Lowassa anasafishwa!

Siku za dunia hii zitakavyokuwa ngumu, na usiku kuwa na giza nene kuliko maelfu ya vipindi vya usiku, tukumbuke kwamba ulimwengu umeumbwa na nguvu inayoweza kuangusha milima mikubwa ya dhambi, nguvu ambayo inaweza kutengeneza njia mahali pasipokuwa na njia na kubadilisha giza la siku iliyopita kuwa mwanga siku zinazofuata. Tumatakiwa kutambua fimbo ya ulimwengu ni ndefu na inaadhibu kutenda haki," Martin Luther King
 
Tafuteni makala ya Mwananchi iliyopita jumapili ya Theodatus Muchunguzi. Ninamshangaa sana anapodai ktk makala yake kuwa tuache kumjadili Lowassa kuwa tumwache apumzike, Je inaingia akilini kweli??
Nimeanza kuwataja majina hapa bila uoga na wengine mfuate kutaja majina.

Nitawaletea majina mengine zaidi hapa.

Nguvu ya rushwa ni kubwa sana hata vitabu vitakatifu vimeweka wazi hili, naona Theodatus Muchunguzi na bahasha ya kakhi ameanza kurudisha fadhila kwa kutumia kalamu yake....nitafatilia makala zake nyingine, ama abadili ziwe na (mwandishi wetu) bila kuweka jina lake
 
Nilimuuliza mwanaume mmoja, ni kwa nini wanaume wanataka sana kuwa viongozi wa nchi? akanijibu ni kwa sababu wanataka kuweka MARK hapa duniani.
Sasa kwa Lowassa ataweka hiyo MARK hata kama ni kwa damu ya watu yeye hajali, as long as amerudi madarakani na kuishia kuwa raisi hilo ndio la maana kwake. Yaani yeye haoni hata aibu tu, akaachia hayo madaraka kimya kimya! Kama ni hela anazo, sasa naona ni jeuri tu anayotaka kuonyesha watu.
Tofauti ya wazungu na waafrica ndio hii, mzungu akishakamatwa kwa wizi, basi yeye atakemea hata kitendo chake mwenyewe, lakini mwaafrica akikamatwa kwa wizi atajitahidi kwa hali na mali asafishe jina lake hata kama ni kwa kutumia nguvu atatumia tu,lakini hatokubali kushindwa kwa kweli.
Poleni Tz, kwani huyo ndio raisi wenu anakuja kwa nguvu.
Sielewi ni kwa nini watanzania hakuna kabisa kuangalia mambo kwa kufikiria kesho kutatokea nini, hao waandishi wa habari wanaonunuliwa kwa hela leo hii, hawawezi kufikiria je kesho watoto wao wataishi vipi, kama EL atarudi madarakani kwa nguvu namna hiyo, na kama mtu anathubutu kutaka kurudi madarakani kwa hali kama hii, it makes you wonder, Why!
Maanake madaraka kwa madai yao ni magumu sana, lakini hawataki kuyaachia. MUone Kibaki, mkewe anaikashfu ikulu ya kenya kwa madai kuwa ni ya kizamani, lakini at the same time, bwana yuko radhi watu almost elfu moja wafe kuliko yeye mtu mmoja aachie madaraka tu na sio kufa wala. Sijui huku kuweka MARK hapa duniani kwa waafrica kunamaanisha nini kwa kweli. Kwani mobutu ndio hivyo hivyo kang'ang'ania madaraka na wizi mpaka ameiuwa nchi kubwa sana Africa, na yeye mwenyewe kafia ugenini kama mbwa gani sijui, inatia hata aibu, japo ameshakufa.
Kuna kilio sana kati yetu sisi watu weusi tunaposikia wazungu wakisema kuwa watu weusi ubongo wao ni kama wa watoto wadogo, basi tutakasirika we! lakini ukiangalia viongozi wetu tunaowachagua! kuna utata kwa kweli,
 
