Lowassa ndani ya Monduli, ajiandikisha BVR

Lowassa ndani ya Monduli, ajiandikisha BVR

Wanaosema Lowassa ni fisadi ni nyie Chadema unakumbuka Dr.Slaa orodha yake ya mafisadi Lowassa yupo.

CCM wamemkata Lowassa siyo sababu ya ufisadi wamekatwa wengi tu na wana CCM wenyewe wakamchagua Dr.Magufuli.
Lowassa hakutajwa.
 
Makofuli kama atafanikiwa kuchaguliwa kuwa rais basi atakuwa pale kama sanamu tu kwani kuna remote ya kumuelekeza nini cha kufanya.

JPM atawanyoosha walala hoi tu, ma Don waliomuweka pale lazma awasikilize matakwa yao unlike Lowassa on my understanding on the whole game ana nguvu na uwezo sanaa inakua ngumu kuyumbishwa.
It made me agree he was the right material.
 
Kitendo cha kamati ya maadili na nidhamu kupeleka majina matano tu kwa kamati kuu, hakikuwa cha bahati mbaya bali kilifanyika kwa makusudi. Madhara yake waliyafahamu yakiwemo ya wajumbe wa kamati kuu kulalamika na hata sintofahamu ya wajumbe wa NEC na mkutano mkuu. Aidha, hekaheka zinazoendelea za kumtaka EL ahamie vyama vya upinzani zinafahamika kabisa kwa magwiji wa siasa wa CCM. Hivyo, sidhani kama CCM imekaa tu bila kuweka mikakati ya kufanikisha nia yake ya kumkata. Kwa msingi huo, iwapo EL ataamua kuihama CCM atakuwa amejimaliza kabisa kisiasa kwani itaonekana si mwaminifu bali msaka Urais kwa gharama yoyote. CCM wataitumia turufu hiyo kummaliza yeye na hicho chama kitakachompokea. Kwa hali ilivyo, ashauriwe kutulia CCM na ikiwezekana amuunge mkono mgombea wa CCM. Hili litamjengea heshima kubwa zaidi ya hiyo aliyonayo kwa sasa. Mchakato wa kumpata mgombea wa CCM unalo la kutufundisha.
 
Afanye hivyo, make anaweza kukosa haki yake ya msingi na kikatiba, akamilishe hilo swala, hayo mengine baadae
 
Kitendo cha kamati ya maadili na nidhamu kupeleka majina matano tu kwa kamati kuu, hakikuwa cha bahati mbaya bali kilifanyika kwa makusudi. Madhara yake waliyafahamu yakiwemo ya wajumbe wa kamati kuu kulalamika na hata sintofahamu ya wajumbe wa NEC na mkutano mkuu. Aidha, hekaheka zinazoendelea za kumtaka EL ahamie vyama vya upinzani zinafahamika kabisa kwa magwiji wa siasa wa CCM. Hivyo, sidhani kama CCM imekaa tu bila kuweka mikakati ya kufanikisha nia yake ya kumkata. Kwa msingi huo, iwapo EL ataamua kuihama CCM atakuwa amejimaliza kabisa kisiasa kwani itaonekana si mwaminifu bali msaka Urais kwa gharama yoyote. CCM wataitumia turufu hiyo kummaliza yeye na hicho chama kitakachompokea. Kwa hali ilivyo, ashauriwe kutulia CCM na ikiwezekana amuunge mkono mgombea wa CCM. Hili litamjengea heshima kubwa zaidi ya hiyo aliyonayo kwa sasa. Mchakato wa kumpata mgombea wa CCM unalo la kutufundisha.

Weka sawa analysis yako pale unaposema CCM watatumia turufu hiyo kumumaliza! Kwani kile kilichotokea kwenye chama chake si walishammaliza! Halafu haya mambo ya kuogopaogopa CCM mnakuwa kama watoto wadogo kwa nini? CCM ni watu yaani binadamu tu hawana umungu wowote! EL anaweza amua anavyoona inafaa na hata hivyo hana cha kupoteza tena kwenye masuala ya kisiasa labda agombee ubunge !
 
samahani kuuliza si ujinga hawa ni wapambe au mabodigadi

au ndo wafadhili; naona miili yao imeiva; imekuwaje kutoka uwanja wa ndege bila kuongea na Radio yake Radio 5
IS IT TRUE

attachment.php

Hiyo ni full PSU ya mheshimiwa japokuwa si prezidaaaaa!
 
