Lowassa anasafishwa!

Je, ilikuwaje kila mara wabunge walipohoji mkataba wa Richmond ulikuwa unawazuia wasifanye hivyo!? Ulikuwa unafanya hivyo kwa maslahi ya Tanzania, CCM au wewe mwenyewe? Hili la Netgroup Problems Watanzania wengi tulilijua tangu mwanzo. Kampuni ambayo ilikuwa inashughulikia kuuza stationery na ambayo haijui lolote kuhusiana umeme kwenda kupewa management ya shirika kubwa kama TANESCO ilikuwa ni ufisadi wa hali ya juu, lakini wakati huo hatukukusikia kusema chochote kupinga uamuzi huo, kwani ni dhambi kuwa upande mmoja na wananchi katika kupinga maamuzi yasiyo na maslahi kwa wananchi?

Watanzania wengi wakiwemo wafanyakazi wa TANESCO tulilipinga kwa kila hali hadi ikabidi waingizwe TANESCO wakiongozwa na FFU na mtutu wa bunduki, na hatima ya makaburu hao kupewa management ya TANESCO tunaijua pamoja na kulipwa mabilioni ya pesa ambazo hawakustahili.


Posted Date::2/23/2008
Lowassa ajitetea kutopata chochote kutoka Richmond
*Asema ni mkewe pekee aliyejua kuwa atajiuzulu
*Askofu Laizer akataza Wamasai kuitwa Richmond


Na Daniel Mjema, Arusha
Mwananchi


 
Hii nimenakili kwenye hansard za tarehe 7 feb 2008, kikao cha saa 11 jioni baada ya Lowassa kutangaza asubuhi yake kuwa anajiuzulu.

(Saa 5.11 Asubuhi Bunge lilifungwa mpaka Saa 11.00 Jioni)
(Saa 11.00 jioni Bunge lilirudia)

 
Hapa mama Kilango-Malecela akaamua kumkoma nyani giladi, mchana kweupe!

 
Utetezi wa Karamagi! Mbona ilikuwa raha huko! Nimeyamisi sana haya mambo! Mtaniwia radhi, ni marefu haya ma-hansard!

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa
kunipa fursa hii na mimi kuweza kuchangia hoja iliyo mbele yetu na kwa sababu ya
muda, nitachangia kwa yale ambayo yananigusa mimi.

Mheshimiwa Spika, naomba kwanza Bunge lako Tukufu na wananchi wote
Tanzania watambue kwamba nilihamishiwa Wizara ya Nishati na Madini mwezi Oktoba,
2006 wakati mkataba wa Richmond ulikuwa na uhai wa miezi sita tayari. Mimi
sikuhusika katik…. (Makofi/Kelele/Miguno)
Mheshimiwa Spika, naomba unilinde!

SPIKA: Utulivu jamani! Waheshimiwa utulivu, utulivu! Tumpe nafasi yake ya
kujieleza.
48
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mimi sikuhusika. Kama kuna vielelezo
ndani ya kabrasha ambalo lilikuwa linaelezwa ambapo kuna barua yangu ama kuandaa
mkataba ama kuongoza mkataba kwa njia yoyote, vingetoka. Lakini hilo haliniondolei
wajibu kwamba nilikuwa Waziri katika Serikali hii katika collective responsibility wakati
maamuzi haya yanatokea.

Mheshimiwa Spika, vilevile, nataka niwarudishe nyuma mwezi wa Oktoba.
Nilipoingia Wizara hii hali ya umeme ilikuwaje katika nchi yetu? Umeme wetu ambao
kiasi kikubwa unatokana na mabwawa (hydro) ulikuwa umeshuka kutoka megawatt 560
mpaka megawatt 120. Hiyo ndiyo hali tuliyokuwa nayo. Gridi ya Taifa ingeweza
kukatika wakati wowote na nchi ikawa gizani. Hayo ndiyo mazingira ambayo
wanaohusika wote katika kufanya maamuzi walikuwa wanafanya kazi nayo. Katika nchi
nyingine hiyo ungeiita kama state of emergency ku-declare state of emergency! Mimi
mwenyewe nilipoingia pale kila siku ilikuwa nnapokea ripoti ya mabwawa yote Tanzania
na wakati mwingine kuweza kusema hapa zima na hapa washa ili kuinusuru nchi yetu
katika giza.

