Lowassa hatimaye kujitoa kinyang'anyiro cha urais 2015

Lowassa hatimaye kujitoa kinyang'anyiro cha urais 2015

Ndugu Tusidanganyane, kama LOWASSA anauwezo wa kupeleka Majina matatu CC anayoyataka yeye, sasa ni kwanini ashindwe kuweka watu PROXY amabao watatizmiza idadi hiyo ya majina matatu na yeye akiwemo, na kwa kutumia nguvu hiyohiyo akawtupilia mbali majina ya wapinzani wake?

Tuache porojo maana as long as anapower hii unayoisema basi hakika jina lake lazima liwepo siku ya mwisho na anauwezo wa kupitisha majina mengine kabisa hata la KOMBA kwa Uraisi atakavyo.

Inawezekana asiwepo hata ktk hayo majina matano yatakayopendekezwa na kamati kuu.
 
Lowasa ndio kiongozi pekee anaefaa kuiongoza Tanzania kwa sasa
Lakini si mmeambiwa lowasa ni mgonjwa? Sasa mnataka nchi ianze kuweka bajeti ya kuzika rais? Mbona nchi in watu milioni zaidi ya milioni 45 kwani hatuwezi kupata mtu credible, responsible, realiable, accountable kushka hii taasisi ya urais hadi kila siku ni Lowasa, Membe, Januari, Ngeleja, Wasira, Sumae? Haya majina na matendo yao yametuchosha tunataka kusikia majina ya Watanzania wengine ambao hawajachafuliwa na utoko wa CCM.
 
Mnyisanzu "Nipe certificate of evidence kuthibitisha kuwa Lowassa ni fisadi. Don't work on rumours and speculation." Supported. Narudia tena. Richmond in wenyewe. Tajeni ufisai wa Lowassa. Full stop!
 
Maneno ya mwalimu nyerere yazngatiwe..no fisadiz
 
Maneno ya mwalimu nyerere yazngatiwe..no fisadiz

Naona nyerere amekuwa kivuli cha kuwabeba wauza unga kuingia ikulu.huyo unayempigia debe mwenyewe ni drug dealer,kamwe hatutakaa tuingize wauza unga ikulu.
 
hata chadema walishawahi kumuomba lowassa agombee uraisi kupitia chama chao. ndesamburo anampenda sana lowasa ndio maana anatoa matamko ya kumkampenia EL
 
Lowasa ndio kiongozi pekee anaefaa kuiongoza Tanzania kwa sasa

Ila huko mitaani ukisikiliza watu kwenye viunga vya magazeti na kahawa huwezi kuamini mawazo yao! Wanasema nchi inahitaji rais mkali na mwenye msimamo. Hii imetokana na mambo mengine kwenda shaghalabaghala na kukosa maamuzi magmu.

Watamtaja Dr. Slaa au Lowasa kwamba ndio wanaweza kuibadilisha hii nchi kwa sababu wana msimamo na wanachukua maaumuzi. kwa dr dr. salaa historia yake ya kupambana na ufisadi inambeba. Watz. kwa sasa wananchukia sana ufisadi.
Kwa Lowasa wanasema japo ni mzee wa dili lakini huwa ana uwezo mkubwa wa kuchukua maamuzi bila kumuangalia mtu usoni. Yaani sio mtu wa kuahirisha kuchukua maamuzi. Ambalo ndilo watz wengi wanataka kwa sasa. pamoja na tuhuma za kuhusika kwenye madili ya richmondi lakini watu wanasema ni mchapakazi na wanaunganissha hilo na damu ya kimasai ambalo pia hilo Slaa analo. Wanasema bora upige dili lakini kazi ionekane sio na sio ucheka cheka tu. Huibi wala hufanyi kazi,.

Watz amini usiamini hawataki tena rais legelege anechekacheka na wahalifu na asiye na msiamo km huyu tuliye naye sasa. ndio maan mtu km membe hawavutii watu wengi anapotajwa kwenye urais kwasabu ana tabia zilezile za kikwete.
 
hizi habar hazna ukweli ni za kupuuzia unajua kutunga mkuu me nakushaur ukatunge vitabu nadhan vitakusaidia kwenye maisha yako mana utaingza mshko,lowasa mwendo uleule hakuna kurud nyuma hadi kieleweke
 
Katika Team Lowasa siamini kama kuna mtu ambaye alikuwa na uthuubutu wa kutamka kwamba Lowasa aongee na waandishi wa habari kutangaza kwamba hatagombea.

Pia mimi naamini kwamba katika team yoyote lazima kuwe na reserve, mbona hiyo team Lowasa haijasema ni nani atachukua nafasi ya Lowasa? Au ndio team inasambaratika moja kwa moja?
Hiyo team lazima isambaratike tu kwa kuwa msingi wao mkuu ni ufisadi
 
hahaha angeguswa membe ungetukana ila lowasa unasifi uchambuzi mzuri...msipompa lowasa bendera ya ccm lazima muwe wapinzani 2015-2045 mkishajisafisha tofauti na lowasa ccm haina mtu mngine lowasa mwizi lakini mchapa kazi sio hao wengine wezi alafu wavivu wanashinda na kulala angani.

CCM CHAMA KIDOGO CHA UPINZANI TANZANIA 2015-2045

UKAWA FANYENI MAZOEZI NCHI HIYOOOO INAWAHUSU


Uchambuzi mzuri
 
hapo penye afya, nyerere, uadilif pana utam lkn el n mbish acha 2subir 2 wadau
 
Mbona hilo lilijulikana mapema kwamba KIZINGITI cha Lowassa kufikia safari ya ndoto yake ni CC ya CCM?! FYI hata MUKULU mwenyewe alishamuita personally Lowassa na kumueleza achane ni suala la u_rais. Lakini Lowassa akamukatalia na kumueleza kwamba aache demokrasia ichukue mkondo wake.

Kwa mukhutada huo, sidhani kama Lowassa anaweza kuwakubaliwa TEAM LOWOSSA kuhusu wazo la kuachana na hiyo ndoto yake.

But all in all, wether anakubali au kukataa mwisho wa ndoto za Lowassa ni CC ya CCM. Kamwe CC ya CCM chini ya JK haiwezi kabisa kupeleka jina la Lowassa kwenye NEC ili kupigiwa kura, jina lake litachinjiwa baharini.

Mpaka sasa hivi ni jina moja tu ambalo halijajulikana litakalopelekwa NEC ya CCM ili kupigiwa kura. Mengine 4 tayari yameshajulikana, ni kama ifuatavyo IN PRIORITY ORDER

  1. Mizengo Kayanza Pinda
  2. Jina moja la Mzanzibari (bado halijakubaliwa ni yupi)
  3. Prof Mark Mwandosya
  4. Asha-Rose Migiro au Prof Anna Tibaijuka (gender balance)
  5. ......................... (???) Litategemea na upepo wa kisiasa, lakini Lowassa si miongoni mwao

Lakini hao wote ni katika kutimiza demokrasia MLENGWA NI No. 1

Ndio mnavyojidanganya?
 
Hivi nilini Lowassa alitamka anagombea alafu Leo useme anajitoa jajipange vizuri nadhani kwa kutuma post hii umesha pewa bahasha yako jitahidi sana lakini angalia isije jikwaa tu.....
 
GREAT THINKERS,
I have been RELIABLY informed nammoja wa watu walio ndani kabisa ya TEAM LOWASA kwamba Mh. EDWARD NGOYAI LOWASAaliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye alisifika kwa uchapa kazi na utendajibora wa kazi ulioambatana na utoaji wa maamuzi magumu mara moja na bila kusitana hivyo kujitofautisha na 99% ya Viongozi wa Tanzania ambao wengi wao kazi yaoni kulialia, kuchekacheka na kuwa waoga wa kutoa maamuzi magumu, muda wowoteatatangaza kujitoa kwenye kinyanganyiro cha kuelekea Magogoni.

Hii ni kutokanana Kikao cha watu wa ndani kabisa wa TEAM LOWASA ambacho kilikaa mjini Idodomiana kutafakari kwa kina hatma ya mgombea huyo katika Safari yake ya matumaini.Sababu zilizopelekeaTEAM LOWASA
kufikiauamuzi huo mgumu ni hizi zifuatazo:



  1. KIGINGICHA KAMATI KUU (CC)
TEAM LOWASA katika uchaguziuliopita wa CCM kule Idodomia ilifanikiwa kuweka “Watu wake” kwenye NEC kwa 65%ya Wajumbe wa NEC. Ikumbukwe kwamba NEC ndicho chombo chenye mamlaka ya kuyapokea majina 5 yaliyowasilishwa mbele yakena Kamati Kuu (CC) na kisha kuyapigia kura na kuyapeleka majina 3 kwenyeMkutano Mkuu.

TEAM LOWASA inaamini NEC haitakuwa kikwazo kwake na hata MkutanoMkuu nako hakutakuwa na tatizo kwani 85% ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu ni NJAAKALI. Tatizo kubwa kwa LOWASA ni CC. Hii CC mpya ina wajumbe wapya walioshindaambao imebainika wengi wao hawampendi kabisa LOWASA mfano akina Jerry Slaa etc na wamekuwa wakielezea hivyo hadharani bila woga wala kumungunya maneno.

Aidha,kana kwamba hiyo haitoshi, Wajumbe wengine wengi wa CC ambao waliteuliwa naMwenyekiti wa CCM Mh JK nao pia ni ANTI-LOWASA. Juhudi za chinichini zakuwaweka sawa wajumbe hao hadi sasa zimekwama. Ni kutokana na hali hii, TEAMLOWASA imeoana kwamba kupenya kwenye CC itakuwa kazi kubwa mno

2. KIGINGICHA SECRETARIAT YA MAADILI
TEAM LOWASA inaamini kwamba 98%ya Wajumbe wa Secretariat ya Maadili ya CCM imejaa wajumbe ambao niANTI-LOWASA. TEAM LOWASA inaamini hata kufungiwa kwa wale waTanzaniawalioonyesha nia ya kutaka Urais ni danganya toto kwani mlengwa alikuwa niLOWASA kutokana na michango yake lukuki aliyokuwa akiitoa kwa jamii na kasi yakimbunga aliyokuwa akienda nayo iliyokuwa ikiwatimulia vumbi vibaya sana wagombeawengine.

