Lowassa kuizindua Helcopta ya Ufufuo na Uzima

Lowassa kuizindua Helcopta ya Ufufuo na Uzima

Wazee wa misukule dah, unajua mwanzoni nilikua naamini haya makanisa mchicha kama ni kweli yana Mungu ndani yake na ilibaki kidogo niangukie huko. lakini siku nilipokuja kugundua issue ya misukule na jinsi wanavyowapata hawa misukule nilishtuka sana. na sitaki kabisa kusikia haya makanisa mchicha.

Umewaacha watu ma maswali mengi yanayokosa majibu. Kama unaweza eleza jinsi ujuavyo wewe namna hao misukule wanavyopatikana maana hii inapelekea wao kutafasiri tofauti na kumbe haiko hivyo au iko hivyo lakini kumbe ni tofauti. Toa maelezo aisee!!!!
 
Mliopo Dar nendeni kwa Bishop Gwajima mkajionee uzinduzi wa Chopper. I wish I could be there nijionee hayo mambo makubwa!
 
hawa ni wachungaj au wachumia tumbo?hakika mungu awaathibu mno. Ufisadi tu.
 
Suala la Viongozi wa Makanisa ya kipentecoste au kiroho kujilimbikiziamali na kujipatia mali na umaarufu duniani huku waumini wakiogelea kwenye dibwila umaskini fukara ndio mtindo wa kisasa.
Kimataifa;
Mchungaji Bil Grahams ni Bilionea amekuwa tajiri kuptia waumini wake, ana ndegebinafsi kama Raisi na kanisa amelirithisha kwa mtoto. Marekani wanapata pesakupitia kwake na kufumbia macho mambo yake.
TB joshua ni Bilionea kupitia wafuasi maskini. Alipewakibali cha jengo la ghorofa tano akajenga nane, likaporomoka na kuua 116. Sasa Ana kesi ya kujibu mahakamani naanaweza kufungwa. Nigeria inapata pesa za watalii wa kidini kupitia kwake.
Mchungaji Gilbert Deya Mkenya tajiri amejificha London, yeye na mkewe wana kesi ya kuiba watotowachanga Kenya, kuwapatia waumuni wagumba kwa kisingizio cha miujiza. Anatakiwamahakamani Kenya kujibu mashtaka. Pia amemnyanyasa Kingono msichana wa miaka 14.
Tanzania;
Kiongozo wa Makanisa ya Kiuroho, mfano GetreadyTukare wanawashirikisha wa-Kongo man kwenye biashara za kusafirishabinadamu na nyinginezo.. Ni bilionea na wanalaghai maskini kutumia NGO ya yatima na dirisha la siasa kupata mapesa /kuhadaaumma.
Mch Fuata, ana laghai waumini, kuchukua viwanja mpaka vyabeach, anamiliki ardhi Sumbawanga naanamiliki benki yake. Ana migogoro na kesi ya ardhi/ unyumba wa watu.
Mch Yusuf Kwajina, anamiliki magari ya lukuki ya kifahari -FOGO la Kivita au Amercan Hummer , pia helikkopta binafsi na anaishi maisha yastarehe na anamiliki majumba ya maghrofa (Global Publisher).
Mch. Zake Kobe, Jaaji wa Mahakam ameripotiwa akisema kanisani yake mali ni yake, anachukua 10% pensheni ya waumini maskini, anapokelewa Burundi na JNIA kama Raisi. Wauminiwamemfikisha mahakamani kudai chao.
Wengine: Huko Tegeta na kwinginepo wametuhumiwa kushirikibiashara ya Mihadarati.
Wale Wachungaji wa DECI nao wameshtakiwa kwa kuwaibia wauminimaskini.
Mzee Upapako alisema Kanisa lake lingekuwa barabaraniwenzake wangemkoma kwani angewaazoa waumini wote !
Viongozi hawa wanalichafua kanisa, wamwinue na kumweka Mungujuu badala ya kujiinua wenyewe nakutafuta sifa na umaarufu duniani.
 