simbajike umesema kweli kwa nini atandikiwe zuria jekundu (red carpet)kwa lugha ya wenzetu, lakini ukweli ni kwamba hakuna aliyeandaa maandalizi hayo zaidi ya wewe mwenyewe EL kuratibu maandamano hayo na kuchapisha fulana zaidi ya 200 na kumpokea kama shujaa, uliona mabango yao, ati, maasai hatuibi pesa tunaiba ng'ombe! monduli watu hawana kazi jamani kuota kitu kama hicho? kweli kuna baadhi waandishi walianza kumsafisha 4m day 1, halafu ukiangalia ni hao hao kila siku wanatoka na mpya ya kumsafisha bosi wao. simbajike huu si utani kuna wahariri tunawafahamu wamejenga nyumba kupitia EL tangu akiwa waziri wa mifugo hadi uwaziri mkuuu jamaa wanaye hadi sasa wanajitahidi kutomtupa lakini historia itawahukumu kwa kutolitendea haki taifa lao.imagine mhariri mzima??????find them @ habari corporation! na mkamatwe wkt wachangiaji wengine, kudadadeki!
 
Baadhi waandishi wahongwa na lowassa wamsafishe

Hili ni tatizo la kutokupevuka kifikra na kukosa kipaji cha kusoma nyakati.

Ni upuuzi kufikiri Mtanzania wa leo unaweza kumsafisha kwa "sabuni" ya Muadishi wa habari goigoi. Siku zinakuja wote watakao itumia hii sabuni watarushiwa mawe na kuzomewa kama mawaziri walioshangazwa kuzomea ndani ya Taifa la watanzania "wapole" sana!

Sio Leo!

Lowassa aje hadharani atubu wazi kabisa...! Kama alionewa anajisafisha nini? Aje atuonyeshe ambavyo alifanya kosa na mabavyo hatalirudia Nina mhakikishia anaweza kuwa kufikiriwa kuliko anavyofanya.

Ukweli ndio silaha pekee anayoweza kuitumia kwa sasa...mengine yamepitwa na wakati!

Kuwa nyuma ya Nyakati hata dakika moja madhara yake ni makubwa sana.

Ninategeema sana asichelewe na afuate ushari huu!
 
kamanda mbona hilo sio swali kabisa, yaani haina mjadala! jamaa ameanza kusafishwa 4m day 1, na magazeti ya rai, mtanzania na the african ambao baadhi ya wahariri wake wamejengewa mahekalu makubwa tu mithili ya uwanja wa basket!

hata ukisoma gazeti la mwanahalisi la leo linaelezea bayana kinachoendelea kwenye kwmpuni ya habari corporation ambayo mmiliki ni Rostam Aziz.

balile aliyesomeshwa na mbowe(inavyosemekana) kwa ajili ya kufanyia kazi magaeti ya ytanzania daima alimchenjia na kwenda habari corp. ambako aliahidiwa uhariri mtendaji lakini kutokana na mbwembwe zake hakupendwa na yeyote kwenye kampuni hiyo kuanzaia kwa CEO, Rosemary Mwakitwange hadi waandishi wenyewe.

alisimamishwa cheo cha uhariri kwa kujifanya bora kuliko aliowakuta, amini usiamini jana tu amesababisha mhariri mtendaji, attilio tagalile, mwalimu chrisostom rweyemamu na ben mhina kujizulu nyadhifa zao kutokana na kutaka kumsafisha bwana mkubwa EL wazi wazi. soma mwanahalisi kamanda kwani haukuna kilichoachwa na vyote ni ukweli mtupu! hakika waandishi wa bongo wanapotea!
 
Kuna taarifa za Kujipenyeza kutoka kwa usalama wa taifa na wafanya biashara wa daladala kuwa walikodiwa na mheshimiwa Lowasa kwenda kumpa kampani wakati anarudi jimboni kwake.
Jamaa wamekula hela za kutosha tu na kuna madai kuwa baadhi ya fedha zimetokaa kwa mkuu mwenyewe.
Wenye taarifa zaidi tunaomba mchango
 
Kuna taarifa za Kujipenyeza kutoka kwa usalama wa taifa na wafanya biashara wa daladala kuwa walikodiwa na mheshimiwa Lowasa kwenda kumpa kampani wakati anarudi jimboni kwake.
Jamaa wamekula hela za kutosha tu na kuna madai kuwa baadhi ya fedha zimetokaa kwa mkuu mwenyewe.
Wenye taarifa zaidi tunaomba mchango

Salaam toka Arusha .Nimesoma habari na kubaki nashangaa .Una maana kwamba madaladala yalitoka Dar ? Walilala wapi ? Mkuu alichangia pesa ili iweje ? Kukatwa kwa mahojiano LIVE nayo vipi ?Mkuu tupe nyepesi kadiri uzipatavyo .Usalama wa Taifa kitu gani kimewafanya waseme habari hii ? Je walihusika kwa namna moja ama nyingine ?
 
