Lowassa hatimaye kujitoa kinyang'anyiro cha urais 2015

Lowassa hatimaye kujitoa kinyang'anyiro cha urais 2015

lowassa ana uzalendo na nchi yake kuliko mtu yeyote ndani ya Ccm.ndiyo kiongozi pekee aliyebakia kuwaongoza watanzania kwenda hatua nyingine na kundi la membe linawatumia watu kumchafua lowasa huku mitandaoni.

Kweli kabisa Lowasa ni mzalendo na anaijua vizuri Tanzania.. Lowasa ndio kiongoz pekee atakaetupeleka kwenye nchi ya asali.na maziwa
 
Mkuu, kumbe na wewe ni ukoo wa Mafisadi? Poleni sana. Mmefanikiwa kuiondoa TAKUKURU kwenye Katiba Mpya. Ila kazi mnayo


Hivi HILI si GAMBA ?
Sasa waliofanikiwa si MACCM wenzio na yalikuwa maazimio ya Chama?
au mimi sielewi?
by the way unategemea nini pale mwenyekiti w auandishi w akatiba anapokuwa FISADI CHENGE ?
kweli kabisa kutoka moyoni ulitegeema mapya?

Hivi Hushangai Bunge kinauwezo wa kumuwajibisha Spika, Waziri mkuu na Raisi pia, ila wananchi hawana uwezo huo wa kuwawajibisha Wabunge?
 
Katika Team Lowasa siamini kama kuna mtu ambaye alikuwa na uthuubutu wa kutamka kwamba Lowasa aongee na waandishi wa habari kutangaza kwamba hatagombea.

Pia mimi naamini kwamba katika team yoyote lazima kuwe na reserve, mbona hiyo team Lowasa haijasema ni nani atachukua nafasi ya Lowasa? Au ndio team inasambaratika moja kwa moja?
Hakuna lisilowezekana Mkuu
 
Hivi HILI si GAMBA ?
Sasa waliofanikiwa si MACCM wenzio na yalikuwa maazimio ya Chama?
au mimi sielewi?
by the way unategemea nini pale mwenyekiti w auandishi w akatiba anapokuwa FISADI CHENGE ?
kweli kabisa kutoka moyoni ulitegeema mapya?

Hivi Hushangai Bunge kinauwezo wa kumuwajibisha Spika, Waziri mkuu na Raisi pia, ila wananchi hawana uwezo huo wa kuwawajibisha Wabunge?
Usiwe kama mtoto unadhani wananchi wangetumia sheria gani kumwajibisha mbunge huwezi kumwajibisha mtu bila kuongozwa na sheria jitambue kwanza.
 
Mkuu, kumbe na wewe ni ukoo wa Mafisadi? Poleni sana. Mmefanikiwa kuiondoa TAKUKURU kwenye Katiba Mpya. Ila kazi mnayo

watanzania wanamhitaji lowassa kuliko yeye anavyowahitaji. ndiye kiongozi pekee aliyebakia ndani ya Ccm mwenye uthubutu wa kufanya maamuzi
 
Mlaji mla leo...mla jana kala nini? na anayeshikwa na ngozi ndie MWIZI...Mzee wenu kakutwa na ngozi nyama wamekula wengine

Ni nani ndani ya CCM sio mwizi, sio fisadi aanze kumnyooshea mkono Lowassa. Nyie mnampinga Lowassa sio kwa ufisadi wake bali kwa maslahi yenu binafsi, ndio maana watanganyika tunamuonea HURUMA. Mbona Chabruma anatembelea V8 hamumsemi kuwa fisadi
 
GREAT THINKERS,
I have been RELIABLY informed nammoja wa watu walio ndani kabisa ya TEAM LOWASA kwamba Mh. EDWARD NGOYAI LOWASAaliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye alisifika kwa uchapa kazi na utendajibora wa kazi ulioambatana na utoaji wa maamuzi magumu mara moja na bila kusitana hivyo kujitofautisha na 99% ya Viongozi wa Tanzania ambao wengi wao kazi yaoni kulialia, kuchekacheka na kuwa waoga wa kutoa maamuzi magumu, muda wowoteatatangaza kujitoa kwenye kinyanganyiro cha kuelekea Magogoni. Hii ni kutokanana Kikao cha watu wa ndani kabisa wa TEAM LOWASA ambacho kilikaa mjini Idodomiana kutafakari kwa kina hatma ya mgombea huyo katika Safari yake ya matumaini.Sababu zilizopelekeaTEAM LOWASA kufikiauamuzi huo mgumu ni hizi zifuatazo:

  1. KIGINGICHA KAMATI KUU (CC)
TEAM LOWASA katika uchaguziuliopita wa CCM kule Idodomia ilifanikiwa kuweka “Watu wake” kwenye NEC kwa 65%ya Wajumbe wa NEC. Ikumbukwe kwamba NEC ndicho chombo chenye mamlaka ya kuyapokea majina 5 yaliyowasilishwa mbele yakena Kamati Kuu (CC) na kisha kuyapigia kura na kuyapeleka majina 3 kwenyeMkutano Mkuu. TEAM LOWASA inaamini NEC haitakuwa kikwazo kwake na hata MkutanoMkuu nako hakutakuwa na tatizo kwani 85% ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu ni NJAAKALI. Tatizo kubwa kwa LOWASA ni CC. Hii CC mpya ina wajumbe wapya walioshindaambao imebainika wengi wao hawampendi kabisa LOWASA mfano akina Jerry Slaa etc na wamekuwa wakielezea hivyo hadharani bila woga wala kumungunya maneno.

