Lowassa to strike back ; Mbowe to quit chairmanship?

Are you real a Fair Player? Nakubaliana na wewe kuwa Lowasa ni mchapa kazi na wote tunajua hilo wala hakuna ubishi. Tusichompendea Lowasa ni Fisadi. Kama hujui Lowasa ameanza ufisadi siku nyingi sana tangu akiwa mkurugenzi mkuu wa AICC. Wakati huo alijenga nyumba nyingi sana pale Namanga na Arusha mjini kwa kufuja hela za AICC. Alipochaguliwa kuwa waziri mdogo ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa ndo alipotajirikia kabisa tena kipindi kile cha elnino. Alipopata uwaziri wa ardhi alikamata viwanja vingi sana kwenye prime areas such as masaki and upanga. Alipokuwa waziri mkuu aliwatimua walalahoi kwenye machimbo ya kunduchi kwa lengo la kuweka appartments na aliweza kuamuru nyumba ya mfanyabiashara mmoja ufukweni mwa bahari ya hindi ivunjwe nasikia kwa sababu ilizuia nyumba/biashara yake (hili sina hakika nalo). Nasikia kiwanja kilichozungushiwa mabati karibu na Denmark Embassy kinachotizamana na viwanja vya gymkhana ni chake. Je unataka mtu wa namna hii awe rais si matatuuza tukiwa vitandani? Fikiri mara saba sabini kabla ya kumsupport.

Very fair mzee. Wewe unataka rais mchapa kazi au asiyechapa kazi?.

Kama EL ni mchapa kazi basi tumpe KAZI.

Hiyo hadith ulizotunga ambazo huna uhakika nazo ziweke kapuni kwa sasa. sio kweli kuwa anamiliki vyote ulivyotaja.

Yule mhindi alijenga jengo refu kuliko inavyo ruhusiwa pale kaka. Msimpake matope hata hasipohusika.

Kuhusu Richmond..huna INSIDE story kwahiyo kaa kimya.
 
Uuwiiiii mwili unasisimka,nchi hii akipewa Lowassa itakuwa zaidi ya Abacha huko Nigeria,huyu bwana ni wa visasi hakuna mfano nafikiri wengine mnamsikia tu.Waulizeni walioonja anga zake.
 
Amebebeshwa au amejibebesha? Ni kweli kuwa Lowassa hakuitwa, lakini alipewa nafasi ya kuelezxa na akashindwa kufanya hivyo. Yet, aliamua kukaa kimya wakati wote huo hadi sasa, kwa nini?

Si hivyo tu, ndani ya Bunge, kabla ya kupima (aliambiwa apime) na KUJIHUKUMU (hakuhukumiwa), alipata muda wa kujieleza tena LIVE lakini badala yake alianza kulia lia na kusema, "nimeonewa sana" sasa pale angesema, "Hao ni waongo na ukweli ni huu na nimepima nimeona natakiwa kuombwa radhi na kamati na kwa kutumia kanuni ..... naomba mtoa hoja athibitishe kauli yake vinginevyo aifute", na ikawa katika kumbukumbu na mambo yangekuwa kibao kimewageukia kina Mwakyembe, lakini sasa!!!!!!???
 
Umefika wakati wa kuonkana na fikra mgando. Natamani Lowasa atoe tamko na atangaze kambi yake nasi tuweze pima utashi wao kisiasa.
 
Siasa za chuki zimewajaa wabongo. Ama kweli ndivyo tulivyo! The Nyani alishajisemea.
 
Lowassa ku-hit back kutasaidia sana Tanzania. It could be the first move to real change. Ivi kikao kikuu cha CCM kuchagua mgombea wao ni lini?
 
mvurugano ndani ya ccm utatusaidia sana,ili taifa liendelee tunatakiwa kuwa na vitu 5(WATU,ARDHI,SIASA SAFI,UONGOZI BORA NA KUGAWANYIKA CCM)Kwani without a divided ccm nothing ever will change,the whole system have to change.
 
Ndugu yangu mbona unakuja na hadithi za alfu lela ulela ama hekaya za abunuwasi?. Ufisadi wa Lowasa ni kujenga nyumba kule Namanga, je una uthibitisho kwamba zile nyumba ni za Lowasa?. Hata kama ni za kwake una uhakika gani kwamba aliiba pesa za AICC ili kujengea majumba hayo?. Ni viwanja vipi vya Upanga na Masaki ambavyo Lowasa alijimilikisha?, unaweza kutupa uthibitisho pia katika hili?. Uwanja uliozungushiwa mabati hapo city centre nao unasema ni mali ya Lowasa, kwa uthibitisho upi?. Sintaona haya kutokubaliana na wewe kwenye hili suala. Jamani mtendeeni haki Lowasa, alistahili kupewa nafasi ya kujieleza mbele ya watanzania kabla ya kuanza kumrushia madongo ya lawama na kejeli.

Kama Lowasa alikuwa mchafu kwanini Jakaya alimteua kuwa WM?, ina maana wana usalama hawakuona machafu hayo na kumshauri Jakaya?.

