Lowassa: Tuzo ya amani imewaumbua CCM

Lowassa: Tuzo ya amani imewaumbua CCM

Kuna watu wanahangaikia kutafuta amani Burundi, Somalia, Afrika ya kati na Nigeria hawapewi tuzo......mnampa tuzo mtu ambaye yupo kwenye taifa ambalo halijui nini maana ya kupigana......

Kilicho yafikisha hayo mataifa kupigana ni nini???
 
Kuna watu wanahangaikia kutafuta amani Burundi, Somalia, Afrika ya kati na Nigeria hawapewi tuzo......mnampa tuzo mtu ambaye yupo kwenye taifa ambalo halijui nini maana ya kupigana......

Dah unaakili sana mkuu
 
Huyu jamaa hajaacha tu sarakasi zake?
 
Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na kuungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa amesema anashangaa kuona anaambiwa mleta vurugu wakati dunia inamkubali kuwa ni mlinzi wa amani.Kauli ya Lowassa imekuja ikiwa ni siku moja baada ya taasisi za kidini 1,200 duniani kupitisha jina lake kwa ajili ya kumpatia Tuzo ya Amani.?Nimepokea kwa unyenyekevu na furaha tuzo ya amani duniani ninayotarajiwa kupewa na taasisi za kidini 1200 duniani,? alisema Lowassa akinukuliwa na msemaji wake, Aboubakar Liongo.Lowassa alisema tuzo hiyo ni kithibitisho cha uongo wa CCM na Serikali yake kuwa wapinzani ni watu wa vurugu.Taasisi hizo katika kikao chake huko Bukavu DR Congo, zilitangaza kumpa tuzo hiyo Edward Lowassa kutokana na utulivu aliyouonyesha kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu Kwa jamii, Mchungaji William Mwamalanga ilisema kiasi wajumbe 1,400 wa mkutano huo kutoka kote duniani walikubaliana kumpa tuzo hiyo Lowassa kati ya wanasiasa 1,000 waliyoshindanishwa ili kumpata kiongozi bora wa Amani mwaka 2015, ambaye anajali na kuangalia maslahi ya jamii badala ya madaraka.Alisema yeye ni muungwana na ana hofu ya Mungu na hata siku moja hatoweka mbele maslahi binafsi, na ndiyo maana aliwatuliza wananchi waliyokuwa wakimtaka kutoa tamko baada ya matokeo kutangazwa.?Siko tayari kuingia Ikulu huku mikono yangu ikibubujika damu. Nashukuru taasisi hizo za kidini duniani, zimeliona hilo,? alisisitiza Lowassa. Chanzo: Mwananchi
wanaompa mh Lowasa hyo tuzo wana akili nyingi sana..,nimewaelewa.
 
Oh naomba unitajie Dini za kubadilisha katiba Burundi ,ni dini mpya au ?? Na Somalia pia ni udini ??

Hivi wewe hujui kama mauaji ya kimbari Burundi na Rwanda yalisababishwa na ukabila? Na chembe chembe zake zimeendelea hadi Leo.....watawala wanataka kukaa milele kwa kisingizio cha kuzuia ukabila ( Rwanda)....

Boko haram nijeria

Alshabab Somalia

Waislam na wakristo CAR....

Usijitoe ufahamu
 
Watu wanacheza na saikolojia yake tu,wanajua hajatulia toka mambo yamuharibikie
 
1. TUNAOMBA SANA UTUWEKEE ORODHA YA HIZO TAASISI ZA DINI ZILIZOTOA HIYO TUZO. BILA ORODHA YAKE INAONEKANA ULE USANII UNAENDELEA.

2. VIPI WALE WALIOKUFA NA MKASEMA WANAKUFA KWA SABABU WALIMTUKANA MHE.LOWASA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE NDIO MAANA MUNGU KAWAUA. JE HIYO DAMU HAIHESABIKI????

3. WATUMISHI WA MUNGU WENGI WAMEPOTEZA MVUTO KWA WAUMINI KUTOKANA NA MATAMKO YENYE KUPINDUKAPINDUKA. HEBU SOMENI NENO LA MUNGU TENA MTUAMBIE NI WAPI MANABII WA KWELI WA MUNGU ALIYEHAI WALIKUWA NA KAULI ZENYE MAGUMASHI?? Nabii Eliya alisema mvua hainyeshe ila kwa neno langu na haikunyesha nk

4. HAWA WATUMISHI WALISEMA LOWASA ATAKUWA RAIS MAAANA WANA HAKIKA NA MUNGU ALICHOSEMA NAO. TENA KUNA MMOJA ALISEMA LOWASA ASIPOKUWA RAIS WAMUUE???? Hivi wameshamuongoza sala ya toba????