Sasa hapa suala la kwanza linalonigusa, wanasema kwamba mimi nilishiriki
kukataa ama kushinikiza TANESCO isifute mkataba wa Richmond Oktoba, 2006.
Mheshimiwa Spika, mimi nilipoingia Wizarani pale pamoja na Katibu Mkuu, kazi
yetu kubwa ya kwanza ilikuwa kuona namna gani ya kufuta huu mkataba. Lakini si
kufuta mkataba kwamba tusiongezewe gharama, ni kufuta mkataba ili tuweze kumpata
mwingine kwa sababu wakati ule umeme ulikuwa haupo, tulikuwa tunahitaji umeme.
Ilikuwa ni namna gani ya kufuta mkataba na kumpata mwingine…… (Miguno)
Mheshimiwa Spika, naomba unilinde!
SPIKA: Endelea Mheshimiwa Waziri!

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Kwa hiyo, tukaanza tarehe 5 – haya
mambo ya Dowans yamekuja baadaye. Tarehe 5 Oktoba, Katibu Mkuu kamwandikia
Mwanasheria Mkuu ili kutupa vigezo ambavyo tunaweza kutumia katika kuvunja huo
mkataba na ili kutomwezesha Richmond kwenda mahakamani kwa sababu ya kuvunja
mkataba. Tulipewa ushauri ambao tuliwaagiza TANESCO waangalie vipengele gani
wanaweza kutumia katika kufanikisha huo mchakato ambao ulikuwa umeanzishwa na
Katibu Mkuu.

Barua ambayo imeambatanishwa ya tarehe 27 Oktoba, 2006, ilikuwa ni jibu la
hiyo barua na ukiisoma vizuri, iliandikwa na Meneja Mkuu wa TANESCO wakati ule
alikuwa ni…. Jina lake silikumbuki, wale wa Net Group Solution. Pamoja na mengine
alitaja katika kifungu kwamba mkataba huu tuondokane nao kwa sababu Richmond
hajaweza kutoa umeme unaotakikana ambao ingebidi upatikane on commercial operating
date, haijaandikwa ndani ya mkataba, imeachwa blank. Akaomba, na mwenyewe
ameweka kwenye barua ambayo iko bayana kwamba pengine tunaweza kutumia zile
minutes ambazo tulikuwa tunakaa tunazungumza, labda ziwe ndiyo vithibitisho vya
kuweza kusema ameshindwa.

