Lowassa na Kiingereza chake!

Lowassa na Kiingereza chake!

Mswahili eti akijua kingereza na yeye anataka aongee kwa kubana pua Kama Raia wa America, huu ulimbukeni unapaswa ukemewe kwa nguvu kwani Wenye Lugha Yao wao hawana shida kwenye matamshi na hata ukiongea kingereza kibovu wanakuelewa pasipo kukushangaa kwani wanajua kuwa wewe haukuzaliwa London.

Hivi nani alikudanganya kuwa huko London ndiyo wanazungumza Kiingereza kizuri!!? Tatizo siyo accent bali ni ufahamu wa lugha!!
 
Mkuu hatuongelei Kiingereza kama taaluma bali kama lugha ya Taifa. kwa kuwa tumechagua Kiingereza kuwa lugha Taifa na ni ya kufundishia ni lazima tuielewe na kuimaster. Failure to do that ni KUSHINDWA KWA ELIMU!! Haiwezekani tuamue kutoa elimu kwa kiingereza halafu siku kijana anahitimu hawezi hata kujieleza kwa lugha aliyofundishiwa. Kwenda kutoa hotuba UN that is something else. Kama tungekuwa hatufundishwa kwa kiingereza au kama Kiingereza kisingekuwa ni lugha ya Taifa sidhani kama tungekuwa tunabishana hapa!!

Kuingereza sio lugha ya taifa. Hadhi ya kiingereza hapa Tanzania ni Lugha ya kigeni, pia ni lugha inayotumika kwa mawasiliano na kufundishia mashuleni kuanzia sekindari mpaka elimu ya juu. Ni lugha ya biashara na official.
 
Acha ujinga,kagame anaalikwa kutoa mada kwenye vyuo vikuu ughaibuni na anaongea na wasomi wale very comfortable kiingereza,hajikakamui kama huyu mwanaume wenu wa shoka hapo kideoni,tafute video za kagame akiongea kiingereza zipo nyingi tu u tube,ya lowassa ni hii moja tu,hakurudia tena kuthubutu kuongea tena hadharani,

Acha hizo inabidi utambue kuwa mazingira ya kagame na Lowasa hayafanani kagame mda mwingi tokea akiwa Uganda hadi sasa huwa anaongea kingereza, kifaransa na kinyarwanda, mda mwingi yupo na hiyo Lugha, Lowasa mda mwingi ni Kiswahili na pengine kimasai kingereza kasoma vizuri sana lakini tambua kuwa hiyo Lugha huingea mara chache chache na si muhumu sana kwake kwani wapo Marais wengi hawajui kingereza na maisha yanaenda kwenye Nchi zao, Mfano Angola msumbiji, Cameron, Senegal nk huko viongozi hawajui kingereza na hakuna malimbukeni wa kuwashangaa kama Tz.
 
Huyo jamaa sio kingereza tu hata kiswahili hawezi kujielezea bila kusoma
 
Hivi nani alikudanganya kuwa huko London ndiyo wanazungumza Kiingereza kizuri!!? Tatizo siyo accent bali ni ufahamu wa lugha!!
Lugha ya Taifa ni Kiswahili na Kama shida ni ufahamu wa lugha wapo wakalimani watafanya kazi.
 
Huyo jamaa sio kingereza tu hata kiswahili hawezi kujielezea bila kusoma

97% ya viongozi wa Tz husoma kila wanachokizumgumza zile enzi za Nyerere na akina malichela kufunguka pasipo kusoma popote hazipo siku hizi.
 
Pamoja na kukosea kuongea kiufasaha baadhi ya sentensi...

Tatizo kubwa nililoliona hapa ni ishu ya kuombaomba...

Hivi kweli tunahitaji kwenda uzunguni kuomba chakula cha kuwalisha watoto wa shule zetu?
 
Kuingereza sio lugha ya taifa. Hadhi ya kiingereza hapa Tanzania ni Lugha ya kigeni, pia ni lugha inayotumika kwa mawasiliano na kufundishia mashuleni kuanzia sekindari mpaka elimu ya juu. Ni lugha ya biashara na official.

Ok, ngoja nikubaliane nawe kuwa Kiswahili ni lugha ya Taifa halafu Kiingereza ni official language!!

Point yangu ni kuwa Kiingereza kuwa ni official language Tanzania ina maana ni lazima tukifahamua na tuweze kukiongea. Haiwezekani tujifunze kwa Kiingereza, tufanyiwe interview za kazi kwa Kiingereza halafu kesho tuseme siyo lazima kikijua Kiingereza sawasawa!! What the Heck!! I repeat and I will repeat again, HUKO KUTAKUWA NI KUSHINDWA KWA ELIMU YETU!! Kwa nini tusifanyiwe interview za kazi kwa lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili!!

Tanzania ni nchi pekee Duniani ambao watu wake hawawezi ku-communicate kupitia their own official language!!
 
Samahan wadau,naombeni mnijuze,HIVI LOWASA ANA DEGREE YA NIN?
 
Ok, ngoja nikubaliane nawe kuwa Kiswahili ni lugha ya Taifa halafu Kiingereza ni official language!!

Point yangu ni kuwa Kiingereza kuwa ni official language Tanzania ina maana ni lazima tukifahamua na tuweze kukiongea. Haiwezekani tujifunze kwa Kiingereza, tufanyiwe interview za kazi kwa Kiingereza halafu kesho tuseme siyo lazima kikijua Kiingereza sawasawa!! What the Heck!! I repeat and I will repeat again, UKO KUTAKUWA NI KUSHINDWA KWA ELIMU YETU!! Kwa nini tusifanyiwe interview za kazi kwa lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili!!

Tanzania ni nchi pekee Duniani ambao watu wake hawawezi ku-communicate kupitia their own official language!!

Hata mimi sipingani na wewe kwenye issue ya kutumia au kutotumia Kiswahili katika mambo mbali mbali. Ni watawala wetu tu waliotufikisha hapa. Tujiulize ni kwa nini tulazimishe kujieleza kwa Kiingereza kama hatufahamu vizuri?
 
Tatizo ni yeye kuongea kiingereza kwa kujikoga pasina haja ya kuongea kiingereza.
 
Tatizo liko wapi? Ameongea vizuri na zaidi alichoongea ni kizuri zaidi na kinaonesha jinsi gani alivyo makini. kamwe mtoto hawezi kusoma vema na kuelewa kile anachofundishwa kama ana njaa.
wangapi wanaongea kiingereza kama waingereza wenyewe lakini wanachofanya ni utumbo mtupu.

Una akili sana japo mie zimezidi kidogo.
 
Tuwekee na ex padre akiongea kiingereza tulinganishe ili tujue kama kiingereza ni kigezo cha kuwa Rais. Ujinga mwingine mpaka unatia kinyaa.
 
Acha matusi ya rejareja,mi nimeuliza tu,nataka kujua kwani sijawah kusikia akijinadi kwa elimu yake kama wengne wanavofanya! Afu naogopa KUONGOZWA na MBUMBU!

Kwani umefariki mwaka gani wewe? Maana walioko hai wanajua Gooooogle
 
Mdau umewahi kumsikia Lowassa akizungumza kiingereza????hebu mtazame hapa rais wetu huyu mpya halafu just imagine siku yuko cnn anahojiwa na Larry King na hivi vingereza vya kuandika kwanza then kukariri


rais wa china au msumbiji au urusi huwa wanaongea kiingereza?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom