Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

NJAA MBAYA ETI WATU WANAENDESHA BODABODA KUTOKA MBEY KWENDA DODOMA KUMUOMBA FISADI AWE RAIS:glasses-nerdy::glasses-nerdy::glasses-nerdy::glasses-nerdy::glasses-nerdy::glasses-nerdy: SHITI


Rkebisha kauli yako hii, ni kauli tata.
watu hawawezi kutoka Mbeya mpaka Dodoma kwaajili ya CCM.
Vijana walitoka Mbalali.
 
Nani afaaye kwako au mpaka tuwasikie wote...na je maneno tu yatosha kutenda? Nchi hii ina shida nyingi sana ifike mahali wakati tunapinga kitu tutoe na solution yake la sivyo itakua ni maneno matupu tu ambayo hayatusaidii. Ifike mahali tusaidiane kusema fulani anafaa kwasababu 1,2,3 n.k. ndio tutafika tunapotaka kwenda. Ushabiki wa kisiasa ni mbaya sana. Binafsi nazidi kuogopa nguvu anayotumia Lowassa kutaka ukuu wa nchi. Amekua akijijenga kwa staili yake na chama na system nzima ikimuangalia hila hatua madhubuti kuchukuliwa...hii sio bahati mbaya...hatuna taasisi amabazo zinaweza kudhibiti matukio kama haya, kweli!!!? Basi hii ni hatari. Ifike mahali tuipende nchi yetu kwanza...tusiwe n ushabiki wa kisiasa...kwangu mimi wanasias wote lao koja ni kushika dola...tuwe na mfumo wa kuwajibisha tabaka hili ambalo linajiona ni miungu watu ndani ya nchi yetu

Muswada wa Katiba mpya chini ya uongozi wa Mzee Warioba ulikuwa una-address hiki hiki unachokisema. Na sio kwamba Watanganyika na Wazanzibari sote tumerukwa na akili. La hasha, ndio maana unaona Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Unga mkono UKAWA upate "mfumo wa kuwajibisha tabaka hili ambalo linajiona ni miungu watu ndani ya nchi yetu."
 
Edward, our big problem in Tanzania is corruption, corruption, corruption and corruption. Our solution will never be Lowasa, Lowasa, Lowasa and Lowasa . Farewell Lowasa.
 
edward-lowassa.jpg


Watanzania wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wanaaminishwa kuwa ana maono ya kiuongozi ambayo yakitumika yanaweza kulinasua taifa letu toka hapa lilipo. Wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa ni kiongozi bora ambaye Watanzania wanapaswa kumwangalia kwa matumaini - ndio maana ya "Safari ya Matumaini".

Wapo kati yetu ambao wameshazugika na pendekezo hilo na wamekuwa kama waliorogwa hivi. Wapo baadhi yetu kwa muda wote wa uongozi wa Lowassa (hasa baada ya kuwa Waziri Mkuu na baadaye) tuliona kile ambacho labda kimefichika kwa wengi - Lowassa hafai.

Hii si hukumu juu ya utu wake, heshima au ubinadamu wake; ni hukumu juu ya uongozi wake na maono yake kama kiongozi. Kumkataa Lowassa, maono yake, uongozi wake na fikra zake siyo kumchukia yeye kama Mtanzania mwenzetu au kama binadamu. Ni kuwa na tofauti naye na vile anavyowakilisha kiasi kwamba tofauti hizo hazijawezi kupatana (irreconcilable differences).

Katika siasa ni lazima tuheshimu uwepo wa tofauti hizi na tuelewe ndio msingi wa kutafuta viongozi bora zaidi au chama bora. Kwa kadiri yeye atakavyojaribu kujiuza ndivyo na sisi wengine tutazidi kuonesha kuwa hauziki au zaidi hanunuliki. Hii si chuki ni tofauti tu ya msingi (fundamental difference).

Pendekezo langu linatokana na hili; kwamba zipo na zimedumu tofauti za msingi kati ya maono ya baadhi yetu na maono ya mgombea huyu mtarajiwa kutoka CCM. Tanzania haihitaji maono na uongozi wa Lowassa kwa sababu nyingi tu; nitaanza na moja ya leo na nitaendelea kwenye mada hii hii kila ninapopata nafasi hadi jina lake litakapotupwa na NEC na yeye akaendelea kuwa Waziri Mkuu wa zamani.

Mara kwa mara baada ya sakata lake na katika jitihada za kujirudisha katika umuhimu (relevance) Lowassa amekuwa akizungumzia mwelekeo wa sera zake na kitu kitakachomuongoza. Aliamua kwenda kinyume na mwelekeo wa serikali ya chama chake ambayo iliweka mkazo kwenye "Kilimo Kwanza"; yeye ameamua kuja na hoja ya "Elimu Kwanza".

Alielezea kupinga kwake hoja ya Kilimo Kwanza miaka michache nyuma alipohojiwa katika kipindi cha Dakika45 (kinachorushwa na ITV). Alinukuliwa kusema "Mpango huu wa Kilimo Kwanza umekosa nguvu kwa sababu kuanzishwa kwake hakukuzingatia dhana ya ukombozi wa mwananchi wa kawaida. Tangu awali ndani ya chama (CCM) nilieleza kuwa sitaunga mkono hoja hiyo mpaka kuongezwe mashiko na kuwa Elimu Kabla ya Kilimo Kwanza"

Hoja hii ameirudia tena juzi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ambao bila ya shaka wengi wamekuwa 'charmed' na wingu la umaarufu wa Lowassa kiasi kwamba hakuna ambaye ameweza kumbana vizuri kwenye maswali. Anasema endapo atachaguliwa basi ataelekeza nchi kwenye "elimu kwanza"; kwamba hiki ndicho kipaumbele chake.

Ndio maana sisi wengine tunasema hafai; kwa sababu inaonekana siyo yeye wala chama chake ambao wamelielewa vizuri tatizo linaloikabili Tanzania; tatizo ambalo limeielekeza (orient) Tanzania kufuata njia ya Nigeria. Kwamba tunaweza kabisa kutengeneza uchumi wenye nguvu lakini wa taifa lenye umaskini uliokithiri, lisilo na usawa na la wasomi wasioweza kulipeleka taifa mbele. Tutakishia kujisifia wingi wa wasomi ambao wengi wataishia kwenda nje ya nchi kutafuta maisha. Taifa ambalo litakuwa limegawanyika sana kama Nigeria - licha ya kuwa na wasomi wengi.

Lowassa inaonekana ameshindwa kuelewa au hataki kukubali kuwa tatizo kubwa la Tanzania ni la aina tatu:
1. Ufisadi
2. Ufisadi
3. Ufisadi

Lowassa hatopambana na ufisadi kwa uzito unaostahili kwani haoni kuelewa kuwa ni tatizo la hatari zaidi kwa taifa "kuliko vita wakati wa amani" kama alivyosema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Kutokuelewa kuwa Ufisadi ndiyo sekta haramu yenye nguvu zaidi katika nchi yetu ni kushindwa kuelewa tatizo letu hasa ni nini. Ufisadi umepenya (permeate) kwenye kila sekta nyingine zote (rasmi na zisizo rasmi). Umeathiri elimu, afya, usalama, na hata umoja wa taifa. Kutokulielewa tatizo hili kwa mtu anayetaka kugombea nafasi ya Urais (haijalishi anatokea chama gani) ni kutokuelewa namna ya kukabiliana na changamoto nyingine zote.

Kwa sababu hii peke yake Lowassa na mgombea mwingine yeyote ambaye haweki "ufisadi" kama ajenda yake ya kwanza na kubwa zaidi basi hafai. Kwa sababu atatuzungusha kwenye madudu mengine yote isipokuwa kwenye kumkoma nyani giledi.