Aidha,kana kwamba hiyo haitoshi, Wajumbe wengine wengi wa CC ambao waliteuliwa naMwenyekiti wa CCM Mh JK nao pia ni ANTI-LOWASA. Juhudi za chinichini zakuwaweka sawa wajumbe hao hadi sasa zimekwama. Ni kutokana na hali hii, TEAMLOWASA imeoana kwamba kupenya kwenye CC itakuwa kazi kubwa mno

2. KIGINGICHA SECRETARIAT YA MAADILI
TEAM LOWASA inaamini kwamba 98%ya Wajumbe wa Secretariat ya Maadili ya CCM imejaa wajumbe ambao niANTI-LOWASA. TEAM LOWASA inaamini hata kufungiwa kwa wale waTanzaniawalioonyesha nia ya kutaka Urais ni danganya toto kwani mlengwa alikuwa niLOWASA kutokana na michango yake lukuki aliyokuwa akiitoa kwa jamii na kasi yakimbunga aliyokuwa akienda nayo iliyokuwa ikiwatimulia vumbi vibaya sana wagombeawengine. Inaaminika LOWASA angepewa adhabu yeye peke yake ingeonekana SECRETARIATwako biased hivyo ikaamuliwa wapewe adhabu wote ndio maana watu waliokuwahawana hata kosa moja mfano Mh. Fredrick Sumaye walilalamikia sana adhabu hiyo.

3. FAILILA LOWASA
TEAM LOWASSA inaamini kwamba faili la Lowasa litakuwa limechafuka sana kutokana na tuhuma mbalimbali ambazozimeenezwa dhidi yake. Aidha, TEAM LOWASA imegundua kwamba mgombea waoanafuatiliwa kwa karibu na kuna watu wamepandikizwa kwenye team yao ambaohurekodi matukio yote machafu ya TEAM LOWASA kwa lengo la kuyapeleka Kamati yaMaadili ili watakapokuwa waoa marks kwa kila mgombe na kwa jina la LOWASA wawena ushahidi wa kutosha ili kusiwe na malalamiko toka kundi la TEAM LOWASAwatakapomchinjia baharini. Kutokana na jambo hili, wajumbe wa TEAM LOWASAwalizozana mno kwamba miongoni mwao kuna Mamluki na kukatokea na mtiti mkubwabaina yao.

4. MWALIMUNYERERE
Mwaka 1995 Mwalimu Nyerere bilakumungunya maneno aliasema wazi kwamba LOWASA kijana mdogo wa miaka 42 alikuwani FISADI hivyo hafai kabisa kuwa kiongozi. TEAM LOWASA inaona kwamba minutesza Kikao hicho cha Kamati Kuu bado zipo na upo uwezekano mkubwa zikatumiwa naCC kumngoa kama ilivyofanyika kwa Mh. John Malecela ambaye nae Mwalimu alisemahafai kuwa Kiongozi.

5. UGUMUWA KUUNGWA MKONO NA VIONGOZI WASTAAFU
TEAM LOWASA wamepata shida sanakuweza kuwavuta Viongozi wastaafu wa ngazi za juu wa CCM ili wawe upande waokutokana na sifa ya Ufisadi ya mgombea wao, ingawa viongozi hao walisema LOWASAanaweza kugombea kama mwanachama yeyote wa CCM lakini hawakuonyesha kumuungamkono kwa dhati kwa maana ya kuwa tayari kumfanyia kampeni. Viongozi haowanaona kwamba mtu kama LOWASA akiwa ndiye anaeibeba bendera ya CCM basi chamakitakuwa kama kinakubaliana na maovu ya LOWASA. TEAM LOWASA inaona mgombea waoanaonewa tu kwa tuhuma za UFISADI ambazo hakuna mahakama iliyozithibitisha.TEAM LOWASA imeenda mbali zaidi na kusema iwapo CCM ilisema ANDREW CHENGE naeni FISADI mbona kapewa nafasi nyeti mfano CHENGE ni MWENYEKITI wa Kamati nyetiya Uchumi ya Bunge na pia ni MWENYEKITI wa Kamati nyeti ya Uandishi wa KATIBAmpya sasa iweje LOWASA nae asipewe madaraka???6. AFYAYA LOWASA
TEAM LOWASA ililijadili jambohili kwa kina sana na kulikuwa na ubishanaji wa hali ya juu. Ilifikia mahali madaktarimbalimbali watoe expert opinion kuhusu afya ya LOWASA. Aidha, experts haowaliulizwa iwapo LOWASA angweza kuhimili mikikimikiki ya kuzunguka nchi nzimakutafuta kura na akifanikiwa kuvuka kikwazo hicho kama ataweza kuiongozaTanzania hadi 2025.

