.

Lowassa anatakiwa awasaidie wana CHADEMA kwa kuwaeleza mali zake ili wasijikute wanampiga ‘’madongo’’ ya kisiasa wakidhani wanaipiga serikali bila kufahamu kutokana na ukosefu wa uwazi kutoka kwa Lowassa.

Hii inadhirihisha kuwa wanaCHADEMA wengi hawamjui Edward Lowassa pamoja na kuimba nyimbo zinazosema Mabadiliko Lowassa, Lowassa Mabadiliko.

Niliwahi kusema, katika mambo yote ambayo Lowassa amelitendea haki taifa ni kuhama CCM.

VIDEO ikionyesha nyumba ya Kaka yake Edward Lowassa ikibomolewa kwa nguvu na serikali kupisha ujenzi wa bomba la maji.


tin4.jpg

Iliyokuwa nyumba ya Kaka yake na Edward Lowassa ikibomolewa kupisha ujenzi wa bomba la Maji kwa wakazi wa Dar es Salaam

Lowassa kamwe hawezi kutaja mali zake hata Mbowe na Lissu wanalijua hilo
 
Back
Top Bottom