"Nimetafakari sana kwa niaba ya wananchi wangu wa jimbo la Monduli na kwa niaba ya chama changu Chama Cha Mapinduzi....." EL siku alipojiuzuru. Kama EL bado anaamini katika filosofia/falsafa ya kutafakari mambo kwa niaba ya chama chake (kitu ninachoamini bado anafanya) hawezi hata siku moja kurusha mashambulizi dhidi ya JK (M/kiti wa chama chake). Ni Mrema pekee yake aliweza kuondoka akiwa na umaarufu kumzidi Bosi wake (AHM). Waliobaki wote, Kilango, EL, Mwakyembe mbali ya kuwa ni wanaCCM lakini pia wanamaslahi binafsi yanayweza kuathirika iwapo wataamua kuondoka CCM au kusema kitu cha kuhatarisha ustawi wa M/kiti.
kwa Mfano EL kuwageuka akina JK anakuwa anaweka kwenye risk mafao yake anayoendelea kupata kama PM mstaafu, Mama Kilango hawezi kumuweka rehani mumewe mwenye dhamana kubwa ya kimapato ndani ya chama na WM mstaafu. Wakati huo huo watoto wao wanategemewa kugombea ubunge huko Mtera dingi atakapo stafu. Kama huyu mama Mheshimiw akifyatuka tofauti sana basi nafasi ya vijana wake kupewa uwakilishi na labda hata uwaziri inakuwa mashakani.
Mwakyembe pamoja na ukali wote na mbwembwe za kusoma report ya tume ya Bunge hawezi kutoka Chichiem kwasababu anaamini miradi yake ya Umeme haiwezekani kutekelezeka kama hujakingiwa kifua na wakulu wa nchi wanokubali kupindisha sheria upewe mkopo au grant kutoka benki au mashirika ya pesa.
Kama utakumbuka vizuri kuna kipindi Mwakyembe alikasirika sana, akasema kuna mambo ambayo hawakuyaweka kwenye report yao na kama yangewekwa wazi nchi ingetikisika. Unadhani ni mambo gani hayo? Lazima ujue Mwakyembe sio mjinga kusema ile sentensi, Mwakyembe anajua wahusika wote vizuri sana, inawezekana anajua kuwa kuna mkubwa zaidi ya Mh. EL alihusika kwa njia moja au nyingine.
Pia Makyembe na akina Stella walijua kuwa ni lazima wakinusuru CHAMA na M/kiti wake. Kwani wangesema yote maana yake wengi zaidi wangejiuzuru au serikali kuvunjwa na uchaguzi mkuu uitishwe na Uchaguzi mkuu ukiitishwa katika hali kama ile CHAMA kingepoteza ushindi (assume utakuwa huru na wa haki). Kwa hiyo wakabana baadhi ya mambo. (Kidumu Chama Chetu!)
Ndio maana kipindi cha EL kilipokatishwa hakulalamika, ndio maana maelezo ya RA yalipokataliwa bungeni hakuyatoa kwenye media au kwa public ingawa angeweza kufanya hivyo, kwani hayakuwa mali ya bunge tena.
Kwa Ujumla sitegemei wala sioti EL kutoa tamko litakalo mpinga au kumpaka matope JK. Utatu wao usio mtakatifu yaani JK, EL na RA hauvunjiki kwa moto wa kuni, unahitaji moto wa makaa ya mawe wa kupepewa na mafeni yanayozungushwa na injini za jeti. Na malaika wanaotumika madhabahuni kwa hawa waheshimiwa ni akina Chenge, akina Karamagi, sijui kama Mgonja hayumo humu? Hawa ni wamoja wenye kunia mamoja amini amini nawaambieni. na siku zote wanasema Zidumu Fikra sahihi za m/kiti.
Akina Manyika, akina Hosea wanashindikana kutupwa kwenye tanuru la moto hata ikibidi basi nje kwasababu wanajua mengi mno, kuwatupa nje ni kurisk kuvuja kwa sensitive informations. Mwanyika sio mwanasheria aliyesomea sheria kindergaten, anajua fika nini kiliendelea kwenye sakata la Rich-Mond. Lazima mjue huu sio uzembe wa kawaida kuna more than uzembe ukizingatia issue yenyewe ilivyokuwa hot, mpaka watu wanataka kutengeneza mvua, kwa hiyo lazima alipitia documents zote na alijiridhisha kuwa zile kampuni zilikuwa feki na ni kampuni za kuja kuchoto vijisenti vya watanzania. kwanini hakuchukua hatua, eidha aliogopa kwa kuwa iliwahusu wakubwa au alikuwa mshiriki kama kaka yeke aliyemtangulia bw. VG cent alivyoshiriki deal kibao inc. Meremeta, TANGOLD. Unaona?
Na Bw. Hosea alipopeleleza aligundua kabisa pamoja na kuwa hao TAKURU walikuwa wameota meno manne tu, lakini haimaanishi walikuwa hawana macho. Actually walikuwa wanaona lakini hawawezi kutafuna. Kwa hiyo waliona na wakawastua wahusika kuwa tunaona. Inawezekana walifungwa mdomo wasibweke au waliingizwa kwenye kundi la hao wanufaika. Mbwa akishakuwa analala na binadamu ndani ya nyumba huyo sio mbwa wa ulinzi tena anabadirishwa hata jina anaitwa Petty. Ukitaka kujua wewe jiulize kwanini sasa haleti ma-issue tunayoyalalamikia kila siku kama ya TRL wakati sasa ana meno 24 na amekuwa mkubwa mpaka tunamuita TAKUKURU na sio TAKURU?? (Wizi Mtupu!)
Kuhusu Mh. Mbowe kuachia ngazi ya Uenyekiti, Binafsi sijui sana uwajibikaji wa ndani wa CHADEMA. Kwa mfano CCM wapo makini sana kwenye masuala ya nidhamu ndani ya chama chao, wanademokrasia ya kukubaliana hata kama ni jambo litakalo muua mmoja (km Nnauye) au kumjenga na kumlinda mmoja hata kama ni mchafu (Km Mzee VG Cent).
Kama Madai ya marehemu Chacha Wangwe (RIP) ni ya kweli basi ningependekeza CHADEMA wakubali kubadili safu nzima ya uongozi wa juu (sio lazima kuwaacha nje hata kubadilishana) na kuunda upya kamati zao. Na kukubaliana kuanza upya ujenzi wa demokrasia watakayo hama nayo kwenda kwenye kuongoza nchi watakapo pewa ridhaa ya watanzania. Wakubali kuwa Nchi hii haitakuwa kama ilivyo sasa, baada ya mabadiriko kutakuwa na uwezekano wa chama kutoshnda zaidi ya 50% miaka ijayo, kwa hiyo hali ya demokrasia ya kusikilizana na kuheshimiana itahitajika sana, hasa kusikiliza maoni ya walio wengi. Nchi hii Pindi CCM Itakao ng'olewa madarakani uwezekano wa chama kutawala miongo miwili mfululizo huko mbeleni utakuwa ni mdogo mno. Ni wale tu watakaoweza kuprove kuwa wanaweza kufanya tofauti ndio watakaokuwa na nafasi.
Kama Madai ya Chacha Wangwe hayakuwa ya kweli ningependekeza CHADEMA wamwache Mh. Mbowe katika nafasi ya uenyekiti wa chama na agombee Ubunge kama wengi wanavyomuunga mkono. Mgombea wa nafasi ya Urais (Mwingine) afahamike mara moja iwe kwa njia na vikao halali vya chama (kama sheria inaruhusu) baada ya Mkutano mkuu. Lakini pia tungeweza kuanza kumjua kwa njia zisizo rasimi kama sheria ya uchaguzi hairuhusu kumtangaza mgombea mwaka mmoja kabla.
Hii itamaanisha kuwa sio lazima mwenyekiti wa Chama awe mgombea wa Urais na pia itamsaidia mgombea wa Urais kuacha majukumu ya kuratibu uchaguzi mikononi mwa watu wengine na lisiwe jukumu lake binafsi kama zilivyo kamati za Arusi. Maana mwenyekiti wa Chama atawajibika kuhakikisha Chama Chake kinashinda kwa hiyo kutakuwa na mkakati wa kichama zaidi na sio wa kimgombea.
Lakini kubwa kupita yote ni majibu ya serikali juu ya Tuhuma zote hizi ilizopewa hivi karibu. Ukiusoma vizuri waraka wa kanisa katoliki utakuta zile ni tuhuma za wazi dhidi ya serikali na chama tawala kushindwa kutawala na kuwaendeleza watanzania kiuchumi, kiafya, kielimu na nyanja zingine muhimu na sio watu binafsi inavyotafsiriwa na wengi. Waraka unaonyesha bayana kushindwa kukua kwa demokrasia, unaonyesha bayana ufisadi na ubadihirifu wa mali za umma, kujilimbikizia madaraka na kushinwa kuwajibika kwa watendaji wa ngazi zote za serikali.
Ukisoma Report ya MJJ ya Downs, Report ya MJJ ya meremeta hapo hutakuwa na la kusema ila kujua kuwa nchi hii haina wenyewe ilishapigwa mnada siku nyingi na sisi tunaopiga kelele ni kama mbuzi wanaosubiri kugeuzwa mishikaki.
Kwa hiyo mimi ningependekeza wanaharakati badala ya kusukuma EL kutoa majibu yatakayowasambaratisha (kitu ambacho hakiwezekani) msukumo uwekwe kweye hizi hoja na tuhuma zilizotolewa. Huku hawana majibu. Inahitajika nguvu kubwa zaidi ofcourse, lakini huku ndiko kwenye faida iliyowazi, huku ndiko kuna kazi hata baada ya kupewa dola. Kazi ya kuanzisha upelelezi mpya na huru ma tuhuma zote, kufungua kesi za makosa ya jinai, kuwakamata na kuwafungulia kesi wale wote waliohusika na makosa yanyohusiana na uvunjaji wa haki za binadamu (against humanity au sijui wanziita attrocities) nadhani watahitajika kupelekwa ICC. Pia kurudisha mali zote zilizopolwa na warohi wachache na baadaye kutafuta njia za kuziba mianya yote ya kuibiana kiana aina na pia kujenga jamii watu walio sawa na huru na wanaofaidi matunda ya nchi yao.
Mungu Ibariki Tanzania