Ndio nyie mkiambiwa mkewako malaya mnajitetea kwa kusema wanawakewote malaya. Ila siku ukiletewa ukimwi ndio unajuta.[/QU
Najua umethubutu kutoa mfano huu kwa sababu mtoa mada anamzungumzia lowasa. Lakini mtoa mada angekuwa anamzungumzia Mbowe hakika usingetoa mfano huu. Labda tu niseme kwamba, humu Jf kumekuwa na kasumba ya HOJA BORA NI KUSIFIA CHADEMA NA HOJA MBOVU NI KUONGELEA CCM(POSITIVELY)/KUONGELEA MADHAIFU YA CHADEMA
Naamini humu Jf 95℅ wanakubaliana na huu msemo HAKUNA BINADAMU ALIYE MKAMILIFU/BINADAMU SI MALAIKA. Lakini wakereketwa wa CHADEMA humu ndani wamekuwa wakileta hoja ambazo ni kama zinarasmisha kuwa viongozi wa CHADEMA ni malaika, hawana makosa na wala hawatafanya makosa. Viongozi & wabunge wa CHADEMA kila wanapopanda kwenye majukwaa ya siasa wanawasema CCM kuwa ni mafisadi,wafujaji wa Mali za umma na wapo kwa ajili ya kuwanyonya tu watanzania. Lakini wamewahi kujiuliza kwamba ni nani aliyemsafi ndani ya CHADEMA? Je, Mbowe/Slaa au wengine hawana elements za ufisadi, hawafuji Mali za chama au hawapo kwa ajili ya kuwatumia watu wengine(wafuasi wa CHADEMA) ili kujinufaisha wenyewe? Ninachotaka kusema ni kwamba tuwe wakweli juu ya hawa wanaowania uongozi wa nchi yetu, tuache kila mtu azungumze kile anachokifahamu juu ya hawa wagombea ili tuwaweke kwenye mzani tuone nani anatufaa watanzania. Mashabiki wa CHADEMA/ukawa msitumie maneno ya kejeli,dharau ,dhihaka na matusi kuwalinda viongozi wa CHADEMA/ukawa ambao nao hawana sofa za kushika hatamu kuongoza nchi yetu.
Muungwana hutafakari kwa kina na kujibu kwa hoja Bali mpumbavu hukurupuka na kulopoka bila kutafakari matokeo ya anachokizungumza. Hapo ndipo huuanika upumbavu wake kwa hadhara
Maneno mengi point hakuna. Kwakifupi Sisemi viongozi wa chadema wala chama chochote cha upinzani ni malaika. Nachosema ni CCM ni bonafide fisadi na ushaidi ni kibao kwaiyo hafazali tumkabizi nchi mtu mwingine tuone itakuwaje. Nisawa na ukiwa demu ukamkuta akiuza mtaani unampiga chini na unajaribu mwingine uone kama nayeye ni malaya pia nasio kungangania unaemjua ni malaya mpaka akuletee ukimwi.
![]()
Watanzania wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wanaaminishwa kuwa ana maono ya kiuongozi ambayo yakitumika yanaweza kulinasua taifa letu toka hapa lilipo. Wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa ni kiongozi bora ambaye Watanzania wanapaswa kumwangalia kwa matumaini - ndio maana ya "Safari ya Matumaini".
Wapo kati yetu ambao wameshazugika na pendekezo hilo na wamekuwa kama waliorogwa hivi. Wapo baadhi yetu kwa muda wote wa uongozi wa Lowassa (hasa baada ya kuwa Waziri Mkuu na baadaye) tuliona kile ambacho labda kimefichika kwa wengi - Lowassa hafai.
Hii si hukumu juu ya utu wake, heshima au ubinadamu wake; ni hukumu juu ya uongozi wake na maono yake kama kiongozi. Kumkataa Lowassa, maono yake, uongozi wake na fikra zake siyo kumchukia yeye kama Mtanzania mwenzetu au kama binadamu. Ni kuwa na tofauti naye na vile anavyowakilisha kiasi kwamba tofauti hizo hazijawezi kupatana (irreconcilable differences).