Kuna taarifa za Kujipenyeza kutoka kwa usalama wa taifa na wafanya biashara wa daladala kuwa walikodiwa na mheshimiwa Lowasa kwenda kumpa kampani wakati anarudi jimboni kwake.
Jamaa wamekula hela za kutosha tu na kuna madai kuwa baadhi ya fedha zimetokaa kwa mkuu mwenyewe.
Wenye taarifa zaidi tunaomba mchango

wewe mwenyewe ndio utupe mchango maana ndio uliyeleta hii hoja, ingawa hivyo hili mimi silipingi linawezekana, maana kama mtu anaweza kupokea sh.152m kwa siku kwa nini asitafute magari 400 yampeleke Monduli? huyu jamaa afunguliwe mashtaka mengi tutayajua.
 
Source zangu zinadai daladala zilitoka Dar. Na mkuu anajikosha kwa kumtosa mshkaji wake kwenye hii ishu ya Monduli. Pia tetesi zinadai kuwa mahojiano TVT aliyakata Mh. Spika katika kujitahidi kuuokoa mtandao.
 
I have two analogies on this one:

1. Mh. Lowassa huwa ana norm ya kuthrow party ya mwaka mpya nyumbani kwake Ngarash Monduli na waalikwa na wasioalikwa huwa wanakuwa lukuki.
Sitashangaa kwamba watu wengi wa Maeneo ya Arusha waliopata kula ya bure kila mwisho wa mwaka, wakijitokeza kwa wingi either kwa hiari ama kwa kulipwa kulipa fadhila.

2. Mheshimiwa Lowassa ana tabia ya kuhonga: Mwaka 1995 wakati wa kampeni za uraisi wakati ule Mrema ni red hot, alikuja kufanya kampeni Monduli. Lowassa na washauri wa CCM wa wilaya wakapanga kufanya mkutano wao pale pale wilayani kwenye kiwanja kingine...lakini ilipoonekana kwamba Tsumani ya Mrema ingewatoa nishai kwani wangeweza kupata 0 audience, plan ikawa changed kufanya mkutano Mto wa Mbu the same day. Kulikuwa na mabasi yaliyoandaliwa ya kuwa ship watu kutoka Monduli kwenda Mto wa Mbu. Kigezo kwa wale waliokubali kwenda ilikuwa kuchukua gears za CCM (t-shirt na kofia)na walikuwa wanatoa shs 500 kwa kichwa. Hata hivyo, hawakupata watu wengi wa kwenda kwenye huo mkutano wa Lowassa.
 
EL,

Mbona hata askofu wa KKKT Arusha alikuwa wa kwanza kumpokea na kumsifia?

Kwani hamjui EL hutoa sadaka kubwa sana kanisani kwa hii pesa ya wizi?
 
Source zangu zinadai daladala zilitoka Dar. Na mkuu anajikosha kwa kumtosa mshkaji wake kwenye hii ishu ya Monduli. Pia tetesi zinadai kuwa mahojiano TVT aliyakata Mh. Spika katika kujitahidi kuuokoa mtandao.

Mh Spika anahusikaje na TvT, ana madaraka gani huko? Yaani Spika ndie bosi wa TvT au unamaanisha nini hapa? Tetesi yako inatia shaka!
 
Naomba msome hii ArticleDAWASCO wamkataa Mkurugenzi wao...

2008-03-22 09:41:24
Na Mashaka Mgeta


Wafanyakazi wa Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), wamemtaka Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wao, Bw. Alex Kaaya, wanayedai kuwa `aliwekwa` madarakani na aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, aachie ngazi kwa kushindwa kuendeleza kampuni.

Pia, wanadai kuwa Bw. Kaaya, aliyeshika wadhifa huo, wakati Bw. Lowassa akiwa Waziri wa Maji, amepandikiza chuki na mgawanyiko miongoni mwao.

