Elections 2015 Lowassa: Serikali yangu itaangalia jinsi ya kuvunja mkataba wa bandari ya Bagamoyo


Itafika wakati wachina watatukalia kooni in such a way kwamba hatutaweza kuwaambia chochote.

The time is coming.
 

Ms[/QUOTE]
Mkuu umeandika sana lakini mwisho tuna rudi kwenye jibu nililotoa mapema leo hii ambalo sitalirudia. Ila kuna kipengele kimoja au viwili ambavyo umekuja navyo lazima ni viongelee.# Hata kama una shida kiasi gani usikubali mtu anaye taka kukupa msaada wa kukujengea nyumba kuleta masharti ya kulala na mkeo kwanza. Watu wana kuja hapa na miradi yao na kuwapangia watanzania masharti kwamba ni lazima wavune gus kwa miaka 10 bure ndipo waanze kulipa kodi. HAYA TUMEYAKATAA NA TUMECHOKA KUINGIA KWENYE MIRADI YENYE KUWEKA UNAFUU UPANDE MOJA WA ( wawekezaji ). Issue ya pili ni hii ya " SIO KOSA LA MRADI " Hapa sijakuelewa unataka kuzungumzia nini maana nisije kukanusha kitu au kukikubali pasipo kupata ufafanuzi. Ukiamka ni jibu hilo.
 
prizash,

..kwa uelewa wangu bandari ya Bagamoyo inajengwa kwa fedha za Wachina.

..wataimiliki bandari hiyo mpaka watakaporudisha fedha zao ndiyo itakuwa mali yetu.

..mimi tatizo langu na bandari ya Bagamoyo ni uwezekano wa bandari hiyo kuiua bandari ya Dsm. vilevile inaonekana hatujajipanga kuhakikisha tunafaidika na uwekezaji huo ambao ni mkubwa kufanyika hapa Tanzania.

..ningependa mamlaka yetu ya bandari iwe na significant amount of shares ktk mradi wa Bagamoyo ili tuweze kufaidika na mapato yanayotokana na bandari hiyo. pia kuna eneo la huduma kwa bandari hiyo mfano upakiaji na upakuaji ambayo inaweza kufanywa na mamlaka yetu ya bandari.

..pia tusisahau kwamba SEKTA YA USAFIRISHAJI itakuwa kwa kiasi kikubwa ikiwa mradi wa Bagamoyo port utakamilika. vilevile ukumbuke kwamba OMAN FUND wanawekeza ktk eneo la viwanda linalounganishwa na bandari hiyo. sasa hapo napo tujipange na siyo kuanza kuupinga mradi huu.

..kwa bandari ya TANGA, labda tungekuwa wabunifu kidogo kwa kuifanya iwe kituo kikuu cha kuteremsha MAFUTA nchini. vilevile Tanzania ipiganie bomba la MAFUTA toka UGANDA liishie katika bandari ya Tanga.


..kuhusu bandari ya MTWARA; eneo la kusini, pamoja na nyanda za juu kusini kuna miradi ya gesi, chuma, na makaa ya mawe, hivyo bandari hiyo inapaswa kuwa mahsusi kwa usafirishaji wa madini hayo, pamoja na bidhaa zitokanazo.

..MRADI WA BAGAMOYO TUSICHEZEE SHILINGI KTK TUNDU LA CHOO. WATU WAMEAMUA KUWEKEZA $10++ BILLIONS HALAFU TUNAWALETEA LONGOLONGO NA KUWATISHA?? TUANGALIE NI JINSI GANI TUNAWEZA KUFAIDIKA NA MRADI HUO NA SIO KUUPIGA VITA.


cc Kimweri, msemakweli, Bavaria, samurai, Jigsaw, Crimea
 
Last edited by a moderator:
Bandari ya Mtwara ni uti wa mgongo kwa mikoa ya kusini.Uchumi ungekuwa mara dufu katika biashara za kimikoa na nchi jirani kama Zambia na malawi na zingine. Tungepunguza kwa asilimia kubwa population ya wahamiaji walio kimbilia Dar. Kwa Tanga vile vile bandari hizo zingesaidia katika kusafirisha bidhaa za biashara kwa wakazi wa mikoa ya kaskazini na nchi jirani na kuondoa matabaka katika ukuaji wa uchumi kimikoa. Hii ya kujenga Bandari kubwa Bagamoyo imekaa kinafiki nafiki na kiushabiki wa kwamba mimi nimewafanya nini wakaazi wangu.Hatutaki vijana na ndugu zetu waendelee kujazana Dar es salaam na Bagamoyo.
 

Jigsaw usipumbazwe na wataka urais kwa hila yoyote, fuatilia katika mtandao mradi unaoitwa Mtwara Corridor ambao utkelezani wake umeanza. Unahusu miradi ya Umeme, Barbara, reli na bandari ya Mtwara, maalum kwa ajili ya uchumi wa Chuma (Mchuchuma, Liganga)
 
Aisee kanigusa sana. Halafu lowassa ana hekima sana. Kajiepusha ku msema ovyo jk. Yaani huyu ndugu ni muungwana sana. Ana bahati mbaya kuwa alikuwa na rafiki mnafiki
. Hilo jambo la bandari ya bagamoyo kama magu ni kidume alizungumaie

Ukweli ni kwamba bandari ya bagamoyo ni kitanzi cha tanzania. Tunaongeza deni la trl 10 kwenye deni la taifa la trl 40. Ni deni litakalowatesa hata vitukuu vyetu. Halafu ni mradi usiokua na umuhimu ukilinganisha na reli au angalau kuboresha bandari za tanga na mtwara.
 
Aisee kanigusa sana. Halafu lowassa ana hekima sana. Kajiepusha ku msema ovyo jk. Yaani huyu ndugu ni muungwana sana. Ana bahati mbaya kuwa alikuwa na rafiki mnafiki
. Hilo jambo la bandari ya bagamoyo kama magu ni kidume alizungumaie
Haya maneno mbona yanajirudia? Bampani naye kaandika hivi hivi (Ame-Paste maneno haya). Ni watu wawili tofauti au wewe!
 

Swali la kujiuliza, je, tulijipanga kuupokea huo mradi?

Tuliweka mazingira ya kuhakikisha huo mradi unanufaisha wananchi?

Kwa jinsi ninavyoona, huo mradi utaua bandari zote.

Tukianza na ya DSM na ya Tanga.

Bandari ya mtwara haiwezi kufufuliwa kwasababu hayo madini yatapitishwiwa hukohuko Bagamoyo.

Way Forward.

TPA imiliki 50% ya mradi ili kuweza ku-monitor shughuli za hapo bandarini.
 
Hili linashangaza Bandari ya Mtwara haikuuzwa kwa Dangote? Bagamoyo ni mradi wa JK, Watanzania wengi bado hawafahamu nini kinaendelea kwenye nchi yao. Inakuwaje miradi inapitishwa kabla ya kukubalika? Sasa hii ni vita kati ya JK na Mwizi Lowasa. Lakini kwa vyovyote vile huwezi kumchagua mwizi Lowasa then Mbowe ndio anakuwa anamwamrisha what type of a country that will be? Hata hivi sasa tunamshambulia JK combination ya Jambazi sugu na Mbowe ndio itaturudisha nyuma kwa miaka 1000. No chance kwa Jambazi Sugu or Mbowe and UKAWA et al.
 
Watu hawajaelewa why bandari ya Dar es Salaam haiwezi kutufikisha 50yrs to come! Na ndio sababu ya kujengwa bandari ya Bagamoyo!
Kama bandari haitaweza panuliwa mara2 ya pale ilivo na uchumi wa TZ uko Dar solution pekee n bandari ya bagamoyo ndo maana ikajengwa, of course JK amelazimishwa ijengwe mapema ila uhalisia unabaki pale pale kwa maendeleo ya haraka Dar inahitaji bandari kubwa zaidi
Lastly kama hamfaham tu! Bandari ya Bagamoyo inajengwa kussupoort viwanda 1000 vitakavyojengwa dar+pwani, ambapo bandar ya dar isingeweza kuhudimia export ya viwanda vyote hivo ndo maana ikajengwa hiyo specifically kwa ajili ya exportation
 


Jokakuu, unaendelea kurudia vitu vilevile, bila mpangilio maalum. Mwanasiasa huyo amesema anayotakiwa kusema apate kura. Hata wangelalamika jua kali anegsema anafikiria kulisogeza jua pembeni kidogo ili kusiwe na jua kali.


kuhusu matumizi ya badnari za TZ, yako obvious, tafuta mipango ya TPA usome. ukisoma hautaendelea kuandika vitu kama bagamoyo itauwa dar port, world bank isingetoa $600M hivi majuzi tu, kama ni bandari inayokuja kuuliwa., Jamani kama kitu hatuna exposure nacho tujaribu kusoma kwanza au kufanya utaifit kabla ya kuandika au kuchukua porojo za wanasiasa.
 
Kimweri,

..ndiyo maana nimeandika "kwa uelewa wangu"....

..baada ya kufanya utafiti nimetoka na hicho nilichoandika.

..kwa sababu inaelekea uko-exposed, umefanya utafiti, na una uelewa mpana kuhusu suala hili, labda ungetueleza mahusiano ya bandari ya Dsm na hii inayojengwa Bagamoyo yatakuwaje. Je, TPA wana hisa kiasi gani ktk mradi huu wa Bagamoyo? Vilevile TPA wana mamlaka gani na bandari ya Bagamoyo? Bandari ya Dsm itafaidika vipi na bandari ya Bagamoyo and vice versa?

..kuna mambo mengi sana hayaeleweki kuhusu hii bandari ya Bagamoyo. Tunaomba utusaidie kutupa mwanga na kutuelimisha kuhusu mradi huu.
 
Last edited by a moderator:
Leo mbona unamuunga mkono na mguu zito??
 
Aisee kanigusa sana. Halafu lowassa ana hekima
sana. Kajiepusha ku msema ovyo jk. Yaani huyu
ndugu ni muungwana sana. Ana bahati mbaya
kuwa alikuwa na rafiki mnafiki
. Hilo jambo la bandari ya bagamoyo kama magu
ni kidume alizungumaie
Hatimaye kafanya kama ulivyotaka, vipi sasa unaungana na zitto?
 
Unachukuliaje haya maamuzi ya kiongozi unaempondea sana, ya kuachana na huo mradi, naomba nikusikie ukimpongeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…