Mzalendo_Mwandamizi
JF-Expert Member
- Dec 12, 2007
- 1,117
- 4,764
Tulioamua kuacha kuiunga mkono Chadema baada ya kumpokea "fisadi" Lowassa Julai 2015 tuliitwa kila aina ya majina mabaya. Juu kabisa ya orodha ndefu ya majina hayo ni "wasaliti." Dokta Slaa pia hakusalimika kutopachikwa jina hilo.
Fast forward to March 2019, Lowassa aliyepelekea baadhi yetu kuitwa wasaliti ametupatia ahueni baada ya kuachana na Chadema na kurudi CCM.
Nadhani huu ni wakati mwafaka wa kujadili dhana ya "usaliti" kwenye siasa zetu. Na tunaweza kuanzia mjadala huu kwa kufanya tafakuri jadidu kwenye jambo hili:
"Kabla ya Lowassa kujiunga na Chadema, alikuwa Mtanzania anayeongoza kwa kuandamwa na chama hicho, akituhumiwa kuwa ni fisadi mkubwa kabisa. Kwa minajili ya kumbukumbu, Lowassa alianza kuandamwa Februari 2006 na akaendelea kuandamwa hadi alipojiunga na Chadema Julai 2015."
Je, kama baadhi ya tulioiunga mkono Chadema (+Dkt Slaa) tuliitwa wasaliti kwa "kosa" la kubadili msimamo, kwanini basi Chadema nayo si wasaliti kwa kufanya "kosa" hilohilo?
Ni picha iliyozoeleka: mwanasiasa wa CCM akihamia upinzani anageuka shujaa lakini mwanasiasa wa upinzani akihamia CCM anageuka msaliti. Kwa bahati mbaya, picha hiyo hutukumba hata sie "political civilians."
Kwa mtazamo wangu, tatizo ni udikteta. Kwamba "usipoafikiana nami basi wewe msaliti." Kwamba sote tunatakiwa kuwa na mitazamo inayofanana,kitu ambacho si tu hakiwezekani hata kama sote tungekuwa mapacha bali pia ni hatari. Imagine kabla ya uhuru, sote tungekuwa na mtazamo kama huu "wakoloni waliletwa na wamisionari. Wamisionari walileta neno la Mungu. Kwahiyo wakoloni si wabaya kwa sababu waliletwa na watu walioleta neno la Mungu."
Tofauti za kimtazamo ni muhimu sana kwa ajili ya mustakabali wa Tanzania yetu. Tunapokerwa na "mitazamo ya kidikteta ya kina Kabudi wanaotaka wote tuimbe mapambio ya kumsifu Jiwe" basi pia tukerwe na kasumba ya kutaka wenzetu wote wawe na mitizamo inayofanana nasi.
Je tutarajie "samahani" kutoka kwa waliotuita wasaliti kwa "kuikimbia Chadema kisa ujio wa Lowassa"? No way. Utamaduni wa kuomba msamaha bado ni mgeni katika Tanzania yetu. Na ukiona mtu anaomba msamaha basi ujue ana matarajio flani zaidi ya kusamehewa. Anyway life goes on but I hope ni funzo muhimu kwa jamii.
View attachment 1038469
Sent using Jamii Forums mobile app