Mugo"The Great"
JF-Expert Member
- Oct 7, 2007
- 262
- 26
Duh jamaa mi sikumwelewa anaongea nini pale, na niliwaambia ile kitu si live mana hata yeye anajua wananchi wana hasira naye. yani tulijiandaa na simu ana bahati sana huyu baba yeye anadhani anaweza kubaili mawazo ya watanzania kw sasa?na hao waliompokea nina mashaka ufisadi uliwapitia, mtz mwenye akili hawezi kwenda pale. wewe kiongozo wa ccm [mkoa unampokea kamanani kwa kweli sipati jibu na hao waliotandika red carpet sijui wamedata au?yetu macho ila 2010 si mbali watanzania tutachagua tunayeona atafaa.Ati kamati haikumtendea haki,alitaka aulizwe nini wakati alikubali yote yatokee chini yake.halafu anasema ndege ya tz inapaa?sasa imeanguka naye na asubiri hata huo ubunge atakosa mana original wamasai wataamua wanamtaka nani kati yake na sokoine
Lowassa ni too senior kwenda kuwa balozi...
At most may be kwasababu kuna mwanamtandao UN (Dr. Migiro), kwa mtazamo wangu finyu, Lowassa anaweza pewa kazi ya heshima kusimamia mambo fulani serbia huko etc lakini Lowassa mwenyewe akitaka. Otherwise ni kubanana banana humu humu tu Tanzania.
Mugo"The Great";145531 said:Hao waliotandika red carpet akili yao imeshughulikiwa na fedha za Richmonduli kiasi kwamba ile "Conscience" imewatoka na wanaendeshwa kwa "Remote Control" Ndege ya EL iliyokuwa inapaa ikiwa imebeba 'Mshiko"-152 Milioni za Watz imetunguliwa na Kombora la JF, hitima ikasomwa na Kamati Ya Mwakyembe.
Wewe Askofu .please stay aside huu MZIKI (JF) huuwezi .ni mzito kweli kweli, tukiingia anga zako usije lalamika .maana ndioukuni huo huo unaosema kwani itakuwa zamu yako kuungua
Nadhani mchango wake ungekuwa na maana zaidi angechangia bungeni akiwa kama mbunge wa kawaida.
Haya mambo ya kukimbilia vichochoroni ( Yes.. TvT ni kichochoroni ) hayamsaidii chochote kujisafisha.
Ili mtu ujisafishe kwanza unatakiwa utumie maji safi, vyombo/nyenzo safi, na mikono yako iwe safi. Lowassa huwezi kujisafisha kwa kutumia tope unajichafua zaidi, better remain quite unawatia machungu watu bure..
Pesa za wananchi hzio ndugu...sasa analakiwa na umati ili iweje...nashangaa sana. Kwa kweli ni kufilikisa kimawazo na inaonyesha jinsi watu wetu walivyo na uwezo mdogo wa kufikiria...
Eeeh bwana kwa taarifa yako hata kama Migiro yuko UN hawezi kuwa na influence yoyote ya kumuunganisha Lowassa ilo haliwezekani kabisa...kwani kuna watu kibao wenye uzoefu sana ambao Lowassa kwao ni mtoto...sana sana ana uzoefu wa hapo Tanzania lakini anga za kimataifa hamna kitu....wala usitarajie kitu kama hicho.
Lunyungu,
Lete habari zaidi. Ila jamani acheni kuwaita Wamasai wote Richmond. Hii ya kuadhibu Wamasai wote shauri ya kosa la mtu mmoja sio sahihi kabisa.
Waliomshauri wamekosea, angetulia kwanza kama miezi kabla ya kujitetea kwenye TV. Watanzania sasa bado tuna hasira za kutuibia, hata aseme nini, hatuwezi kumwamini.
Bila kujali katendewa haki au hapana, kujiuzulu kwake kwa scandal ni somo zuri mno kwa viongozi wa TZ na faida yake ni kubwa kuliko hasara chache
kwa Lowassa.
Muda wake umepita na sasa tuangalie hao walioingia madarakani.
Mbona Pinda sasa karibu wiki mbili na hatuoni hata strategies mpya za kuifanya Tanzania ipae?
Mvua....atawapelekea wamasai wenzake wakati anachunga nao...hakuna cha mvua wala manyunyu hapo....
Msee K, ikiwezekana pungusa ukali ya maneno yako sidi ya jamii ya Kimasai, nafikiri mfua ni jambo muhimu kwa makabila yote!! Hiyo mfua ya Richmond hatuitaki huku lengai
Kishaju,
Hiyo juu haijapendeza. Ukabila tena ndugu yangu duh. Tupunguze hasira katika kujenga hoja na tufikishe ujumbe pasipo kuwaumiza wasiohusika.
Kishaju, apology accepted. Now lead the way please!oooh samahani sana....kwa kweli sikuwa na nia mbaya na kosa kama ilo halitajitokeza sana....samahani kwa wote ambao wameguswa moja kwa moja...na ninaapa kwamba kosa kama ili ili halitatokea tena maana mafisadi wanatoka pande zote za Tanzania,,,
Habari ambazo zimepatikana hivi punde kutoka kwa chanzo chetu zinasema kwamba,kuna baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari inasemekana wamehongwa na mmoja wa aliyekuwa waziri ktk baraza la mawaziri lililovunjwa aliyekuwa anahusishwa na ufisadi wa richmond ili wamsafishe kwa kumwandika vizuri na kuwa tume haikumtendea haki,chanzo chetu kinasema kuwa waandishi hao wenye roho za kimaskini na wasio na uchungu na nchi yao wamehongwa kiasi kikubwa cha pesa na hivyo wamehaidi kuifanya kazi hiyo.kwa mtindo huu jamani ufisadi utaisha?
Aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa (Monduli-CCM)hatimaye akishuka kwenye ndege yake ndogo iliyotua mjini Arusha akielekea kijijini kwake kuzungumza na wapiga kura wake. Picha kwa hisani ya Mroki Mroki