THINKINGBEING
JF-Expert Member
- Aug 9, 2010
- 2,779
- 1,304
Kabla ya ujio wa Lowassa CHADEMA wapinzani walikuwa wakikishambulia sana ACT kwamba si chama halisi cha upinzani na kina mpango wa kupokea Lowassa kuwa mgombea wake.
ACT ambacho kilishajengewa sura ya usaliti kwa sababu ya kiongozi wake Zitto ambaye hapakuwa na shaka kuwa amesaliti upinzani kilikuwa kikikabiliwa na shutuma nyingine kwamba kiliandaliwa kumtengenezea njia Lowassa ambaye kwa mtazamo wa upinzani wakati huo Lowassa alikuwa nembo ya ufisadi.
Minong'ono kwamba Lowassa anakuja CHADEMA ulipokelewa kwa mtazamo hasi na wapinzani wa kweli kwa hoja kwamba alikuwa na tuhuma nyingi chafu na hakuwa material ya upinzani.
Minong'ono hiyo iliwafanya wapinzani kuzua mijadala ya wazi ndani na nje ya mitandao kujadili hatma yao.
Wakati wa kampeni kauli ya Lowassa kwamba watu wapige kura tu na wamuachie kazi ya kuzilinda iliwafanya wafuatiliaji wa siasa wapate mashaka na uelewa wa Lowassa kuhusu hali halisi ya kuendesha upinzani nchini ama huenda akawa na lengo tofauti.
Baada ya uchaguzi kufanyika na kuwa na matokeo yenye utata mkubwa Lowassa aliwashangaza zaidi wapinzani kwa staili yake ya kukaa kimya huku wapinzani wakitaka kusikia kauli yake kuhusiana na matokeo hayo.
Hata hivyo baada ya ukimya huo kiliibuka kioja kingine.Lowassa alitangazia umma kuwa jeshi la polisi litaombwa kibali yafanyike maandamano yasiyo na kikomo.Wakati wapinzani wakiwa na uzoefu wa kunyimwa vibali vya maandamano ya kawaida na hata mikutano yeye alisema yaombwe maandamano yasiyo na kikomo.
Watu wenye akili walitafsiri mpango huo wa kuomba maandamano yasiyo na kikomo kuwa ulikuwa mpango wa kuzuia maandamano kabisa.
Jeshi la polisi lilikataa maandamano hayo kama ilivotarajiwa na wengi na ndipo alipoibuka tena Lowassa na kusema hakuna maandamano kwa sababu jeshi la polisi limeamua hivyo.Wenye akili walijua hili ni changa la macho.
Hatimaye Lowassa ameamua kutoa makucha yake na kuonesha misimamo rasmi inayopingana na maazimio ya chama.Wakati BAVICHA wanasema wanaelekea Dodoma kuzuia mkutano wa CCM huyu Lowassa yeye anasema CHADEMA sasa kiachane na harakati. Anasisitiza kwa kusema hapatakiwi maandamano tena wala kuizuia serikali kufanya kazi zake.
Ni wakati sasa wakujiuliza ni nini maana ya tamko hili kutoka wakati BAVICHA wakielekea Dodoma?
Ni wakati wakujiuliza ni nini maana ya kauli hizi tatanishi za Lowassa?
Ni wakati wa kujiuliza je Lowassa ni opposition material?
Ni wakati wa kujiuliza je Lowassa ni liability ama asset?