Lowassa: CHADEMA tutatoa chakula kwa wenye njaa

Lowassa: CHADEMA tutatoa chakula kwa wenye njaa

Alianzaga kutoa toka enzi makanisani na misikitini ataendeleza tu
 
Hili toto linakula kwa wazazi bado. Ndo maana watu wazima tukiwa tunajadili hali ngumu na baa la njaa unashindwa kuelewa. Wewe endelea kupata msosi wa shikamoo hapo. Haujui jasho lake
 
Lowasa endelea na katafunua kama hizi tutaonana 2020. Kauli za kizembe huenda zikapungua kwa watawala.
 
Unajua kama nakufuata baba unipe viatu nivae shule,ukiniambia sina ela ,na mama akaja aksema nitampa,baadae wewe(baba)ukatoa,basi najua bila mama nisingepata,nextime natamani mama ndiyo awe na ela nipate moja kwa moja bila kuanza kwa baba kusiko na uhakika.
Hii ni impact ya baba kukosa kujali au huruma ya moja kwa moja.
Pole sana Jay One.
Duh!
 
Huenda wakatoza kodi hata huo msaada kutoka kwa wahisani

Siyo huwenda ila watatoza kodi na maana maghufuli ameshasema na nakumbuka miriam odemba alileta maboya ya kujiokolea majini bandari ya mwanza lakini walimlazimisha kulipa kodi
 
Kama maneno hayo yametoka kwa Lowasa , basi kaishiwa pumzi au anauota U-PM. Chama cha siasa kina fanya mambo yake kwa kuzingatia katiba yake na sheria za nchi. CDM akina uwezo wa kugawa chakula kwa mujibu wa katiba yake. Huu ni usanii ulio pitiliza kiwango. Emu tafakari kwa mfano, serikali inashindwa kukusanya kodi ya majengo, alafu kinajitokeza chama cha siasa kinasema chenyewe kitakusanya!! Sio usanii huo jamani. Alafu kuna watu humu wanajitoa ufahamu kushabikia. Huu ni uchochezi; JPM shughulikia hawa watu kabla mambo hayaja enda kombo..
ndugu wakati mwingine kuficha ujinga ni busara kuliko kuongea.

Kwani chadema kugawa chakula kuna tatizo gani? Au ninyi mnafuraia wengine wafe na njaa?

Watanzania tumejengwa kusaidiana na dhani hata serikali italiunga mkono jambo hili kama ilivyopokea misaada ya wahanga wa tetemeko la bukoba.

Kama serikali haina chakula cha kuwapa wenye njaa wapo watu watakao jitolea kuwa saidia wahanga maana utanzania ni kusaidiana.
 
Baba asipowajulia mlo watoto wake kwa sababu yeyote huukosa ubaba wake. Nadhani, baba ataangalia upya mtizamo wake na awatafutie watoto chakula hata kama ni kwa kuwauzia. Swali la kizushi tu; Kuna nini huko Ghala la Taifa?? Kwa nini wasitoe takwim wazi kuwa chakula kipo au hakipo?? Huyo mwenye tani 25 elfu bandarini, ni mpinzani au mpiga dili?? Si kitaifishwe kipelekwe kwenye ghala?? Maswali ni mengi ila sipendi baba awaongoze wenye njaa. Njaa! Hainaga adabu. Pia chuki haiondolewi kwa chuki. Bukoba mliichukia ccm sawa lakini hatutairudisha ccm kwa chuki.
 
Nywele nyeupe pia moyo mweupe, Maneno ya hekma sana ata asipo tekeleza..

Maneno yenye kuonyesha kujalia, kutia moyo..

Ameonyesha yeye ndie aliekua tumaini la watanzania wanyonge, masikini

Mungu hubariki kinywa kinenacho maneno ya hekma. Ameni
 
Unajua kama nakufuata baba unipe viatu nivae shule,ukiniambia sina ela ,na mama akaja aksema nitampa,baadae wewe(baba)ukatoa,basi najua bila mama nisingepata,nextime natamani mama ndiyo awe na ela nipate moja kwa moja bila kuanza kwa baba kusiko na uhakika.
Hii ni impact ya baba kukosa kujali au huruma ya moja kwa moja.
Pole sana Jay One.

Nimekubali.. uko sahihi..!!
 
Maneno maridhawa toka uvungu wa moyo, Mungu ibariki Tanzania
 
Mjumbe wa kamati kuu CHADEMA, Mhe Edward Lowassa akiwa na mbunge wa Bukoba mjini wameudhuria ibada katika kanisa la KKKT. Akiwa kanisani Mhe Lowassa ametoa kauli.

''Mh rais amesema hatatoa chakula. Mimi nimewasiliana na chama changu tumeona tuwape chakula watanzania. Naamini dunia itasikia'', alisema Lowassa.
Naomba serikali imwache atoe hiko chakula ili kwa mara ya pili aoneshwe jinsi watanzania walivyokuwa wanafiki kwasababu kura wataipa CCM tu.
 
Nywele nyeupe pia moyo mweupe, Maneno ya hekma sana ata asipo tekeleza..

Maneno yenye kuonyesha kujalia, kutia moyo..

Ameonyesha yeye ndie aliekua tumaini la watanzania wanyonge, masikini

Mungu hubariki kinywa kinenacho maneno ya hekma. Ameni
Nimeipenda hyo. Barikiwa sana na wewe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom