Lowassa kuizindua Helcopta ya Ufufuo na Uzima

Lowassa kuizindua Helcopta ya Ufufuo na Uzima

Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, ambao ndio wamiliki wa helcopter hii limemaliza taratibu nyingi za kusajili hadi kupata ruhusa ya Kuruka zilizochukua miezi Toka ilipo wasili nchini. Mbali na shughuli za kanisa lakini kanisa limeitoa helkopter hii ifanye shughuli za kijamii na ndio lengo mama hasa. shughuli hizi ni pamoja na Uokoaji wakati wa majanga.

helkopter hii aina ya Robinson R44 ambayo kwenye dunia ya vyombo vya angani inaitwa 'TOP-Vision' imeundwa kwa muundo wa kisasa zaidi wenye kioo kikubwa kinacho saidia abiria na rubani kutazama pande zote wawapo ndani. muundo huu unasaidia sana kwenye majanga kama mafuriko au vyombo vinavyozama majini. Chopaa hii ina uwezo wa kunyanyua mzigo unaokaribia tani moja ikiwa na maana inaweza kuwainua watu zaidi ya kumi kwa kamba.

lakini pia Chopaa hii ina uwezo wa kutua juu ya maji na kuendelea na safari zake. ni moja kati ya helcopter ambazo zinapendwa zaidi ulimwenguni kwa sasa. Robinson zimeundwa kwa mtindo wa kuinua pangaboi lake JUU sana kuepusha ajali. Chopaa hili halina makelele mengi wala Vumbi.


lakini pia kanisa limeanza mchakato wa kuagiza ndege ndogo za abiria sita na nane Jet aircraft zenye uwezo wa kukimbia kwa kasi kiasi cha kilometa 1200 kwa saa, kiasi cha kutumia dakika hamsini (50 minutes) kutoka Dar hadi Kigoma.

mbali na hapo kanisa linatarajia kuleta ndege 'cessna aircraft' zenye uwezo wa kuchukua hadi abiria 32, hizi zitafanya huduma za jamii kwa ujumla. Yote haya ni kufanya miji ifikike kwa urahisi na wepesi ili nchi yetu ipige hatua za kasi kwenye maendeleo. Mtu anaweza kutumia Jet Aircraft ndani ya masaa 11 akaitembelea Mikoa Yote Tanzania.

Kanisa linakamilisha ujenzi wa Kiwanja Cha ndege eneo la Kinzudi Salasala na wakaazi wote wa jiji hili la Darisalam na mikoani wanakaribiswa kupata huduma hizi ambazo hapo awali tulikaririshwa kwamba ni za watu wenye pesa nyingi mno kitu ambacho si kweli. .

....Hivi priority ipo wapi hapa??angalia hayo uliyoyaandika na angalia eneo la ibada, na kumbuka kuna wakati wa jua kali na kuna wakati wa mvua...HILI LA ENEO LA IBADA LILIPASWA LIWE LA DHARURA na sio ndege wala viwanja vya ndege...
2.jpg


IMG_0381.JPG
 
Ushauri wangu: Lowassa akishazindua, helikopta hiyo itumike kumrudisha Monduli direct ili asisumbuke na usafiri
mwingine alioandaa. Huu wa helikopta direct utamfaa sana.
 
Nimependa maelezo ya mleta mada kama yatatima itakuwa poa sana maana watz maneno mengi vitendo zero
 

Lowassa kuizindua Helcopta ya Ufufuo na Uzima
Third world leaders, no work to do.

Huwezi kusikia mbunge wa Uingereza au senator wa Marekani ameenda kuzindua kindege cha kanisa. Never! I mean, that is a colossal waste of time.
 
mimi nina was was na huyo mungu wenu mnaye mtegemea, nahisi anawapa masharti ya kutojenga kanisa kubwa.Mungu wa kweli ambaye Sulemein alimjegea hekalu, hawezi kukubari watu wakae kwenye kiwanja tu cha kupewa eti kisa watu ni wengi arafu mchungaji gwajima eti ana maono ya kufungua chuo cha marubani huo ni upuuzi kabisa. kama mna nia nzuri ya kuisaida jamii mmefanya utafiti na kuona mashirika mangapi ya ndege tz yemekosa marubani ndo mfungue chuo? mge anzisha shule zingine za kuisaidia jamii kutoka kwenye umaskini angalu tunge ona mna nia nzuri na jamii. mnapenda misifa tu pelekea mbali ufree masoni wenu!

Majuzi nimemsikia askofu Gamanywa na mpango wa kuwafundisha vijana ujasilia mali, nafikiri kama ni kweli huyo ndo tunaweza kuona anataka kuisaidia jamii. vijana wengi hawana ajira kabisa. jamii yetu watu wanatafuta ajira, kazi hakuna, fungua miradi ya kuleta ajira kwa jamii kama mashule ili walimu wapate kazi, hospital madocta na manurse wapate kazi, nyie mnakimbilia kufungua shule ya urubani mmmmmmmm!!!!!! mashart ya ufree-mason tu

unatudanganya suala la kuokoa watu wanao pata ajali majini, matukio ya ajali yametokea mala ngapi mpaka mkaona hiyo suala sugu linalo isumbua jamii na hivyo inatakiwa chopa la kuwaokoa? nyie kama watumishi wa Mungu si ndio mnao tuzuia kukiri mabaya na kutwambia ulimi unaumba? sasa inakuwaje nyie wenyewe muwe na mtazamo wa kupata matatizo ya ajari ya maji mbeleni bila kuamini huyo mungu mnaye muhamini anaweza kuondoa majanga hayo? au imani yenu haba?

Nina was was na huyo mungu wenu. Mungu wa kweli lazima angempa maono mchungaji wenu amjegee nyumba nzuri ya ibada siyo kwenye viota au viwanjani tu. na kama umeweza kutwambia habari zote bila kuulizwa na mtu yeyote, unaficha nini sasa kumalizia na kusema kanisa kubwa mnalojenga liko wapi na limefikia wapi? badara yake unasema taharifa kamili itatolewa badae, kwani unaficha nini sasa? mashart ya ufree-mason huo!

Mwisho: ukisoma mwenendo wa wana waisrael walipo kuwa wanataka kuweka vitu wakfu kwa bwana, walikuwa wanawatumia makuhani na watumishi wa makuhani siyo mtu yeyote tu wa mataifa. na kila kitu kilipokuwa kinaenda kuwekwa wakfu kilisogezwa madhabauni palipo itwa patakatifu ambako palikuwa ni sehumu tukufu sana. sasa iweje mnamkaribisha Lowasa asiye kuwa na chembe hata kidogo ya kupakwa mafuta na Mungu aje kuzindua chopa na kuiweka wakfu wakati mapadir,wachungaji wa ruthelan, maaskofu wa kipentekoste wote wapo ambao kibiblia tunaweza kuwaita ndo makuhani wa Mungu. manaenda kumtafuta Lowasa fisadi!

hata kama si fisadi na hakuna uhakika wa ufisadi wake. mtume Paulo anasemaje kuhusu utumishi wa Mungu? si anasema atakaye kufanya kazi ya Mungu na kuwa mkuu asiwe mtu wa kulaumiwa na watu? au hamjui hilo andiko niwape mistali? kitendo cha kuacha maaskofu walio wekwa wakfu na kumfuata mwanasiasa tu hiyo ni dhaili kuwa ni mashart ya ufree-mason!!
 
Hongera sana UFUFUO NA UZIMA . Songeni mbele majeshi ya Bwana. Injili ya Bwana Yesu iwafikie hawa wapondaji . Siku helkopa itakapo msaidia mwananchi ambae kakumbwa na maafa ya mafuriko na Serikali ikaomba wakapewa watajua umuhimu wake. Mchungaji Gwajima nakufagilia sana uko juu. Fanya kazi ya Mungu ipasavyo.
 
Binafsi nampongeza sana Bishop Gwajima. Watanzania wachache kama yeye ni majasiri kufanya mambo makubwa makubwa.
 

