Lowassa is not opposition material

Lowassa amezeeka akili. Kwa mitazamo aliyo nayo ni vigumu sana kuitoa ccm madarakani kwa miaka ya hivi karibuni.
Kuitoa ccm ili iwe nini? Lowassa ana maono, anataka kuwatoa kwenye magwanda ya mgambo ili mvae vizuri na kiheshima kama ccm.
 
Mkimfukuza tu mumlipe na chenji yake yoooote! Mliyataka wenyewe na mkalikoroga sasa wacha mlinywe.
 
"Anamuunga mkono fisadi Lowassa apimwe akili,"- Msigwa
"CCM imempa fomu fisadi Lowassa kugombea urais ni hatari,"-Lissu
"Nashangaa wanaowachoma Moto vibaka mitaani na kumwacha Lowassa akitamba,"-Mbowe.
"Nina ushahidi wote wa ufisadi wa Lowassa na Rostam,"-Mnyika.
"Lowassa ni dhaifu,"-Mbowe
Sasa leo mnalia nini. Mnalo hilo limewaganda.
 
"Anamuunga mkono fisadi Lowassa apimwe akili,"- Msigwa
"CCM imempa fomu fisadi Lowassa kugombea urais ni hatari,"-Lissu
"Nashangaa wanaowachoma Moto vibaka mitaani na kumwacha Lowassa akitamba,"-Mbowe.
"Nina ushahidi wote wa ufisadi wa Lowassa na Rostam,"-Mnyika.
"Lowassa ni dhaifu,"-Mbowe
Sasa leo mnalia nini. Mnalo hilo limewaganda.
Waliotamka hayo yanawahusu wenyewe.Mimi niliamini Lowassa hafai kabla hajaja na sasa akiwa CHADEMA bado naamini hafai na ni fisadi.
 
Mtoa post sisi bado kwetu kwafukuta ndo tuijadili chadema na lowasa? Mi naona tujadili je tunampa chama ngosha au
 
Ukawa walitaka kumtumia Lowassa kufanikisha ndoto yao kuingia ikulu; walichokosea ni kwamba Lowassa hakuwa na chochote cha kumuwezesha kuingia ikulu. Hakuwa na nguvu aliyodhaniwa anayo. Isitoshe, kama mtu aliyewahi kushika nafasi kubwa ya uongozi, hakuwa na vision yeyote ya uongozi ya maana. Ulipofika uchaguzi, aliishia tu kusema: "education, education, education" akipigia chapua initiative yake ya shule za kata - which was a failure. Wakati huohuo ni yeye mwenyewe alishawahi kusema kwamba mfumuko wa wahitimu wa vyuo nchini ni janga, maana ajira ni chache sana. Kwa kifupi Lowassa "siyo riziki", kama kiongozi. Niliamini hivyo tangu mwanzo. Sipendi dictatorial leadership style ya Magufuli, but undoubtedly Magufuli is much better than Lowassa, as a leader, at least so far. Magufuli has something positive to show; Lowassa has nothing.
 
So far lowasa yuko right,hakuna chama cha kutawala milele,wananchi ni walewale, kama walikuamini wakakuongezea majimbo ya ubunge watashindwa kukupa nchi?,issue ni kuwashawishi watu positively wakupe dola,waonyeshe watu way foward utafanya nini pale utakapopewa mamlaka,sio purukushani za kwenda ikulu kufanya majaribio,binafsi siwezi kumkubali mwanasiasa anaeniaminisha kuwa barabarani ni better option ya kumpa dola wakati ballot inawezekana.
 
Mchango wako ndani ya chama chenu ni upi??
Je upinzani kwako ni harakati na maandamano??
We "ulipo tupo"huwezi kujua hiki chama tumefikaje nacho hapa.Unachojua ni kumfuata Lowassa nyuma na kumuimbia nyimbo za sifa na kuabudu.
 
Mkuu una tstizo la kimsingi kabisa.
Ati watu wanaichukia CCM , alafu huku wanaichagua kuongoza nchi?

Sema wewe unaichukia, na isemee nafsi yako!

