Lowassa to strike back ; Mbowe to quit chairmanship?

Lowassa to strike back ; Mbowe to quit chairmanship?

ni dhairi kabisa kikwete alikuwa anajua lowasa atamsumbua.

kitendo cha kuhakikisha lowasa anajiuzulu kwa kashfa ya richmond ilikuwa ni character assassination ambayo imeongozwa na kanali JK. kama lowasa angekuwa waziri mkuu mpaka sasa hivi angekuwa na nguvu zaidi ya kikwete na ingekuwa ni tishio sana kwa kikwete.
sasa hivi kuna gap kubwa sana ya popularity ndani ya ccm (kutoka kikwete mpaka mtu anayemfuatia) lakini kama lowasa angekuwa waziri mkuu mpaka sasa hivi angekuwa popular sambamba na JK

ukiangalia mwandosya na magufuli wizara walizopewa ni dhairi kabisa kikwete amefanikiwa kuwanyamazisha wapinzani wake wa karibu.


Unfortunately, Mwandosya is not a shrewd politician; ameshindwa kuwa na network ya watu wa kumtetea come rain come sunshine kwasababu ameshindwa kutumia nafasi zake alizopata kufanya hivyo; he does not have what it takes kuwa RAIS; he does not have the spine, ni mwoga!!
 
- Lowassa ana tatizo moja kubwa sana la binafsi, ni kwamba anamu-under-estimate sana Muungwana, inapokuja kwenye power na popularity, mpaka leo haelewi kwamba mwenziwe anaishi just for those two things,

- Hivi karibuni nilipata bahati ya kuongea na "mtu" mmoja toka wizara ya maji, anawajua wote wawili vizuri sana tena kuliko, ndiye aliyeniambia hata sababu ya conflict ya Mwandosya na Muungwana, yaani ilianzia kwenye demu, akanitajia na jina la demu ambaye nilimfatilia na kuhakikisha mwenyewe kwamba yupo pale maji mpaka leo hii, sitamtaja jina kwa leo,

- Akasema inapokuja kwenye power na popularity, Muungwana ni moto wa kuotea mbali sana, sawa habari ni nzito sana jinsi Lowassa anavyojitayarisha kurudi, na sio siri tena maana ni wazi kabisa na hata viongozi wetu wanaokwenda kujigonga gonga huko nyumbani kwake saa za usiku kwa siri, lakini ni mbio za sakafuni tu!

- Maana soon atagundua kwamba rais wa Tanzania ana nguvu za ajabu sana kisheria, ninamuonea huruma sana Lowassa.

Respect.

FMEs!


Tafadhali mkuu maneno hayo niliyobold yanahitaji prove ya hali ya juu sana! Unless otherwise lakini kulinganisha ufuska wa Muungwana na Mwandyosya nadhani humtendei haki mwandosya! Fuatilia vizuri ugomvi wao vizuri! Kwa jinsi ninavyojua huo ugomvi unatokana na utendaji zaidi na si wanawake! Kikwete alionekana goigoi asiyekuwa na uwezo wa kutoa idea wakati huo mwandyosya akiwa chini yake na mawazo mengi yalikuwa haliyokuwa anayatoa hayakuwa na tija.
 
Hili la Mbowe linanishtua kidogo. Huyu ameongoza kipindi chake cha kwanza kwa mafanikio makubwa kuliko kiongozi yeyote wa chama cha siasa (including ccm) baada ya mfumo wa vyama vingi. Kugombea ubunge badala ya urais inaweza kuwa kwa maslahi ya CHADEMA, lakini kuachia uenyekiti katika kipindi hiki atakaye sherehekea ni CCM!

Ningefurahi sana kusikia kuwa ni kwanini Mbowe hafai. Labda Uchagga na waasisi wa chama ndo tabu.....
 
