Lowassa kukanusha au kutokanusha kuhusika ktk kashfa ya Richmond amechelewa. Hata kama kuna Wabunge watakaomsaidia kukanusha, wamachelewa. Majority ya umma wa Watanzania wanaamini alihusika na hawatamsamehe kwa kuchangia kwake ktk kututumbukiza zaidi ktk lindi la umaskini.
Huenda Lowassa akicharuka na kuungwa mkono na Wabunge walioko ktk mtandao wake, ataweza kuigawa CCM na kuwa tishio kwa J.K. mwaka wa 2010. Wana mtandao wake wamhimize wakati ukiwa muafaka.
Kuhusu Freeman Mbowe kuachia ngazi kama Mwenyekiti wa Chadema itakuwa ni jambo la kusikitisha kweli. Kama mwanaJF Gagnija alivyotamka hapo awali, Mbowe amedhihirisha ni kiongozi bora wa chama cha siasa, zaidi hata yeyote wa CCM, tangu Tanzania iingie ktk mfumo wa vyama vingi. Akiachia uenyekiti Chadema, uongozi wa CCM watasherehekea na nina hakika kuna wanaCCM wanaochochea Freeman aachie ngazi. Chadema chukueni tahadhari. CCM wajanja sana.
Chadema kimeonyesha kinaweza kubadilisha uongozi wa juu kitaifa bila kugawanyika. Bila shaka kinaweza kuteuwa Mgombea Urais kutoka miongoni mwa viongozi wake, bila kuwa na ulazima wa kumteuwa Mbowe.
Mwana JF Mwita Maranya amemtaja Dr. Kitila Mkumbo kama Mtanzania anayeweza kuwa Mwenyekiti wa Chadema. Mimi simjui, na nadhani siyo MwanaChadema mwenye wadhifa wa juu sana. Hata hivyo CHADEMA hakina shida ya kupata wanachama maarufu kitaifa au hata kimataifa. Watanzania wanaovalia suti za combati kutokana na kukereketwa kwao na uanachama wa Chadema wako wengi: waume kwa wanawake, jasiri , wazalendo, waadilifu na wasomi. Mmoja wao anaweza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti endapo Mbowe ataachia kiti. Mwingine, au huyo huyo, anaweza kuteuliwa na CHADEMA kuwa Mgombea urais.
Nilivyosema hapo mwanzo, Edward Lowassa, kutokana na kuhusika ktk kashfa ya Richmond na ushiriki wake na wahusika wengi wa kashfa nyingine kama za EPA na ufisadi kwa jumla, jina lake ni chafu. Licha ya kwamba Chadema wanaweza kumkaribisha kuwa mwanachama, kama Mtanzania yeyote anayesaini fomu ya kuomba uanachama, itakuwa ni foolhardy kumteua kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema. Wazo la Samwel John eti Lowassa ataleta ushindi kwa Chadema ni naivity in the extreme. Historia ya Lowassa haiwezi kushangiliwa na wanaChadema.