49
Lakini hapa Waheshimiwa Wabunge, tunao wanasheria na Kamati Teule ilikuwa
na Mwansheria tena aliyebobea, kama minutes za vikao hazikuandikwa ndani ya mkataba
kwamba zitakuwa viambatanisho kwenye mkataba, ukizitumia mahakamani,
hazitakubalika. Palikuwepo na vipengele vingine ambavyo tungeweza kuvitumia,
kampuni haijaorodheshwa hapa, haiko Marekani. Lakini, mkisoma vizuri hiyo ripoti na
mimi nimeisoma vizuri, utaona kwamba kufuatilia hivyo vipengele, Richmond angeweza
kwenda mahakamani, akatuchelewesha hata kama tungempata mkandarasi mwingine
ambaye tulikuwa tunamhitaji sana wakati anazalisha megawatts 120 za nchi nzima, siyo
kitu kidogo. Angeweza kuweka Court Injunction za kutukataza, tungeweza kupoteza
muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tulichukua njia mbili: Moja, tuache mkataba ufe
wenyewe ukifika mwezi wa pili na kwa kutumia njia hiyo, wengine ambao tunaweza
kuwapata ambao wanaweza kutunusuru kwenye hili tunaweza tukawa-engage bila kupata
Court Injunction ya Richmond. Na kwa njia hiyo ndiyo sababu tuliweza kumpata Alstom,
kuweza kumchukua Mwanza ku-stabilize gridi ya taifa bila kuwa na matatizo na
Richmond kwa sababu hatukuwagusa. Tulijua tukiwagusa, atatuchukua kortini.
Tukivunja mkataba, anaweza kudai fidia ama akaweka injunction ya kutuchelewesha, na
sisi wakati ule hatukuwa Mungu, tusingeweza kujua kwamba Januari mvua itanyesha.
Tulikuwa tunajitayarisha kwa muda mrefu na wataalamu walikuwa wanasema inaweza
ikachukua takriban miaka mitatu hivi ili mabwawa yetu yaweze kurejea hali yake ya
kawaida.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ili Kamati Teule kutenda haki kwa maamuzi
waliyosema, kwanza, wangeonyesha wapi Karamagi nimeshinikiza? Maana yake wote
huko katika vielelezo wameeleza: "Wakati Waziri anashinikiza ama anaandika barua au
anaita Menejimenti kuiagiza au Bodi, kwa hili sikuona mahala popote zaidi ya ile kwa
Kiingereza wanaita circumstantial na nafikiri kuhukumu mtu kwa hili wakati
hujajirudisha kwenye mazingira wakati ule tulipokuwa tunafanya maamuzi, mimi
kwangu naona kwamba haikuwa sahihi.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu sina muda mrefu, kuna hoja nyingine ambayo
ilikuwa inaelekeza kwamba mimi mwenyewe kama Waziri niliwekea shinikizo
TANESCO ili i-assign (kuhuisha) huo mkataba wa Richmond kwa Dowans.
Tunachokizungumzia hapa kama nilivyokwisha sema, ni mwezi wa Novemba na
mwezi wa Desemba na sijui kama kwenye viambatanisho wameonyesha level ya maji
ilivyokuwa Mtera ambayo tayari ilikuwa chini kabisa. Ilikuwa ama mashine zile karibu
zlikuwa zinavuta upepo. Kwa hiyo, tulikuwa tumeanza kuzima mashine Mtera na Kidatu
kusudi tuzitumie tu gridi ya taifa ambayo ilikuwa inakatika katika mara kwa mara
inapozima, kwa sababu bila ya Mtera na Kidatu, gridi ya taifa ingezimika, nchi nzima
ingekuwa kwenye giza na hata ukiwa na hizi za Songas, IPTL, Aggreko, haziwezi
kuwasha gridi ya taifa. Kwa hiyo, ilibidi hayo maji yaende chini, ilikuwa hatari kabisa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nilikuwa safarini Canada. Nilipopata kwenye EMail
yangu kwamba Richmond wana mpango wa ku-assign ile contract kwa Dowans,
50
kwanza nilifurahi kwamba sasa tuna opportunity labda ya kuweza kumpata mtu
anayeweza. Lakini nikaona tusije tukaingia kwenye tatizo kama la Richmond kwa sababu
tulikuwa tumekwishagundua kuwa Richmond ni kama tapeli. Hivyo mpaka nafika pale,
tulikuwa tumekwishagundua kwamba Richmond ni tapeli. Kwa hiyo, ili tusiingie tatizo
kama la Richmond, mimi kama Waziri wa Nishati na Madini nikaona nisingoje hiyo ziara
ambayo sijui ilikuwa inachukua muda gani, nikaona nimpigie simu Mwenyekiti wa Bodi
ya TANESCO, Mheshimiwa Kazaura, nikamwambia: "chonde chonde nimesikia taarifa
hizi, chonde chonde msi-assign huo mkataba bila kufanya yafuatayo:-….."

Yameorodheshwa kwenye page 90 na kweli Kamati imenifanyia haki kwa sababu
imeeleza vilevile kama nilivyotahadharisha. Lakini pamoja na tahadhari hizo,
hawakunipongeza kwamba angalau na mimi nilianza kuchukua due diligence.
Wakanituhumu kwamba hiyo tahadhari ni kama shinikizo kwa TANESCO. (Kicheko)
Mheshimiwa Spika, Baniani mbaya, kiatu chake dawa! Akifanya jambo zuri,
jamani mpongezeni! Najua inaweza kuwa ni jambo jema siku hizi style nzuri unapotaja
jina la Karamagi, inaonekana vizuri. Labda ilionekana kama hii ripoti kama haikutaja
Karamagi, haitanoga. Lakini kwa hili…! (Kicheko/Miguno)
SPIKA: Lakini Mheshimiwa Waziri, kama tapeli anapendekeza mkataba wake
uende kwa mwingine, hushituki?! (Makofi)

