Akitoka ndani ya CCM hata maisha yake siyo mbali kufika mwisho.
Halafu mimi sielewi kama walikuwa 38 akachaguliwa mmoja mbona hao wengine wote wameamua kukijenga chama chao hata kama kinaonekana kuwa na Siha mbaya mbele ya Hadhira?
Yeye ana kitu gani cha pekee alichonacho asichoweza kumshauri Magufuli kama ni kizuri kikafanyiwa kazi?mpaka atake kuingia ikulu mwenyewe?
Sasa ndiyo naelekea kuamini kuna kitu kimejificha moyo mwa Lowasa na siyo kizuri kwa Watanzania Lowasa atatugharimu.
Mtu mmoja alisema kuwa "Sumu hainjwi"ila huyu jamaa akihama na kwenda Upinza halafu Watanzania tukamchagua kuwa raisi tutakuwa tumeonja Sumu na kiukweli ukionja Sumu kuna matokeo ya kufa tu na utakufa tu maana hamna namna nyingine.
Ni ndoto kwa watanzania kumchagua Lowasa kuwa rais wa nchi yao. Hao watu aliowapa pesa wampigie debe mara kwa vijana au boda boda ni wachache sana hawawakilishi watanzania hata chembe. Akitaka kujimaliza yeye pamoja na upinzani ajaribu kuingia upinzani. Mrema alipata wafuasi wakati ule kwa sababu kuna watu ambao moyoni mwao (labda kiusahihi au kimakosa) waliamini Mrema ni mchapa kazi mwenye nia nzuri na nchi hii. Ndio maana japo hakuondoka na viongozi wa serikali au CCM alipata sapoti ya hao wananchi walioamini uwezo wake. Ni tofauti sana na Lowasa. Yeye Lowasa anaondoka na sapoti ya viongozi walliopokea pesa kutoka kwake ili wamsapoti, haondoki na wananchi. Badala yake wananchi wanajua kuwa Lowasa ni fisadi asiyeitakia mema nchi hii. Sasa akiruhusu CCM nayo iingie katika kumtangaza kuwa ni fisadi ndio maana akaenguliwa basi itakuwa mwisho mbaya sana kwa Lowasa. Abaki tu CCM watamheshimu hawataanika uozo wake uliosababisha aenguliwe.