Katika siasa ni lazima tuheshimu uwepo wa tofauti hizi na tuelewe ndio msingi wa kutafuta viongozi bora zaidi au chama bora. Kwa kadiri yeye atakavyojaribu kujiuza ndivyo na sisi wengine tutazidi kuonesha kuwa hauziki au zaidi hanunuliki. Hii si chuki ni tofauti tu ya msingi (fundamental difference).
Pendekezo langu linatokana na hili; kwamba zipo na zimedumu tofauti za msingi kati ya maono ya baadhi yetu na maono ya mgombea huyu mtarajiwa kutoka CCM. Tanzania haihitaji maono na uongozi wa Lowassa kwa sababu nyingi tu; nitaanza na moja ya leo na nitaendelea kwenye mada hii hii kila ninapopata nafasi hadi jina lake litakapotupwa na NEC na yeye akaendelea kuwa Waziri Mkuu wa zamani.
Mara kwa mara baada ya sakata lake na katika jitihada za kujirudisha katika umuhimu (relevance) Lowassa amekuwa akizungumzia mwelekeo wa sera zake na kitu kitakachomuongoza. Aliamua kwenda kinyume na mwelekeo wa serikali ya chama chake ambayo iliweka mkazo kwenye "Kilimo Kwanza"; yeye ameamua kuja na hoja ya "Elimu Kwanza".
Alielezea kupinga kwake hoja ya Kilimo Kwanza miaka michache nyuma alipohojiwa katika kipindi cha Dakika45 (kinachorushwa na ITV). Alinukuliwa kusema "Mpango huu wa Kilimo Kwanza umekosa nguvu kwa sababu kuanzishwa kwake hakukuzingatia dhana ya ukombozi wa mwananchi wa kawaida. Tangu awali ndani ya chama (CCM) nilieleza kuwa sitaunga mkono hoja hiyo mpaka kuongezwe mashiko na kuwa Elimu Kabla ya Kilimo Kwanza"
Hoja hii ameirudia tena juzi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ambao bila ya shaka wengi wamekuwa 'charmed' na wingu la umaarufu wa Lowassa kiasi kwamba hakuna ambaye ameweza kumbana vizuri kwenye maswali. Anasema endapo atachaguliwa basi ataelekeza nchi kwenye "elimu kwanza"; kwamba hiki ndicho kipaumbele chake.
Ndio maana sisi wengine tunasema hafai; kwa sababu inaonekana siyo yeye wala chama chake ambao wamelielewa vizuri tatizo linaloikabili Tanzania; tatizo ambalo limeielekeza (orient) Tanzania kufuata njia ya Nigeria. Kwamba tunaweza kabisa kutengeneza uchumi wenye nguvu lakini wa taifa lenye umaskini uliokithiri, lisilo na usawa na la wasomi wasioweza kulipeleka taifa mbele. Tutakishia kujisifia wingi wa wasomi ambao wengi wataishia kwenda nje ya nchi kutafuta maisha. Taifa ambalo litakuwa limegawanyika sana kama Nigeria - licha ya kuwa na wasomi wengi.
Lowassa inaonekana ameshindwa kuelewa au hataki kukubali kuwa tatizo kubwa la Tanzania ni la aina tatu:
1. Ufisadi
2. Ufisadi
3. Ufisadi
Lowassa hatopambana na ufisadi kwa uzito unaostahili kwani haoni kuelewa kuwa ni tatizo la hatari zaidi kwa taifa "kuliko vita wakati wa amani" kama alivyosema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Kutokuelewa kuwa Ufisadi ndiyo sekta haramu yenye nguvu zaidi katika nchi yetu ni kushindwa kuelewa tatizo letu hasa ni nini. Ufisadi umepenya (permeate) kwenye kila sekta nyingine zote (rasmi na zisizo rasmi). Umeathiri elimu, afya, usalama, na hata umoja wa taifa. Kutokulielewa tatizo hili kwa mtu anayetaka kugombea nafasi ya Urais (haijalishi anatokea chama gani) ni kutokuelewa namna ya kukabiliana na changamoto nyingine zote.
Kwa sababu hii peke yake Lowassa na mgombea mwingine yeyote ambaye haweki "ufisadi" kama ajenda yake ya kwanza na kubwa zaidi basi hafai. Kwa sababu atatuzungusha kwenye madudu mengine yote isipokuwa kwenye kumkoma nyani giledi.