Kwa salary ipi na per dm ipi inayomwezesha a public servant to own a vast number of bangaloos in TZ as well as in the RSA?? EL ameshachafuka na ananuka, asitake kuwaambukiza na wenzake kwa kuwatuma watu visionless kama nyie!! Lets gets on the serious business ya kuokoa rasilimali za nchi hii ... EL ... EL .. who the hell is he?? kama alikuwa na ndoto za kuja kuwa army-in-chief wa nchi hii nendeni mkamwambie AMESHAFULIA ... atulie tu na miradi yake ya kifisadi ... Muungwana si mjinga kiivyo manvyofikiri ... EL atamalizwa tu ... take it as a note!!
 
Have you seen title deeds of those Bangalows Sir? Zina jina la Lowassa?
 
Serikali hii yaani itukanganya ile mbaya, ikulu ilivyoongea imeonyesha kabisa kuwa kuna mtu alikaidi agizo la Rais, lakini upande wa pili inaonyesha huyo mtu anaogopwa sana.
 
Indeed,two huors ago niliwasikia watu fulani wanaongea,and they seem to be in the know,wanasema,kama Luhanjo anasema Kikwete hana makosa,hii ina maana moja tu, kwamba mwenye makosa ni Lowassa,na tunategemea kwamba Lowassa ni lazima ataongea kupinga kabisa jambo hilo.
 
LET HIM COME BACK, WE ARE WAITING. TATIZO BADO WANAAMINI KWAMBA PESA ZITAFANYA KAZI KWENYE KAMPENI. NAAMINI VIJANA WANAOMALIZA VYOU WANATAKIWA WAWE MACHO SANA NA HILI, BECAUSE THEY ARE THE LOSERS. WAWASAIDIE WAZEE VIJIJINI KUELEWA PUMBA NA MCHELE. You pocket their filthy money, they exploit you for the rest of your life.
 
- Lowassa ana tatizo moja kubwa sana la binafsi, ni kwamba anamu-under-estimate sana Muungwana, inapokuja kwenye power na popularity, mpaka leo haelewi kwamba mwenziwe anaishi just for those two things,

- Hivi karibuni nilipata bahati ya kuongea na "mtu" mmoja toka wizara ya maji, anawajua wote wawili vizuri sana tena kuliko, ndiye aliyeniambia hata sababu ya conflict ya Mwandosya na Muungwana, yaani ilianzia kwenye demu, akanitajia na jina la demu ambaye nilimfatilia na kuhakikisha mwenyewe kwamba yupo pale maji mpaka leo hii, sitamtaja jina kwa leo,

- Akasema inapokuja kwenye power na popularity, Muungwana ni moto wa kuotea mbali sana, sawa habari ni nzito sana jinsi Lowassa anavyojitayarisha kurudi, na sio siri tena maana ni wazi kabisa na hata viongozi wetu wanaokwenda kujigonga gonga huko nyumbani kwake saa za usiku kwa siri, lakini ni mbio za sakafuni tu!

- Maana soon atagundua kwamba rais wa Tanzania ana nguvu za ajabu sana kisheria, ninamuonea huruma sana Lowassa.

Respect.

FMEs!

Mzee FMES.
Umeandika vizuri sana.Lakni swali langu ni dogo.. ina maana huo urafiki wote tulioambiwa huko nyuma kati ya President na huyu Edward ndio umekwisha kabisa? Najaribu kutazama nguvu aliyokua nayo president naiona lakini nachelea kusema je ataweza kuitumia ka Lowasa.Sitaki kuwa Thomaso lakini nina hakika haya mambo yana weza kuwa zaidi ya vile tunavyowaza na vigumu sana kuamini kuwa hawa mabwana hizi siasa zimewatenganisha kwa kiasi tunachofikiri.Anyway ngoja tuone
 
Wanaodhani JK ni dhaifu wawaulize akina Mramba na Yona. EL hawezi kuthubutu kutoa tamko lolote angalau kwa sasa ingawa hicho ndicho wanachotaka kitokee akina Sitta & Co kule Mjengoni.
 
Are you real a Fair Player? Nakubaliana na wewe kuwa Lowasa ni mchapa kazi na wote tunajua hilo wala hakuna ubishi. Tusichompendea Lowasa ni Fisadi. Kama hujui Lowasa ameanza ufisadi siku nyingi sana tangu akiwa mkurugenzi mkuu wa AICC. Wakati huo alijenga nyumba nyingi sana pale Namanga na Arusha mjini kwa kufuja hela za AICC. Alipochaguliwa kuwa waziri mdogo ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa ndo alipotajirikia kabisa tena kipindi kile cha elnino. Alipopata uwaziri wa ardhi alikamata viwanja vingi sana kwenye prime areas such as masaki and upanga. Alipokuwa waziri mkuu aliwatimua walalahoi kwenye machimbo ya kunduchi kwa lengo la kuweka appartments na aliweza kuamuru nyumba ya mfanyabiashara mmoja ufukweni mwa bahari ya hindi ivunjwe nasikia kwa sababu ilizuia nyumba/biashara yake (hili sina hakika nalo). Nasikia kiwanja kilichozungushiwa mabati karibu na Denmark Embassy kinachotizamana na viwanja vya gymkhana ni chake. Je unataka mtu wa namna hii awe rais si matatuuza tukiwa vitandani? Fikiri mara saba sabini kabla ya kumsupport.

Ahsante sana kwa kututahadharisha kuhusu huyu fisadi EL. Lakini hafiki mbali katika mbio zake. Tayari ana laana za Baba wa Taifa. ambaye nina uhakika huko aliko anafuatilia kwa makini sana nyendo za dhulumati huyu!
 
Back
Top Bottom