Lowassa, Nchi ilipokuwa njiapanda kwanini ulikaa kimya?

Lowassa, Nchi ilipokuwa njiapanda kwanini ulikaa kimya?

Rushwa hupofusha, Mungu atatuepusha na mafisadi. Baba yake Mako aliona mbali sana
 
Mtoa post nafikiri bado uelewi bado utaratibu wa bungeni.Nadhani unasahau CCM as a party kilichukua a collective cohesive decision ya kuunga mkono katiba pendekezi na Mh hasingeweza kwenda kinyume na msimamo wa chama chake. Mtendaji mkuu wa shughuli za kibunge ni Prime minister, sasa ulitaka aingilie mamlaka ambayo sio yake?

Tunataka majibu hapa kwa nini alikaa kimya kwenye escrow? Achana na katiba mpya inajulikana alipiga kura ya wazi yeye ni serikali 2. Huu ububu ni udhaifu mkubwa sana.

Pia asiwadanganye vijana kwamba atawapa ajira muongo mkubwa huyu, atawapa ajira anaviwanda vyake ulaya au china? Tuseme ukweli tusidanganyane.

Tunataka rais atakae kemea rushwa na kusimamia rasilimali zetu na kukuza uchumi. Lowassa wambia ukweli vijana wa vyuo vikuu wasome wapate elimu ili watumia elimu yao kubuni ajira kama anavyofanya Dr mengi.

Kama uwezo wa kuwapa ajira vijana unao, ulishindwa nini kumaliza madeni ya walimu ukiwa Waziri mkuu? Wito wangu kwa vijana msidanganyike na huyu msaka urais kwa pesa bali someni na kujikita kufanya tafiti za kijasiliamali ili mjiajiri wenyewe. Atakae bahatika akaajiriwa na serikali amshukuru Mungu.
 
alishasema yeye siyo mtu wa kusema sema sana ni vitendo tu! ulitaka afanye nn wakat hayupo kwenye mamlaka ya uamuz maswal hayo waulize akina pinda , makamba, mwigulu na membe walioko kwenye kabinet hapo lowasa unamuonea bure! waulize hao washaur wa rais!

issue alisema nini sio alifanya nini
 
Suala la Mbunge kuchangia siyo lazma aongee anaweza kuchangia kwa kuandika

Pia lazima ujue Edward alikuwa Waziri mkuu na anaheshima yke ktk serikali, kiutaratibu mtu kama yeye hufuatwa na wahusika ktk kutoa mawazo yke ..

Pia Lowassa si mtu wa kukurupuka ktk kufanya mambo na maamuzi hivyo apelekeshwi na upepo km wafanyavyo wanasiasa uchwara
 
alishasema yeye siyo mtu wa kusema sema sana ni vitendo tu! ulitaka afanye nn wakat hayupo kwenye mamlaka ya uamuz maswal hayo waulize akina pinda , makamba, mwigulu na membe walioko kwenye kabinet hapo lowasa unamuonea bure! waulize hao washaur wa rais!

Ona sasa Zigo umewatika akina Mwigulu, haya basi yeye kama akiwa PM alifanya kitendo gani kutuokoa watz na mkataba wa kitapeli wa Richmond?
 
Uwe unaongea kwa facts sio unaongea tu ili kumchafua mtu kisa hana mpinzani nafikiri unapomtuhum mtu lazima achukuliwe hatua sa sijawahi sikia mh kama kweli alichukuliwa hatua za kisheria hii inanifanya niamini kuwa lowasa hana kosa coz angelikuwa ameshiriki hao waliomtaja wangemchukulia hatua,,,,tuacheni siasa na chuki za vijiweni hebu tuwe na utaratibu wa kufuatilia mambo na sio kudanganywa na wanasiasa

kwaiyo Chenge hajawai kuiba maana hakushitakiwa?'lowasa ni mwizi kama vibaka wengine
 
Tusipoteze muda wa kuchangia baadhi ya post za kijinga ...

Tuleteeni hoja zenye maana zinazogusa mustakabali wa taifa cyo kuleta ----- km hii thread
 
Chademakwanza

sera ni siasa na siasa ni mikakati ambayo usipokuwa makini inaweza ikakurudi. Lowassa ni mwanasiasa mashuhuli na mkongwe katika siasa za Tanzania sababu iliyompelekea kuwa na ndoto ya kuwania urais hivyo kauli na matendo yake ni lazima viwe na baadhi ya miiko kisiasa hasa katika safari yake. katiba ni sawa na sera hivyo ni lazima kuwe na mvutano katika kufikia muafaka kwani ni lazima utambue ya kuwa kuna pande tofauti tofauti zenye malengo tofauti, umuhimu na nguvu tofauti katika kufanikisha malengo yao na siku zote lazima kuwe na washindi na washindwa japo pia huwa kunakuwa na kaharufu kadogo ka (win-win) japo hata siku moja haiwezi ikawa sawa.