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika, wewe ni
Mwanasheria, kama tapeli, amekuingiza katika mkataba ambao uko halali, ukiukatisha
kinyume na mkataba huo, unampa uwezekano wa yeye kunufaika, akakuchukua
mahakamani, ukamlipa pesa ya bure!
SPIKA: Aah! Endelea tu Mheshimiwa!

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Labda ile isingenoga, kwa hiyo,
ikaonekana niunganishwe kwenye hiyo ripoti. Lakini kweli nilichokuwa nafanya kwa
moyo wangu, nikatumia profession yangu ya Finance kwamba wafanye due diligence
physically. Mheshimiwa Spika, naomba zile minutes nilizotumia uniongezee kidogo.
Wafanye physical due deligence, amezitaja. Nikizitaja, ziko ukurasa wa 90, utazisoma,
physical.

Lakini wakati ule management ya TANESCO na yenyewe ikatoa kwamba zaidi ya
physical, watafanya financial due diligence ambayo ni sawa! Sasa jamani, naomba kwa
hili mtupongeze kwamba angalau kwa mara ya kwanza tulifanya mambo ambayo yako
sahihi.

Mheshimiwa Spika, sasa nimalizie, kwa sababu kengele ya pili karibu ilie, nikuquote
tu wakati unaomba msamaha ambapo ulisema kwamba, "tafsiri ya mambo
ukiyatumia vibaya ama kwa ubinafsi, yana matatizo". Na mimi naona hapa mtiririko wa
mambo yalivyokuwa ni sawa, lakini inapokuja conclusion, inakuja tafsiri nyingine. Kwa
hiyo, naona hiyo hainifanyii haki.
51

La pili, niwapongeze Waheshimiwa Wabunge walio wengi, wamenitumia
messages mbalimbali za kunipa faraja. Lakini wa mwisho ambaye amenifurahisha,
ambalo niliseme, amesema, "Yesu hakutenda dhambi, lakini alitolewa kafara", ukienda
kwenye vitabu vya dini, ili kusudi atusaidie sisi wengine duniani tusiwe na dhambi. Kwa
hiyo, kwa kuzingatia hilo na kwa kuzingatia dhana ya uwajibikaji na maslahi ya taifa na
heshima ya Chama changu, leo asubuhi, nimemwandikia Mheshimiwa Rais barua ya
kujiuzulu wadhifa wangu, bado nangoja maamuzi yake kwa sababu ndiye aliyeniteua.
Lakini hiyo barua nimekwishamtumia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache, naona tujadili hii ripoti lakini tujadili
siyo kwa ushabiki. Aliyekosea azungumzwe, lakini yale mengine ambayo yananifaa,
tuyaweke pembeni. Naomba kuwasilisha! (Makofi/Kicheko)
SPIKA: Spika anaruhusu ushabiki kwa nchi ya Tanzania. Ushabiki uwepo tu
lakini tushabikie maslahi ya nchi yetu! (Makofi)
 
..............WAKUU NASIKIA ANNA KILANGO AMELAZWA MUHIMBILI..nani ana nyeti??..maana mimi nipo nje ya masikani yangu ya kupiga box...
 
Namalizia na hii ya Bangusilo Ibra Msabaha. Kwanza aliongea kisomi (kamkumbusha Mwakyembe kuwa ana PhD pia, na siyo ya "desa"), kistaarabu sana kwa kweli, na sense of humor (utani na wanyamwezi na wasukuma).

WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa
Spika, awali ya yote, naomba kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunifikisha hadi leo
nikiwa hai na pia kumshukuru kwa yote.
Mheshimiwa Spika, pili, napenda nitoe pongezi za dhati kwa Kamati,
Wanakamati, Mwenyekiti wa Kamati na Bunge lako Tukufu. Napenda hasa nimpongeze,
Ndugu yangu, Mheshimiwa Harrison Mwakyembe kwa sababu yeye na mimi
tunafahamiana kutokana na huko tulikotoka kihistoria kwenye mambo ya taaluma katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Napenda nimpongeze kwa jinsi alivyowasilisha kwa
staili yake na alipomaliza baada ya saa moja na nusu akamfanya kila mtu aamini yote,
nampongeza sana. Nampongeza pia kwa kuonyesha kwamba yeye pamoja na Kamati
walikuwa na dhamira ya kufanya kazi hii na kufanikisha dhamira nzuri waliyokuwa
nayo.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba nichukue nafasi hii kwa
namna ya pekee kabisa, kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu. Amekuwa Waziri
Mkuu wangu kwa miaka yote hii miwili na hasa kwa kitendo chake cha leo cha
kutangaza kwamba anakusudia kujiuzulu.
Mheshimiwa Spika, kule nyumbani kwetu sisi, wewe Mnyamwezi sisi Wazaramo,
mtu kama huyu tunamwita Kilongola yaani anayeonyesha njia. Kwa hiyo, nampongeza
59
sana Mheshimiwa Lowassa kwa kuwa Kilongola, kaonyesha njia na sisi wengine
tutafuata. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sikusidii kujibu hoja kwa hoja, hakuna haja, hapa lipo jambo
muhimu sana linajadiliwa na kama yapo mambo au upungufu katika taarifa ile, hayo ni
mambo ya kushauriana namna ya kuyaboresha ili iwe nzuri zaidi kwa ajili ya
kumbukumbu za Bunge na kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, isipokuwa nataka nitoe mfano mmoja tu. Kwa mfano, jana
wakati Mheshimiwa Mwakyembe, anawasilisha hoja yake, alinishtua kidogo alipotaja
kwamba Richmond walilipwa dola milioni 10/-. Kama ni kweli basi kulikuwa na tatizo
kwa sababu nakumbuka suala hili lilizuiwa wakati mimi nikiwa Waziri wa Nisahati na
Madini mpaka naondoka. Sasa kama walilipwa wakati ule, itakuwa ni suala la kutafuta
ilikuwaje kwa sababu najua lilizuiwa na Waziri wa Fedha alilizuia na mpaka viongozi wa
juu walilizuia. Natoa mfano wa vitu ambavyo vinaweza pengine vikaboreshwa pengine
wakati wa kupitia upya.
Mheshimiwa Spika, mfano mwingine ni kama ile hali yenyewe ya dharura na
ufanyaji maamuzi nyakati za dharura, huko mbele ya safari tunafanyaje, mfumo wa
mawasiliano unakuwaje, kwa sababu mambo mengine ni mambo ya kimfumo unayakuta
katika Serikali!
Mheshimiwa Spika, wewe ni mzoefu wa mambo haya na jinsi yanavyokwenda ni
hivyo hivyo, dokezo linatoka kwa Waziri linakwenda kwa Waziri Mkuu, linatoka kwa
Waziri Mkuu linakwenda kwa Rais, tuchukue mfano, au pengine ni mambo
yanayokwenda kwenye Kamati Maalumu au Cabinet, yakitoka kule yanakwenda kupata
idhini na kadhalika. Sasa haya ni mambo ambayo nadhani yanaweza yakatizamwa ni
namna gani tunaweza kuboresha mfumo wetu kwa kuzingatia Sheria zetu.
