Lowassa Sema Sasa au Nyamaza Milele!

Lowassa Sema Sasa au Nyamaza Milele!

Mangisandy

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
2,644
Reaction score
2,273
Kwako EL, ulichofanyiwa ndicho tunachofanyiwa wanyonge nchi hii, Kila siku! TUMEKATWA majina yetu kwenye haki zetu za msingi, nyingi, Mara nyingi tu!

Sijui kama kweli Nyerere aliKUKATA kama ameacha usia uendelee KUKATWA kila siku, lakini hao wateule waliopewa jukumu la KUKATA, wanaKATA sana, tena bila huruma, mpaka wewe wamekuKATA??!!!

KUKATA kumesababisha tabaka, kuna WANAOKATA na WANAOKATWA, hili lipo wazi, lakini ninachosisitiza, TULIOKATWA tupo wengi, tabaka la WAKATAJI ni la wachache. Wewe mwenyewe EL ulikua MKATAJI, lakini bila huruma wametumia Kisu hicho hicho KUKUKATA, hata wewe!

Nina uhakika hata wewe ni mwanadamu kama mimi na maumivu ya KUKATWA, hasa kwako, yapo, yapo EL, maumivu ya KUKATWA na maswahiba wa karibu ni makubwa!

Lakini EL umefanya vyema kukaa kimya, ila inatosha sasa, sema neno. Amua moja, kubali KUKATWA, nenda kafanye mambo mengine, kama WAKATAJI wanavyotaka!

Au jiunge na walioKATWA, hata kama hutaingia ikulu, vunja na kufifisha makali ya KISU, kesho na keshokutwa ukumbukwe kwamba uliukana huo mfumo wa ukataji wenye masilahi na kulinda masilahi hayo ya wachache!

Au Kaa kimya ukumbukwe na wajukuu zako kwamba uliKATWA ukakubali! I challenge you mr. EL; SEMA SASA AU NYAMAZA MILELE!
 
Mbona wengi wamekatwa! Walikuwa watu 38 na wamekatwa 32. Sasa mbona kama ni watetezi wa haki hamuwasemii na wengine! Kila mtu akilazimisha mtu wake kupitishwa mbona hatutafika!
 
Mbona wengi wamekatwa! Walikuwa watu 38 na wamekatwa 32. Sasa mbona kama ni watetezi wa haki hamuwasemii na wengine! Kila mtu akilazimisha mtu wake kupitishwa mbona hatutafika!
Ni kweli, lakini hapa nimemzungumzia EL kama EL! Ukiangalia vizuri katika wote waliokatwa EL ana hali tofauti kidogo, ule uswahiba, zile pesa na mengine mengine, najua unaelewa, between the lines, kama ni mfuatiliaji wa mambo!
 
Mbona wengi wamekatwa! Walikuwa watu 38 na wamekatwa 32. Sasa mbona kama ni watetezi wa haki hamuwasemii na wengine! Kila mtu akilazimisha mtu wake kupitishwa mbona hatutafika!

wengine wamezoea kukatwa,wanapenda kukatwa,hawaoni shida kukatwa,walitarajia kukatwa....hayo yote hayafanyi basi wote kwa asilimia mia moja wakubali kukatwa!aliyekatwa na akapiga kimya shauri yake,yeye kachagua kuchukia kukatwa!
 
Ni kweli, lakini hapa nimemzungumzia EL kama EL! Ukiangalia vizuri katika wote waliokatwa EL ana hali tofauti kidogo, ule uswahiba, zile pesa na mengine mengine, najua unaelewa, between the lines, kama ni mfuatiliaji wa mambo!

Mi ni mfuatiliaji sana
Lowasa katumia pesa kuaminisha watu kwamba anapendwa. Ametumia media na kutumia uelewa mdogo wa watz wanaoamini vyombo vya habari kama msahafu/biblia. Hilo ndo linaleta tatizo lakini anazidiwa na wengine waliokatwa.
 
wengine wamezoea kukatwa,wanapenda kukatwa,hawaoni shida kukatwa,walitarajia kukatwa....hayo yote hayafanyi basi wote kwa asilimia mia moja wakubali kukatwa!aliyekatwa na akapiga kimya shauri yake,yeye kachagua kuchukua kukatwa!

siyo hivo. Lowasa analazimisha mambo na hao wajumbe wa CCM wameongwa na wengine kuahidiwa vyeo. Hakuna lolote na ni bora amekatwa. Hii watu watasema itapita na Lowasa hawezi fanya lolote nje ya CCM. Stay tuned utaniambia!
 