Hali hiyo ilijitokeza jana jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa wafanyakazi hao, kupitia Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO).

Wakati wafanyakazi hao wakitoa shutuma hizo, Bw. Kaaya na Katibu Mkuu wa TUICO, Bw. Bonifas Nkakatisi, walikuwepo.

Risala ya wafanyakazi hao, ilisomwa kwa niaba yao na Katibu Msaidizi wa TUICO wa matawi yaliyopo DAWASCO katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, Bw. Geroge Lugendo.

Bw. Lugendo, alisema tangu aingie madarakani takribani miaka mitatu iliyopita, Bw. Kaaya, ameshindwa kutimiza ahadi za kuboresha mazingira ya kazi, huduma na maslahi ya wafanyakazi.

``Alituahidi kutupatia viwanja kwa kila mfanyakazi, kufanya mikutano kila baada ya miezi mitatu, kutuletea maisha bora ili tumudu kuwasomesha watoto wetu, hajatekeleza hayo yote,`` alisema.

Bw. Lugendo, alisema chini ya uongozi wa Bw. Kaaya, DAWASCO imeibua kundi la wafanyakazi wa zamani ambao wengi wao hawana elimu na wasomi walioajiriwa hivi karibuni.

Alidai kuwa, wafanyakazi wa zamani wanalipwa mishahara duni na kunyanyaswa, wakati wasomi wasiokuwa na ujuzi wanapata uongozi na mishahara mikubwa, hivyo kuwa `vinara` wa unyanyasaji.

Walidai kuwa, mmoja wa Mameneja hao, (wakamtaja jina), aliwahi kutishia kumuua mfanyakazi mwenzake kwa bastola.

Aidha, walimshutumu mkurugenzi wao kwa kuzuia kuunda mabaraza ya wafanyakazi na kutowashirikisha wafanyakazi katika maamuzi na mwenendo wa shughuli za DAWASCO.

``Tunamuomba Waziri wa Maji na Umwagiliaje aje amchukue Dk. Kaaya, sisi hatumtaki huku DAWASCO,`` alisema mmoja wa wafanyakazi aliyechangia risala hiyo.

``Kutokana na shutuma hizo, na uzito wa nafasi yake, apime mwenyewe na kuchukua hatua kama walivyofanya wanasiasa kule bungeni,`` alisema mfanyakazi wa DAWASCO, Bw. Abdallah Jongo.

Hata hivyo, Bw. Kaaya alijaribu kusimama ili ajitetee dhidi ya shutuma hizo, lakini wafanyakazi hao walipiga kelele wakisema ``ondoka, ondoka, ondoka.``

Bw. Kaaya aliendelea kuzungumza, lakini kelele za wafanyakazi hao na wengine zilipozidi akaamua kuacha.

Bw. Shaban Chezo, Bi. Happy Martine na Bw. Said Mfaume, walisema kwa nyakati tofauti kuwa, licha ya shutuma hizo, kuna michango ya SACCOS wanayokatwa wafanyakazi, lakini haifiki inapotakiwa.

Naye Bw. Staha Mrisho, alisema Bw. Kaaya, anaponzwa na utendaji wa mameneja wapya wanaoongoza kundi la wasomi katika kampuni hiyo.

Hata hivyo, Bw. Nkakatisi, aliwataka wafanyakazi hao kufuata sheria, kanuni na taratibu, ili kupata suluhu ya kero zinazowakabili.

Bw. Nkakatisi, aliyekabidhiwa risala ya wafanyakazi hao, alisema hatua yoyote itakayokuwa kinyume cha sheria, kanuni na taratibu zilizopo, itaashiria vurugu na hivyo kuwafanya wasifikie malengo yao.

Kuhusu Bw. Kaaya kuteuliwa na Bw. Lowassa, Katibu Mkuu huyo wa TUICO, alisema hatua hiyo ilitokana na mamlaka ya Uwaziri aliyokuwa nayo (Lowassa) na si vinginevyo.

SOURCE: Nipashe
imetoka kwa Nipashe 22/03/08
 
Kutunza heshima yako japo hiyo ndogo iliobaki namshauri KAAYA aanza tuu, kama anabisha aendelee kusubiri.
 
Back
Top Bottom