Mzee FMES.
Umeandika vizuri sana.Lakni swali langu ni dogo.. ina maana huo urafiki wote tulioambiwa huko nyuma kati ya President na huyu Edward ndio umekwisha kabisa? Najaribu kutazama nguvu aliyokua nayo president naiona lakini nachelea kusema je ataweza kuitumia ka Lowasa.Sitaki kuwa Thomaso lakini nina hakika haya mambo yana weza kuwa zaidi ya vile tunavyowaza na vigumu sana kuamini kuwa hawa mabwana hizi siasa zimewatenganisha kwa kiasi tunachofikiri.Anyway ngoja tuone
- Mkuu siyajui yote ninayoyajua madogo ni kwamba toka amuondoe kwenye u-PM, hajawahi tena kuongea naye kama zamani yaani one on one, wala kukutana wawili tu, baada ya kuweka mguu chini kwamba lazima awe waziri mkuu wake kule Chamwino, kuna mzito mmoja wa taifa alimuonya Muungwana na kumtaka aweke bet naye kwamba in two years ya uongozi wao hawatakuwa marafiki tena, na kwamba Lowassa atagombea naye urais mwisho wa first term yake, ndio maana sasa hivi muungwana habanduki kwa huyo mzito, aliyemtabiria.
- Wa-Tanzania tutakuwa tumelala sana usingizi kama hatuwezi ku-figure out kwamba ya kina Yona na Mramba, yalikuwa ni about nothing than popularity, sasa the question should be what else mkulu hawezi fanya, maana kumbuka yeye na rostam sasa hivi ni paka na panya, mara ya mwisho Rostam alijaribu kumfuata SA ili aongeee naye japo kidogo lakini akatolewa nje, Rostam kwenye kikao cha siri na mafisadi wenziwe alitaka kuacha ubunge, wakamwambia tena kwa sauti kali sana kwamba Muungwana atamtupa Segerea na kuchaguliwa tena urais kwa urahisi sana, ndio maana sasa jamaa anatafuta tena ubunge! Meaning kwamba kuna baadhi ya mafisadi wanamjua vizuri muungana na power!
- Halafu kuna membe factor, wanao-deal naye on a presonal level, wanasema siku hizi ana new attitude ya kitarajiwa tarajiwa hivi, maana ilikuwa very un-usual kwa yeye kupigiwa kampeni ya NEC na muungwana mwenyewe na sio wapambe wake kama desturi yake, na siku hizi yeye ndiye co-ordinator wa message za muungwana kwa viongozi wengine in private, sasa hili nalo ni tatizo kubwa sana kwa Lowassa kuliko hata Muungwana mwenyewe!
- Nafikiri unakumbuka yaliyowakuta Mwanahalisi, ambao the word ni kwamba walikuwa watu wa karibu sana na Mkulu, lakini walipogusa line ya popularity yake na power, wakagonga mwamba ninasema hivi ni kweli kwamba Lowassa is working hard na arround the clock, na kuna viongozi wengi sana wa juu ambao wako naye kwa siri na wanaamini kabisa kwamba atamu-outsmart muungwana, ni ndoto za mchana na halafu wanachoharibu kuliko yote ni pale wanapodai kwamba watatimiza revenge kwa viongozi waliomshambulia sana Lowassa, hapo ndipo wanapoharibu kuliko!
Naona nimesema mengi sana, haya ni maoni yangu tu na ni analysis yangu kwa kuunganisha dots.
Respect.
FMEs!