Wakuu zanguni,
Ama kweli Jamatin kaingia Gorro!
Huyu Lowassa mbona anakusumbueni sana!..Hivi kweli watu bado mnatabia kama za Waganda ambao kila siku wanaendelea kumlilia Idd Amin hata baada ya majanga yote yaliyowahi tokea. Hivi kweli kuna mtu anaweza kufkiria Uganda ingekuwaje leo kama Idd Amin angeendela kuwa rais wa nchi hiyo!

Huyu ndiye Lowassa, mshenzi mmoja alotuingiza hasara kubwa leo hihi amekuwa chaguo la wananchi hata katika mazungumzo!.. Hivi kweli kama Jk asingemwondoa Lowassa katika nafasi ile hii Tanzania ingekalika kweli?.. I mean guys jaribuni kufikiria Lowassa akiwa waziri mkuu na ile scandal nzima ya Richmond sijui imezimwa vipi, hivi kweli hicho chama CCM kingekuwa na sauti kwa wananchi au hata hapa JF...

Wakuu zangu, Lowassa ni mtu wa kusahaulika, Ijipange atakavyo huyu mtu tumfute kabisa ktk kumbukumbu zetu..Huyu ni mtu alopewa kila nguvu ya madaraka na JK. Huyu ndiye alichagua mawaziri karibu wote wa JK, ndiye aliyepanga secretariat ya CCM, ndiye alotufungashia mikataba kibao mikubwa na midogo kwa kutumia nguvu ya wadhifa wake.
Matokeo, kanya anapolia chakula..tena basi akiwa na bahati kajiuzuru hata kabla ya kuhojiwa tuhuma hizo, na ajabu bado ati yupo bungeni ambako anatakiwa kujibu maswali mengi muhimu sana, leo ati anajipanga kurudi ktk uongozi na anapewa sifa zote...Bila shaka wapo wanamtaka na kuomba Mkapa arudi kugombea Urais kwani sisi Miafrika Ndivyo Tulivyo!

Mkuu

Lowasa hakufanya madudu haya pekee yake. Uchafu wote huu ulifanywa na timu ya viongozi wakubwa wa chama tawala. Suala la Richmond ni kubwa hivyo si rahisi kulifanya ama kufanyika na mtu mmoja. Lilijulikana mpaka na mkuu wa nchi. Bado napenda ieleweke wazi kwamba Lowasa katolewa kafara katika suala hili ili kuziba ama kutetea nafasi za watu fulani fulani ikiwa ni pamoja na mkuu wa nchi. Hili linajidhihirisha pale Lowasa aliponyimwa haki na uhuru wa kuulizwa maswali na kujieleza mbele ya tume ya Mwakyembe.
Kumbukeni kwamba Mwakyembe mwenyewe kwa mdomo wake alikiri kwamba kuna mambo mazito waliyoyaona wakati wa uchunguzi wao na hawezi kuyasema wala kuyaandika katika ripoti yao kwa manufaa ya nchi na serikali, cha kujiuliza ni kitu gani hicho ambacho ni siri?, na kwanini iwe siri wakati walipewa kazi ya kuchunguza na kuanika kila kitu hadharani?.
Lowasa hakutetendewa haki hata kidogo na ana kila sababu ya kufight back kwa kadri ya uwezo wake. Jamani tumpe nafasi na yeye ajieleze kiundani kabla ya kumuhukumu, si vyema wala busara kumchafua bila kujua vitu kiundani.
 
Selous,
Kwamba Mbowe hafai? Hapana, sikumaanisha hivyo. Reality ni kuwa hakuna kitakachomzuia Kikwete kushinda kipindi cha pili. Tunaweza kuongeza idadi ya wabunge, na ni vema Mbowe akawa mmoja wa hao wabunge tutakaoongeza kwani kwa wale tunaokumbuka ubunge wake 2000 - 2005 tunafahamu kazi aliyoifanya.

