Lowassa amtisha Rais Kikwete

Lowassa amtisha Rais Kikwete

..Aidha, watu kadhaa akiwamo Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete, Salma Kikwete, Bernard Membe, George Madafu, Jack Zoka na Othuman Rashid, wataweza kufikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa madai ya matumizi mabaya ya madaraka.

Huu utakuwa ni ''uamuzi mgumu lakini sahihi''; na ndio maana kuna genge kubwa la wahuni linahaha usiku na mchana kumzuia Lowassa asiingie Ikulu
 
Nasikia fisadi lowasa leo atajaribu kujisafisha kupitia vyombo vya habari.ngoja tusubiritunaoma mtakao kuwepo kwenye kikao mtupatie live updates.
 
Hakuna sababu ya kuhangaika na wapinzani kwa sasa wale ni weupe sana dawa yao ndogo, ni CCM kuja na mgombea anayeuzika siyo Lowassa ambaye upinzani wanaomba CCM wafanye makosa ili kwao iwe rahisi wakati wa kampeni

Mkuuu Lowasa yeye anachotakiwa ni kusafishwa na yeye kutoa maelezo.
Yeye aliwajibika kutokana na walikuwa chini yake kufanya makosa. Yeye akaamua kubeba msalaba kwani bila yeye Serikali isingekalika.
Kuamua kuokoa serikali na gharama sisizo za lazima akaona yeye angatuke
 
Katiba hairuhusu rais mstaafu kushtakiwa kwa lolote alilotenda akiwa madarakani!

Katiba inaweza kubadilishwa muda wowote. Lowasa atakuwa mjinga kama akienguliwa kinyemela halafu akaendelea kubaki CCM!!
 
Yaani kumbe watu wanamuogopa Lowassa mahakamani!!! Hii nchi si ya watu fulani tu; Hata asipochukua nchi na wakichukua UKAWA, Watafikishwa mahakamani tu na kama watakuwa na hatia!!!?
 
Mkuuu Lowasa yeye anachotakiwa ni kusafishwa na yeye kutoa maelezo.
Yeye aliwajibika kutokana na walikuwa chini yake kufanya makosa. Yeye akaamua kubeba msalaba kwani bila yeye Serikali isingekalika.
Kuamua kuokoa serikali na gharama sisizo za lazima akaona yeye angatuke

Aliwajibika kuficha uozo?

Let him pay the price ya unafiki... Kwani kama hakuhusika si angejiuzulu kabla ya tume kuundwa?

Alikuwa anasubiri tume ndiyo ajiuzulu?

Tetezi zingine ni kuendelea kumfanya achukuwe zaidi hata na wale ambao hawakuwa na sababu ya kumchukia
 
edward lowassa, mmoja wa wanachama wa chama cha mapinduzi (ccm), waliojiapiza kufia katika urais, amekimega chama hicho vipande viwili. Anaripoti yusuf aboud … (endelea).

lowassa aliyekuwa mmoja wa wanachama sita wa chama hicho walikuwa katika uangalizi, anadaiwa kuwa ameshindikiza kuondolewa mapema adhabu hiyo, vinginevyo angeondoka.

“ni kweli chama chetu kimemshindwa lowassa na sasa kimemuondoa kifungoni. Hii maana yeka ni kwamba sasa lowassa yuko huru kuwa mgombea urais wa chama chetu katika uchaguzi mkuu ujao,” anaeleza mjumbe mmoja wa nec aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa gazetini.

amesema, “kwa maoni yangu, hatua hii itakidhoofisha zaidi ccm kuliko kukiimarisha. Kama ccm inajitakia mema, hakiwezi kuruhusu lowassa kuwa mgombea wake. Huyu mtu amekivuruga chama chetu. Amenunua watu wetu na amekigeuza chama kuwa genge la wanunuzi wa kura.”