5. HEBU HUBIRINI INJILI JAMANI YESU KARIBU ANARUDI. DUNIA IMEJAA DHAMBI NA MAOVU. HEBU TAFAKARINI TENA UPOSO WENU???

6. HALAFU HAWA NDIO WALE WANAOTOA PHD FEKI. NATAMANI SERIKALI ITOE TAMKO LA KUFUTA HIZI PHD ZA TAASISI ZA DINI. ZINAONDOA KABISA MAANA. YAANI WACHUNGAJI MITUME NA MANABII WANAKIMBIZANA NA HIZI PHD. SASA HIVI HUO UGONJWA UMEKUJA MPAKA KWA WAUMINI.

7. HEBU ACHENI KUIRAHISISHA IMANI NA NENO LA MUNGU KWA MATUMBO YENU. Shame on you.

Queen Esther

Pole sana dada hii tuzo imekujazibisha sana.
 
Hivi wewe hujui kama mauaji ya kimbari Burundi na Rwanda yalisababishwa na ukabila? Na chembe chembe zake zimeendelea hadi Leo.....watawala wanataka kukaa milele kwa kisingizio cha kuzuia ukabila ( Rwanda)....

Boko haram nijeria

Alshabab Somalia

Waislam na wakristo CAR....

Usijitoe ufahamu

Mauaji ya Kimbari yalitokea Burundi ?? Kinachotokea sasa hivi Burundi source yake ilikua udini na ukabila ?? Unataka kuniaminisha nini wewe
Ni wapi nilipotaja Rwanda mimi ??? Ubongo kazi yake sio ku stimulate testestorone peke yake una kazi nyingine utumie huenda ukakusaidia
 
Hebu jamani tujiulize hizo taasisi zimeanza lini kuto tuzo kama hizi? Nani anayeongoza hizo taasisi katika utoaji wa hizo tuzo. Je hao wanaoshindanishwa ni wagombea tu wa upinzani au wanasiasa wote? Nani kabla ya Lowassa akiwahikupata tuzo hii? Amani hiyoinayosemwa aliyoinesha Lowassa ni ya muda gani? Tangu alipokuwa CCM au baada ya kuondoka CCM? Kama baada ya kuondoka CCM tujiulize kwani Lowassa ana muda gani toka atoke CCM mpaka hii leo? Hao alioshindanishwa nao ni akina nani? Wakristo watupu au mchanganyiko wa dini mbalimbali? Hayo majina ya walioshondanishwa yalichaguliwaje? Yalipendekezwa? Kama yalipendekezwa ni akina nani walipendekeza. Kama hayakupendekezwa mchakato wake na vigezo vya kuyapata vilikuwaje? Tukipata majibu ya maswali haya ndipo tunaweza tukaiongelea hiyo tuzo. Ingekuwa ni yenye kufahamika na kueleweka kama ile ya Nobel aaaah mbona isingekuwa shida, lakini kwa jinsi usanii ulivyo sasa waweza kuta hiyo tuzo inaitwa 'Monduli Northern Tanzania Peace Prize'
Hapo kwenye red ni swali la muhimu sana, kuna amani gani iliyoonyesha dalili ya kutoweka ambayo lowassa aliilinda ndani ya hiyo miezi miwili?
Na kama toka akiwa sisiemu, kulikuwa na dalili za machafuko yoyote enzi hizo?
Je hao alioshindanishwa nao 'wamepigania' amani ktk maeneo yao kwa muda gani?
 
Mauaji ya Kimbari yalitokea Burundi ?? Kinachotokea sasa hivi Burundi source yake ilikua udini na ukabila ?? Unataka kuniaminisha nini wewe
Ni wapi nilipotaja Rwanda mimi ??? Ubongo kazi yake sio ku stimulate testestorone peke yake una kazi nyingine utumie huenda ukakusaidia

Soma andiko langu la mwanzo uliloninukuu........sikuitaja Burundi peke yake?....ndo maana mnaitwa nyumbu au malofa

Mauwaji wa wahutu na watutsi yalikua Rwanda....lakini hata Burundi kuna ukabila wa kutisha hali inayowapelekea kubaguana......hivyo kusigina katiba.......

All in all hoja yangu mimi ilikua kuna watu wanapigania amani ya nchi hizi ndio wanastahili pongezi....na sio huyu lowasa wenu kupewa tuzo isiyo na kichwa wala miguu.....tuzo ambayo hatujui ni nani aliyewahi kupewa kabla na ilianzishwa mwaka gani.....
 