Kwenye uenyekekiti, kama nilivyoandika awali, kipindi chake kimekuwa cha mafanikio makubwa sana kwa chama. Kwa wanachama on the ground, hatujasahau maumivu tuliyosababishiwa na Wangwe, na ninafahamu kuwa hata baada ya mkakati wa Wangwe kushindwa mafisadi bado hawajachoka. Kwa kadri ya ufahamu wangu, CHADEMA haijamzuia mwanachama yeyote kugombea uenyekiti. Wajitokeze wapambane na Mbowe, lakini si Mbowe kujiuzulu, bado tunamhitaji kukiongoza chama. We just don't want the Party to be hijacked by the Lowasas!
 


Chairman Mbowe's move to give up the party's chairmanship will be a wise decision. I hope Dr. Kitila Mkumbo is ready to take the party's chairmanship, as well run for the Presidency.


thanks for the dataz.

Thanks mkuu, i see Kitila as a young prosperous and talented man... but i am not sure if he is ready to be the chairman!!!! Sometimes wanasema ukubwa dawa [age matters]

He may be the best manager, but give him a few more year before he starts leading CHADEMA
 
"Nimetafakari sana kwa niaba ya wananchi wangu wa jimbo la Monduli na kwa niaba ya chama changu Chama Cha Mapinduzi....." EL siku alipojiuzuru. Kama EL bado anaamini katika filosofia/falsafa ya kutafakari mambo kwa niaba ya chama chake (kitu ninachoamini bado anafanya) hawezi hata siku moja kurusha mashambulizi dhidi ya JK (M/kiti wa chama chake). Ni Mrema pekee yake aliweza kuondoka akiwa na umaarufu kumzidi Bosi wake (AHM). Waliobaki wote, Kilango, EL, Mwakyembe mbali ya kuwa ni wanaCCM lakini pia wanamaslahi binafsi yanayweza kuathirika iwapo wataamua kuondoka CCM au kusema kitu cha kuhatarisha ustawi wa M/kiti.

kwa Mfano EL kuwageuka akina JK anakuwa anaweka kwenye risk mafao yake anayoendelea kupata kama PM mstaafu, Mama Kilango hawezi kumuweka rehani mumewe mwenye dhamana kubwa ya kimapato ndani ya chama na WM mstaafu. Wakati huo huo watoto wao wanategemewa kugombea ubunge huko Mtera dingi atakapo stafu. Kama huyu mama Mheshimiw akifyatuka tofauti sana basi nafasi ya vijana wake kupewa uwakilishi na labda hata uwaziri inakuwa mashakani.

Mwakyembe pamoja na ukali wote na mbwembwe za kusoma report ya tume ya Bunge hawezi kutoka Chichiem kwasababu anaamini miradi yake ya Umeme haiwezekani kutekelezeka kama hujakingiwa kifua na wakulu wa nchi wanokubali kupindisha sheria upewe mkopo au grant kutoka benki au mashirika ya pesa.

Kama utakumbuka vizuri kuna kipindi Mwakyembe alikasirika sana, akasema kuna mambo ambayo hawakuyaweka kwenye report yao na kama yangewekwa wazi nchi ingetikisika. Unadhani ni mambo gani hayo? Lazima ujue Mwakyembe sio mjinga kusema ile sentensi, Mwakyembe anajua wahusika wote vizuri sana, inawezekana anajua kuwa kuna mkubwa zaidi ya Mh. EL alihusika kwa njia moja au nyingine.

Pia Makyembe na akina Stella walijua kuwa ni lazima wakinusuru CHAMA na M/kiti wake. Kwani wangesema yote maana yake wengi zaidi wangejiuzuru au serikali kuvunjwa na uchaguzi mkuu uitishwe na Uchaguzi mkuu ukiitishwa katika hali kama ile CHAMA kingepoteza ushindi (assume utakuwa huru na wa haki). Kwa hiyo wakabana baadhi ya mambo. (Kidumu Chama Chetu!)

Ndio maana kipindi cha EL kilipokatishwa hakulalamika, ndio maana maelezo ya RA yalipokataliwa bungeni hakuyatoa kwenye media au kwa public ingawa angeweza kufanya hivyo, kwani hayakuwa mali ya bunge tena.

