Nadhani kuna cha kujifunza katika katiba ya Namibia hasa kipengere cha Rais ,Kimekaa kizalendo zaidi

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Jan 9, 2022
449
1,009
Habari JF , baada ya kupata taarifa za kicho cha Rais wa Nambia Hage Geingob ,82 kwa masikitiko makubwa nliamua kupitia kipengere cha urais katika katiba yao .

Kwa kifupi uchanguzi wa haraka hautafanyika sababu ndani ya Mwaka mmoja kuna uchaguzi mkuu lakini ingekuwa kama ilivyotokea kwa JPM yaani kuna zaidi ya mwaka basi uchaguzi ungefanyika .
Uchaguzi Namibia ni Nov 2024 .
  1. If a President dies, resigns or is removed from office in terms of this Constitution, the vacant office of President shall be filled for the unexpired period thereof as follows:
    1. if the vacancy occurs not more than one (1) year before the date on which Presidential elections are required to be held, the vacancy shall be filled in accordance with the provisions of Article 34;
    2. if the vacancy occurs more than one (1) year before the date on which Presidential elections are required to be held, an election for the President shall be held in accordance with the provisions of Article 28 within a period of ninety (90) days from the date on which the vacancy occurred, and pending such election the vacant office shall be filled in accordance with the provisions of Article 34.
-------article 34​

Article 34 [Succession]​

  1. If the office of President becomes vacant or if the President is otherwise unable to fulfil the duties of the office, the following persons shall in the order provided for in this paragraph act as President for the unexpired portion of the President's term of office or until the President is able to resume office, whichever is the earlier:
    1. the Prime Minister;
    2. the Deputy-Prime Minister;
    3. a person appointed by the Cabinet.
  2. Where it is regarded as necessary or expedient that a person deputise for the President because of a temporary absence from the country or because of pressure of work, the President shall be entitled to nominate any person enumerated in Paragraph (1) to deputise for him or her in respect of such specific occasions or such specific matters and for such specific periods as in his or her discretion may be considered wise and expedient, subject to consultation with the Cabinet.

Hivyo inapunguza matumizi yasiyo ya lazima wakati uchaguzi upo karibu na pia ina kuhitaji mpate kiongozi mnae mtaka haraka kama muda bado mrefu .

IMG-20240205-WA0019.jpg

Siasa safi
 

Attachments

  • Namibian Constitution.pdf
    807.3 KB · Views: 5
waroho wa madaraka mara zote wao huwaza uchaguzi tu

kuna Watu hawakuitisha maandamano kwa ajili ya kupanda gharama za maisha wala Mgao wa Umeme

lakini ilipokuja marekebisho ya sheria ya uchaguzi haraka haraka wakaitisha maandamano kushinikiza Serikali iongeze idadi yaani kila jambo liwe na Wabunge wawili
 
waroho wa madaraka mara zote wao huwaza uchaguzi tu

kuna Watu hawakuitisha maandamano kwa ajili ya kupanda gharama za maisha wala Mgao wa Umeme

lakini ilipokuja marekebisho ya sheria ya uchaguzi haraka haraka wakaitisha maandamano kushinikiza Serikali iongeze idadi yaani kila jambo liwe na Wabunge wawili
Daaa ila hili la umeme halijakaa vizuri
 
waroho wa madaraka mara zote wao huwaza uchaguzi tu

kuna Watu hawakuitisha maandamano kwa ajili ya kupanda gharama za maisha wala Mgao wa Umeme

lakini ilipokuja marekebisho ya sheria ya uchaguzi haraka haraka wakaitisha maandamano kushinikiza Serikali iongeze idadi yaani kila jambo liwe na Wabunge wawili
Watu wana majenereta makubwa nyumbani, pesa ipo ya kutosha hawawazi watakula nini waitishe maandamano kwasababu za umeme?

Wao shida yao kubwa iliyobaki ni madaraka tu, hayo ya umeme na kupanda kwa gharama za maisha tukipenda tutayatumia kama ngazi ya kupandia kwenye madaraka.
 
Nikilinganisha na katiba ya Mama Tanzania ,katiba yetu ni bora kabisa na Haina mfano wa kulinganishwa nayo.

Kwanza, hiko kipengele Cha kwanza ambacho maelezo yake yapo kifungu Cha 34 ni unfair. Vacancy ya urais kushikiliwa na Waziri mkuu sio sawa Kwa sababu Waziri mkuu ni mteule na kumpatia nafasi ya kuongoza nafasi ya mtu aliyechaguliwa na wengi sio sawa. Katiba yetu imeondoa utata Kwa kupendekeza Makamu wa Rais atakuwa Rais ambapo Makamu wa Rais alikuwa ni mgombea mwenza wa Rais aliyechaguliwa.