Kikwete - kwa wanaokumbuka - alishabikiwa na wengi si kwa sababu ya "Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya" bali zaidi kwa kuwapa Watanzania matumaini kuwa atashughulikia ufisadi vikali. Hotuba yake ya kulifungua Bunge na ile ya Ngurdoto na zile ziara zake za kutembelea Wizara ziliwafanya watu waamini kidogo kuwa hatimaye "kipele kimepata mkunaji". Leo hii miaka tisa baadaye ripoti ya CAG imeonesha kidogo tu kuwa tatizo hili la ufisadi halijapata mtatuzi ndani ya CCM na hata mtu anayeshabikiwa sana kuwa ati anaweza kuwa Rais inaonekana tatizo hili limempita kabisa.

Nikisema "hafai" simsingizii; nasema kilicho dhahiri; I'm just stating the obvious.

Wanaomtaka Lowassa - wapenzi, mashabiki na waumini wake - watuambie vita dhidi ya ufisadi ina umuhimu na uzito gani katika agenda za Lowassa. Wakituambia kuwa "ni mojawapo" ya mambo atakayoyashughulikia tuendelee kumkataa kwa sababu bado atakuwa hajaelewa tatizo letu hasa ni nini kama taifa.

Nitandelea...

NB: Kwa wageni wa hoja hizi warejee mada yangu ya 2007: Kikwete Siyo Safi, Yes I said it


Hapa chini ni hotuba ya Lowasa! Angalia ktk road map 9 Yake ile hoja ya 3 amezungumzia rushwa! Unaweza kuona amejikaza kuongolea hayo maswala lkn kwa mtazamo wangu ni kwamba sio kz rahisi kipamba na rushwa ktk chama chake.