rejea michango yake katika kuzungumzia ajira, elimu na utendaji serikalini mambo ambayo yana ustawi katika taifa letu na sio kutafuta udhaifu mmoja ambao nao hatuna uhakika yawezekana pengine alichangia mawazo na maoni yake kwa nijia ya maandishi kwani pia ni namna mojawapo ya kuchangia bungeni na sio lazima kila kitu mtu aongee. Jana mlisema wakimsimamisha Lowassa mnapata ushindi kabla ya ibada ya kwanza, leo hii ndio mnaweweseka kuona ana nafasi kubwa ya kupokea kijiti na ndio maana mnadunduliza hoja mfu kutaka kumkwamisha. ashawaambia hafikirii kushindwa khaaaa!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Lowasa ni jipu, ukitumbua vibaya utachafuka wewe, linahitaji timing sana
 
Wewe ndiyo hujui lolote kuhusu haya maswala, yaani wewe ndiye utakaeenda kuchunga ng'ombe mwezi wa kumi wakati Lowassa aneyoyoma kwenda Ikuyu, utaelewa tuuuuu

Let us wait and see!
 
Aliahidi ataleta mvua ya kutengeneza. Baada ya Richmond Mbunge wa Monduli hats huko kwao haikuonekana
 
Chademakwanza

Mimi najiulizaga kwa nini yeye mwenyewe hakuweka ushahidi bungeni wa kusingiziwa kama kina Mwakyembe waliupuuza? kama yeye mwenyewe aliuona feki iweje awabebeshe wengine kupeleka upuuzi bungeni???
 
Last edited by a moderator:
Chademakwanza

Nchi yetu haijawahi kuwa njia panda labda kipindi kile cha Nyerere walivyotaka kumpindua.
 
Last edited by a moderator:
Wanataka tuamini kuwa aliamuwa kuwaachia uPM. Kwa nini hakujibu hoja bungeni. Kwa nini mpaka sasa hajibu?
 
Umeongea ukweli mtupu tatizo nchi wajinga wengi hawatumii akili zao kumpima mtu kazi yao kubwa ni kufuata mkumbo tu.

Huyu mtu bungeni alikuwa ni bure kabisaa!Huu ni ushahidi kuwa anashindwa kukemea ufisadi kwasabu amelalia blanketi zito la tuhuma za ufisadi.
 
Acha kumsakama baba wa watu, kwani amekufanya nini?

1. Hiyo njia panda unayoisema aiongelee kwani yeye ni msemaji wa srikali?

2. Kwanini Lowasa tu, vipi Msuya, Sumaye, Warioba, Salim wao wapo kundi lipi? Maana Warioba aliongea mawazo yake tofauti na "zidumu fikra" alinaswa vibao na makonda na akaambiwa kajitakia.

3. Lowassa alishaongelea au kutia neno juu ya mgogoro na Malawi, akaonyesha upande.....fasta akashambuliwa na viongozi waandamizi kila kona kwakuwa tu ana mawazo mbadala! Sasa hayo uliyo yaorodhesha, endapo angetoa neno tofauti na wanachotaka kusikia "wakuu" unadhani wangemfanyaje?

4. Wewe hujiulizi, ni kwanini kuna nguvu nyingi sana kuliko kawaida inatumika kumzuia yeye asiwe rais ukijijumlisha na wewe, hii inatokana na ukweli kuwa.....maswali yoote ulijiuliza na ukimya woote unaodhani anao......wanaogopa akiwa rais watashaaa! Anajua Bdalali wa BoTii wapi yupo.....(Lowasa akiwa rais, atafufuka). Anajua waliokwapua Escrow na mwenyewe hasa mwenye Rihchimondul, akiwa rais kila kitu kitakuwa wazi........kwahiyo, nani anataka Lowasa awe rais ili aharibu maslahi yao?

5. Wanamwita fisadi. ndio maana hafai kuwa rais........swali, je nani ni msafi ccm kumpita lowas? Infact, jinsi mnavyomchafua, ndio mnampa promo hata tuliokuwa hatumpendi tunaanza kumkubali sasa!

Hivyo basi;-
Mitume woote waliokuja hapa duniani, walikuja kwa ajili ya kuwakomboa wakosefu ili tumrejee Mnyaaazi Mungu kwa kuacha mabaya. Hivyo basi, what if Lowasa kaamua kutubu yoote aliyotukosea watanzania na akaamua agombee urais kwa ajili ya kuyalipa makosa yake?
 
Back
Top Bottom