Lowassa: Tuzo ya amani imewaumbua CCM

Lowassa: Tuzo ya amani imewaumbua CCM

Kuna watu wanahangaikia kutafuta amani Burundi, Somalia, Afrika ya kati na Nigeria hawapewi tuzo......mnampa tuzo mtu ambaye yupo kwenye taifa ambalo halijui nini maana ya kupigana......
 
Jamaani Mwacheni Mhe Lowassa ajijengeye imani, he cannot believe watanzania hawakumchagua despite spending 130 Billion Shillings ( $60M). This action is to morali boost himself.

nawahakikishia hata tokea hapa JF, hata mmoja wa wapenzi wake atakayeweza kutuletea Majina/Adress/Tovuti za hizo taasisi zilizo mtunza hiyo heshima.

Isije hili tunzo likawa kama haya majanga ya Shahada feki yanayo tumika TZ.
 
hao watoa tozo nadhanj wamepigwa na upofu. -wangejua jamaa jinsi alivyompeperusha Dr Slaa na Prof Lipumba kutoka ukawa nadhanj wangegairi.
- wangejua jinsi alivyoagiza mamluki kutoka nje ya nchi kuja kudukua kura kwenye database ya tume ya uchaguzi wangegairi
-wangejua mpango aliokuwa ameuandaa wa kutawala nchi akizungukwa na mafisadi wafanyabiashara wangengairi
-wangejua alivyotaka kuchaguliwa kuwa candidate wa ukawa na akakataa asishindanishwe na mtu yoyote wangegairi
-wangejua kuwa alinunua viongozi baadhi wa ukawa ili wamuunge mkono wangegairi
-wangejua Bashir Awale, mkuu wa Stanbic bank aliyekwapua 6 bilion na kampuni ya Kitilya ndie alikuwa mshauri wake wa karibu na mkenya wangegairi.
kuna mengimengi mengi ambayo tumekuja kugundua, yaani Mungu ni mkubwa. mpaka leo hatujui jamaa huyu angeshinda urais nchi hii ingekuwaje.
 
Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na kuungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa amesema anashangaa kuona anaambiwa mleta vurugu wakati dunia inamkubali kuwa ni mlinzi wa amani.

Kauli ya Lowassa imekuja ikiwa ni siku moja baada ya taasisi za kidini 1,200 duniani kupitisha jina lake kwa ajili ya kumpatia Tuzo ya Amani.

?Nimepokea kwa unyenyekevu na furaha tuzo ya amani duniani ninayotarajiwa kupewa na taasisi za kidini 1200 duniani,? alisema Lowassa akinukuliwa na msemaji wake, Aboubakar Liongo.

Lowassa alisema tuzo hiyo ni kithibitisho cha uongo wa CCM na Serikali yake kuwa wapinzani ni watu wa vurugu.

Taasisi hizo katika kikao chake huko Bukavu DR Congo, zilitangaza kumpa tuzo hiyo Edward Lowassa kutokana na utulivu aliyouonyesha kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu Kwa jamii, Mchungaji William Mwamalanga ilisema kiasi wajumbe 1,400 wa mkutano huo kutoka kote duniani walikubaliana kumpa tuzo hiyo Lowassa kati ya wanasiasa 1,000 waliyoshindanishwa ili kumpata kiongozi bora wa Amani mwaka 2015, ambaye anajali na kuangalia maslahi ya jamii badala ya madaraka.

Alisema yeye ni muungwana na ana hofu ya Mungu
na hata siku moja hatoweka mbele maslahi binafsi, na ndiyo maana aliwatuliza wananchi waliyokuwa wakimtaka kutoa tamko baada ya matokeo kutangazwa.

?Siko tayari kuingia Ikulu huku mikono yangu ikibubujika damu. Nashukuru taasisi hizo za kidini duniani, zimeliona hilo,? alisisitiza Lowassa.



Chanzo:
Mwananchi
Acheni kujikomba kwa watu wasiotubu dhambi zao.
Huyo Mch Mwamalanga naye ataingia dhambi ya kumtukuza mwizi wa kiwanja cha Kanisa.
Lowassa aulizwe kile kiwanja cha KKKT Mbezi Beach mbona hajatubu?
 
Mafisadi wako CCM, Hakuna fisadi anayeweza kusavaivu nchi hii bila kivuli cha CCM.

Kabla ya fisadi Lowasa kupewa tuzo hii......hapo kabla ni nani aliyewahi kupewa tuzo hii? Au huwa inakosa watu kama ile ya Mo Ibrahimu?
 
Lowassa amekosa mvuto,hiyo tuzo ni magumashi na usanii mtupu,ili impandishe chati.asubiri tu 2020

Hivi vidini dini si ndo alikuwa 'anavinunua' kila wiki, leo vinajaribu kulipa fadhila baada ya kugonga ukuta kumpeleka ikulu!

Swali: hii tuzo ilianzishwa lini? Kabla ya hii nani iliichukua? Ni nani waasisi wa hii tuzo? Na tunaomba LINK tukaone wenyewe nomminees walikuwa kina nani!
 
Hebu jamani tujiulize hizo taasisi zimeanza lini kuto tuzo kama hizi? Nani anayeongoza hizo taasisi katika utoaji wa hizo tuzo. Je hao wanaoshindanishwa ni wagombea tu wa upinzani au wanasiasa wote? Nani kabla ya Lowassa akiwahikupata tuzo hii? Amani hiyoinayosemwa aliyoinesha Lowassa ni ya muda gani? Tangu alipokuwa CCM au baada ya kuondoka CCM? Kama baada ya kuondoka CCM tujiulize kwani Lowassa ana muda gani toka atoke CCM mpaka hii leo? Hao alioshindanishwa nao ni akina nani? Wakristo watupu au mchanganyiko wa dini mbalimbali? Hayo majina ya walioshondanishwa yalichaguliwaje? Yalipendekezwa? Kama yalipendekezwa ni akina nani walipendekeza. Kama hayakupendekezwa mchakato wake na vigezo vya kuyapata vilikuwaje? Tukipata majibu ya maswali haya ndipo tunaweza tukaiongelea hiyo tuzo. Ingekuwa ni yenye kufahamika na kueleweka kama ile ya Nobel aaaah mbona isingekuwa shida, lakini kwa jinsi usanii ulivyo sasa waweza kuta hiyo tuzo inaitwa 'Monduli Northern Tanzania Peace Prize'
 
Back
Top Bottom