Saturday, May 30, 2015
Hotuba Ya Mh. Edward Lowassa
Aliyoitoa LEO jijini Arusha Wakati
Akitangaza Nia Ya Kuomba Kuteuliwa
na CCM Kuwa Mgombea Urais Wa
Tanzania
UTANGULIZI:
Ndugu zangu wana-CCM na Watanzania wenzangu,
Hii ni siku muhimu kwangu na kwa nchi yetu. Leo nimeamua
kuwaita ili kuwatangazia rasmi Watanzania wenzangu azma yangu
ya kutaka kuomba ridhaa ya chama chetu, Chama Cha Mapinduzi
(CCM), niweze kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Nasema hii ni siku muhimu kwangu kwa sababu naamini historia
yangu itainakili kama ni siku ambayo kwa mara ya pili katika maisha
yangu nimejitokeza kuwania kuiongoza nchi yetu kupitia chama
chetu. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1995 wakati wa uchaguzi
wa kwanza wa vyama vingi hapa nchini nilipojitokeza nikiwa
pamoja na Rais Jakaya Kikwete; wakati ule sote tulikuwa wanasiasa
vijana. Tulikwenda pamoja kuchukua fomu ndani ya Chama na
baadaye tukafanya mazungumzo ya pamoja na waandishi wa
habari. Tulileta hamasa kubwa pale tulipofanya jambo ambalo
halikuzoeleka kwa Watanzania kwa kutangaza kwamba yeyote
atakayepita kati ya wawili sisi basi mwenzake ambaye hatafanikiwa
angemuunga mkono.
Ningeweza kujitokeza tena mwaka 2005 lakini nikaamua kwa dhati
kabisa kumuunga mkono moja kwa moja Rais Jakaya Kikwete.
Nikiwa Mwenyekiti wa Kampeni niliwaongoza wenzangu
kufanikisha ushindi mkubwa wa mgombea tuliyemuunga mkono na
baadaye ushindi mkubwa wa asilimia 80 wa Chama Cha Mapinduzi
kwenye uchaguzi mkuu wa 2005.
Nitaeleza kwa nini nimeamua kujitokeza tena mwaka huu na kwa
nini naamini mimi ndiye mtu sahihi wa kuiongoza nchi yetu wakati
huu. Mpaka hapa itoshe tu kuwaeleza ni kwa kwa nini naamini leo
ni siku muhimu kwangu.
Lakini nasema ni siku muhimu kwa nchi yetu pia. Nasema hivyokwa
sababu naamini inajibu wito wa mahitaji ya sasa ya uongozi wa
Taifa letu wa kumpata kiongozi imara atakayewaongoza
Watanzania kujenga taifa imara. Na hili pia nitalieleza kwa kina.
Hali ya Nchi na Matarajio ya Watu:
Miaka 48 iliyopita katika jiji hili la Arusha, Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Kambarage alianzisha mchakato wa kujenga taifa huru
kiuchumi na kupiga vita maadui umaskini, ujinga na maradhi
kwakutumia silaha ya kujitegemea.
Leo hii, wakati taifa likijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu ujao, hatuna
budi kutafakari tulikotoka, tulipo na tunapotaka kwenda ili tuweze
kubuni upya mikakati ya kuhitimisha azma aliyo kuwa nayo
Mwalimu, ili tujenge taifa huru, lenye utulivu, mshikamano, amani
na maendeleo.
Nchi yetu hivi sasa inapita katika kipindi kigumu cha mpito katika
maeneo yote makuu ya maisha yetu – katika siasa, katika uchumi
na katika maisha ya kijamii.
Kisiasa, tumeshuhudia kuongezeka kwa vuguvugu la mfumo wa
vyama vingi ambapo ushindani kati ya vyama vya siasa unazidi
kuwa mkali na kwa bahati mbaya kufikia sura ya kuonekana kama
vile ni mapambano ya watu binafsi badala ya mapambano ya sera
na dira ya kuongoza nchi.
Tunashuhudia kuongezeka uhasama binafsi kati ya wanasiasa
ndani ya chama kimoja kimoja na pia kati ya wanasiasa wa chama
kimoja dhidi ya kingine. Kadiri siku zinavyokwenda, hali inazidi
kuzorota na ikiachiwa kuendelea nchi yetu inaweza kujikuta mahali
pabaya.
Kukua kwa ushindani ni jambo jema linalokomaza na kurutubisha
demokrasia yetu na tukiwa na ushindani wenye afya unaweza kuwa
chachu ya kuleta mabadiliko mema kwa wananchi na kupelekea
kuongezeka kwa kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika
nchi yetu.
Kinyume chake ushindani unaochukua sura ya chuki binafsi au
kukomoana na hata kulipizana visasi si ushindani wenye tija na
tunapaswa kuutafutia tiba.
Tunahitaji uongozi imara kusimamia kipindi cha mpito kutoka siasa
muflisi za aina hii na kuelekea kwenye siasa mpya zinazoimarisha
ushindani wenye tija unaojikita katika kushindana katika kuwapatia
huduma bora Watanzania.
Kiuchumi, tumeshuhudia ukuaji mzuri na kuongezeka kwa mapato
ya ndani ya Serikali na uimarishaji wa mfumo wa uwajibikaji na
ulipaji kodi.
Kwa upande mwengine, Serikali ya Rais BenjaminiMkapa na Rais
Jakaya Kikwete imefanya kazi kubwa katika uendelezaji wa sekta ya
mafuta na gesi asilia ambapo kiwango kikubwa cha gesi asilia
kimegunduliwa.
Tanzania sasa imekuwa ni miongoni mwa nchi zinazovutia
uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo ambayo inatajwa kwamba
inaweza kuja kubadilisha kabisa maisha ya Watanzania.
Hata hivyo, kipindi hiki cha mpito kuelekea ujenzi wa uchumi wa
kisasa kimeshuhudia kuongezeka kwa hofu na wasiwasi miongoni
mwa wananchi kwamba hawatonufaika naukuaji huu wa uchumi na
ugunduzi wa utajiri mkubwa wa gesi asilia.
Kwa upande mwingine, vijana wanataka kuona ukuaji wa uchumi
na ugunduzi wa utajiri huo unakwenda sambamba na uzalishaji wa
ajira zenye maana ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha
yao.
Niliwahi kusema kwamba tatizo la ukosefu wa ajira likiachiwa bila
ya kutafutiwa ufumbuzi imara ni bomu linalosubiri kulipuka.
Vijana wasio na ajira hupoteza matumaini na ni rahisi kughilibiwa
kuingiza nchi katika machafuko.Tunahitaji uongozi imara kuweza
kuikabili hali hiyo na kuitafutia suluhisho maridhawa.
Kijamii, kipindi cha karibuni tumeshuhudia mabadiliko makubwa ya
tabia miongoni mwa raia katika hali ambayo haijawahi kuwa
sehemu ya utamaduni wa Watanzania.
Kumekuwa na ongezeko la kutisha la matukio ya uhalifu
linalokwenda sambamba na wananchi kuonyesha wanapoteza
imani na taasisi zinazosimamia sheria na usalama na kuamua
kujichukulia sheria mikononi mwao.
Kumeripotiwa matukio mengi yakiwemo ya kuvamiwa vituo vya
polisi, askari kupigwa na kuporwa silaha, matumizi makubwa ya
nguvu katika utatuzi wa migogoro mbalimbali hasa ile ya kijamii,
mathalani migogoro ya wakulima na wafugaji, mivutano ya kidini na
pia mivutano baina ya viongozi wa dini wenyewe kwa wenyewe na
baina ya viongozi wa dini na wale wa Serikali.
Matokeo yakemshikamano wa taifa nao unaingia majaribuni. Mara
nyingine wananchi wanatuuliza viongozi iwapo hii ndiyo nchi
tuliyoachiwa na waasisi wetu. Tunahitaji uongozi imara wa
kukabiliana na changamoto hizi na kurudisha mshikamano wa taifa
letu na watu wake.
Watanzania Wanataka Mabadiliko;
Ndugu zangu, mnaweza kujiuliza kwa nini nimeyaeleza yote hayo
na yana mahusiano gani na dhamira yangu ya kutangaza nia ya
kutaka kuiongoza nchi yetu kupitia CCM?
Nimeyaeleza haya kwa sababu haya na matukio mengine
yanayoendelea nchini yamepelekea Watanzania kutaka mabadiliko.
Watanzania wanataka mabadiliko yatakayowawezesha kuzishinda
changamoto hizi na kuwaongoza kujenga Taifa imara ambalo kila
mwananchi wake anaishi akiwa na uhakika wa mahitaji yake
muhimu na papo hapo akijiridhisha kwamba leo yake ni bora kuliko
jana yake, na kesho yake itakuwa bora zaidi kuliko leo yake.
Kwa maneno mengine, Watanzania wanahitaji mabadiliko
yatakayowapa uongozi imara unaoweza kuwaongoza kujenga
taifaimara. Hii ndio Safari ya Matumaini.
Chama chetu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), na watangulizi wake,
TANU na ASP, kimepata bahati ya kuungwa mkono na Watanzania
tokea enzi za kupigania uhuru, wakati wa Uhuru wa Tanganyika na
Mapinduzi ya Zanzibar, na pia miaka yote tokea Uhuru, Mapinduzi
na hatimaye Muungano wetu. Watanzania hawajawahi kushuhudia
chama kingine kikiongoza Serikali zetu zaidi ya CCM. Wamekiamini
na wanaendelea kukiamini.
Hata katika yale majimbo machache ya nchi yetu ambayo
hatukufanya vizuri katika uchaguzi, ukiangalia kwa undani utaona si
kwamba watu wa maeneo hayo wana matatizo na CCM kama
Chama bali wana matatizo na baadhi ya viongozi ambao
walishindwa kukiwakilisha vyema Chama na kutambua matakwa ya
wananchi hao.
Mimi naamini kwamba hata katika kipindi hiki ambapo Watanzania
wanaonekana kutaka mabadiliko bado wanaendelea kuamini
kwamba watayapata mabadiliko hayo ndani ya CCM.
Lakini kama alivyotupa wasia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere, mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya
mfumo wa vyama vingi hapa nchini, Watanzania wasipoyapata
mabadiliko hayo ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM.
Mimi naamini kwamba CCM tunao uwezo wa kuwapa Watanzania
mabadiliko wanayoyataka. Tuwape imani na imani hiyo iwe ni ya
dhati na ya ukweli kwamba CCM inao uwezo wa kuwapa uongozi
imara wanaouhitaji kwa ajili ya kujenga taifa imara.
Vyama vya siasa vinajumuisha watu na vinaongozwa na watu.
Moja ya hulka ya binadamu ni kubadilika kulingana na mahitaji ya
mazingira anayoishi.
Kwa maneno mengine, binadamu ni ‘dynamic’. Kwa sababu hiyo
basi, hata vyama vya siasa vinapaswa kuwa ‘dynamic’.
CCM haijapata kuwa na upungufu wa sifa ya ‘dynamism’. Kwa zaidi
ya miongo mitano sasa, CCM (na kabla yake TANU na ASP) iliweza
kubadili dira na mwelekeo wake ili kwenda sambamba na mahitaji
ya Watanzania ya wakati husika.
Ndiyo maana tumepita katika vipindi tofauti vya mpito kwa
mafanikio makubwa licha ya changamoto nyingi zilizotukabili.
Tanzania imeendelea kuwa nchi ya amani licha ya kubadili mfumo
wetu wa siasa kutoka ule wa chama kimoja kuja vyama vingi; licha
ya kubadili mwelekeo wa uchumi wetu kutoka ule wa dola kumiliki
njia zote kuu za uchumi kuja katika uchumi wa soko unaozingatia
ushiriki mpana wa Watanzania wa matabaka yote; na hata karibuni
kabisa katika mchakato wa kuipatia nchi yetu Katiba mpya.
Tanzania tumeweza kufanya mabadiliko ya uongozi mara nne
katika hali ya amani na maelewano, jambo ambalo nchi nyingi za
Afrika zimeshindwa.
Ni imani yangu kwamba tukijikubalisha tunaweza tena kuwapa
Watanzania wanachokitaka katika zama hizi za sasa.
Lakini ni lazima tuoneshe dhamira hiyo kwa dhati ili, kama
alivyotuasa Mwalimu Nyerere, Watanzania wasiyatafute mabadiliko
hayo nje ya CCM.
Nasisitiza tena kwamba CCM inao uwezo wa kuwapa Watanzania
mabadiliko wanayoyataka, lakini pia wananchi wana hiali kuchagua
mabadiliko wanayoyataka.
Uongozi unaohitajika kuleta mabadiliko yanayotakiwa:
Rais Jakaya Kikwete amefanya kazi kubwa katika kipindi chake na
kama ambavyo amekuwa akisisitiza mara kwa mara katika hotuba
zake za karibuni ni kwamba yeye ametekeleza wajibu wake kwa
kuweka misingi imara ya ujenzi wa Taifa la kisasa lenye uchumi
madhubuti na unaoweza kukua kwa kasi.
Amesema anamwachia atakayemkabidhi uongozi wa nchi yetu
baada ya yeye kumaliza muda wake kuendeleza pale atakapoachia.
Kwa maoni yangu ili kuifanya kazi hiyo na kuzikabili changamoto
nilizozieleza, nchi yetu inahitaji uongozi wenye sifa zifuatazo:
- Uongozi wenye uthubutu, usioogopa kufanya kufanya maamuzi
magumu;
- Uongozi thabiti na usioyumba;
- Uongozi makini na mahiri;
- Uongozi wenye ubunifu na wenye upeo mkubwa;
- Uongozi utakaozikabili changamoto kifua mbele na siyo
kuzikimbia;
- Uongozi unaoamini katika mfumo shirikishi katika ujenzi wa
Taifa;
- Uongozi unaozingatia muda katika kutekeleza majukumu yake.
Naamini pia kwamba wananchi wanataka Rais ajaye wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania awe na sifa kuu zifuatazo:
- Aweze kuwaunganisha Watanzania (kukabiliana na viashiria vya
migawanyiko ya aina mbali mbali inayoinyemelea Tanzania);
- Aweze kuja na sera na mikakati ya kuinua uchumi wa Tanzania
na kukuza pato la Mtanzania;ikiwemo kupunguza tofauti ya kipato
kati ya aliyekuwanacho na wasiokuwanacho;
- Aweze kuja na sera na mikakati ya kuzalisha ajira kwa vijana
wetu;
- Aweze kutokomeza mianya ya rushwa kwa vitendo;
- Aweze kuwa mfano wa kuchapa kazi na kuwajibika;
- Asimamie nidhamu ya matumizi ndani ya Serikali;
- Aweze kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali;
- Aweze kutumia fursa yetu ya kijiografia kibiashara
Uongozi Imara,Taifa Imara
Naamini kwamba uongozi wa juu wa nchi katika nafasi ya Urais si
kazi ya lelemama na unahitaji utashi. Kabla hata ya kutakiwa na
wenzako ni lazima kwanza wewe mwenyewe uamini na
uwaaminishe wenzio kwamba unao uwezo wa kuwaongoza
wananchi wenzako. Na katika hilo, rekodi yako ni lazima izungumze
na kulithibitisha hilo.
Binafsi nina hazina ya uzoefu na rekodi njema ya matokeo ya kazi
nilizozifanya katika uongozi na utumishi wa umma ndani ya CCM na
ndani ya Serikali. Nilianza kazi nikiwa Katibu Msaidizi wa CCM
katika mikoa ya Shinyanga, Arusha na Moshi.
Nimekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu ya
CCM. Niliingia Bungeni mwaka 1985 na baadae mzee wangu, Rais
Ali Hassan Mwinyi, akaniamini kwa kuniteua kuwa Waziri.
Nimekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Ardhi,
Makaazi na Maendeleo ya Miji, Waziri wa Mazingira, Waziri wa Maji
na hatimaye Waziri Mkuu.
Miongoni mwa mafanikio ninayojivunia katika uongozi na utumishi
wangu, na ambayo Watanzania wanayatambua na naamini
wanayathamini, ni pamoja na:
- Nikiwa Waziri wa Maji chini ya uongozi mahiri wa Rais
Mkapa,tulithubutu kushawishi na kuongoza hatua za kukataa
kufungika na makubaliano yaliyowekwa na wakoloni ambayo
yalikuwa yanazizuia nchi zilizopakana na Ziwa Victoria zisiweze
kufaidika ipasavyo na maji ya Ziwa hilo. Leo hii ndugu zangu wa
Kanda ya Ziwa wanafaidika na ujasiri wetu katika kukabiliana na
suala hilo zito.
- Nikiwa Waziri wa Mazingira, tulipanda miti mingi zaidi kuliko
wakati mwingine wowote tokea Uhuru na pia kuwakabili kikamilifu
na kuwachukulia hatua waliochafua na kuharibu mazingira.
- Nikiwa Waziri Mkuu, tulisimamia agizo la Rais Kikwete na
kufanikisha utekelezaji wake ndani ya miaka miwili kwa kujenga
shule nyingi za sekondari kuliko wakati mwingine wowote tokea
Uhuru.
- Kipindi hicho hicho, tulisimamia agizo la Rais Kikwete la
kuanzisha Chuo Kikuu cha Dodoma na kuhakikisha kinakamilishwa
kwa wakati. Leo hii Chuo Kikuu hicho ni fahari ya Tanzania.
Tunapomtafuta Rais wa Jamhuri ya Muungano ni lazima
tukumbuke kwamba tunamtafuta mtu ambaye atakuwa pia ni Amiri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika nchi yetu. Na
kwa Chama Cha Mapinduzi tunamtafuta mtu ambaye atakuwa pia
Mwenyekiti wa Chama chetu.
Naamini kwa vigezo vyote, nina kila sifa ya kubeba dhamana hizo
nzito. Katika mambo ambayo najivunia na sitoyasahau katika
historia yangu ni kushiriki kwangu kuilinda nchi yangu pale
ilipohitajika.
Nilishiriki kikamilifu katika Vita vya Kagera nikiwa miongoni askari
wa mstari wa mbele wa mapambano. Nikiwa Mbunge nilipata
heshima ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Naamini Watanzania hawatakuwa na wasiwasi wa usalama wao
nikiwa Amiri Jeshi Mkuu.
Nimeeleza uzoefu wangu kwenye Chama na huo hauhitaji maelezo