Inaaminika LOWASA angepewa adhabu yeye peke yake ingeonekana SECRETARIATwako biased hivyo ikaamuliwa wapewe adhabu wote ndio maana watu waliokuwahawana hata kosa moja mfano Mh. Fredrick Sumaye walilalamikia sana adhabu hiyo.

3. FAILILA LOWASA
TEAM LOWASSA inaamini kwamba faili la Lowasa litakuwa limechafuka sana kutokana na tuhuma mbalimbali ambazozimeenezwa dhidi yake. Aidha, TEAM LOWASA imegundua kwamba mgombea waoanafuatiliwa kwa karibu na kuna watu wamepandikizwa kwenye team yao ambaohurekodi matukio yote machafu ya TEAM LOWASA kwa lengo la kuyapeleka Kamati yaMaadili ili watakapokuwa waoa marks kwa kila mgombe na kwa jina la LOWASA wawena ushahidi wa kutosha ili kusiwe na malalamiko toka kundi la TEAM LOWASAwatakapomchinjia baharini.

Kutokana na jambo hili, wajumbe wa TEAM LOWASAwalizozana mno kwamba miongoni mwao kuna Mamluki na kukatokea na mtiti mkubwabaina yao.

4. MWALIMUNYERERE
Mwaka 1995 Mwalimu Nyerere bilakumungunya maneno aliasema wazi kwamba LOWASA kijana mdogo wa miaka 42 alikuwani FISADI hivyo hafai kabisa kuwa kiongozi. TEAM LOWASA inaona kwamba minutesza Kikao hicho cha Kamati Kuu bado zipo na upo uwezekano mkubwa zikatumiwa naCC kumngoa kama ilivyofanyika kwa Mh. John Malecela ambaye nae Mwalimu alisemahafai kuwa Kiongozi.

5. UGUMUWA KUUNGWA MKONO NA VIONGOZI WASTAAFU
TEAM LOWASA wamepata shida sanakuweza kuwavuta Viongozi wastaafu wa ngazi za juu wa CCM ili wawe upande waokutokana na sifa ya Ufisadi ya mgombea wao, ingawa viongozi hao walisema LOWASAanaweza kugombea kama mwanachama yeyote wa CCM lakini hawakuonyesha kumuungamkono kwa dhati kwa maana ya kuwa tayari kumfanyia kampeni. Viongozi haowanaona kwamba mtu kama LOWASA akiwa ndiye anaeibeba bendera ya CCM basi chamakitakuwa kama kinakubaliana na maovu ya LOWASA.

TEAM LOWASA inaona mgombea waoanaonewa tu kwa tuhuma za UFISADI ambazo hakuna mahakama iliyozithibitisha.TEAM LOWASA imeenda mbali zaidi na kusema iwapo CCM ilisema ANDREW CHENGE naeni FISADI mbona kapewa nafasi nyeti mfano CHENGE ni MWENYEKITI wa Kamati nyetiya Uchumi ya Bunge na pia ni MWENYEKITI wa Kamati nyeti ya Uandishi wa KATIBAmpya sasa iweje LOWASA nae asipewe madaraka?

6. AFYAYA LOWASA
TEAM LOWASA ililijadili jambohili kwa kina sana na kulikuwa na ubishanaji wa hali ya juu. Ilifikia mahali madaktarimbalimbali watoe expert opinion kuhusu afya ya LOWASA. Aidha, experts haowaliulizwa iwapo LOWASA angweza kuhimili mikikimikiki ya kuzunguka nchi nzimakutafuta kura na akifanikiwa kuvuka kikwazo hicho kama ataweza kuiongozaTanzania hadi 2025.

Suala hili liliumiza mno vichwa vya TEAM LOWASA lakiniLOWASA mwenyewe aliwaambia kwamba yeye yuko Gado kama chuma cha pua.
Baada ya kuyatafakali mambo yotehaya kwa kina sana, TEAM LOWASA ambayo ilkuwa imefika mbali sana katika kumuuzamgombea wao, kwa shingo upande ikamshauri aite waandishi wa habari ili atangazekwamba yeye akuwemo kwenye kinyanganyiro cha Urais. Hata hivyo, LOWASA alieonekanakutofurahia uamuzi huo kutokana na muda na hela zote alizotumia hadi sasakuusaka Urais na hivyo aliwambia TEAM LOWASA kwamba ataenda kuongea na mkeweMama Regina Lowasa na wanawe kisha atakutana na TEAM LOWASA.

HIVYO, GREAT THINKERS
STAYTUNED!!!

Mimi siyo mwana ccm,lakini kwa ulivyo amua kumchafua lowasa hatokaa akusahau.
 
Hakuna wa kubishana na Lowasa. Wengine wanafosiwa na makundi yenye malengo yao binafsi, japo wao wenyewe wanajijua kua hawana uwezo wa kuongoza.Lowasa juuu!!!! Hilo ndilo jembe la kuendeleza mazuri ya JK
 
Back
Top Bottom