Aiseee kwa yeyote aliye leo katika eneo la tukio naomba unijize kinacho endelea huko kawe
 
Nduguzetu

Jumapili hii ya tarehe 9-Novemba, kwenye viwanja vya wazi vya Tanganyika packers , eneo la Kawe ndani ya Jiji la Dar-es Salaam ile Helcoptel iliyotajwa sana na vyombo vya habari Itazinduliwa na Mheshimiwa Edward Lowasa aliyekuwa Waziri wetu mkuu. Helcopter Itatua katika viwanja hivi saa nane mchana kwenye eneo maalum ilipo tengewa.

Mbali na Mheshimiwa lowassa pia Maaskofu wakuu zaidi ya 40 Kutoka makanisa ya Kipentekoste nchini watahudhuria. lakini pia Maaskofu wa makanisa ya Lutheran, Englican na Catholic sambamba na masheick kutoka BAKWATA nao watahudhuria uzinduzi huu wa kihistoria.

Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, ambao ndio wamiliki wa helcopter hii limemaliza taratibu nyingi za kusajili hadi kupata ruhusa ya Kuruka zilizochukua miezi Toka ilipo wasili nchini. Mbali na shughuli za kanisa lakini kanisa limeitoa helkopter hii ifanye shughuli za kijamii na ndio lengo mama hasa. shughuli hizi ni pamoja na Uokoaji wakati wa majanga.

helkopter hii aina ya Robinson R44 ambayo kwenye dunia ya vyombo vya angani inaitwa 'TOP-Vision' imeundwa kwa muundo wa kisasa zaidi wenye kioo kikubwa kinacho saidia abiria na rubani kutazama pande zote wawapo ndani. muundo huu unasaidia sana kwenye majanga kama mafuriko au vyombo vinavyozama majini. Chopaa hii ina uwezo wa kunyanyua mzigo unaokaribia tani moja ikiwa na maana inaweza kuwainua watu zaidi ya kumi kwa kamba.

lakini pia Chopaa hii ina uwezo wa kutua juu ya maji na kuendelea na safari zake. ni moja kati ya helcopter ambazo zinapendwa zaidi ulimwenguni kwa sasa. Robinson zimeundwa kwa mtindo wa kuinua pangaboi lake JUU sana kuepusha ajali. Chopaa hili halina makelele mengi wala Vumbi. watu wengi kwenye ulimwengu wa sasa huitumia kwenye sherehe na harusi mbalimbali. viongozi wengi wa siasa huzitumia kwenye kampeni.

baadhi ya watu wanahoji gharama za mafuta, Robinson inatumia kimiminika cha +petrol inayoitwa AV-Gas ambayo kwa lita ni Tsh3,200 tu. kutoka hapa hadi dodoma na kurudi unaweza kutumia mafuta ya 540,000 tu sawa na gari dogo. Robinson R44 inakimbia hadi kilometa 300 kwa saa. ina maana ni dakika 32 kutoka Dar hadi Morogoro.

uzinduzi wa Chopaa hii ni mwangaza mzuri kwa Watanzania. ni chachu kwa kila mmoja apendaye maendeleo kununua mashine zinazoleta faida sana kwa jamii. sisi sote tunakumbuka Ndugu zetu wengi wamemezwa na maji kwa kukosa nyenzo za kuwaokolea. tatizo la helikopter nyingi ni ukosefu wa marubani mahiri "Compitent pilot" Toka kanisa limeweka mawazo ya kuanza Kumiliki vyombo hivi vya angani pia tumeweka nguvu nyingi Kusomesha vijana wetu wenye akili safi nje ya nchi ili wawe marubani wazuri kwenye Ulimwengu wa anga tunao ukaribia. Ni maono ya Mchungaji Kiongozi kuwa na Chuo cha urubani Tanzania ambacho maandalizi yake yameshaanza. lakini pia kanisa limeanza mchakato wa kuagiza ndege ndogo za abiria sita na nane Jet aircraft zenye uwezo wa kukimbia kwa kasi kiasi cha kilometa 1200 kwa saa, kiasi cha kutumia dakika hamsini (50 minutes) kutoka Dar hadi Kigoma.

mbali na hapo kanisa linatarajia kuleta ndege 'cessna aircraft' zenye uwezo wa kuchukua hadi abiria 32, hizi zitafanya huduma za jamii kwa ujumla. Yote haya ni kufanya miji ifikike kwa urahisi na wepesi ili nchi yetu ipige hatua za kasi kwenye maendeleo. Mtu anaweza kutumia Jet Aircraft ndani ya masaa 11 akaitembelea Mikoa Yote Tanzania.

