Mkuu
Bukyanagandi
kuna haki za kiraia, haki za kikanuni, yaani stahili na haki za kisiasa!, kujiunga na chama chochote cha siasa ni hiari na kujitoa ni hiari, hakukuondolei haki zako za msingi za kiraia wala za kikanuni!. Miongoni mwa haki za msingi za kiraia, ni pamoja na haki ya kupata ulinzi wewe, jamii yako na mali zako!. Viongozi wale sita ambao ni wakuu, miongoni mwa stahili zao, ni mshahara asilimia 80% ya the sitting position, ulinzi, usafiri, safari 4 za ng'ambo, matibabu nje ya nchi, etc. Mtu hata akihama chama, stahili zake zote zipo palepale!.
Ila kwa vile ulinzi hutolewa na serikali, mlindwa hana mamlaka ya kuchagua anataka kulindwa na mlinzi gani!, na mlinzi pia ni mtumishi wa umma, hana mamlaka ya kuchagua amlinde nani, utumishi wa umma ni kazi popote kwa yoyote!.
Serikali kama imeamua kumhamisha huyo mlinzi aliyepo, itampatia mlinzi mwingine!, ila mlindwa pia yuko huru, kama hataki tena ulinzi wa serikali, yuko huru kujiwekea ulinzi binafsi!, ila atajigharimia!.
Na sio Lowassa tuu, hata Maalim Seif, ulinzi ni wa serikali, gari la serikali, dereva wa serikali, matibabu ya serikali, na mashahara wa serikali mpaka pale atakapokwenda ile safari ya 6feet under!.
Heri ya Mwaka Mpya!.
Pasco