Wabongo kwa kupondea tu wako njema balaa kuna dini hazijafanya chochote kwa ajili ya ustawi mzuri wa jamii kwa madai siyo lengo kuu lake uwepo wake.

Kama wewe unawaona waumini wa hilo dhehebu ni wajinga then hata wewe Kuna watu wanakuona wewe ni ---- kutokana na dini yako na Mimi nisiye na dini nawaoneni nyote ni mafala tu.

Kikubwa kama wewe huoni umuhumu wa akifanyacho mwingine,kaa kimya.Ebooo
.
 
edited japan daddy8.jpg


Baadhi ya watu wa Mungu wa nchini Japan ambao ni washirika wa Kanisa la Ufufuo na Uzima nchini Japan, wakiwa na furaha kubwa kummpokea Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la ufufuo na uzima Josephat Gwajima (wa nne kutoka kulia) na Mchungaji Msaidizi Grace Gwajima (wa pili toka kulia).
 
Kweli Ufufuo na Uzima mko juu na mna maarifa sana, hongereni kwa hatua mliyoifikia kweli mnastahili kupongezwa.
 
Nduguzetu

Jumapili hii ya tarehe 9-Novemba, kwenye viwanja vya wazi vya Tanganyika packers , eneo la Kawe ndani ya Jiji la Dar-es Salaam ile Helcoptel iliyotajwa sana na vyombo vya habari Itazinduliwa na Mheshimiwa Edward Lowasa aliyekuwa Waziri wetu mkuu. Helcopter Itatua katika viwanja hivi saa nane mchana kwenye eneo maalum ilipo tengewa.

Mkuu Eng. Biha, asante kwa taarifa, nilidhani mngemleta Dr. Mwakyembe ambaye ndie waziri wa usafirishaji, au Samweli Sitta ambao wote wawili hawa ni waumini wenu!, kwa nini mmewaacha na kwenda kumchukua Lowassa?!.

Kila ulipolitaja jina la baba mchungaji, mimi ninamkubuka tuu dada yetu yule!.

Nilibahatika kushiriki ibada hapo kanisani kwenu, nikafurahishwa sana na ile gari ya mchungaji na ile PA yenu, jinsi vilivyo vya gharama, ila kiukweli, nilisikitishwa na vile viti plastiki kama vya grocery zetu huku uswahilini, na kukosekana hata mahema, kulikopelekea baadhi ya waumini kuabudu huku jua lao, mvua yao!.

Msisahau kumwalika Mchechu, ili labda akiziona juhudi zenu, anaweza kuingia huruma, akaachie muendelee kulitumia eneo hilo!, vinginevyo tujiandae mapema tuu kuhamia Sala Sala!.

All the best.

Pasco
 
Kwani wabongo huwa mnataka mfanyiwe mini ? Kila MTU na mawazo take alopangiwa na Mungu . Jamaa kamiliki Helkopta nyie mnawaza mini. Hats waumini wakikaa juani we unateseka mini ? Kwao jua au mvua so tatizo na ndo maana wako pale maana wanapokea chakula cha uzima. Shida yenu kila kitu kibaya tu. Gwajima ye kaamu kinunua helkopta ili ahubiri injili kwa urahisi ndivyo aliandikiwa na Mungu. So na nyie muwaambie wachungaji wenu au maaskofu wanunue.. Hii nchi INA Uhuru na kila MTU. Gwajima songs mbele kwanza nakufagilia sana. Hongera sana sana tena sana. Watu wanaishi kiuoga uoga tu... Songs mbele Chopa kwanza mengine yatafata . kama MTU anawaza jengo kwanza asubiri jengo analotaka kuliona.
 
Mhandisi, mimi issue yangu ni moja tu, kwa nini uzinduzi usifanywe na mmoja kati ya Maaskofu hata kama ni wastafu. Kwa nini Lowassa?

Mipango mizuri, ufunguzi unafanywa na Fisadi

Fisadi bibi yako
 
Kila huduma au kanisa linatimiza maono na utume wake kama waonavyo wao.
Ask.Gwajima astahili pongezi na tuache husuda nk
 
Back
Top Bottom