zaidi. Ninakijua vyema Chama Cha Mapinduzi kiasi cha kutosha
kabisa kukiongoza kama Mwenyekiti wake pale wakati utakapofika.
Wana-CCM wanajua nikikabidhiwa uongozi, Chama chetu kitakuwa
chini ya nahodha madhubuti, mzoefu na asiyeyumba.
Kutokana na rekodi yangu hii, naamini ninazo sifa za kuwaongoza
Watanzania wenzangu katika zama mpya za ujenzi wa Taifa la
kisasa lenye watu wazalendo walioshikamana na lenye uchumi
imara unaomnufaisha kila Mtanzania. Naamini ninao uwezo wa
kuwapa Watanzania Uongozi imara kwa ajili ya ujenzi wa Taifa
Imara.
Dira yangu na Matarajio ya Watanzania
Mfumo tuliojiwekea hapa nchini unaelekeza kila chama cha siasa
kinachosimamisha mgombea Urais na kinachowania kuongoza nchi
yetu kuja na Ilani ya Uchaguzi ambayo ndiyo inayoweka misingi ya
sera zitakazofuatwa na Serikali itakayoongozwa na chama hicho
pale kinapopewa ridhaa ya kuongoza nchi.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa ni cha kupigiwa mfano
katika kutayarisha Ilani bora na ndiyo maana mara zote kimepewa
ridhaa ya kuongoza nchi yetu. Tumefanya hivyo tokea enzi za
mfumo wa chama kimoja na tumeendelea kufanya vizuri katika
mfumo wa kushindanisha sera kupitia vyama vingi.
Najua kwamba Ilani ya CCM ya mwaka 2015 imo katika hatua za
mwisho za kukamilishwa na itakapopata baraka za vikao vya
Chama itakuwa ndiyo msingi wa utendaji wa Serikali ya Awamu ya
Tano itakayochaguliwa Oktoba mwaka huu.
Hata hivyo, naamini pia kwamba mgombea mwenyewe anayetaka
ridhaa ya Chama na ya Watanzania kuongoza nchi naye anapaswa
kueleza dira yake.
Mimi, baada ya kutafakari kwa kina changamoto tulizo nazo na
matarajio na matumaini waliyo nayo Watanzania, naamini kwamba
Uongozi imara unaolenga kujenga Taifa imara unapaswa kuwa na
dira yenye malengo yafuatayo:
- Kuimarisha Muungano wetu kwa kuyashughulikia
yanayotutenganisha na kuyafanyia kazi ili yasivuruge yale
yanayotuunganisha ambayo ni mengi zaidi na makubwa zaidi.
- Kushughulikia matumizi mabaya ya siasa za udini na ukabila
kwa kuimarisha siasa zilizoshiba uzalendo na zenye kutuelekeza
kwenye Utanzania wetu.
- Kujenga uchumi imara na wa kisasa, na ambao ni shirikishi
unaomnufaisha kila Mtanzania aliyeko mjini au kijijini. Tunapaswa
kubadili hali tuliyo nayo sasa ambapo Kilimo kinaonekana kama
kimesahauliwa na wakulima wetu wanaonekana wanakata tamaa.
Wafugaji na wavuvi nao wanahisi sekta zao hazijapewa umuhimu
unaostahiki. Tunahitaji kuondokana na hali iliyopo sasa ya kuwa
Taifa linalouza malighafi na badala yake kuwa Taifa linalosindika na
kusarifu mazao na kutengeneza wenyewe bidhaa zitokanazo na
malighafi yake.
Ndani ya miaka mitano ijayo tutahakikishatunaiondolea Tanzania
sifa ya kusafirisha malighafi na badala yake kusindika mazao
yanayozalishwa hapa nchini kama pamba, kahawa, chai na korosho
na kuyaongezea thamani (value addition).Mkakati huu utazalisha
ajira nyingi na kuongeza mapato ya fedha za kigeni nchini.
Tunahitaji kujielekeza kwenye kujenga viwanda na kuleta ajira.
Tuna vivutio vingi sana vya utalii lakini bado Tanzania inapitwa na
nchi kama Afrika Kusini katika kuingiza idadi kubwa ya watalii.
Kwa nini nchi kama Dubai iweze kuvutia watalii kwa mamilioni na
Tanzania tushindwe? Tunapaswa kukabiliana kikamilifu na hisia
zilizopo miongoni mwa wananchi kwamba Tanzania hainufaiki
ipasavyo na utajiri wa rasilimali zake nyingi ilizo nazo.
Tutajipanga zaidi kuhakikisha tunanufaika kama nchi na rasilimali
zetu kama madini na gesi asilia. Hii ndio Safari ya Matumaini
- Kukuza kipato cha wananchi na kunyanyua hali za maisha ya
watu wetu. Tunapaswa kuhakikisha kuwa ukuaji wa uchumi
tunaouzungumzia unamnufaisha Mtanzania aliyeko mjini au kijijini
na kwamba hali za Watanzania wa matabaka yote zinanyanyuka na
kwamba wanaridhika na kuuona uhalisi wa ukuaji wa maendeleo
tunayoyazungumzia.
- Kuondokana na sifa mbaya ya kuwa Taifa ombaomba. Kwa wingi
wa rasilimali tulizo nazo na neema ya ardhi, maziwa, mito na bahari
Tanzania tuna kila sababu ya kuacha kuwa ‘bakuli la ombaomba’ na
badala yake kuwa ‘mkoba wa neema’ katika Afrika.We can
transform our nation from being the begging bowl to become the
bread basket of Africa.
- Kujenga mfumo mpya wa elimu unaojielekeza kuwatayarisha
vijana wetu waweze kuajirika, kujiajiri na kushindana katika soko la
ajira.
Tumepiga hatua kadhaa katika elimu lakini kiwango cha elimu bado
ni hafifu. Pamoja na kuwa na shahada (degrees), bado wahitimu
wetu hawawezi kushindana kwenye soko la ajira.
Wakati tunazungumzia kuunganisha soko la ajira katika Afrika
Mashariki,hatuna budi kujikita kubadili mfumo wetu wa elimu na
kuuelekeza kwenye mafunzo ya ufundi na stadi yanayowajenga
wahitimu wetu kuwa wabunifu na wenye kujiamini katika
kukabiliana na changamoto za maendeleo duniani.
- Kuhakikisha tunakabiliana ipasavyo na kulipunguza kwa kiasi
kikubwa kama si kulimaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa maji safi
na salama. Ni jambo la kusikitisha kwamba tumezungukwa na mito
na maziwa lakini bado watu wetu hawana maji ya kunywa hata
ndani ya Dar es Salaam.
- Kujenga na kusimamia mfumo imara wa kutekeleza sera na
sheria tunazozitunga na kuzipitisha kwa lengo la kumtumikia
Mtanzania na kumjengea uwezo wa kubadili maisha yake ili tuweze
kwenda sambamba na viwango vya kimataifa. Tanzania imepata
sera na sheria nzuri sana lakini utekelezaji wake umekuwa hafifu.
Tumekuwa wepesi wa kutunga sera na sheria lakini wazito mno wa
kuzitekeleza na kuzisimamia. Uongozi imara wenye kulenga ujenzi
wa Taifa imara utahakikisha tunakuwa mfano wa utekelezaji wa
sera na sheria tulizo nazo na mpya zitakazotungwa kukabiliana na
malengo tuliyojiwekea.
Mambo haya niliyoyaeleza hapa ndiyo yatakayokuwa msingi mkuu
wa utendaji wa Serikali nitakayoiongoza pale nitakapopewa ridhaa
ya kubeba bendera ya CCM katika nafasi ya Urais na pia
nitakapopewa ridhaa ya kuliongoza Taifa letu kupitia uchaguzi
mkuu wa mwaka huu.
Ramani ya Uongozi Imara Ninaouamini 9 Leadership Roadmap)
Kama nilivyotangulia kusema, kazi ya kuongoza nchi si lelemama
na hasa unapoongozwa na dhamira ya dhati na msukumo wa ndani
ya nafsi unaojielekeza kubadilisha maisha ya wananchi wenzako
waliokuamini uwaongoze. Kwa vyovyote vile, hiyo haiwezi kuwa
kazi ya mtu mmoja. Ni kazi ya pamoja.
Lakini ili muweze kufanya kazi kama timu moja iliyojipanga
kisawasawa kuleta mabadiliko yanayohitajika na ili muweze kweli
kutoa Uongozi imara unaojikita kujenga Taifa imara hapana budi
kiongozi mkuu anayeongoza timu hiyo aweke ramani anayokusudia
kuifuata katika kutoa uongoziimara anaoukusudia yaani ‘Leadership
Roadmap’.
Pamoja na kuwa sehemu ya uongozi huko nyuma, kutakuwa na
maamuzi na matumaini mapya. Ramani ya uongozi
imaraninayokusudia kuutoa kwa wenzangu na ambayo nitaitumia
kuiongoza timu yangu katika kuwatumikia Watanzania wenzangu
itajikita katika maeneo yafuatayo :
1. Kurejea kwenye Katiba katika kuainisha nia, dhamira na malengo
yetu ya kujenga jamii inayozingatia misingi ya demokrasia, udugu
na amani. Muhimu katika hili ni kukemea tabia mbaya
zinazochochea mfarakano katika jamii kama vile matumizi mabaya
ya siasa za udini na ukabila.
Aidha moja ya misingi muhimu ya Katiba ni Muungano wetu.