Kikwete - kwa wanaokumbuka - alishabikiwa na wengi si kwa sababu ya "Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya" bali zaidi kwa kuwapa Watanzania matumaini kuwa atashughulikia ufisadi vikali. Hotuba yake ya kulifungua Bunge na ile ya Ngurdoto na zile ziara zake za kutembelea Wizara ziliwafanya watu waamini kidogo kuwa hatimaye "kipele kimepata mkunaji". Leo hii miaka tisa baadaye ripoti ya CAG imeonesha kidogo tu kuwa tatizo hili la ufisadi halijapata mtatuzi ndani ya CCM na hata mtu anayeshabikiwa sana kuwa ati anaweza kuwa Rais inaonekana tatizo hili limempita kabisa.
Nikisema "hafai" simsingizii; nasema kilicho dhahiri; I'm just stating the obvious.
Wanaomtaka Lowassa - wapenzi, mashabiki na waumini wake - watuambie vita dhidi ya ufisadi ina umuhimu na uzito gani katika agenda za Lowassa. Wakituambia kuwa "ni mojawapo" ya mambo atakayoyashughulikia tuendelee kumkataa kwa sababu bado atakuwa hajaelewa tatizo letu hasa ni nini kama taifa.
Nitandelea...
NB: Kwa wageni wa hoja hizi warejee mada yangu ya 2007: Kikwete Siyo Safi, Yes I said it
Heko kwa Mwanakijiji kwa mada nzuri. Story yako imenikumbusha ya mitaani, kwa zaidi ya mara 3 sasa tangu NEC ya CCM itoe taarifa yao fupi, Nimeshuhudia taflani mitaani kwenye vimeza vya Magazeti pale anapo jitokeza mtu Kumsifia Lowassa kwamba jamaa anafaa....... ehhhhhhhhh..... analaluliwa kama nini bwana!
Haya tusonge mbele na mada,
Sijawahi kusikia Mh Lowassa akisema jambo lolote linalo husu tatizo la wizi wa fedha za Wananchi (UFISADI)!
Tatizo letu kubwa Watanzania ni
1. UFISADI (Wizi wa fedha za wananchi)
2. RUSHWA (kutokupata haki na kusababisha hasara kwa wananchi na Watanzania kwa ujumla kama rushwa inahusisha miradi mikubwa ya Kitaifa)
Miaka ileeeee,, Nyerere alisema adui wakubwa kwa Watanzania ni
1. Maradhi
2. Ujinga
3. Umaskini
Kwa sasa idadi ya maadui imeongezeka na kubwa kuliko zote ni UFISADI. Hata hivyo, ili tuepuke na maadui hao nyenzo aliziona wakati ule na bado zinafaa, soma hapa chini
Ili Taifa lisonge mbele tunahitaji vitu vine
1. Watu; Kwa sasa watu tunao
2. Ardhi; Ardhi inazidi kuporwa na wachache
3. Uongozi Bora; Kwa sasa hatuna
4. Siasa Safi; Kwa sasa hili ni janga
Angenda ya kutokomeza ufisadi iwe namba moja na isiwe tu kuitaja! Bali anaye taka urais atuwekee yafuatayo
1. Plan and time frame(namna gani atashughulikia na kwa ratiba maalum)
2. Implementation strategies (atalitekeleza kwa taratibu zipi, yepi yatakayofanyika kukomesha UFISADI)
3. Monitoring and Evaluation (Namna gani atafanya tathimini ya mafanikio)
Yeyote anaye utaka Urais aje na agenda na utekelezaji wake kama nilivyo ainisha hapo juu, hakuna bla bla.... matumaini hewa ya Kikwete 2005 yanatosha! This time tuwe wazungu zaidi, hakuna Ubongo bongo!

Kwa maana nyingine ni kuwa ukitaka kusema habari au kui-name CCM weka mbele yake UFISADI as kama SI unit kipimo pekee cha CCM, Uccm na wanaCCm.
Ni kama vile, Pope Francis aanze kupambana na Kanisa katoliki.
Sijui kama kuna watu baada ya kumsikiliza au kumsoma Lowassa leo wamebadilisha mawazo yao kuhusu yeye. Binafsi nimethibitika kuwa hafai.