Kipengele Cha pili kinachotaka uchaguzi uitishwe siku 90 baada ya nafasi kuwa vacant kama umesalia mwaka mmoja na zaidi kabla ya kuisha Kwa kipindi cha uongozi wa aliyetangulia ni matumizi mabaya ya fedha. Pata picha kunatokea vifo zaidi ya vitatu katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kuisha uongozi.

Ipo hivi, Rais aliyetangua pengine alitakiwa kumaliza kipindi chake oktaba, 2025 lakini Kwa kuwa ni mwaka mmoja zaidi kabla ya kumaliza Kwa aliyetangulia ukaitishwa uchaguzi ambaye ataanza urais katika kipindi cha miaka 5 lakini kafika mwaka 2 akafariki maana yake itabidi uitishwe uchaguzi mwingine. Je, Hilo huoni kama ni mzigo mkubwa Kwa wananchi?

Nionavyo Mimi ,katiba ya Namibia kama ndio ipo hivyo iliandikwa katika mtazamo kwamba Rais hawezi kufa kabla hajamaliza kipindi chake ndio maana unaona hoja ya uchaguzi mkuu mpya kuitishwa ni katika mazingira kwamba Rais kamaliza muda wake na si kufariki

Hapa tukubali tu kwamba waliotengeneza katiba yetu walikuwa na uwezo mkubwa wa kutazama vitu Kwa mbali. Kwanza, wametuondoloa matatizo ya mtu ambaye hajawahi kuchaguliwa wala kugombea kuchaguliwa. Pili, wametuondoloa matatizo ya kuitishwa uchaguzi mara Kwa mara nafasi ya urais inapokuwa Wazi.

Marekebisho kidogo yanayohitajika ni kubadilisha kipengele cha Sasa Cha Makamu wa Rais kuwa Rais na badala yake itamke Makamu wa Rais ambaye hakuwa mgombea mwenza hatoshika nafasi ya Urais na badala yake uchaguzi mkuu uitishwe
 
Kwenye na 3 eti Baraza likimteua mtu!
Kukiwa na jenerali anautaja urais atawakamata wote na kuwasweka ndani Kisha anajitangaza kuwa ametuliwa na Baraza kuwa rais wa mpito.


Katiba la bongo zuri sana
 
waroho wa madaraka mara zote wao huwaza uchaguzi tu

kuna Watu hawakuitisha maandamano kwa ajili ya kupanda gharama za maisha wala Mgao wa Umeme

lakini ilipokuja marekebisho ya sheria ya uchaguzi haraka haraka wakaitisha maandamano kushinikiza Serikali iongeze idadi yaani kila jambo liwe na Wabunge wawili
Alhaji Lipumba na maalimu Zitto hata kuthubutu kulisemea hilo wamekauka kimya
 
waroho wa madaraka mara zote wao huwaza uchaguzi tu

kuna Watu hawakuitisha maandamano kwa ajili ya kupanda gharama za maisha wala Mgao wa Umeme

lakini ilipokuja marekebisho ya sheria ya uchag wauzi haraka haraka wakaitisha maandamano kushinikiza Serikali iongeze idadi yaani kila jambo liwe na Wabunge wawili
Haya mambo huyajui kabisaa ni vema ukauliza ueleweshwe na siyo kupayuka kichawa chawa unaonekana una majungu yaani mshakunaku shakunaku
 
Waasisi wa nchi zao wanajua how choice works, nchi yetu hatujui KUCHAGUA lipi la kwenda nalo mpaka sasa,

Fikiria tulivyoingia:-

(a)kwenye sera za ujamaa,

(b) mpaka mwaka 2024 still in our country
mtu anaona katiba yetu iko sawa eti anaogopa gharama za uchaguzi!

Taifa laweza kulinda uhai au hata kuanzisha vita kwa ajili ya kumwokoa mtu mmoja tu kwa gharama yoyote.

Kwa usalama wa Rais na pia hata wa Makamu wa Rais katiba ya Namibia iko sawa sana!

Haiweki rehani usalama wa rais kisa gharama za uchaguzi!
(c) fikiria aina ya Muungano wetu,
(d) fikiria elimu tunavyoiendesha.
(e) fikiria kodi na namna zisivyorudi zilikokusanywa kwa uwiano kuendeleza nchi kwa usawa
etc
 
Kama hicho ndio kigezo basi ya Tz ni katiba bora zaidi. Sababu sisi hatufanyi kabisa uchaguzi mpya makamu anapokea kijiti na tunaokoa gharama za uchaguzi
Bora kuingia gharama za uchaguzi kuliko kua na kiongozi mbovu madarakani.kwasababu hasara yake ni kubwa maelfu elfu kuliko gharama za uchaguzi.Inawezekana usielewe kwasababu unafikiria hapa karibu ila ukifikiria ata miaka 20 ijayo utaona tatizo lilipo.
 
Back
Top Bottom