Mi ni mfuatiliaji sana
Lowasa katumia pesa kuaminisha watu kwamba anapendwa. Ametumia media na kutumia uelewa mdogo wa watz wanaoamini vyombo vya habari kama msahafu/biblia. Hilo ndo linaleta tatizo lakini anazidiwa na wengine waliokatwa.

Bila shaka yo yote wewe ndiye mwenye uelewa mdogo!

Sisi tunaoelewa tunajua kanuni za kuteua mgombea wa CCM zimekiukwa tena kwa kudhamiria na si bahati mbaya!
 
Bila shaka yo yote wewe ndiye mwenye uelewa mdogo!

Sisi tunaoelewa tunajua kanuni za kuteua mgombea wa CCM zimekiukwa tena kwa kudhamiria na si bahati mbaya!

Wanaolalamika nyote mlishapata mshiko. Na ndiyo maana jina lake halikutoka kwenye maadili. nyinyi endelea ila tu ifikapo oktoba mtakubali matokeo tu.
 
Huna hoja jinga wee!!
Akili yako inafikiria mshiko tu, wataku-tigolise mtoto wa kiume!!

Huyu mtu mwenyewe mgonjwa lakini watu mmekazania Lowasa. Nyie ndo hamna uzalendo na nchi hii. Kuba watu wengi wa kuweza kuongoza Tanzania. Msitake kutuaminisha kwamba bila Lowasa nchi haitakwenda.
 
Mi ni mfuatiliaji sana
Lowasa katumia pesa kuaminisha watu kwamba anapendwa. Ametumia media na kutumia uelewa mdogo wa watz wanaoamini vyombo vya habari kama msahafu/biblia. Hilo ndo linaleta tatizo lakini anazidiwa na wengine waliokatwa.
Labda kuna ukweli, lakini, mbona mimi sijala hela zake na naona hajatendewa haki? Labda huoni uwezekano wa EL nje ya CCM, lakini hata hili wazo la kufikiria uwezekano tu wa yeye kuondoka CCM, ilikua ngumu kuwa nalo siku za nyuma! Ninachozungumzia ni kile kile alichowai kutabiri Nyerere! Labda huoni lakini CCM wameondoka kwenye kuwa miungu watu wamekuwa "zimwi" limekula watu, limekula watoto wake na juzi limekula mkia wake lenyewe, kama EL asiposhiriki kuliua, litakufa tu!!
 
Huyu mtu mwenyewe mgonjwa lakini watu mmekazania Lowasa. Nyie ndo hamna uzalendo na nchi hii. Kuba watu wengi wa kuweza kuongoza Tanzania. Msitake kutuaminisha kwamba bila Lowasa nchi haitakwenda.
Ugonjwa anaweza kuugua mtu yoyote ndugu yangu, usimnyanyapaye EL, mkatae kwa hoja nyingine maana hata mtia nia wa kundi lako hujampima na hujui kesho ataugua nini.
 
Natamani Pinda, Bilal na Sitta wafanye collabo ya kichinichini kuwamaliza CCM. Aibu waliyopata Pinda na Bilal haisameheki.Pamoja na udhaifu wao, ni bora mkwere angewatonya mapema kwamba nyie achaneni na hii kitu maana hamtoshi!
 
uwazi utatuweka huru.hizo sababu za kukatwa zingesemwa tu.mambo ya kusema mwenyekiti anajua sababu ni aibu.ni zama nyingine sasa.chama ni taasisi na sio mwenyekiti.na pili italeta picha kwamba m/kiti kashinikiza.sio sawa
 
Natamani Pinda, Bilal na Sitta wafanye collabo ya kichinichini kuwamaliza CCM. Aibu waliyopata Pinda na Bilal haisameheki.Pamoja na udhaifu wao, ni bora mkwere angewatonya mapema kwamba nyie achaneni na hii kitu maana hamtoshi!

mzee pinda ... yaani pm akose 5 bora,!!!tujifunze jambo hapo.
 
Hata akisema hamna mabadiliko yatakayofanywa... Kwa usalama na heshima yake bora anyamaze milele
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom