SIYO KWELI! Hakuna huyo unayemuita graduate aliyezaliwa TanZania akakulia TanZania, akasomea shule ya msingi hapa akafaulu darasa la saba, akaenda sekondari akafaulu kidato cha nne akaenda kidato cha tano na sita akafaulu akaenda chuo Kikuu hakafu asijue kuandika Kiswahili!
Huko kote alipitaje?
Hakuna kitu kama hicho! ukisema kwamba kuna WatanZania ambao hawajabatika kwenda shule wana shida ya kuongea na kuandika Kiswahili fasaha hapo sawa, mfano hai mimi Bibi yangu hajasoma hata darasa la kwanza kuandika na kusoma Kiswahili tumemfundisha sisi na leo anaweza kuandika barua ya Kiswahili fasaha kabisa!