Ulitaja Burundi na Somalia ,nikakuuliza chanzo cha wao kupigana ukaniambia udini na ukabila ,nikakuuliza mauaji yanayotokea Burundi au Somalia source yake ni udini na ukabila ?? Ukaishia kuileta Rwanda na kusema mauaji ya Kimbari yalitokea Burundi kwenye hoja

Umeshindwa kuelewa kinacho sababisha Lowasa apewe tuzo ni kutokutumia influence aliyokua nayo vibaya kwa kutaka madaraka
Mimi na wewe nani Nyumbu ?
Yaani mshenzi mmoja kubadilisha katiba ili aendelee kuwa madarakani amefanya hivyo kwa sababu ya ukabila ??
 
Ulitaja Burundi na Somalia ,nikakuuliza chanzo cha wao kupigana ukaniambia udini na ukabila ,nikakuuliza mauaji yanayotokea Burundi au Somalia source yake ni udini na ukabila ?? Ukaishia kuileta Rwanda na kusema mauaji ya Kimbari yalitokea Burundi kwenye hoja

Umeshindwa kuelewa kinacho sababisha Lowasa apewe tuzo ni kutokutumia influence aliyokua nayo vibaya kwa kutaka madaraka
Mimi na wewe nani Nyumbu ?

Sikuitaja Burundi na somalia peke yake nyumbu wewe.....Nigeria na CAR mbona unaziacha? Na kwa ujumla matatizo yao yanasababishwa na either udini au ukabila

Hivi ni lini amani imetoweka hapa Tanzania....hiyo influence aliyokua nayo ni ipi hadi asababishe amani itoweke?

Naomba unitajie orodha na address ya taasisi hizo na zilianza kutoa tuzo hii mwaka gani.....na washindi kabla ya Lowasa ni akina nani?.

Kama huna majibu piga kimya lofa wewe
 
Asante uwe na siku Njema Mwerevu
 
Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na kuungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa amesema anashangaa kuona anaambiwa mleta vurugu wakati dunia inamkubali kuwa ni mlinzi wa amani.

Kauli ya Lowassa imekuja ikiwa ni siku moja baada ya taasisi za kidini 1,200 duniani kupitisha jina lake kwa ajili ya kumpatia Tuzo ya Amani.

?Nimepokea kwa unyenyekevu na furaha tuzo ya amani duniani ninayotarajiwa kupewa na taasisi za kidini 1200 duniani,? alisema Lowassa akinukuliwa na msemaji wake, Aboubakar Liongo.

Lowassa alisema tuzo hiyo ni kithibitisho cha uongo wa CCM na Serikali yake kuwa wapinzani ni watu wa vurugu.

Taasisi hizo katika kikao chake huko Bukavu DR Congo, zilitangaza kumpa tuzo hiyo Edward Lowassa kutokana na utulivu aliyouonyesha kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu Kwa jamii, Mchungaji William Mwamalanga ilisema kiasi wajumbe 1,400 wa mkutano huo kutoka kote duniani walikubaliana kumpa tuzo hiyo Lowassa kati ya wanasiasa 1,000 waliyoshindanishwa ili kumpata kiongozi bora wa Amani mwaka 2015, ambaye anajali na kuangalia maslahi ya jamii badala ya madaraka.

Alisema yeye ni muungwana na ana hofu ya Mungu na hata siku moja hatoweka mbele maslahi binafsi, na ndiyo maana aliwatuliza wananchi waliyokuwa wakimtaka kutoa tamko baada ya matokeo kutangazwa.

?Siko tayari kuingia Ikulu huku mikono yangu ikibubujika damu. Nashukuru taasisi hizo za kidini duniani, zimeliona hilo,? alisisitiza Lowassa.

Chanzo:
Mwananchi

....inatia shaka! kwamba taasisi zaidi ya alfu moja kidini, huko bukavu zimeamua kumtunuku tuzo ya amani bwana lowassa ...! inatia shaka, nia ya "hizo taasisi zaidi ya elfu oja", ukitilia ukarimu na uwezo wa bwana lowassa kuhamasisha harambee...lkn pia ni tuzo akishindanishwa na nani? ktk eneo gani? kama ni afrika, GoodluckJonathan wa Nigeria ambae sio tu alikubali kushindwa, na mpinzani wake wa dini ingine, lakini alimpigia na simu kumpongeza kwa ushindi, alishirikishwa? kisha ? hii tuzo si ni afadhali hata "madigirii ya udaktari wa falsafa" ambayo kiongozi wetu mmoja amekuwa akipatiwa kwa heshima! au? kujiliwaza na kujisifu katika up...zi?
 
Back
Top Bottom