Suala hili liliumiza mno vichwa vya TEAM LOWASA lakiniLOWASA mwenyewe aliwaambia kwamba yeye yuko Gado kama chuma cha pua.
Baada ya kuyatafakali mambo yotehaya kwa kina sana, TEAM LOWASA ambayo ilkuwa imefika mbali sana katika kumuuzamgombea wao, kwa shingo upande ikamshauri aite waandishi wa habari ili atangazekwamba yeye akuwemo kwenye kinyanganyiro cha Urais. Hata hivyo, LOWASA alieonekanakutofurahia uamuzi huo kutokana na muda na hela zote alizotumia hadi sasakuusaka Urais na hivyo aliwambia TEAM LOWASA kwamba ataenda kuongea na mkeweMama Regina Lowasa na wanawe kisha atakutana na TEAM LOWASA.HIVYO, GREAT THINKERS STAYTUNED!!!

Toa upumbavu wako hapa Kenge wewe
 
Mbona hilo lilijulikana mapema kwamba KIZINGITI cha Lowassa kufikia safari ya ndoto yake ni CC ya CCM?! FYI hata MUKULU mwenyewe alishamuita personally Lowassa na kumueleza achane ni suala la u_rais. Lakini Lowassa akamukatalia na kumueleza kwamba aache demokrasia ichukue mkondo wake.

Kwa mukhutada huo, sidhani kama Lowassa anaweza kuwakubaliwa TEAM LOWOSSA kuhusu wazo la kuachana na hiyo ndoto yake.

But all in all, wether anakubali au kukataa mwisho wa ndoto za Lowassa ni CC ya CCM. Kamwe CC ya CCM chini ya JK haiwezi kabisa kupeleka jina la Lowassa kwenye NEC ili kupigiwa kura, jina lake litachinjiwa baharini.

Mpaka sasa hivi ni jina moja tu ambalo halijajulikana litakalopelekwa NEC ya CCM ili kupigiwa kura. Mengine 4 tayari yameshajulikana, ni kama ifuatavyo IN PRIORITY ORDER

  1. Mizengo Kayanza Pinda
  2. Jina moja la Mzanzibari (bado halijakubaliwa ni yupi)
  3. Prof Mark Mwandosya
  4. Asha-Rose Migiro au Prof Anna Tibaijuka (gender balance)
  5. ......................... (???) Litategemea na upepo wa kisiasa, lakini Lowassa si miongoni mwao

Lakini hao wote ni katika kutimiza demokrasia MLENGWA NI No. 1
 
Namkubali sana magufuli , tumpe nchi kama tunataka mabadiliko ya kweli

Kama CCM imekosa kabisa mgombea ni bora isiweke mtu nafasi ya uraisi. Huyu magufuli kwenye ranchi yake pale Chato amejenga bonge la ghorofa kwa ajili ya kukaa wachunga ng'ombe. Lowassa ana ng'ombe 800 Tu wakati Magufuli anazo 3000. Wote ni walewale
 
Kweli kabisa Lowasa ni mzalendo na anaijua vizuri Tanzania.. Lowasa ndio kiongoz pekee atakaetupeleka kwenye nchi ya asali.na maziwa

mkuu ni kweli tupu, lowassa ndiye kiongozi mwenye tunu zile ambazo warioba amezitaja kwenye katiba mpya. lowasa anakwenda kuingia magogoni nipo tayari kufanya lolote huyu mtu Wa watu Angie ikulu
 
Semeni yote, ila muda ukifika na kama Mh EL atahitaji Urais hakuna wa kumzuia maana naamini EL ana siri nzito ndani yake. Kama mtakumbuka kwenye kikao kimoja mjini Dodoma alimuuliza mwenyekiti wake JK, "hivi mwenyekiti natukanwa, nasemwa vibaya na wanaCCM/wananchi umekaa kimya!, hivi nikipi nilichokuwa nafanya ulikuwa hukijui?". Tusubiri tuone hatima yake maana 2015 sio mbali.
 
Nimeamua kuachana na siasa nakwenda kuwa mwalimu wa kufundisha chuo cha uchumi.
Mkuu we mbugila kweli yani uliacha kuwa mwalimu akaingia kwenye siasa hujui kuwa siasa ni ujinga watu wanahonga watu kupata uongozi kama huna pesa nani atakuchagua Lowasa anahonga mpaka ambao siyo wapiga kula.
 
Back
Top Bottom