Weka sawa analysis yako pale unaposema CCM watatumia turufu hiyo kumumaliza! Kwani kile kilichotokea kwenye chama chake si walishammaliza! Halafu haya mambo ya kuogopaogopa CCM mnakuwa kama watoto wadogo kwa nini? CCM ni watu yaani binadamu tu hawana umungu wowote! EL anaweza amua anavyoona inafaa na hata hivyo hana cha kupoteza tena kwenye masuala ya kisiasa labda agombee ubunge !

Afadhali na we umeliona hilo!
 
Japo siamini kwamba Lowasa ana ujasiri kama wa JK,Nape ,Makonda na Kinana walioonyesha wazi ujasiri wa kumkataa Lowasa asiingie hata 5 bora lakini naona ni muhimu sasa akaonyesha ujasiri wake na maamuzi magumu kwa ama kujitoa kabisa kwenye siasa za Tanzania na kubaki kama mbunge mstaafu au kujiunga na vyama vya upinzani.

Kama kweli Lowasa ana nia ya dhati ya kuijenga nchi na sio kubomoa na anaamini na kutuhakikishia kuwa tuhuma alizo nazo ni za kupangwa kwa chuki za kikundi cha watu wachache kwa faida binafsi basi huu ndio wakati wake muhimu katika maisha yake kujitoa CCM ,chama alichokitumikia kwa juhudi zake zote lakini hakikumthamini kabisa.

Kama Lowasa ataendelea kukijenga chama cha mapinduzi ajue wazi kuwa endapo wabunge wa CCM na makada waliomuunga mkono watashindwa kupenya kwenye uwakilishi wa majimbo ndani ya CCM na wakati huo huo CCM ikaendelea kupata uwakilishi wa wabunge wengi bungeni ataishi kwenye hii nchi kwa machungu makubwa sana kwani atazidi kupuuzwa ndani ya chama chake bila mtu wa kumtetea.
Lowasa ajifunze toka kwa Warioba. CCM ndiyo iliyomtukana na kumdhalilisha Mzee warioba kwa nguvu zote mpaka kufikia hatua ya kuwaangalia vijana wadogo wamtukane na kumpiga makofi hadharani bila aibu. Chaa ajabu UKAWA ndio waliojitolea kusimama na wananchi na kumtetea Warioba kwa nguvu zote.

Kupitia mzee warioba ni vyema Lowasa akajifunza kuwa CCM inaendeshwa na kikundi cha watu wachachi na kupuuza mahitaji ya wananchi wengi kama walivyopuuza na kukata jina lake japo yeye ndio alikua anakubalika ndani na nje ya chama.

Kwa sasa CCM sio rafiki kabisa wa Lowasa. Na wala asijidanganye.
Ni bora atafute chama kingine hata kama ni Chama kidogo ili apate wabunge hata 50 wa kusimama imara bungeni ili kutetea demokrasia ya kweli kwenye nchi yetu.
Nchi hii haina demokrasia ya kweli zaidi ya fitina za kuwagawa watanzania kwa maslahi ya watu wachache.