Kwa Ujumla sitegemei wala sioti EL kutoa tamko litakalo mpinga au kumpaka matope JK. Utatu wao usio mtakatifu yaani JK, EL na RA hauvunjiki kwa moto wa kuni, unahitaji moto wa makaa ya mawe wa kupepewa na mafeni yanayozungushwa na injini za jeti. Na malaika wanaotumika madhabahuni kwa hawa waheshimiwa ni akina Chenge, akina Karamagi, sijui kama Mgonja hayumo humu? Hawa ni wamoja wenye kunia mamoja amini amini nawaambieni. na siku zote wanasema Zidumu Fikra sahihi za m/kiti.

Akina Manyika, akina Hosea wanashindikana kutupwa kwenye tanuru la moto hata ikibidi basi nje kwasababu wanajua mengi mno, kuwatupa nje ni kurisk kuvuja kwa sensitive informations. Mwanyika sio mwanasheria aliyesomea sheria kindergaten, anajua fika nini kiliendelea kwenye sakata la Rich-Mond. Lazima mjue huu sio uzembe wa kawaida kuna more than uzembe ukizingatia issue yenyewe ilivyokuwa hot, mpaka watu wanataka kutengeneza mvua, kwa hiyo lazima alipitia documents zote na alijiridhisha kuwa zile kampuni zilikuwa feki na ni kampuni za kuja kuchoto vijisenti vya watanzania. kwanini hakuchukua hatua, eidha aliogopa kwa kuwa iliwahusu wakubwa au alikuwa mshiriki kama kaka yeke aliyemtangulia bw. VG cent alivyoshiriki deal kibao inc. Meremeta, TANGOLD. Unaona?

Na Bw. Hosea alipopeleleza aligundua kabisa pamoja na kuwa hao TAKURU walikuwa wameota meno manne tu, lakini haimaanishi walikuwa hawana macho. Actually walikuwa wanaona lakini hawawezi kutafuna. Kwa hiyo waliona na wakawastua wahusika kuwa tunaona. Inawezekana walifungwa mdomo wasibweke au waliingizwa kwenye kundi la hao wanufaika. Mbwa akishakuwa analala na binadamu ndani ya nyumba huyo sio mbwa wa ulinzi tena anabadirishwa hata jina anaitwa Petty. Ukitaka kujua wewe jiulize kwanini sasa haleti ma-issue tunayoyalalamikia kila siku kama ya TRL wakati sasa ana meno 24 na amekuwa mkubwa mpaka tunamuita TAKUKURU na sio TAKURU?? (Wizi Mtupu!)

Kuhusu Mh. Mbowe kuachia ngazi ya Uenyekiti, Binafsi sijui sana uwajibikaji wa ndani wa CHADEMA. Kwa mfano CCM wapo makini sana kwenye masuala ya nidhamu ndani ya chama chao, wanademokrasia ya kukubaliana hata kama ni jambo litakalo muua mmoja (km Nnauye) au kumjenga na kumlinda mmoja hata kama ni mchafu (Km Mzee VG Cent).

Kama Madai ya marehemu Chacha Wangwe (RIP) ni ya kweli basi ningependekeza CHADEMA wakubali kubadili safu nzima ya uongozi wa juu (sio lazima kuwaacha nje hata kubadilishana) na kuunda upya kamati zao. Na kukubaliana kuanza upya ujenzi wa demokrasia watakayo hama nayo kwenda kwenye kuongoza nchi watakapo pewa ridhaa ya watanzania. Wakubali kuwa Nchi hii haitakuwa kama ilivyo sasa, baada ya mabadiriko kutakuwa na uwezekano wa chama kutoshnda zaidi ya 50% miaka ijayo, kwa hiyo hali ya demokrasia ya kusikilizana na kuheshimiana itahitajika sana, hasa kusikiliza maoni ya walio wengi. Nchi hii Pindi CCM Itakao ng'olewa madarakani uwezekano wa chama kutawala miongo miwili mfululizo huko mbeleni utakuwa ni mdogo mno. Ni wale tu watakaoweza kuprove kuwa wanaweza kufanya tofauti ndio watakaokuwa na nafasi.