jana jumatatu, kamati ya maadili ya chama hicho iliyodai ilikuwa na “faili la lowassa na watuhumiwa wengine sita,” imesema kuwa mwanasiasa huyo “hana tena hatia na kwamba adhabu aliyopewa tayari imemalizika.”

wachambuzi wa mambo ya kisiasa ndani ya chama hicho wanasema, “kuachiwa huru lowassa” kunathibitisha udhaifu wa mwenyekiti wa chama hicho, katika kusimamia chama chake.

taarifa zinasema, ikiwa lowassa atakapitishwa na chama hicho kuwa mgombea wake urais, taifa litaendelea kutumbukia katika visa vya visasi, kutekwa na kuteswa, kumwagiwa tindikali na matukio mengine dhidi ya wananchi na vyombo vya habari.

aidha, watu kadhaa akiwamo rais jakaya kikwete, ridhiwani kikwete, salma kikwete, bernard membe, george madafu, jack zoka na othuman rashid, wataweza kufikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa madai ya matumizi mabaya ya madaraka.

wengine wanaoweza kufikishwa mahakamani, waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari, ambao watatuhumiwa kuandika uchochezi na kudhoofisha serikali.

jakaya kikwete ambaye ndiye rais wa jamhuri, amewahi kunukuliwa na mmoja wa marafiki zake akijiapiza kuwa “lowassa hawezi hata kufikiriwa kuwa mgombea urais.”

hivi karibuni, gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki lilichapisha taarifa kuwa lowassa anaungwa mkono katika mbio zake za kugombea urais na aliyekuwa mbunge wa igunga (ccm), rostam aziz.

kwa mujibu wa gazeti hilo, rostam ametajwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa, col. Apson mwang’onda ambaye alitajwa kuwa mwenyekiti wa “kamati ya ushindi ya lowassa.”

rostam ambaye amehamishia sehemu kubwa za biashara zake nchini kenya na dubai kwa sasa, ndiye aliyekuwa mfadhili mkuu wa kikwete katika mbio za urais mwaka 2005.

mfanyabiashara huyo ambaye amewahi kuwa mbunge wa igunga (ccm), alikuwa miongoni mwa kundi lililohodhi ccm na kufanya maamuzi mengi kwa niaba ya chama na serikali. Katika miaka mitano ya kwanza ya utawala wa kikwete, rostam alifanywa mweka hazina wa chama hicho.

mbali na rostam aziz, lowassa amezunguukwa na watu wengi wanaotiliwa shaka uadilifu wao mbele ya jamii, akiwamo andrew chenge na nazir karamagi.

kikubwa wana jf tuombe mungu atupe kiongoz mwenye hofu yake na atakae simamia haki,na pia tumwombe mungu pia atupe hekima na akili ya kupima sera na kufanya maamuzi sahihi ndani yetu na tukumbuke tukapige kura wote,ili tupate viongoz tulioelekezwa na mungu kwa hekima zake
 
Hebu tufikirie Baraza la Mawaziri la ENL

  1. Waziri Mkuu Prof Juma Kapuya
  2. Makamu wa Rais Amani Abeid karume Jnr
  3. Waziri wa Sheria na Katiba Andrew Chenge
  4. Waziri wa Nishati na Madini William Ngereja
  5. Waziri wa maliasili na Utalii Mgana Msindai
  6. Waziri Mawasiliano na Uchukuzi Peter Serukamba
  7. Waziri wa Jinsia na watoto Beatrice Shelukindo
  8. Bunge Sera na Uratibu Hamis Mgeja
  9. ......................

Hebu Watanzania tuwe serious kwa safu hii mnatagemea kitu chochote kipya?!