Juu ya Lowassa, alipojiondoa CCM kwa uchu wake wa madaraka mlifikiri mmelamba dume, kumbe garasa!
And mind you Lowasa yuko hapo si kwa vile ameitwa, kaja kwa hela yake na hamna ubavu wa kumtosa.
Alitoa shilingi ngapi ?
 
So far lowasa yuko right,hakuna chama cha kutawala milele,wananchi ni walewale, kama walikuamini wakakuongezea majimbo ya ubunge watashindwa kukupa nchi?,issue ni kuwashawishi watu positively wakupe dola,waonyeshe watu way foward utafanya nini pale utakapopewa mamlaka,sio purukushani za kwenda ikulu kufanya majaribio,binafsi siwezi kumkubali mwanasiasa anaeniaminisha kuwa barabarani ni better option ya kumpa dola wakati ballot inawezekana.

sawa bana
 
Kabla ya ujio wa Lowassa CHADEMA wapinzani walikuwa wakikishambulia sana ACT kwamba si chama halisi cha upinzani na kina mpango wa kupokea Lowassa kuwa mgombea wake.

ACT ambacho kilishajengewa sura ya usaliti kwa sababu ya kiongozi wake Zitto ambaye hapakuwa na shaka kuwa amesaliti upinzani kilikuwa kikikabiliwa na shutuma nyingine kwamba kiliandaliwa kumtengenezea njia Lowassa ambaye kwa mtazamo wa upinzani wakati huo Lowassa alikuwa nembo ya ufisadi.

Minong'ono kwamba Lowassa anakuja CHADEMA ulipokelewa kwa mtazamo hasi na wapinzani wa kweli kwa hoja kwamba alikuwa na tuhuma nyingi chafu na hakuwa material ya upinzani.

Minong'ono hiyo iliwafanya wapinzani kuzua mijadala ya wazi ndani na nje ya mitandao kujadili hatma yao.

Wakati wa kampeni kauli ya Lowassa kwamba watu wapige kura tu na wamuachie kazi ya kuzilinda iliwafanya wafuatiliaji wa siasa wapate mashaka na uelewa wa Lowassa kuhusu hali halisi ya kuendesha upinzani nchini ama huenda akawa na lengo tofauti.

Baada ya uchaguzi kufanyika na kuwa na matokeo yenye utata mkubwa Lowassa aliwashangaza zaidi wapinzani kwa staili yake ya kukaa kimya huku wapinzani wakitaka kusikia kauli yake kuhusiana na matokeo hayo.

Hata hivyo baada ya ukimya huo kiliibuka kioja kingine.Lowassa alitangazia umma kuwa jeshi la polisi litaombwa kibali yafanyike maandamano yasiyo na kikomo.Wakati wapinzani wakiwa na uzoefu wa kunyimwa vibali vya maandamano ya kawaida na hata mikutano yeye alisema yaombwe maandamano yasiyo na kikomo.

Watu wenye akili walitafsiri mpango huo wa kuomba maandamano yasiyo na kikomo kuwa ulikuwa mpango wa kuzuia maandamano kabisa.

Jeshi la polisi lilikataa maandamano hayo kama ilivotarajiwa na wengi na ndipo alipoibuka tena Lowassa na kusema hakuna maandamano kwa sababu jeshi la polisi limeamua hivyo.Wenye akili walijua hili ni changa la macho.

Hatimaye Lowassa ameamua kutoa makucha yake na kuonesha misimamo rasmi inayopingana na maazimio ya chama.Wakati BAVICHA wanasema wanaelekea Dodoma kuzuia mkutano wa CCM huyu Lowassa yeye anasema CHADEMA sasa kiachane na harakati. Anasisitiza kwa kusema hapatakiwi maandamano tena wala kuizuia serikali kufanya kazi zake.

Ni wakati sasa wakujiuliza ni nini maana ya tamko hili kutoka wakati BAVICHA wakielekea Dodoma?

Ni wakati wakujiuliza ni nini maana ya kauli hizi tatanishi za Lowassa?

Ni wakati wa kujiuliza je Lowassa ni opposition material?

Ni wakati wa kujiuliza je Lowassa ni liability ama asset?

too late

mwombeni msamaha zitto, mfute laana

CDM imeanguka, maneno ya faraja ruksa
 
Back
Top Bottom