Kama Madai ya Chacha Wangwe hayakuwa ya kweli ningependekeza CHADEMA wamwache Mh. Mbowe katika nafasi ya uenyekiti wa chama na agombee Ubunge kama wengi wanavyomuunga mkono. Mgombea wa nafasi ya Urais (Mwingine) afahamike mara moja iwe kwa njia na vikao halali vya chama (kama sheria inaruhusu) baada ya Mkutano mkuu. Lakini pia tungeweza kuanza kumjua kwa njia zisizo rasimi kama sheria ya uchaguzi hairuhusu kumtangaza mgombea mwaka mmoja kabla.

Hii itamaanisha kuwa sio lazima mwenyekiti wa Chama awe mgombea wa Urais na pia itamsaidia mgombea wa Urais kuacha majukumu ya kuratibu uchaguzi mikononi mwa watu wengine na lisiwe jukumu lake binafsi kama zilivyo kamati za Arusi. Maana mwenyekiti wa Chama atawajibika kuhakikisha Chama Chake kinashinda kwa hiyo kutakuwa na mkakati wa kichama zaidi na sio wa kimgombea.

Lakini kubwa kupita yote ni majibu ya serikali juu ya Tuhuma zote hizi ilizopewa hivi karibu. Ukiusoma vizuri waraka wa kanisa katoliki utakuta zile ni tuhuma za wazi dhidi ya serikali na chama tawala kushindwa kutawala na kuwaendeleza watanzania kiuchumi, kiafya, kielimu na nyanja zingine muhimu na sio watu binafsi inavyotafsiriwa na wengi. Waraka unaonyesha bayana kushindwa kukua kwa demokrasia, unaonyesha bayana ufisadi na ubadihirifu wa mali za umma, kujilimbikizia madaraka na kushinwa kuwajibika kwa watendaji wa ngazi zote za serikali.

Ukisoma Report ya MJJ ya Downs, Report ya MJJ ya meremeta hapo hutakuwa na la kusema ila kujua kuwa nchi hii haina wenyewe ilishapigwa mnada siku nyingi na sisi tunaopiga kelele ni kama mbuzi wanaosubiri kugeuzwa mishikaki.

Kwa hiyo mimi ningependekeza wanaharakati badala ya kusukuma EL kutoa majibu yatakayowasambaratisha (kitu ambacho hakiwezekani) msukumo uwekwe kweye hizi hoja na tuhuma zilizotolewa. Huku hawana majibu. Inahitajika nguvu kubwa zaidi ofcourse, lakini huku ndiko kwenye faida iliyowazi, huku ndiko kuna kazi hata baada ya kupewa dola. Kazi ya kuanzisha upelelezi mpya na huru ma tuhuma zote, kufungua kesi za makosa ya jinai, kuwakamata na kuwafungulia kesi wale wote waliohusika na makosa yanyohusiana na uvunjaji wa haki za binadamu (against humanity au sijui wanziita attrocities) nadhani watahitajika kupelekwa ICC. Pia kurudisha mali zote zilizopolwa na warohi wachache na baadaye kutafuta njia za kuziba mianya yote ya kuibiana kiana aina na pia kujenga jamii watu walio sawa na huru na wanaofaidi matunda ya nchi yao.

Mungu Ibariki Tanzania
Imen.GREAT THINKER!
 
Mbowe alikwisha zungumza kugombea jimbo
 
Kusema ukweli kama ni kuchapa kazi na kujenga nchi I will vote for Edward Lowassa!!


Pinda hana msimamo kama anaendeshwa kwa remote control vile. Lowassa ndie anayefaa kuongoza hii nchi, sema tu hakupewa nafasi ya kujieleza. Naye kama kiongozi shupavu akajiuzulu.