Be The Juror yourself

hili labda ni baraza la rais umpendaye member/ kwa lowasa waziri mkuu ni j.magufuri/
 
Mkuuu Lowasa yeye anachotakiwa ni kusafishwa na yeye kutoa maelezo.
Yeye aliwajibika kutokana na walikuwa chini yake kufanya makosa. Yeye akaamua kubeba msalaba kwani bila yeye Serikali isingekalika.
Kuamua kuokoa serikali na gharama sisizo za lazima akaona yeye angatuke

Kwa hiyo ndio maana ana taka apewe malipo ya urais na watanzania kwa kazi ya kuwabebea msalaba mafisadi?.
 
thread hii inapanda chuki dhidi familia ya Kikwete,waandishi wa habari,wamiliki wa vyombo vya habari na Lowassa.

Sivyo alivyo Laigwanani hana mpango wa kulipiza kisasi.
 
hivi mwaka huu kwa nini hawataki mafisadi wagombee? wameshtuka nini? mbona miaka yote mafisadi yenye pesa za kuhonga ndo yanayoshinda kupitia chama? mwaka huu kunani kwani? na jee ni mafisadi wote watazuiwa au ni baadhi tu na baadhi wanaachiwa? Kama mafisadi wengine wanahonga mihela na wanachaguliwa kwa nini iwe kwa wengine hapana? waacheni mafisadi nayo yagombee, ni haki yao.
 
ivi ni nini kitatokea endapo lowasa atapita kuwa raisi wa Tanzania?baadhi ya watu si watapata strock?watazificha wapi nyuso zao...jiandaeni pia kwa pande zote kukosa au kupata

tatizo ushabiki ndugu mtu anashadadia kushindwa akasahau kuna kushinda pia! ushabiki, ushabiki!
 
hili labda ni baraza la rais umpendaye member/ kwa lowasa waziri mkuu ni j.magufuri/

Sasa hilo baraza la mawaziri amepanga Lowassa au ni wewe umepanga kwa mtazamo wako ! kwani lazima uandike na kupost?
 
Amtishe Kikwete tu ila hataweza kuwatisha watanzania.
 
EDWARD Lowassa, mmoja wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliojiapiza kufia katika urais, amekimega chama hicho vipande viwili. Anaripoti Yusuf Aboud … (endelea).

Lowassa aliyekuwa mmoja wa wanachama sita wa chama hicho walikuwa katika uangalizi, anadaiwa kuwa ameshindikiza kuondolewa mapema adhabu hiyo, vinginevyo angeondoka.

“Ni kweli chama chetu kimemshindwa Lowassa na sasa kimemuondoa kifungoni. Hii maana yeka ni kwamba sasa Lowassa yuko huru kuwa mgombea urais wa chama chetu katika uchaguzi mkuu ujao,” anaeleza mjumbe mmoja wa NEC aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Amesema, “Kwa maoni yangu, hatua hii itakidhoofisha zaidi CCM kuliko kukiimarisha. Kama CCM inajitakia mema, hakiwezi kuruhusu Lowassa kuwa mgombea wake. Huyu mtu amekivuruga chama chetu. Amenunua watu wetu na amekigeuza chama kuwa genge la wanunuzi wa kura.”

Jana Jumatatu, Kamati ya Maadili ya chama hicho iliyodai ilikuwa na “faili la Lowassa na watuhumiwa wengine sita,” imesema kuwa mwanasiasa huyo “hana tena hatia na kwamba adhabu aliyopewa tayari imemalizika.”

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa ndani ya chama hicho wanasema, “kuachiwa huru Lowassa” kunathibitisha udhaifu wa mwenyekiti wa chama hicho, katika kusimamia chama chake.

Taarifa zinasema, ikiwa Lowassa atakapitishwa na chama hicho kuwa mgombea wake urais, taifa litaendelea kutumbukia katika visa vya visasi, kutekwa na kuteswa, kumwagiwa tindikali na matukio mengine dhidi ya wananchi na vyombo vya habari.

Aidha, watu kadhaa akiwamo Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete, Salma Kikwete, Bernard Membe, George Madafu, Jack Zoka na Othuman Rashid, wataweza kufikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa madai ya matumizi mabaya ya madaraka.

Wengine wanaoweza kufikishwa mahakamani, waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari, ambao watatuhumiwa kuandika uchochezi na kudhoofisha serikali.

Jakaya Kikwete ambaye ndiye rais wa Jamhuri, amewahi kunukuliwa na mmoja wa marafiki zake akijiapiza kuwa “Lowassa hawezi hata kufikiriwa kuwa mgombea urais.”

Hivi karibuni, gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki lilichapisha taarifa kuwa Lowassa anaungwa mkono katika mbio zake za kugombea urais na aliyekuwa mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Rostam ametajwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa, Col. Apson Mwang’onda ambaye alitajwa kuwa mwenyekiti wa “kamati ya ushindi ya Lowassa.”

Rostam ambaye amehamishia sehemu kubwa za biashara zake nchini Kenya na Dubai kwa sasa, ndiye aliyekuwa mfadhili mkuu wa Kikwete katika mbio za urais mwaka 2005.

Mfanyabiashara huyo ambaye amewahi kuwa mbunge wa Igunga (CCM), alikuwa miongoni mwa kundi lililohodhi CCM na kufanya maamuzi mengi kwa niaba ya chama na serikali. Katika miaka mitano ya kwanza ya utawala wa Kikwete, Rostam alifanywa mweka hazina wa chama hicho.

Mbali na Rostam Aziz, Lowassa amezunguukwa na watu wengi wanaotiliwa shaka uadilifu wao mbele ya jamii, akiwamo Andrew Chenge na Nazir Karamagi.

Wafuasi wa Lowassa wamejitokeza na wanatoa hoja si katka magazeti,redio na kwingineko,sasa mtu unatumia muda mrefu kumsema Lowassa lakini hujitokezi KUMJENGA yule unaemtaka! Lowassa hafai sema yule anaefaa na kwanini anastahili kukabidhiwa nchi aiongoze! Wengi mnaodhani mnamchafua Lowassa mimi naona kama ndo mnazidi kumjenga! Lakini mkumbuke lowassa nae ana mazuri yake! simtetei lkn ndio ukweli.!
 
Aliwajibika kuficha uozo?

Let him pay the price ya unafiki... Kwani kama hakuhusika si angejiuzulu kabla ya tume kuundwa?

Alikuwa anasubiri tume ndiyo ajiuzulu?

Tetezi zingine ni kuendelea kumfanya achukuwe zaidi hata na wale ambao hawakuwa na sababu ya kumchukia

mbona sasa kama msafi hausemi huo uozo? anasubili hadi lini? yeye alikuwa waziri mkuu, hawezi kujitenga na uozo, kama aliona uozo na yeye ndo mtendaji mkuu basi angejiuzuru kuonesha uadilifu wake, kitendo cha kuacha uozo akiona ni mapungufu makubwa sana, akiwa Rais si ndo ataacha mengi.
 
EDWARD Lowassa, mmoja wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliojiapiza kufia katika urais, amekimega chama hicho vipande viwili. Anaripoti Yusuf Aboud … (endelea).

Lowassa aliyekuwa mmoja wa wanachama sita wa chama hicho walikuwa katika uangalizi, anadaiwa kuwa ameshindikiza kuondolewa mapema adhabu hiyo, vinginevyo angeondoka.

“Ni kweli chama chetu kimemshindwa Lowassa na sasa kimemuondoa kifungoni. Hii maana yeka ni kwamba sasa Lowassa yuko huru kuwa mgombea urais wa chama chetu katika uchaguzi mkuu ujao,” anaeleza mjumbe mmoja wa NEC aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Amesema, “Kwa maoni yangu, hatua hii itakidhoofisha zaidi CCM kuliko kukiimarisha. Kama CCM inajitakia mema, hakiwezi kuruhusu Lowassa kuwa mgombea wake. Huyu mtu amekivuruga chama chetu. Amenunua watu wetu na amekigeuza chama kuwa genge la wanunuzi wa kura.”

Jana Jumatatu, Kamati ya Maadili ya chama hicho iliyodai ilikuwa na “faili la Lowassa na watuhumiwa wengine sita,” imesema kuwa mwanasiasa huyo “hana tena hatia na kwamba adhabu aliyopewa tayari imemalizika.”

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa ndani ya chama hicho wanasema, “kuachiwa huru Lowassa” kunathibitisha udhaifu wa mwenyekiti wa chama hicho, katika kusimamia chama chake.

Taarifa zinasema, ikiwa Lowassa atakapitishwa na chama hicho kuwa mgombea wake urais, taifa litaendelea kutumbukia katika visa vya visasi, kutekwa na kuteswa, kumwagiwa tindikali na matukio mengine dhidi ya wananchi na vyombo vya habari.

Aidha, watu kadhaa akiwamo Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete, Salma Kikwete, Bernard Membe, George Madafu, Jack Zoka na Othuman Rashid, wataweza kufikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa madai ya matumizi mabaya ya madaraka.

Wengine wanaoweza kufikishwa mahakamani, waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari, ambao watatuhumiwa kuandika uchochezi na kudhoofisha serikali.

Jakaya Kikwete ambaye ndiye rais wa Jamhuri, amewahi kunukuliwa na mmoja wa marafiki zake akijiapiza kuwa “Lowassa hawezi hata kufikiriwa kuwa mgombea urais.”

Hivi karibuni, gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki lilichapisha taarifa kuwa Lowassa anaungwa mkono katika mbio zake za kugombea urais na aliyekuwa mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Rostam ametajwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa, Col. Apson Mwang’onda ambaye alitajwa kuwa mwenyekiti wa “kamati ya ushindi ya Lowassa.”

Rostam ambaye amehamishia sehemu kubwa za biashara zake nchini Kenya na Dubai kwa sasa, ndiye aliyekuwa mfadhili mkuu wa Kikwete katika mbio za urais mwaka 2005.

Mfanyabiashara huyo ambaye amewahi kuwa mbunge wa Igunga (CCM), alikuwa miongoni mwa kundi lililohodhi CCM na kufanya maamuzi mengi kwa niaba ya chama na serikali. Katika miaka mitano ya kwanza ya utawala wa Kikwete, Rostam alifanywa mweka hazina wa chama hicho.

Mbali na Rostam Aziz, Lowassa amezunguukwa na watu wengi wanaotiliwa shaka uadilifu wao mbele ya jamii, akiwamo Andrew Chenge na Nazir Karamagi.

Hiyo list yake ni ya wezi watupu - Rostam Azizi; Andrew Chenge, Nazir Karamagi - hakuna hata msafi mmoja. Tuwape nchi ili watuibie au vipi? Waambie wakaendeshe biashara zao tu - maana wote wana biashara kubwa kubwa.
 
mbona sasa kama msafi hausemi huo uozo? anasubili hadi lini? yeye alikuwa waziri mkuu, hawezi kujitenga na uozo, kama aliona uozo na yeye ndo mtendaji mkuu basi angejiuzuru kuonesha uadilifu wake, kitendo cha kuacha uozo akiona ni mapungufu makubwa sana, akiwa Rais si ndo ataacha mengi.

Cool down life is so sweet!

Ulisoma maelezo ya niliyekuwa namuuliza?

Pole dear... God is still on throne usiweke matumaini makubwa kwa binadamu hadi ukapoteza mwelekeo wakufikiri... Yeye atakuja ataondoka lakini Mungu ni wa milele jaribu kum defend yeye kwa nguvu, akili na uwezo wako wote... Hao wengine ni variables tu they matter less kwenye maisha yako.

Ni ushauri wa mhubiri Ame...

Lakini naongezea hili; mwaka huu ni tamati ya ufisadi upende usipende wenye mamlaka yetu tumeamua kusimama tuhesabiwe!
 
Back
Top Bottom