Lowassa na Kiingereza chake!

Lowassa na Kiingereza chake!

Kiingereza anafahamu kwa kiasi chake,ila si muhimu sana. Je,ulishawqahi kumshuhudia Rais HU Jintao wa china akiongea kiingereza?

Na wewe umekulupuka,ebu soma post za juu!!swali lako tayari lishajibiwa.
 
Usitake kuyeyusha hapa. Ukiamua kuwa kiongozi ni lazima uhakikishe kwamba una-meet standard inayotarajiwa kwa kiongozi, vinginevyo tutakuwa na viongozi vihiyo kwa kisingizio cha kwamba mimi siyo Cameron. Jamaa kasoma na ana Master's degree. Hana kisingizio cha kushindwa kujua lugha kwa ufasaha na kuelewa mambo. Kama hayo yanamshinda hatufai hata kidogo!
Kwani kiingereza ni moja ya standards anazotakiwa kuwa nazo kiongozi? Nadhani hii ni mindset mbovu ya watanzania na ndo maana kila wakisikia mtu anaongea kiingereza wanafikiri ana elimu. ukienda kwenye nchi ambazo sio anglophone utaona kuwa viongozi sawa na raia wao hawajui kiingereza au wanaongea kiingereza cha ovyo mno utafikiri ni wanafunzi wa shule za kata Tanzania lakini mambo yao yako very smart.
 
Hujui tofaui ya wachina na sisi? Wachina hawajawahi kusoma kiingereza maisha yao yote na kwa population yao, lugha yao ni miongoni mwa lugha kuu za duniani. Huyu bwana kapita shule lakini 'kidhungu' cha magumashi. Halafu hapa pia kuna suala la hotuba kukosa mvuto na maneno ya maana na yenye mpangilio. Je hilo nalo unalisemaje kwa wachina? Msaidieni mtu wenu. Hajachelewa, aende angalau british council.
Nani kakudanganya kuwa wachina hawajawahi kusoma kiingereza? Wachina sasa hivi wanasoma kiingereza kwa kasi mno kuliko sie tunaobabaisha shule. Kule kuna english medium na chinese medium shools. Zamani mtu ukienda kusoma china lazima uwe na mwaka wa kusoma kichina lakini siku hizi watu wanasoma china mpaka wanaondoka china hawajui kuandika kichina. Tofauti kati yetu na wachina ni kuwa wachina wana determination wanajua kwanini wanasoma kiingereza, serikali yao pamoja na kupromoti kiingereza kwa kiasi fulani lakini imedhibiti kabisa matumizi ya kiingereza ktk ofisi za serikali zisizowahusu wageni. Serikali yetu inaruhusu matumizi ya kiingereza hata mahali ambapo ofisi zinawahusu waswahili watupu.
 
ni kweli kabisa hata mimi nimemuelewa!ila nilitaka mumuone akiongea kiingereza...

kwani ulikuwa hujamwona? Sisi tulishamwona mara nyingi jamaa ana uwezo tu mzuri wa kuongea kidhungu na kujenga hoja mjarabu kama wengi wetu walivyochangia hapa jukwaani harafu usipinge swala la uraisi limeappear kwenye post yako unnecessarily isome tena utaliona vizuri
 
Anajua KIMASAI ,KIMERU NA KISWAHILI PIA NAWEZA KUSALIMIA KIARUSHA NA KICHAGA KIINGEREZA CHA NINI mbona Putin hajui
 
daaah. yan great thinkers mnadiscuss kiongozi wa tanzania kujua au kutokujua kiingereza? english itakusaidia nini wakat lugha yako ni kiswahili? mbona viongozi kibao wa china hawajui kiingereza.
 
daaah. yan great thinkers mnadiscuss kiongozi wa tanzania kujua au kutokujua kiingereza? english itakusaidia nini wakat lugha yako ni kiswahili? mbona viongozi kibao wa china hawajui kiingereza.
Mdau kwenye mikutano ya kimataifa ataongea kimasai au? Badala ya kumpenda kupita kupita kiasi na kutetea ujinga ni vema mngemshauri akajifunza hiyo lugha vizuri,mbona diamond platnumz now anakiongea vizuri tu na hajasoma uingereza kama lowassa
 
nimekumbuka wakati wa ujio wa Obama wakati wakiwa Magogoni, Kikwete aliulizwa swali na mwanahabari wa Uingereza daaaaah......!!
 
Alafu pole pole naanza kumuelewa Lowasa.

Ni mtu anayejiamini na anafanya anachokisema huyu ndie kiongozi tunayemtaka kwa sasa
 
kwani hapa tupo mashindano ya umiss. kingereza hata diamond amejifunza na kujua.
 
Mdau umewahi kumsikia Lowassa akizungumza kiingereza????hebu mtazame hapa rais wetu huyu mpya halafu just imagine siku yuko cnn anahojiwa na Larry King na hivi vingereza vya kuandika kwanza then kukariri



Lowassa ana kiingereza kizuri sana tu,kumbuka marafiki zake wote ni watu modern na hakuna waswahili-swahili mle,usisahau shahada yake ya uzamili ameifanya huko huko kwa Waingereza wenyewe!
 
Last edited by a moderator:
Kwa mtu aliesomea uingereza kwa kiwango cha shahada kwa kiingereza hiki hapana,hata kama tunampenda hii hapana.Je akikumbana na maswali ataweza kutiririka huyu kama hiki cha kuandikiwa na kukariri tu anajikakamua namna hii,I miss mzee mkapa.
 
Mi nlidhan hawez zungumza kiswahili... well...kiingereza anachozungumza hakina tatizo at all kama ni matamshi nenda kamsikilize andrew chenge msomi wa harvard university. na pia njoo umsikilize padre wetu akizungumza kiswahili utagundua pia naye ana makosa mengi tu. so wala hii si issue ya msing kwenye kujenga taifa. safari hii hatutaki kiongoz msanii sanii... tunataka kiongozi makini.
 
na mtanzania ajuae kiingereza na asimame? rais wa msumbiji alikuja hapa aliongea kiingereza??..kiingereza kinaleta nn kwa nchi?? hatuchagui kiongoz akaongee CNN,
 
Lugha ni kwa ajiri ya kuwasiliana,sasa suala la kujua sana lugha hilo ni suala lengine kabisa,na ndiyo maana hata sie tunajua kuwa wengi hatujui kiswahili fasaha lakini hakuna ambaye amewahi kufikiri et akasome kiswahili ili aje kuongea kiswahili fasaha. Hata hizo nchi zenye kuongeo kiingereza pia si kwamba wote huongea kiingereza fasaha. Cha muhimu ni kuongea na kuelewana.
 
Nawashangaa wachina wanaongozwaje na kiongozi asiyejua kiingereza.

Pia wajapani, wakorea, (korea kaskazini ndyo kabisa hata cha kusalimia hawawezi lakini wana makombora ya nuclear)
Rais wa Mozambique alipotutembelea TZ aliongea kwa Kireno, ingawa anauwezo wa kuongea kiswahili na Kingereza cha kueleweka.
 
Kwani kiingereza ni moja ya standards anazotakiwa kuwa nazo kiongozi? Nadhani hii ni mindset mbovu ya watanzania na ndo maana kila wakisikia mtu anaongea kiingereza wanafikiri ana elimu. ukienda kwenye nchi ambazo sio anglophone utaona kuwa viongozi sawa na raia wao hawajui kiingereza au wanaongea kiingereza cha ovyo mno utafikiri ni wanafunzi wa shule za kata Tanzania lakini mambo yao yako very smart.

Ukweli ndugu tuna safari ndefu kuelewa aina ya kiongozi tunaemhitaji kama taifa! Tusipobadilisha namna yetu ya kufikiri safari ni safari ndefu! Kuzungumza kiingereza siyo kuwa wewe ni msomi au ndiyo elimu !! ???Binafsi nmemsikia Kikwete mara nyingi anazungumza, mbona hana tofauti na watanzania wengine! Tukubali tukatae kiingereza ni lugha ngeni kwetu sisi sote watanzania ! Nafikiri tungetaka kusikia Lowassa anataka kulifanyia nn taifa hili kiuchumi, kijamii na maendeleo ya nchi kwa ujumla wake! mpango mkakati wake wa kuinua hali taabani za watanzania! NI IMANI YANGU KWAMBA LOWASSA ANAZUNGUMZA KIINGEREZA KIZURI KINACHOELEWEKA VIZURI KWA YEYOTE ANAYEMSIKILIZA! Tuibue mambo ya msingi ili Lowassa aweze kutupatia majib! ila kwa kweli inavyoonekana kambi yake imewashika vilivyo!
 
Back
Top Bottom