Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Wadau, amani iwe kwenu.
Jina la Lowasa lilianza kuwa maarufu hasa baada ya sakata la Richmond. Wakati huo umaarufu wake ulitokana na sifa mbaya ya wizi na ufisadi.
Miaka 8 baadaye Lowasa anageuka kuwa mtetezi wa mama lishe, bodaboda na machinga. Haijaeleweka nini kilifanyika mpaka akapata umaarufu kwenye makundi hayo ijapokuwa inaweza kuelezwa ni kutokana na zile rushwa za kimakundi.
Baadaye akajipenyeza ndani ya vyombo vya maamuzi ndani ya CCM. Akaonekana ndiye kiongozi pekee anayefaa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CHAMA hicho. Hatukumuangalia usoni. Tukamkata. Akahamia CHADEMA.
Nako akatumia ujanja ujanja mpaka akapitishwa kuwa mgombea Urais. Ni ujanja tu ulitumika. Hakukuwa na ushindani wowote ndani ya CHADEMA na UKAWA.
Akaingia kwenye kampeni. Nako akatumia ujanja ujanja ili mikutano yake ionekane ina watu wengi. Kumbe walikuwa wanaunga unga tu picha. Ni ujanja tu.
Tukaingia kwenyemkupiga kura. Lowasa na kundi lake wakaandaa vijana wa kuandaa matokeo feki na kuyaweka mitandaoni. Ujanja wake ulikuwa matokeo hayo feki ndiyo wayatumie kuishinikiza Tume kumpeleka Ikulu.
Baada ya kukamatwa wale vijana, Lowasa akatumia ujanja na kulalamika eti walikuwa wanajitolea. Ujanja tu kwani ukweli ni kwamba ni yeye ndiye amewanunulia zile simu na kompyuta. Ndiye aliyewapangisha kwenye mahoteli makubwa makubwa huku wakilala na kula bure.
Nikuambie Lowasa kuwa ujanja hauwezi kukupeleka Ikulu