JK ni weak na mswahili, mnakumbuka alipoulizwa na VOA jambo gani anajutia katika utawala wake alisemaje???!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Bwana Mwita, I respect your idea for Dr. Kitila Mkumbo to take Chadema's Chairmanship but Mkumbo is too young politically to run for Presidency as only few of us know his capability. I do rember his leadership as the DARUSO President was good. My opinion is for him to be a Chadema's Chairperson so that he can show his ability to the Tanzanians while preparing himself for the 2015 general election. Kindly oblige.
 
Are you real a Fair Player? Nakubaliana na wewe kuwa Lowasa ni mchapa kazi na wote tunajua hilo wala hakuna ubishi. Tusichompendea Lowasa ni Fisadi. Kama hujui Lowasa ameanza ufisadi siku nyingi sana tangu akiwa mkurugenzi mkuu wa AICC. Wakati huo alijenga nyumba nyingi sana pale Namanga na Arusha mjini kwa kufuja hela za AICC. Alipochaguliwa kuwa waziri mdogo ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa ndo alipotajirikia kabisa tena kipindi kile cha elnino. Alipopata uwaziri wa ardhi alikamata viwanja vingi sana kwenye prime areas such as masaki and upanga. Alipokuwa waziri mkuu aliwatimua walalahoi kwenye machimbo ya kunduchi kwa lengo la kuweka appartments na aliweza kuamuru nyumba ya mfanyabiashara mmoja ufukweni mwa bahari ya hindi ivunjwe nasikia kwa sababu ilizuia nyumba/biashara yake (hili sina hakika nalo). Nasikia kiwanja kilichozungushiwa mabati karibu na Denmark Embassy kinachotizamana na viwanja vya gymkhana ni chake. Je unataka mtu wa namna hii awe rais si matatuuza tukiwa vitandani? Fikiri mara saba sabini kabla ya kumsupport.
 
Wakuu zanguni,

Huyu ndiye Lowassa, ....Hivi kweli kama Jk asingemwondoa Lowassa katika nafasi ile hii Tanzania ingekalika kweli?.. !

Sina Uhakika kama unamaanisha ulichosema hapo, JK kumuondoa Lowassa au keybord kuteleza. JK ameshindwa kuwaondoa mwanyika na Hosea unadhani angeweza kumwondoa Lowassa kwenye nafasi ya WM? JK ameshindwa kumuondoa mze wa VG Cent kwenye nafasi ya uenyekiti wa kamati ya maadili ya Chama unaamini ana ubavu wa kumng'o EL kwenye u-PM. Think twice.
 
mkuu Nziku hii mimi nimeipenda sana..Ikulu ilikurupuka na ni kuweweseka tu kwa akina Luhanjo,mi sielewi maana yake nini unaposema rais alikataza wasilipwe hela na baadaye wakalipwa then ukashindwa kuchukua hatua unakuja kulalamika mwishoni tena baada ya tamko la serikali kukataliwa bungeni..why hayo aliyotasema Luhanjo yasingeingizwa kwenye taarifa iliyosomwa bungeni.

Naomba mungu anipe maisha marefu nione nchi itakavyo tikisika pale Lowasa atakapo amua kutoa tamko na yeye juu ya haya mambo....

Ikulu haikukurupuka.Mpaka pale lowasa akitokea na kujiondoa ndo tutajua ikulu ILIKURUPUKA au la. Baada ya maelezo ya ikulu tunachokiamini ni kwamba Lowasa na watu wake walikaidi Ikulu na kuingiza taifa kwenye mgogoro.Mpaka hapa Lowasa HATUFAI kutuongoza tena.
 
In order for Tanzania to move forward there is a need to eliminate some of Tanzanians from Tanzanian political life (sio kuwaua wanaweza kuwa eliminated kama Mrema alivyokuwa eliminated without being killed). Kuna watu kuwepo kwao au posibility ya wao kurudi kwenye siasa ni kivuli kikubwa kwenye siasa na kikwazo kikubwa cha maendeleao ya Tanzania. Sitaki kutaja jina la mtu lakini kuna 10 wa haraka ambao najua wanJF mnaweza kuwaorodhesha. Uwepo wao kwenye siasa unatukwamisha sana watanzania. As a result, tunaona kila siku serikali iko on defence kujilinda against kauli zao au move zao, na kuna watu wako nje ya serikali lakini wana remote control zenye nguvu kweli kuliko hata nguvu alizonazo rais kikatiba anazoogopa kuzitumia.
Tunathibitisha ujinga wetu kuwa tuna rais popular, handsome lakini weak na vision less as well as mission less, wana mtandao kumuingiza madarakani kifisadi kumeonda uwezo wake wote imebaki kazi ya kusafiri kila mwezi. Na tunakaribia kukamilisha miaka mitano ya kwanza serikali ikiwa haijafanya lolote zaidi ya struggle for survival, tuna prove ujinga zaidi tunaposema eti JK 2010, kwa kipi? na tuna wananisasa mafisadi na wezi lakini strong na serikali au hata viongozi wa serikali wanasema wazi kuwa wanawaogopa watashindwa kutawala endapo watawashughulikia, as if tumewapa dhamana ya uongozi wa nchi yetu kuwalinda wezi. Inasikitisha sana.
Na mengi tunayofahamu kuhusu EL, lakini inasikitisha sana bado watu wanaona ni mtu anayestahili kurudi kwenye siasa, bado wanaona hata ana chance ya kutuongoza. NI kweli ana nguvu ni mjanja na a bit smarter kuliko muungwana and kutokana na base yake ya support anaweza kurudi na kutingisha, lakini hii haimpi sifa ya kuwa rais wa Tanzania.
Tunahitaji Rais mwingine, sio JK na wala sio anti-Kikwete Camp in CCM. Aje mwenye uwezo, mwenye uchungu na Tanzania, mwenye vision, mwenye lengo la kuendeleza nchi na kuboresha maisha ya watanzania, bila kujali anatoka chama gani. Tutakuwa wajinga sana kama tuta poteza miaka mitano mingine. Lazima tuache kufikiri kama watoto, we have to rescue this country.
 
Are you real a Fair Player? Nakubaliana na wewe kuwa Lowasa ni mchapa kazi na wote tunajua hilo wala hakuna ubishi. Tusichompendea Lowasa ni Fisadi. Kama hujui Lowasa ameanza ufisadi siku nyingi sana tangu akiwa mkurugenzi mkuu wa AICC. Wakati huo alijenga nyumba nyingi sana pale Namanga na Arusha mjini kwa kufuja hela za AICC. Alipochaguliwa kuwa waziri mdogo ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa ndo alipotajirikia kabisa tena kipindi kile cha elnino. Alipopata uwaziri wa ardhi alikamata viwanja vingi sana kwenye prime areas such as masaki and upanga. Alipokuwa waziri mkuu aliwatimua walalahoi kwenye machimbo ya kunduchi kwa lengo la kuweka appartments na aliweza kuamuru nyumba ya mfanyabiashara mmoja ufukweni mwa bahari ya hindi ivunjwe nasikia kwa sababu ilizuia nyumba/biashara yake (hili sina hakika nalo). Nasikia kiwanja kilichozungushiwa mabati karibu na Denmark Embassy kinachotizamana na viwanja vya gymkhana ni chake. Je unataka mtu wa namna hii awe rais si matatuuza tukiwa vitandani? Fikiri mara saba sabini kabla ya kumsupport.

Ndugu yangu mbona unakuja na hadithi za alfu lela ulela ama hekaya za abunuwasi?. Ufisadi wa Lowasa ni kujenga nyumba kule Namanga, je una uthibitisho kwamba zile nyumba ni za Lowasa?. Hata kama ni za kwake una uhakika gani kwamba aliiba pesa za AICC ili kujengea majumba hayo?. Ni viwanja vipi vya Upanga na Masaki ambavyo Lowasa alijimilikisha?, unaweza kutupa uthibitisho pia katika hili?. Uwanja uliozungushiwa mabati hapo city centre nao unasema ni mali ya Lowasa, kwa uthibitisho upi?. Sintaona haya kutokubaliana na wewe kwenye hili suala. Jamani mtendeeni haki Lowasa, alistahili kupewa nafasi ya kujieleza mbele ya watanzania kabla ya kuanza kumrushia madongo ya lawama na kejeli.

