Mbona hilo lilijulikana mapema kwamba KIZINGITI cha Lowassa kufikia safari ya ndoto yake ni CC ya CCM?! FYI hata MUKULU mwenyewe alishamuita personally Lowassa na kumueleza achane ni suala la u_rais. Lakini Lowassa akamukatalia na kumueleza kwamba aache demokrasia ichukue mkondo wake.
Kwa mukhutada huo, sidhani kama Lowassa anaweza kuwakubaliwa TEAM LOWOSSA kuhusu wazo la kuachana na hiyo ndoto yake.
But all in all, wether anakubali au kukataa mwisho wa ndoto za Lowassa ni CC ya CCM. Kamwe CC ya CCM chini ya JK haiwezi kabisa kupeleka jina la Lowassa kwenye NEC ili kupigiwa kura, jina lake litachinjiwa baharini.
Mpaka sasa hivi ni jina moja tu ambalo halijajulikana litakalopelekwa NEC ya CCM ili kupigiwa kura. Mengine 4 tayari yameshajulikana, ni kama ifuatavyo IN PRIORITY ORDER
- Mizengo Kayanza Pinda
- Jina moja la Mzanzibari (bado halijakubaliwa ni yupi)
- Prof Mark Mwandosya
- Asha-Rose Migiro au Prof Anna Tibaijuka (gender balance)
- ......................... (???) Litategemea na upepo wa kisiasa, lakini Lowassa si miongoni mwao
Lakini hao wote ni katika kutimiza demokrasia MLENGWA NI No. 1