Kwa umri wa Lowasa alionao ni bora akajakukumbukwa kwa kuiangusha CCM na kuimarisha demokrasia kuliko kuendelea kukaa ndani ya CCM.Je,ni lipi ambalo CCM watamkumbuka nalo Mh. Lowasa zaidi ya kumwita mwizi,mchafu,mnuka rushwa na gamba?
Je,kama rafiki yake aliyempigania mpaka akaingia ikulu amemtendea hivyo itakuaje chini ya serikali ya CCM itakayokuja ambayo usiku na mchana imekua ikimwombea mpaka umauti.?CCM ni chama ambacho mchana na usiku kinachukizwa kuona afya ya Lowasa inaimarika.
Je,usalama wa Lowasa ndani ya CCM utakuaeje endapo atabakia kuwa kada anayekubalika kuliko rais wake atakayetawala kwa miaka mitano huku akiendelea kubanwa na chama na kushindwa kuwaletea maendeleo bora wananchi na umma ukaonyesha kwamba bado unamuhitaji Lowasa?. Je,rais wake na mwenyekiti wake atakubali kumwona Lowasa anaendelea kukubalika kwenye utawala wa miaka mitano ya mwanzo?
Je, Lowasa na kundi lake lenye vijana machachari kama Husein Bashe na Wengine hawaoni umuhimu wa kujitoa na kuimarisha upinzani na hata ikiwezekana kukifanya CCM kuwa chama cha upinzani ili kuweka uwanja mpana wa demokrasia na kuondoa hulka ya kutishana na hata kutoana kucha kwa sababu tu ya kung'ang'ania madaraka ndani ya CCM huku wote wakiwa na madoa yanayofanana ya ufisadi lakini tofauti ikiwa ni nani anayelinda maslahi ya kakundi kadogo kanakotawala?
Nani asiyejua kuwa kuuza nyumba za serikali ulikua ni ufisadi mkubwa na mbaya kuliko ufisadi wowote uliowahi kutokea Duniani lakini aliyefanya ufisadi huyo anapigiwa debe ili akauze na nchi na bahari yote kabisa?
Hivi ni kweli kuwa hata dhamira ya mtu haihukumu kuwa kuuza nyumba za umma ni kuuza urithi wa watanzania kwa watu wachache tena kwa bei ya kutupa?

Je,mtu aliyeuza nyumba za serikali akiingia ikulu muda wake ukiisha na kuamua kujiuzia Ikulu kwa kisingizio kuwa ni jengo la kizamani na kuwa itajengwa nyingine Dodoma patakua na mtu wa kumzuia?

Je,ni kwa nini serikali ilishindwa kujenga nyumba zingine kwenye maeneo hayo ya zamani yaliyokuwa na nafasi ya kutosha na badala yake mpaka leo hatuoni nyumba mpya za viongozi kila mkoa na wilaya walipouza zile nyumba za zamani?

Mh. Lowasa sasa atimize ndoto yake ya matumaini kwa kupitia chama cha upinzani kura za wananchi zitampeleka ikulu. Sio kwamba Lowasa anaenda msituni kupigana vita ili apate madaraka bali anatumia demokrasia na uhuru wa kikatiba kutimiza ndoto yake.

Kama mtambo wa richmond wataudai basi ni wazi kuwa Lowasa atawadai nyumba 8000 za umma walizopora na ushahidi bado upo wazi kwa sababu wanazimiliki.
Kwa hilo wananchi tutamuunga mkono na kumpigia kura.

Kuna watu wa ajabu wanaomtishia kuwa akijiunga na upinzani atapoteza haki zake kama waziri mkuu mstaafu. Huu ni upuuzi tu kwa sababu Uwaziri mkuu ni nafasi ya kiserikali na ni nafasi ya kuwatumikia watanzania wote bila kujali vyama vyao. Maslahi anayolipwa sio ya CCM bali ni ya umma na ni kodi ya watanzania.
Kama haki yake ipo italindwa na sheria na sio chama cha mapinduzi .
Ni wakati sasa wa kukomesha dhulma na vitisho kwa kuwachagua wabunge wengi toka upinzani ili kulinda haki za kikatiba za kila mwananchi bila kujali chama.

Lowasa sasa atakumbukwa kwa jambo jema moja tu ,la kujitoa CCM na kuimarisha demokrasia kwa ama kupeleka wabunge wengi zaidi wa upinzani ili kupigania haki za kijamii,kiuchumi na kisiasa au kukifanya chama cha mapinduzi kuwa chama kikuu cha upinzani kufikia octoba 2015.
 
Wanaosema Lowassa ni fisadi ni nyie Chadema unakumbuka Dr.Slaa orodha yake ya mafisadi Lowassa yupo.

CCM wamemkata Lowassa siyo sababu ya ufisadi wamekatwa wengi tu na wana CCM wenyewe wakamchagua Dr.Magufuli.

Hivi ile kamati ambayo ilikuwa ikiongozwa na Mwkyembe,ambao ndo wakihitumisha kuwa el ajipime,ni cdm?
 
Safari hii tunataka apatikane rais atakayeingia ikulu bila matumizi makubwa ya hela.

Wanaotumia hela nyingi kuingia ikulu wanafanya madudu kurudisha hela zao na za wapambe wao

Ccm wote wanatumia pesa,BT kwa kiwango tofauti
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom