Lowassa amtisha Rais Kikwete

Lowassa amtisha Rais Kikwete

safari ya matumaini imeanza,hizi ni rasharasha tu,mengi tulipitia hizi taarab hazitotuyumbisha..
TEAM lowassa
 
Last edited by a moderator:
Watanzania watamkataa Lowassa kupitia sanduku la kura!

Ngoja tuone hiyo CC kma itampitisha ila kuna coaster 100 zinasubiria tarehe 30 zikasombe wa2 huko wilayani kuwaleta sheikh amri......hivi kma anapendwa c raia atakuja uwanjani kwa nauli yake au siyo,hii tabia ya kuleta wa2 na mabasi ccm wamezoea ili uwanja ujae dadadeki zao ngoja tungojee tuone mwisho
 
nop to be ignored! / LOWASSA sio MTU WA VISASI by NATURE/ inawezekana wewe ni timu MEMBE au MWANDOSYA
 
Naona kama Mamvi amei-hold CCM under siege vile lakini ajue ti hatafikia raundi ya kupigiwa kura
 
Team membe wameamua kumtisha Jk na familia yake...Lowassa sio mtu wa visasi Lowassa ni mtu wa kazi!
 
Si walimweka madarakani JK...wanaweza fanya watakavyo...kuna ahadi nyingi waliaahidiana hadi mtu kumpiga jeki JK kuingia magogoni... Ahadi ni kuwa baada ya JK... Lowassa ndio atakuwa Rais... hiyo ilikuwa amini yao... yaani kiapo chao na JK, sasa ndio hivyo hali imekuwa ngumu, Lowassa atapita na kuwa Rais...ila hii ni Story imeletwa na Team Membe kumtisha JK, ili JK akate jina la EL... Lowassa si mtu wa visasi... Team Membe hawana mbinu kabisa.. mbinu zao ni attacks to Lowassa tu.. very poor
 
Itakuwa movie nzuri kuwafikisha mahakamani ili watuambie ukweli kuhusu Richmond iliyo sababisha Lowassa achafuliwe jina lake. Gooooooooooo Lowassa magomeni ni kwako. Mahamuzi magumu tunayasubiri kwa hamu.
 
Katiba hairuhusu rais mstaafu kushtakiwa kwa lolote alilotenda akiwa madarakani!

Lowasa hana Time na mabaya ya Nyuma yeye anataka kuingia ikulu na kuanza ukurasa mpya atatawala kama Mwai kibaki na mandela hatakuwa na Visasi.
 
uandishi wa kizandiki namna hii
alafu wanalia lia sheria kali zingitungwa
 
Si walimweka madarakani JK...wanaweza fanya watakavyo...kuna ahadi nyingi waliaahidiana hadi mtu kumpiga jeki JK kuingia magogoni... Ahadi ni kuwa baada ya JK... Lowassa ndio atakuwa Rais... hiyo ilikuwa amini yao... yaani kiapo chao na JK, sasa ndio hivyo hali imekuwa ngumu, Lowassa atapita na kuwa Rais...ila hii ni Story imeletwa na Team Membe kumtisha JK, ili JK akate jina la EL... Lowassa si mtu wa visasi... Team Membe hawana mbinu kabisa.. mbinu zao ni attacks to Lowassa tu.. very poor

Mtu kiongozi wa Fitna juu ya Lowasa ni Membe pekee wengine akina Nape ni wapambe wake tu baada ya kupewa vicent tokea kwenye Yale mapesa ya marehemu Gadafi.
 
EDWARD Lowassa, mmoja wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliojiapiza kufia katika urais, amekimega chama hicho vipande viwili. Anaripoti Yusuf Aboud … (endelea).

Lowassa aliyekuwa mmoja wa wanachama sita wa chama hicho walikuwa katika uangalizi, anadaiwa kuwa ameshindikiza kuondolewa mapema adhabu hiyo, vinginevyo angeondoka.

“Ni kweli chama chetu kimemshindwa Lowassa na sasa kimemuondoa kifungoni. Hii maana yeka ni kwamba sasa Lowassa yuko huru kuwa mgombea urais wa chama chetu katika uchaguzi mkuu ujao,” anaeleza mjumbe mmoja wa NEC aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Amesema, “Kwa maoni yangu, hatua hii itakidhoofisha zaidi CCM kuliko kukiimarisha. Kama CCM inajitakia mema, hakiwezi kuruhusu Lowassa kuwa mgombea wake. Huyu mtu amekivuruga chama chetu. Amenunua watu wetu na amekigeuza chama kuwa genge la wanunuzi wa kura.”

Jana Jumatatu, Kamati ya Maadili ya chama hicho iliyodai ilikuwa na “faili la Lowassa na watuhumiwa wengine sita,” imesema kuwa mwanasiasa huyo “hana tena hatia na kwamba adhabu aliyopewa tayari imemalizika.”

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa ndani ya chama hicho wanasema, “kuachiwa huru Lowassa” kunathibitisha udhaifu wa mwenyekiti wa chama hicho, katika kusimamia chama chake.

Taarifa zinasema, ikiwa Lowassa atakapitishwa na chama hicho kuwa mgombea wake urais, taifa litaendelea kutumbukia katika visa vya visasi, kutekwa na kuteswa, kumwagiwa tindikali na matukio mengine dhidi ya wananchi na vyombo vya habari.

Aidha, watu kadhaa akiwamo Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete, Salma Kikwete, Bernard Membe, George Madafu, Jack Zoka na Othuman Rashid, wataweza kufikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa madai ya matumizi mabaya ya madaraka.

Wengine wanaoweza kufikishwa mahakamani, waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari, ambao watatuhumiwa kuandika uchochezi na kudhoofisha serikali.

Jakaya Kikwete ambaye ndiye rais wa Jamhuri, amewahi kunukuliwa na mmoja wa marafiki zake akijiapiza kuwa “Lowassa hawezi hata kufikiriwa kuwa mgombea urais.”

Hivi karibuni, gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki lilichapisha taarifa kuwa Lowassa anaungwa mkono katika mbio zake za kugombea urais na aliyekuwa mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Rostam ametajwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa, Col. Apson Mwang’onda ambaye alitajwa kuwa mwenyekiti wa “kamati ya ushindi ya Lowassa.”

Rostam ambaye amehamishia sehemu kubwa za biashara zake nchini Kenya na Dubai kwa sasa, ndiye aliyekuwa mfadhili mkuu wa Kikwete katika mbio za urais mwaka 2005.

Mfanyabiashara huyo ambaye amewahi kuwa mbunge wa Igunga (CCM), alikuwa miongoni mwa kundi lililohodhi CCM na kufanya maamuzi mengi kwa niaba ya chama na serikali. Katika miaka mitano ya kwanza ya utawala wa Kikwete, Rostam alifanywa mweka hazina wa chama hicho.

Mbali na Rostam Aziz, Lowassa amezunguukwa na watu wengi wanaotiliwa shaka uadilifu wao mbele ya jamii, akiwamo Andrew Chenge na Nazir Karamagi.

Hao wengine hawakuwa wabaya kwa Lowasa japo watakuwa na ya hapa na pale kidogo. Mtu pekee Adui wa Lowasa ni Benard Membe huyu anatamani hata Lowasa Afe leo atashukuru kwani katumia Pesa nyingi sana kumroga, kumchafua kafanya mbinu mbali mbali ikiwemo kumchonganisha na watu wa Usalama wa Taifa nk, membe anaogopa sana Lowasa akiingia ikulu lazima atahama Nchi na huenda akaenda kumpigia magoti mapema amwombe msamaha kabla hakijanuka juu ya mapesa ya Marehemu Gadafi aliyokwapua kimya kimya na kuyatumia kusaka njia ya kwenda ikilu.
 
Si walimweka madarakani JK...wanaweza fanya watakavyo...kuna ahadi nyingi waliaahidiana hadi mtu kumpiga jeki JK kuingia magogoni... Ahadi ni kuwa baada ya JK... Lowassa ndio atakuwa Rais... hiyo ilikuwa amini yao... yaani kiapo chao na JK, sasa ndio hivyo hali imekuwa ngumu, Lowassa atapita na kuwa Rais...ila hii ni Story imeletwa na Team Membe kumtisha JK, ili JK akate jina la EL... Lowassa si mtu wa visasi... Team Membe hawana mbinu kabisa.. mbinu zao ni attacks to Lowassa tu.. very poor

Mtu kiongozi wa Fitna juu ya Lowasa ni Membe pekee wengine akina Nape ni wapambe wake tu baada ya kupewa vicent tokea kwenye Yale mapesa ya marehemu Gadafi.
 
Membe kahangaika weee hadi alienda Misitu ya Amazoni kusaka waganga ili cc wampitishe sasa ngoja tuone kama uchawi wa membe utafanya kazi.
 
Back
Top Bottom