Mheshimiwa Spika, lingine ambalo linaweza kuboreshwa hata katika presentation
hii, ukurasa 147 mpaka 148. Hii naitoa kwa ajili ya Kamati, ukiisoma unaweza ukadhani
ndiyo mambo yale niliyokuwa ninasema mimi Bangusilo, kuna maneno ambayo
yanazungumzia habari ya uwajibikaji wa Waziri na Katibu Mkuu, ilivyoandikwa
inakuwa kama vile hawa wanawajibika kama kafara na mimi nadhani pengine maana
yenyewe siyo hiyo.
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema awali, nipo tayari kushirikiana na Kamati
katika maeneo ambayo nadhani yakipitiwa tena yanaweza yakaboreshwa vizuri zaidi kwa
ajili ya kumbukumbu sahihi na kwa ajili ya Taifa letu.
Mheshimiwa Spika, pia katika mtiririko huu yapo mambo ambayo nayaita kama
ni ya kiufundi. Nadhani Mheshimiwa Dr. Mwakyembe kwa background ambayo
nimeisema kwamba wote tumetokea huko, atakubaliana nami kwamba wakati mwingine
unapofanya uchunguzi ama utafiti ukiondoka na dhana fulani …
MBUNGE FULANI: Hypothesis!
60
WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Siyo hypothesis,
nasema ukiondoka na kwa mfano uamuzi…
MBUNGE FULANI: A pre-inquest.
WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Ndiyo, a preinquest
of idea siyo hypothesis, unaweza ukaenda nayo ukajikuta wewe tayari
umeshapata jibu sasa unatafuta njia ya kuhalalisha. Ninachosema ni kitu ambacho
unapaswa uwe kidogo mwangalifu na ukiipitia taarifa hii wakati mwingine inatoa sura
hiyo ambayo pengine siyo sahihi kabisa, hiyo ni moja.
Mheshimiwa Spika, lakini la pili, pale mahali ambapo alikuwa anatoa nadhani
kwenye maagizo sijui kama iko humu kwenye taarifa maana sikupitia neno kwa neno,
jana wakati anatoa taarifa hapa alimpa pole ndugu yetu yule Kubenea lakini jinsi
alivyosema ikaonekana kama vile kuna connection baina ya RICHMOND na matatizo
aliyopata ndugu yetu Kubenea, ndiyo!
Mheshimiwa Spika, niliwahi kuulizwa mahali kwamba wewe umewahi kuhojiwa
juu ya ndugu yetu Kubenea? Nikawaambia hili ni jambo la kushangaza lakini
ninachosema yote hii inatokana na jinsi ule mtiririko ulivyo unaweza ukatoa taswira
ambayo siyo sahihi.
Mheshimiwa Spika, unapokuwa unafanya utafiti kama huu wenye mambo ya
kisiasa, ni rahisi sana kuweza kuteleza namna hiyo na mimi nadhani ni vizuri
tukashauriana namna ya kuboresha.
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema, kama ni suala la kwenda hoja kwa hoja,
tutapata muda huo baadaye wa kuweza kushauriana kwa maana ya maeneo yanayohitaji
kuboreshwa. Lakini mimi kwa kweli nia yangu ya kusimama hapa, kwanza, ni kusema
kwamba mimi si mwoga, ni muadilifu, sipendi rushwa na ni mchapa kazi na nashirikiana
na watu. Katika Bunge hili nadhani ni mashahidi, Wasukuma na Wanyamwezi humu
ndani wanaweza wakakubali kwamba mimi ndiye Babu yao humu ndani, sina tatizo na
ushirikiano na watu. Kwa hiyo, nilitaka hili niliseme tu kwa sababu wakati mwingine
inawezekana ni tabia imejionyesha…
SPIKA: Kwa umbile lako Mheshimiwa Waziri, inaonyesha kabisa wewe ni
Mnyamwezi au Msukuma. (Kicheko)
WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa
Spika, nalisema hili kwa sababu wakati mwingine yanaposemwa haya maneno kama
alivyosema ndugu yangu Mwakyembe jana, ya ubabe na kiburi, sasa kiburi naogopa
sana. Sisi Waislamu tunasema kiburi ni sifa ya Mwenyezi Mungu siyo ya binadamu,
naogopa. Sasa inawezekana wameyapata haya huko chini huko kwa watendaji, ni bahati
61
mbaya lakini nataka niseme kwamba kwa kweli si sifa nzuri kwa binadamu ya ubabe,
kiburi, jeuri na kadhalika, Mwenyezi Mungu atupishilie mbali.
Mheshimiwa Spika, nataka niseme tu kwamba nimesimama kusema yale ambayo
yameonekana. Kwanza, nakubali kuchukua collective responsibility pia responsibility ya
wale ambao wako chini yangu kwa yale ambayo wameyafanya ambavyo siyo sawasawa
kama Kamati ilivyoona. Kwa maana hiyo, siogopi kuwajibika na najua kuwajibika katika
context yetu sisi labda katika suala kama hili lakini katika mambo mengine inaweza kuwa
kidogo kila siku Waziri mmoja yupo katika matata kwa sababu ya hali yetu ya maisha
ilivyokuwa duni. Lakini kimsingi mimi ni mtu ninayeamini katika uwajibikaji, katika
utawala bora na katika mambo yale ambayo yanadumisha na kuendeleza wananchi wetu.
Mheshimiwa Spika, niliona niseme kutokana na hali jinsi ilivyo kwa sababu siasa
ni suala la imani ya watu. Kuwa kiongozi wa kisiasa ni imani ya watu na jinsi watu
wanavyoona ni lazima kiongozi wa kisiasa uwe na imani ya wale unaowaongoza na
perception yao ni jinsi wanavyokutazama na lazima pia iwe ni sawasawa. Sasa
inawezekana kabisa hata wakikutazama kwamba uko hivyo lakini hauko hivyo inatosha
kwako kusema kwamba kwa kweli ni vizuri mtu ukae kando ili shughuli za Kitaifa
ziendelee na wewe uweze kuchangia kwa njia nyingine.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimesimama hapa kwa kweli kwa heshima ya nchi
yangu, Chama changu, Jimbo langu na kwa heshima kwa kweli ya Bunge langu, ni
muhimu sana hii taasisi, kusema hivi, ndiyo maana nikamwita Mheshimiwa Waziri
Mkuu, yeye ni Kilongola kwamba alionyesha njia, asubuhi ya leo nimekwenda kumwona
Mheshimiwa Rais na kumweleza dhamira yangu ya kujiuzulu na kama ilivyo kawaida
kama ambavyo wewe mwenyewe ulivyosema wote sisi tunangojea amri yake.
Mheshimiwa Spika, lakini namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa heshima
kubwa aliyonipa, namshukuru mke wangu na familia yangu kwa ujumla kwa msaada
wote ambao wamenipa, nawashukuru wananchi wa Kibaha na hasa Kibaha Vijijini,
Jimboni kwangu, wanakijiji wenzagu wa Kijiji cha Soga na wale Wasukuma na
Wanyamwezi mnakaribishwa, mfundishwe namna ya kula kwa nazi, nakushukuru sana
Mheshimiwa Spika, Naibu Spika na Waheshimiwa Wabunge wote. Hapo Mheshimiwa
Rais atakapokubali, naamini nitapata fursa tena nyingine ya kukaa pamoja nanyi na
kuwashughulikia Wasukuma ipasavyo, nashukuru sana. (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Waziri, unataka kututoa kafara sisi Wasukuma sasa.
Tunaendelea Waheshimiwa, ahsante sana, nimeguswa sana na namna ulivyowasilisha
hotuba yako, ahsante sana. (Kicheko/Makofi)
 