Itakuwa dhamira yangu kuimarisha misingi ya Muungano pamoja
na udugu wa damu nahistoria ya ushirikiano iliyojengwa na waasisi
wetu, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati
Sheikh Amri Abeid Karume na kuyaenzi Mapinduzi matukufu ya
Zanzibar.
2. Kujenga fikra mpya za kurejesha kujiamini na kufufua azma ya
kujitegemea kama Taifa. Ni dhahiri kuwa pamoja na rasilimali zetu,
bado Tanzania ni taifa tegemezi. Bado tunajidanganya kuwa
wafadhili watatujengea nchi. Tukumbuke, nchi zinajengwa
nawananchi wake.
Nasi pia lazima tujikomboe kifkra na tuondokane na utamaduni wa
kuwa tegemezi. Tuanze kwa kujipiga kifua kwa kujiamini kuwa
tunaweza kujitegemea na kuijenga Tanzania sisi wenyewe.Kujiamini
na kujitegemea ndio uhuru wa kweli.
3. Kujenga uzalendo, uadilifu ikiwa ni pamoja na kuimarisha uwazi
katika shughuli zote za serikali na kupambana na
rushwa.Watanzania tumepoteza uzalendo kwa kiasi kikubwa. Kuna
vitendo vinavyoashiria kuwa hatuipendi tena nchi yetu.
Tunashabikia wizi na rushwa. Inabidi turejee kwenye misingi ya
taifa letu misingi ya uadilifu na uzalendo. Tukumbuke kuwa
hatuwezi kujenga uchumi wa kisasa kama tutaruhusu rushwa
ishamiri.
Wawekezaji hawataleta mitaji yao kwa wingi kama rushwa
itaendelea kutawala katika huduma serikali na wananchi hawawezi
kupata huduma bora kama rushwa itaendelea kutawala. Ni lazima
tuipinge rushwa kwa vitendo sio maneno.
4. Kujenga Serikali madhubuti, makini na yenye nidhamu
inayoendeshwa kwa misingi ya sheria, uwazi na
uwajibikaji.Maendeleo ya watu hayawezekani bila serikali
kusimamiautekelezaji sera na miradi na kuleta ufanisi katika kutoa
huduma na kusimamia maendeleo. Tumekuwa wepesi wa kutunga
sera lakini wazito wa kuzitekeleza na kuzisimamia.
5. Kuleta msukumo mpya wa ushirikiano kati ya serikali na sekta
binafsi katika ujenzi wa uchumi wa kisasa na unaojitegemea. Sekta
binafsi ndiyo nyenzo ya uchumi imara. Inazalisha mali, ajira na
kuchangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa kwa kulipa kodi.
Ilisekta hii itoe mchango unaotakiwa katika maendeleo ni lazima
ifanye kazi na serikali kwa karibu. Tukumbuke, bila uchumi
imarahakuna huduma bora!
6. Uwekezaji katika huduma za jamii. Elimu na afya bora, mazingira,
makazi safi na maji salama ndiyo mihimili ya maendeleo ya watu.
Hii inawezekana tu iwapo serikali itakuwa na sera na utashi wa
kuutambua uboreshaji wa huduma za jamii kama ndiyo lengo kuu la
maendeleo ya nchi. Serikali nitayoiongoza itahakikisha kuwa kila
Mtanzania anapata elimu bora na inayogharamiwa na serikali kama
mimi na wenzangu tulivyopata.
Wakatitunazungumzia kuunganisha soko la ajira katika Afrika
Mashariki, hatuna budi kurekebisha mfumo wetu wa elimu na
kuuelekeza kwenye mafunzo ya ufundi na ustadi yanayowajenga
wahitimu wetu kuwa wabunifu, wenye kujiamini, wenye uwezo
kushindana katika soko la ajira na wa kujiajiri. Napenda kusisitiza
kuwa elimu ndiyo muhimili wa maendeleo, ndiyo mkombozi wa
kweli wa binadamu. Mimi ni mfano hai wa ukombozi wa elimu.
Elimu ndiyoimenivusha kutoka kijijini kwetu Ngarash na kunipa
upeo wa kitaifa. Mama akiwa na elimu atajua umuhimu wa
kumpeleka mwanae shule, anapata lishe bora na chanjo stahili na
kuwa anaishi katika mazingira safi. Elimu ndilo jibu la umaskini,
maradhi na ujinga.Taifa lililo elimika ni taifa lenye maendeleo.
7. Kujenga uchumi shirikishi unaolenga kuondoa umaskini.Mkakati
wa kuondoa umaskini Tanzania lazima ujikite kwenye nguzo za
ushiriki wa kila Mtanzania katika uchumi wa taifa.
Kwa misingi hii, tukiweza kupunguza umaskini, tutaweza pia
kupunguzatofauti za kipato ambazo tukiziacha ziendelee kukua kwa
kiasi cha sasa, zinaweza kuhatarisha utulivu na amani katika jamii
yetu.Uchumi shirikishi ndio silaha dhidi ya umaskini.
8. Kuimarisha ulinzi wa nchi na usalama wa raia na ujirani
mwema.Itakuwa nia yangu kuimarisha misingi iliyojengwa kulinda
na kudumisha umoja na amani nchini.
Kadhalika, nitahakikisha kuwa usalama wa mipaka ya Tanzania
unaimarishwa kwa misingi ya ujirani mwema na kutanzua migogoro
na matatatizo yoyote na nchi jirani, kwa njia ya diplomasia na
mazungumzo.
Hitimisho:
Hii ndiyo misingi na dira ya uongozi wangu. Nachelea kusema kuwa
haitakuwa kazi rahisi. Lakini kwa ushirikiano wa kila mmoja na
maamuzi magumu, yote yanawezekana.
Tumeona nchi nyingi zilizosimamiwa na utawala thabiti wa serikali
za kimaendeleo zikikabili na kupunguza umaskini katika kizazi
kimoja. Kama mataifa mengine yamefanikiwa, tena bila raslimali
kama zetu, kwa nini sisi tushindwe?
Tuna kila sababu ya kufanya maamuzi magumu sasa ili kuwajengea
Watanzania matumaini mapya ya maendeleo. Naomba nisisitize
kuwa katika uongozi wangu hakutakuwa na nafasi ya majungu, na
visasi. Hatutaangalia nyuma bali tutasonga mbele kwani ndicho
Watanzania wanakitarajiakutoka kwa uongozi uliojengwa kwenye
misingi bora.
Ndugu Watanzania:-
Ni maono yangu kuwa siku si nyingi nchi yetu itaanza safari yenye
uelekeo wa matumaini na neema tele kwa wananchi.
Ni maono yangu kuwa siku si nyingi sisi kama Watanzania kwa
umoja wetu tutajivunia kuishi katika nchi tunayoipenda na
inayoendeshwa kwa misingi ya utawala bora, chini ya serikali ya
kimaendeleo iliyojengwa kwenye fikra mpya za uzalendo, uadilifu,
utendaji na uwajibikaji.
Ni maono yangu kuwa Peke yangu sitaweza, lakini kwa maamuzi
magumu na ushirikiano wa kila mmoja wetu ikiwa ni pamoja na
wagombea wenzangu ndani ya CCM, inawezekana kuanza safari hii
ya Matumaini Mapya.
Kabla ya kumaliza hotuba yangu hii fupi, kuna mambo matatu
ningependa kuyaweka wazi hapa.
La kwanza, linahusu msingi wa uongozi ninaouamini na ambao
nimeusema mara kadhaa hapa. Msingi huo ni
UWAJIBIKAJI.Watanzania wananifahamu mimi si mtu wa maneno,
ni mtu wa vitendo. Naamini kwa dhati kabisa kwamba huwezi kuwa
na Uongozi imara utakaoweza kusimamia ujenzi wa Taifa imara
iwapo huna ujasiri wa kuwajibika. Mimi nimeongoza kwa mfano, na
pale ilipobidi, nilikubali kuwajibika na kubeba dhamana ya
uongozinilipojiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu.
La pili, mimi si mtu wa visasi. Siamini katika kuangalia ya nyuma.
Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Na kwa nini tuangalie nyuma
wakati kama taifa tuna kazi kubwa sana mbele yetu inayohitaji
kufanywa? Mimi ni Mkristo; najifunza kutoka kwa Bwana Yesu
ambaye alipoulizwa: “Nisamehe mara ngapi?” Alijibu, “Samehe mara
sabini mara saba”. Nitaenzi na kudumisha utamaduni huu wenye
sura ya utu na heshima.
La Tatu, natambua kwamba dhamana ya Urais ni shughuli nzito
hasa kwa taifa ambalo lina changamoto nyingi. Nataka
niwahakikishie Watanzania wenzangu kwamba afya yangu ni njema
kuweza kuwatumikia katika jukumu hili zito. Pamoja na vijineno
vinavyosemwa pembeni, mimi mwenyewe ndiye ninayejijua zaidi.
Nawahakikishia kuwa nisingekuja hapa leo na kueleza nia yangu hii
ingekuwa sina uhakika na afya yangu.
Natoa RAI kwa Chama changu cha CCM, nadhani umefika wakati
kwamba tutende tofauti na mazoea, watu wote walionyesha nia ya
kutaka kuongoza, liundwe jopo la madaktari wa ndani na nje ya nchi
tupimwe afya zetu, kwa hili najitolea kuwa wa KWANZA KUPIMWA
afya yangu
Safari tuianze leo, hatuna kesho nyingine.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.
 
Nimegundua Ujanja mkubwa wa lowasa ni kusahaulisha watu kilichotokea hasa 2007. Asitufanye watu wazima ni mabwege.

Kwa wale wenye nafasi inabidi zitengenezwe dossier kuonesha makosa na ufisadi wa Lowassa na wenzake 2007 kwenye sakata ra richmond.
 
Adolf Hitler alitumia ujanja wake wote hasa mahitaji na madhaifu ya Wajerumani wa wakati ule ili watu wampende, lakini pia alitumia ujanja wake wote ili watu wasijue moyoni kwake amekusudia kufanya nini!!.

Nayasema hayo kwa sababau nimejaribu kumfatilia Lowasa kwa muda sasa, tena nilipata bahati ya kuwa Arusha wakati ndugu Edward Lowassa anatangaza nia tarehe 30/05/2015, nilichokiona ni kundi kubwa la watanzaia wasiomjua Lowasa anaintrest gani, waliopigwa opofu na fedha ya ambayo Lowasa anaiumia kama silaha ya kuwadanganya Watanzania.

Lowasa anajulika na kuwa aliondoka madarakani kwa sababu ya scandal ya RICHMEND, hakuna Mtanzania ambaye hakuisikia, lakini nilishangaa bado watu wanamshangilia.

Taarifa zilizovuja za Wikealeaks cables zilisema wazi kuwa kuwa Lowasa in corrupt person lakini bado uwanja ulifurika kumshangilia bila kujua huwezi kuifuta tabia ya rushwa ndani ya mtu kwa kumwongezea cheo.

Speech ya Lowasa ilijaa udhaifu mwingi sana, hata hajui technics za kujisafisha, serikali ilishawahi kusema Lowasa alipatwa na ajali ya kisiasa, nilifikiri angetumia maneno ya serikali kujisafisha lakini washauri wake ama wanampango wa kumwangamiza au hawajui walimuacha akatoa speech dhaifu ajabu.

Ugonwa siyo dhambi, lakini Lowasa anayesema yuko fiti kiafya siku hiyo aliwaambia watu wacheze wimbo wa Komba wakati yeye mwenyewe hachezi mpaka aliponongonezwa ndipo alipoanza kucheza.

Hii inatosha kuwafahamisha watu afya na umri wake ni kinyume na kile ambacho anataka watu waamini.

Kama Adolf Hitler alivyofanya huyu Lowasa mnayemshangilia bila kujua akipewa urais baada ya miaka michache watanzania wataweka mikono kichwani kama Hitler alivyofanya Ujerumani.
 
Adolf Hitler alitumia ujanja wake wote hasa mahitaji na madhaifu ya Wajerumani wa wakati ule ili watu wampende, lakini pia alitumia ujanja wake wote ili watu wasijue moyoni kwake amekusudia kufanya nini!!.

Nayasema hayo kwa sababau nimejaribu kumfatilia Lowasa kwa muda sasa, tena nilipata bahati ya kuwa Arusha wakati ndugu Edward Lowassa anatangaza nia tarehe 30/05/2015, nilichokiona ni kundi kubwa la watanzaia wasiomjua Lowasa anaintrest gani, waliopigwa opofu na fedha ya ambayo Lowasa anaiumia kama silaha ya kuwadanganya Watanzania.

Lowasa anajulika na kuwa aliondoka madarakani kwa sababu ya scandal ya RICHMEND, hakuna Mtanzania ambaye hakuisikia, lakini nilishangaa bado watu wanamshangilia.

Taarifa zilizovuja za Wikealeaks cables zilisema wazi kuwa kuwa Lowasa in corrupt person lakini bado uwanja ulifurika kumshangilia bila kujua huwezi kuifuta tabia ya rushwa ndani ya mtu kwa kumwongezea cheo.

Speech ya Lowasa ilijaa udhaifu mwingi sana, hata hajui technics za kujisafisha, serikali ilishawahi kusema Lowasa alipatwa na ajali ya kisiasa, nilifikiri angetumia maneno ya serikali kujisafisha lakini washauri wake ama wanampango wa kumwangamiza au hawajui walimuacha akatoa speech dhaifu ajabu.

Ugonwa siyo dhambi, lakini Lowasa anayesema yuko fiti kiafya siku hiyo aliwaambia watu wacheze wimbo wa Komba wakati yeye mwenyewe hachezi mpaka aliponongonezwa ndipo alipoanza kucheza.

Hii inatosha kuwafahamisha watu afya na umri wake ni kinyume na kile ambacho anataka watu waamini.

Kama Adolf Hitler alivyofanya huyu Lowasa mnayemshangilia bila kujua akipewa urais baada ya miaka michache watanzania wataweka mikono kichwani kama Hitler alivyofanya Ujerumani.

Hilo nalo neno! Hii ni ktk harakati za kumuonesha lowasa kuwa watz sio wavivu wa kufikiri km mkapa alivyowatukana
 
Adolf Hitler alitumia ujanja wake wote hasa mahitaji na madhaifu ya Wajerumani wa wakati ule ili watu wampende, lakini pia alitumia ujanja wake wote ili watu wasijue moyoni kwake amekusudia kufanya nini!!.
Kama Adolf Hitler alivyofanya huyu Lowasa mnayemshangilia bila kujua akipewa urais baada ya miaka michache watanzania wataweka mikono kichwani kama Hitler alivyofanya Ujerumani.

Mtumeee! Yaani anafananishwa mpaka na Adolf Hitler! Ama kweli watu mumemchoka Lowassa......sijui kama masapota wake bado wapo?
 
Je, unayo habari kwamba Nigeria inayo wasomi wengi sana na bado maendeleo yake kama nchi si mfano wa kuigwa? Msome tena Mzee Mwanakijiji, hujamuelewa au . . .
Tofauti ya Nigeria na Tanzania ni kwamba sisi tunaendeleza elimu practically baada ya kusoma na kuweka elimu sandukuni kama nigeria.
 
Kwa nini unadhani CCM itachagua mtu anayefaa? Anayefaa kwa maslahi ya nani? Kama 2005 walichagua asiyefaa, watakuwa wajinga hivyo leo wachague anayefaa?

Tulio UKAWA tusiumize kichwa eti 'UKAWA' itashinda URAIS!! cha msingi ni kuiangalia CCM inataka kumleta nani? Bora aje ambaye hata CCM inamwogopa, kuliko kuleta yule CCM inampenda, watuletee mtu anapendwa na Nape! Mtu anapendwa na Kikwete! ama Ridhiwani!

mi naamini tunaweza kushinda ila kupewa ushindi ni ndoto, mfumo wa ki ulinzi na kiusalama na Katiba hairuhusu mpinzani kwenda Ikulu

tuiimarishe Bungeni na Kwenye Halmashauri, Bungeni tuweze kubadili katiba, Bungeni kama tukiwazidi tutoe PM, tutoe Spika

mi naona Bora Rais awe Lowassa, "Ukimjua huyu ni mchawi, mpe mwanao akulelee" atamtunza dhidi ya wachawi...ukimpa mtu legelege haijui hata hirizi, utajuta.
 
Hiyo ni IMANI yako hamna chochote tutakacho faidika kutoka kwa Lowasa. Cdhani kama ni mtu mwema kwetu ccm wote ni family moja. Hata hvo Lowasa haogopeki ndani ya CCM kilichopo hawapendi. Ukawa tumejipanga kwa yote kwanza kuchukua viti vingi vya Ubunge na pili kwenda ikulu uuuuuu
 
Lowasa akiwa rais hii nchi nitahama najua baada ya hapo kitakuja kitu kibaya sana kwa watanzia wote anasema ataweka kipaumbele kwenye elimu baada ya kilimo inamaana wasomi wote watakuwa wanashinda na njaa
 
Rkebisha kauli yako hii, ni kauli tata.
watu hawawezi kutoka Mbeya mpaka Dodoma kwaajili ya CCM.
Vijana walitoka Mbalali.

Kwani Mbarali ipo Mkoa gani? Shule za Kata hzi ni janga la kitaifa
 
Nani afaaye kwako au mpaka tuwasikie wote...na je maneno tu yatosha kutenda? Nchi hii ina shida nyingi sana ifike mahali wakati tunapinga kitu tutoe na solution yake la sivyo itakua ni maneno matupu tu ambayo hayatusaidii. Ifike mahali tusaidiane kusema fulani anafaa kwasababu 1,2,3 n.k. ndio tutafika tunapotaka kwenda. Ushabiki wa kisiasa ni mbaya sana. Binafsi nazidi kuogopa nguvu anayotumia Lowassa kutaka ukuu wa nchi. Amekua akijijenga kwa staili yake na chama na system nzima ikimuangalia hila hatua madhubuti kuchukuliwa...hii sio bahati mbaya...hatuna taasisi amabazo zinaweza kudhibiti matukio kama haya, kweli!!!? Basi hii ni hatari. Ifike mahali tuipende nchi yetu kwanza...tusiwe n ushabiki wa kisiasa...kwangu mimi wanasias wote lao koja ni kushika dola...tuwe na mfumo wa kuwajibisha tabaka hili ambalo linajiona ni miungu watu ndani ya nchi yetu

Hiyo haitoshi, waende mbele zaidi.

Yeyote anaye taka uongozi Tanzania awe Diwani, Mbunge au Rais
Ainishe yafuatayo
1. Sera zake. Wengi wanaimba sera zao. Hizi nashauri kama Taifa... tuchague vipaumbele vyetu. Mwanakijiji au JF admin naomba utuwekee uzi watu wataje vipaumbele vya Taifa kwa sasa.
2. Watueleze jinsi watakavyo tekeleza sera zao. Kwa kimombo kisicho rasmi namaanisha workplan ambayo itaonyesha time frame, implementation strategies, source and availability of funds to implement the policies. Lazima katika hili waweke na watekelezaji (responsible parties), merits and demerits of the policy.

Nitamuunga mkono yeyote bila kuangalia chama (ila siyo Magamba kwa sababbu kubwa moja kwamba hawatekelezi matakwa ya Mwananchi) atakaye kuja na sera na namna ya kuzitekeleza kama nilivyo eleza hapo juu. Sera zisiwe nyingi max 5 zikipangiliwa kwa priorities na bajeti ya Nchi ionekane kwa mtiririko huo. Siyo unasema KILIMO KWANZA harafu bajeti ya Kilimo inashika nafasi ya 10 kwa kiasi cha fedha kilichotengwa! Hiyo ni dhihaka kwa Watanzania.
 
The fact that Ngeleja naye kachukua form tells a lot about ccm. Hakuna siri kuwa wengi bado wanakiangalia hiki chama kwa matumaini. Lakini matumaini aliyonayo mwanachama wa ccm hayana tofauti na matumaini ya mwenye ngoma! Tuhuma zote hawazioni kuwa ni issue licha ya ukweli kuwa hawana majibu ya tuhuma hizo. The whole ccm conglomerate is in shambles and total chaos. It lacks ideology and guiding principles. It is full of power hungry thugs who will do anything to get into power so that to use this power to enrich themselves.
 
Nimekuwa nikipitia nyuzi nyingi sana katika jukwaa hili zinazo zungumzia watangaza nia kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), nimeshangaa kukutana na nyuzi nyingi zikimchafua mtangaza nia mmoja E. N Lowasa kanakwamba ni mgombea aliyekosa hata chembe ya uzuri. Kwa upande wangu nadhani waanzilishi wa nyuzi hizi hawatumii busara maana naamini kila mtu huwa na uzuri wake, sasa iweje mtu anaanzisha uzi ambao mwanzo mwisho yeye ni kukejeli tu. Naamini wanaofanya hivi wapo ktk moja ya makundi haya;
  1. Watu wenye chuki binafsi dhidi ya Mh Lowasa.
  2. Waoga (wanaogopa kuongozwa na kiongozi mwenye maamuzi magumu kama Mh E.N. Lowasa.
  3. Hawajitambui na hawatambui thamani ya utu (hata kama humpendi mtu lazima ukubali mazuri yake)
  4. Wanataka kujifurahisha tuu.
  5. Wanafiki
  6. ........... n.k
Kwa upande wangu naamini kila mtangaza nia ana uzuri na mapungufu yake hivyo ni vema tukaanika mazuri ya kila mmoja pamoja na mapungufu yake ndipo tutaona nani hasa anastahili kuingia magogoni. Huu si wakati wa siasa za kuchafuana.
 
Nimekuwa nikipitia nyuzi nyingi sana katika jukwaa hili zinazo zungumzia watangaza nia kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), nimeshangaa kukutana na nyuzi nyingi zikimchafua mtangaza nia mmoja E. N Lowasa kanakwamba ni mgombea aliyekosa hata chembe ya uzuri. Kwa upande wangu nadhani waanzilishi wa nyuzi hizi hawatumii busara maana naamini kila mtu huwa na uzuri wake, sasa iweje mtu anaanzisha uzi ambao mwanzo mwisho yeye ni kukejeli tu. Naamini wanaofanya hivi wapo ktk moja ya makundi haya;
  1. Watu wenye chuki binafsi dhidi ya Mh Lowasa.
  2. Waoga (wanaogopa kuongozwa na kiongozi mwenye maamuzi magumu kama Mh E.N. Lowasa.
  3. Hawajitambui na hawatambui thamani ya utu (hata kama humpendi mtu lazima ukubali mazuri yake)
  4. Wanataka kujifurahisha tuu.
  5. Wanafiki
  6. ........... n.k
Kwa upande wangu naamini kila mtangaza nia ana uzuri na mapungufu yake hivyo ni vema tukaanika mazuri ya kila mmoja pamoja na mapungufu yake ndipo tutaona nani hasa anastahili kuingia magogoni. Huu si wakati wa siasa za kuchafuana.

Ukimwita FISADI, FISADI nikumkejeli?
 
Anaweza kuwa mwenyekiki wa ccm wakitaka. Lakini urais wa Tanzania kamwe!
 
Back
Top Bottom