Kama Lowasa alikuwa mchafu kwanini Jakaya alimteua kuwa WM?, ina maana wana usalama hawakuona machafu hayo na kumshauri Jakaya?.
 
Sina Uhakika kama unamaanisha ulichosema hapo, JK kumuondoa Lowassa au keybord kuteleza. JK ameshindwa kuwaondoa mwanyika na Hosea unadhani angeweza kumwondoa Lowassa kwenye nafasi ya WM? JK ameshindwa kumuondoa mze wa VG Cent kwenye nafasi ya uenyekiti wa kamati ya maadili ya Chama unaamini ana ubavu wa kumng'o EL kwenye u-PM. Think twice.

Mbogela,

Binafsi nafikiri Mkandara yupo sahihi na anamaanisha alichokisema! Ni possible kukawa na mkono wa JK katika kung'oka kwa EL kama PM, I believe kama JK asingependa aondoke katu hangeondoka....angalau hili ulikubali!

Pili usiwalinganishe Mwanyika, Hosea na Mzee wa vijisenti at al na EL........! hawa wengine si threat kabisa kwa mkulu na wala nawana influence yoyote kubwa kwenye siasa za Tanzania, hawana makundi yoyote, hawana mitandao ya kutisha kama ya EL!! EL level yake kisiasa ungeweza kuilinganisha na JK kabisa (kama member moja alivyosema kule mwanzoni).....so kama JK alifeel hivyo kuwa EL ni threat kwake yes, he could have anything possible to stop him!
 
Ndugu wana JF,

Jambo kubwa na lenye gharama kama la Richmond ni lazima linahusisha viongozi wa ngazi za juu katika serikali. Hapa nina maana kwamba suala la Richmond lilijulikana kwa Raisi, Waziri mkuu, waziri wa madini na nishati mwanasheria mkuu wa serikali, waziri wa fedha na Tanesco. Hili halikuwa suala la kununua na kuuza machungwa pale sokoni kariakoo.

Lowasa amebebeshwa mzigo katika hili suala kimakosa. Mwenye makosa katika hili ni mwenye madaraka na mamlaka ya mwisho, nani mtajaza jedwari wenyewe.

Kama tume ya Dr Mwakyembe ingelifuata haki ingelimwita Lowasa na kumuuliza kwanini aliyatenda yale aliyoyatenda. Lakini Lowasa hakupewa nafasi hata kidogo na pia tumeona hata alipojaribu kujieleza kwenye TV mara tu baada ya kujiuzulu kipindi kilitolewa hewani. Lowasa hana makosa huo ni ukweli usiofichika. Kwanini tume ya Mwakyembe iliacha kuanika kila kitu kama si kufichiana siri?.

Wakati umefika kwa Lowasa kupewa nafasi ya kujieleza ili tukaweza kuelewa nini hasa kinafichwa katika suala zima la Richmond.
Amebebeshwa au amejibebesha? Ni kweli kuwa Lowassa hakuitwa, lakini alipewa nafasi ya kuelezxa na akashindwa kufanya hivyo. Yet, aliamua kukaa kimya wakati wote huo hadi sasa, kwa nini?
 
Lowassa ni vema awe na ujasiri sasa kusema kitu kuhusu Richmond,alishindwa kusema wakati anajiuzulu na juzi Bungeni.Sasa akishindwa tena kujisafisha kwa uwazi na si kwa michezo michafu kwa wabaya wake,akishindwa sasa hata Ubunge ni vizuri ajiuzulu ili akachunge ng'ombe vizuri maana ni Mmeru aliyefundishwa ufugaji na wamasai Monduli.
 
Back
Top Bottom