Mjadala wote wa siku hiyo uko hapa: [media]http://www.bunge.go.tz/Polis/PAMS/Docs/HS-10-8-2008.pdf[/media]
 
..............WAKUU NASIKIA ANNA KILANGO AMELAZWA MUHIMBILI..nani ana nyeti??..maana mimi nipo nje ya masikani yangu ya kupiga box...

Ni kweli Phil, huyo mama alilazwa Muhimbili zile wodi za MOI siku kama 4 hivi zilizopita na inaelezwa alikuwa anasumbuliwa na malaria kali. Habari nilizopata jana asubuhi ni kuwa ilikuwa aruhusiwe maana alishapata nafuu.
 

Mimi I love you wewe JF maana ni nondo tu kila mara .Tuzidi kuchambua tuone wapi Ndanda Kosovo alionewa .Tusikurupuke
 
Lowassa is sinking on quick sand, he is done kauli zake ni za Mfa maji haishi kutapatapa.

I will volunteer to have an interview with him and let any TV station or Radio Station in the world cover the interview.I will strip him naked and he will never dare to call for aninterview for a long time about this RDC sheit!

One pissed off clergy!
 

So I am curios, what did Usalama said at the meeting? what was their role on the whole issue? Was it Apson who was Chief of TISS or Othman when this meeting took place?

Then what was the role of Hoseah and TAKUKURU when they ran their investigation, didn't they compare notes with their cousins at TISS?

If the whole RDC is now known to be bogus, where was TISS on this? aren't they supposed to do a due dilligence and background investigation on behalf of Serikali? or RDC is another Kagoda since the money to finance the whole programme was from WB/IMF and not GVTZ?
 
Ndege ya Lowassa ilipotua... (picha)

Hii statement ina maana kama 6 hivi.... 3 polemical, 1 neutral na 2 positive !!
 
Mnataka kusema kwamba Muungwana anataka kula matapishi yake.
 

Huyu Balile alivyoripoti habari hii utadhani ni makala binafsi (note hizo sentensi bold).Reading between lines,nakubaliana kabisa na tetesi kwamba kuna waandishi wameshanunuliwa kwa minajili ya kumrejesha Lowassa ndani ya serikali.
 

1.Yeye Kurejea na Kuiongoza Tanzania-'Over my dead body' and i suppose i speak for many Tzns.

2.Kujifananisha na Mzee wetu Ruksa ni Kosa lingine kubwa sana-Mzee wetu aliwajibika kikazi,Yeye Aligundulika kwa WIZI wa mali ya Umma.

3.Yeye ndiye mbaya wa Watanzania,na-si vinginevyo!!

4.Hata kama wamechuma pamoja,wanakunywa chai pamoja huku wakijadili jinsi watakavyo PANGISHANA ktk hiyo NYUMBA iliyeko kwenye PRIME AREA,lakini Watanzania Hatutosita kuhoji,isitoshe marehemu Babu alishasema:'...Pale mahala huwa hapakimbiliwi!!!'

**Huyu Bwana amekurupuka na kuanza kujieleza kwenye vyombo vya habari, akidhani labda atabadili 'Moods' & 'Views' za watu,Nani anataka kusikiliza Maelezo yake??Yeye asubiri tutapo mburuza mbele ya vyombo vya Sheria,ndiyo ajieleze kwa minaajili ya kujitetea.
 
Amekuwa akitamba kwenye private kuwa atakuwa rais tu hata iweje 2010, which raises more questions kuliko majibu, including anajiamini nini hasa huyu baba?

Kwani mwenyezi Mungu kuna aliowaumba ili wawe viongozi tu na wasiwe waongozwa? Viongozi wenye busara za siasa hunyamaza kimyaa wanapotoka, na kufanya mambo yao kwa siri, huku wakiwaaachia wananchi kuamua ukweli na uongo, lakini baba huyu toka atoke amekuwa kwenye media hata kuliko alipokuwepo kwenye power, kulikoni? Kwani wa kuamua awe kiongozi au asiwe ni nani yeye au sisi wananchi?

Huyu amekatishwa nini hasa anaocholilia kila kukicha na maneno mengi mapya yuanayojaribu kuikwepa ripoti ya Mbunge Mwakyembe, ambayo ameshindwa kuijibu akiwa madarakani, sasa ataweza vipi kuijibu akiwa nje? It is about time mtu mzima amwambie wazi kuwa we do not miss him, na kwamba as a nation wa are just doing fine!
 
Naona sasa JK anataka azame naye, haina shida tusubiri!!!!!!!!!
 
Haya anayoyasema Lowassa kwenye mikutano ya hadhara alishindwa nini kuyasema bungeni siku ripoti ya Kamati Teule ilipomdondoshea tuhuma hizo? Au ni kwa kuwa hapo hakuna wabunge kama kina Selelii na Kilango wa kumjibu?

Na bado nazidi kuamini kuwa kitendo cha kutokuhojiwa na kamati kilipangwa, pengine hata kina Mwakyembe hawakujua kuwa wanaingizwa mkenge waliposhauriwa ama walipoamua kutokumhoji Lowassa. Huyo aliyepanga na kufanikisha hili ni tactician hasa aliyefuzu intelligensia ya kifisadi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…