Kanisa linakamilisha ujenzi wa Kiwanja Cha ndege eneo la Kinzudi Salasala na wakaazi wote wa jiji hili la Darisalam na mikoani wanakaribiswa kupata huduma hizi ambazo hapo awali tulikaririshwa kwamba ni za watu wenye pesa nyingi mno kitu ambacho si kweli. Ikumbukwe kanisa halitumii mashine hizi kibiashara. mara nyingi tunaamini Mungu amesababisha tukawa na vyombo hivi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. hivyo shughuli zote za lazima kwa washirika wa kanisa na wananchi zitatolewa bure na kama gharama itakuwepo basi ni ndogo sana kama kuchangia mafuta na si vinginevyo. Ni maono ya mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima kuhakikisha kila tulicho fikiri hakiwezekani sasa kinawezekana tena si kwa gharama ambazo wengi tunaziogopa bali kwa gharama za kila mtu hasa mtanzania wa kawaida kuzimudu.

AISEEE....UFUFUO NA UZIMA Wamejipanga mno!!!!
Kila kanisa lina mipango yake na vipaumbele..Kwakweli Mungu awabariki.....sanaaaaaa. Mmetisha..
 
mwakni tunaleta boeing mbili za kibiashara uwanja tunatumia jnia na kule mbezi tuko kwenye hatua z a mwisho kuanza ujenzi wa kiwanja cha ndege

engn waholanzi utatutaka
 
Nyie ufufuo na uzima hizo pesa za kununua helicopter mumepata wapi
 
njooni bonde la kukata maneno, mtajua tunapata wap hizo pesa
 
Lowasa ni mtu wa dini anaependa kuona watu wanapata wanachostahili. Hukumu mnayompa ya matusi na tuhuma hakika mnajizolea dhambi. Hakimu wa kweli ni Mungu. Uvumilivu aliyokuwa nayo ni tuzo kutoka kwa Mungu. Ndio maana kwa sasa ukubali au ukatae ndiyo tumaini la wengi katika nafasi ya uraisi 2015. Mungu atamwinua ili maadui zake wadhalilike. Na katika nafasi hiyo atamwinua ili yote mnayoyasema sasa kuhusu Lowasa mjione mlipotoka na kwamba alichelewa
 
AISEEE....UFUFUO NA UZIMA Wamejipanga mno!!!!
Kila kanisa lina mipango yake na vipaumbele..Kwakweli Mungu awabariki.....sanaaaaaa. Mmetisha..

Aiseee hawa jamaa wa ufufuo na uzima wametikisa dunia mpaka mtandao ya kijamii nchini uingereza inaongelea helicopter ya injili ya ufufuo na uzima
 
Mhandisi, mimi issue yangu ni moja tu, kwa nini uzinduzi usifanywe na mmoja kati ya Maaskofu hata kama ni wastafu. Kwa nini Lowassa?

Mipango mizuri, ufunguzi unafanywa na Fisadi

kwani tangu ajiuzuru uPM ilo ndo kanisa la kwanza kwenda kuzindua au kuchangia?
 
mwakni tunaleta boeing mbili za kibiashara uwanja tunatumia jnia na kule mbezi tuko kwenye hatua z a mwisho kuanza ujenzi wa kiwanja cha ndege

engn waholanzi utatutaka

Hawa jamaa Wamejipanga kweli na wanaweza kuwa chachu kwa wawekezaji toka nchi mbali mbali
 
Back
Top Bottom