Lowassa kurudi CCM ni ahueni kwa "wasaliti"

Lowassa kurudi CCM ni ahueni kwa "wasaliti"

Wala hatuoni hata umuhimu wa kujadili uasi wenu we are okay kura milioni sita zimetosha na nyie milioni nane endeleeni kubaki kwa JPM. Mbona kila siku mnatulazimisha tujadili uasi wenu?

Bakini huko huko CCM mjazilizie hapo kwenye milioni 8. Tumechoshwa kila siku mnakuja kuchokonoa mada hiyohiyo na mnajidanganya mnahisi kuondoka kwa EL kunajustify uasi wenu siyo kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kura milioni 6 zimewaongezea nini? Mnajua mmeshapoteza wabunge wangapi? Nini kimebadilika kisiasa zaidi ya kurudi nyuma?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini kusarenda kwa Lowasa kuwe ni tatizo la Chadema na Mtatiro aliyelelewa Cuf mbona hamuilaumu Cuf?
 
Hili jambo ukiliangalia katika hali ya uwiano ,Mbowe alipaswa kujiuzulu kwa maslahi ya chama ,ili mambo yaende mbele.

Lakini utamaduni huo hakuna ,wanasiasa wangekuwa kabla ya kufikia maamuzi yao wanakuja mtaani kupata maoni yetu,nafikiri lile kosa alilolifanya Mbowe lisingekigharimu chama.

Sasa basi kama Mwenyekiti ilipaswa abebe dhamana aachie ngazi ili mambo yasonge mbele.

Kiukweli mimi binafsi alinikwaza sana,tunapaswa kuamini na kusimamia kile tunachokiamini,lakini siyo kwa sababu mtu fulani katoa maamuzi basi yapite tu,iko wapi dhana ya demokrasia ndani ya chama.

Yaliyopita si ndwele kilichobaki sasa ni kuijenga Chadema upya, chama ni watu ni vizuri tuambiane ukweli.
 
Kwa kitendo cha Mbowe kubadili gia angani na kumtosa Dr Slaa na kumchukua captain Lowassa ilikuwa ni baraka kubwa kule CCM kwani utulivu ulitamalaki.

Sasa kwa kuwa mzee Lowassa na Sumaye wameshamaliza ziara yao hapo mtaa wa Ufipa bado kuna wanaccm ambao mchana wako CCM na usiku wanahamia upinzani ikikupendeza mwenyekiti wa Chadema wachukue hawa jamaa kwa ajili ya kutunisha mfuko 2020.

Maendeleo hayana vyama!
 
Nasikia mshenga wao Gwajima anaendelea na mazungumzo kwa ajili ya kishika uchumba na 2020 kwenye mwezi wa 8 ndio Mahali kamili inatolewa na chadema inaolewa kwa Membe rasimi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Membe ameshasoma alama za nyakati ameona bora alee wajukuu tu
 
Kabla Lowassa Hajarudi CCM
Lowassa Kajinye anavalishwa Pampasi -Msukuma
Lowassa hafai hata kwa ugali wa Kulumangia -Fisadi - PolePole
Lowassa Fisadi anatembea kama Kobe - Magufuli
Lowassa Fisadi Mroho wa Madaraka -Nape
Lowassa Hawezi Kamwe Kupewa Nchi Fisadi -Ridhiwani Kikwete
Lowassa anaugonjwa wa Prkisonism hawezi hata kushika tonge la ugali -Ikulu hatupeleki wa Wagonjwa _Kibajaji

Sasa kwani kapelekwa Ikulu? Yupo mahali panapomstahili kwa status yake
 
Tulioamua kuacha kuiunga mkono Chadema baada ya kumpokea "fisadi" Lowassa Julai 2015 tuliitwa kila aina ya majina mabaya. Juu kabisa ya orodha ndefu ya majina hayo ni "wasaliti." Dokta Slaa pia hakusalimika kutopachikwa jina hilo.

Fast forward to March 2019, Lowassa aliyepelekea baadhi yetu kuitwa wasaliti ametupatia ahueni baada ya kuachana na Chadema na kurudi CCM.

Nadhani huu ni wakati mwafaka wa kujadili dhana ya "usaliti" kwenye siasa zetu. Na tunaweza kuanzia mjadala huu kwa kufanya tafakuri jadidu kwenye jambo hili:

"Kabla ya Lowassa kujiunga na Chadema, alikuwa Mtanzania anayeongoza kwa kuandamwa na chama hicho, akituhumiwa kuwa ni fisadi mkubwa kabisa. Kwa minajili ya kumbukumbu, Lowassa alianza kuandamwa Februari 2006 na akaendelea kuandamwa hadi alipojiunga na Chadema Julai 2015."

Je, kama baadhi ya tulioiunga mkono Chadema (+Dkt Slaa) tuliitwa wasaliti kwa "kosa" la kubadili msimamo, kwanini basi Chadema nayo si wasaliti kwa kufanya "kosa" hilohilo?

Ni picha iliyozoeleka: mwanasiasa wa CCM akihamia upinzani anageuka shujaa lakini mwanasiasa wa upinzani akihamia CCM anageuka msaliti. Kwa bahati mbaya, picha hiyo hutukumba hata sie "political civilians."

Kwa mtazamo wangu, tatizo ni udikteta. Kwamba "usipoafikiana nami basi wewe msaliti." Kwamba sote tunatakiwa kuwa na mitazamo inayofanana,kitu ambacho si tu hakiwezekani hata kama sote tungekuwa mapacha bali pia ni hatari. Imagine kabla ya uhuru, sote tungekuwa na mtazamo kama huu "wakoloni waliletwa na wamisionari. Wamisionari walileta neno la Mungu. Kwahiyo wakoloni si wabaya kwa sababu waliletwa na watu walioleta neno la Mungu."

Tofauti za kimtazamo ni muhimu sana kwa ajili ya mustakabali wa Tanzania yetu. Tunapokerwa na "mitazamo ya kidikteta ya kina Kabudi wanaotaka wote tuimbe mapambio ya kumsifu Jiwe" basi pia tukerwe na kasumba ya kutaka wenzetu wote wawe na mitizamo inayofanana nasi.

Je tutarajie "samahani" kutoka kwa waliotuita wasaliti kwa "kuikimbia Chadema kisa ujio wa Lowassa"? No way. Utamaduni wa kuomba msamaha bado ni mgeni katika Tanzania yetu. Na ukiona mtu anaomba msamaha basi ujue ana matarajio flani zaidi ya kusamehewa. Anyway life goes on but I hope ni funzo muhimu kwa jamii.
View attachment 1038469

Sent using Jamii Forums mobile app

Pia usisahau kuna viongozi wakuu ndani ya chama tawala walikua wanaimba kila siku ‘VUA MAGAMBA’ yaani Mhe Lowassa ndiye alikuwa anaambiwa hafai kwenye chama lakini leo hii kimyaaaaa! and in addition to that mwimbaji mwenyewe na bao lake la mkono yupo kimya! Kulikoniiii?Siasa ni mchezo mchafu = Politics is a dirty game!
 
Back
Top Bottom